Kesi ndogo ya Freeman Mbowe: Shahidi akamilisha ushahidi wake, Shahidi mwingine kuendelea tarehe 12/11/2021

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,818
4,569
Salaam Wakuu,

Leo tarehe 11/11/2021 yanatolewa maamuzi ya kesi ndogo Mwenyekiti wa CHEDEMA Freeman Mbowe.

Kujua jana kesi ilipoishia, soma: Yaliyojiri Mahakama Kuu kesi ndogo ya Mbowe, Superitendent Jumanne Malangahe atoa Ushahidi

Ungana nami katika uzi huu ili kujua kila kinachojiri Mahakamani.

FD5gp2uXoAABf9_

Picha: Watu mbalimbali waliohudhuria Mahakama kuu leo 11/11/2021

UPDATES;
Jaji ameingia Mahakamani Sasa Saa 5 Na Dakika 15 Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa.

Wakili wa Serikali Robert Kidando anatambulisha Jopo la Mawakili wa Serikali
1. Pius Hilla
2. Abdallah Chavula
3. Jenitreza Kitali
4. Nassoro Katuga
4. Esther Martin
5. Tulimanywa Majige
6. Ignasi Mwinuka

Wakili Peter Kibatala anawatambulisha jopo la Mawakili wa Utetezi:
1. Jeremiah Mtobesya
2. Paul Kaunda
3. Fredrick Kihwelo
4. Dickson Matata
5. Iddi Msawanga
6. John Mallya
7. Alex Massaba
8. Khadija Aaron
9. Evaresta Kisanga
10. Maria Mushi

- Jaji anawaita washtakiwa wote wanne, na wanaitika kwamba wapo.

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shauri linakuja Kwa ajili ya kusikiliza Uamuzi wa Mahakama, sisi tupo tayari Wakili Peter Kibatala: Nasi pia kwa Ruhusa yako tupo tayari Kupokea Uamuzi na Kuendelea na Kesi.

- Jaji anaandika Kidogo

Jaji: Jana nilisikikiza Pingamizi la Upande wa Utetezi, Na baada ya Kusikiliza Pande zote Mbili, Maamuzi yapo tayari Jana wakati Shahidi akitoa Ushahidi alieleza Kwamba Baada ya Kupewa Maelekezo ya Kumwandika Maelezo Mshtakiwa namba tatu

Jaji: Na baada ya kupitia Nyaraka hiyo Shahidi alisema anaitambua na baada ya hapo aliomba Mahakama Ipokee Nyaraka hiyo kwa ajili ya Utambuzi, Kitu ambacho Mawakili Wa Washtakiwa wote wanne walipinga Vikali

Jaji: Inapaswa Shahidi ajenge Misingi Kwamba Kwa namna Gani Kielelezo Kimemfikiaje Mahakamani, Na Mawakili Wakasema Kinachotolewa Mahakamani ni Register siyo Entry Kwa Mfano Ingekuwa na Features ambazo zinaonyesha Register hiyo Inatumika Central tu na siyo Mahala Pengine popote

Na Pale ambapo Shahidi ametoa Ushahidi wake anaweza Kufafanua, Wakaomba Mahakama Ione Kielelezo Kilichopo Mahakamani shahidi anaweza Kutoa Ushahidi Wake, Wakaeleza tarehe 07 August 2020 namba alivyo fika Saa 11 Alfajiri na Jinsi ambavyo Shahidi aliweka Entry na aliweza Kukitambua

Jaji: na hicho ndicho kimezua shaka. Na Upande wa Mashtaka Walipata nafasi Ya Kujibu kwa Kuwakilishwa na Abdallah Chavula na Pius Hilla Walisema Kwamba Mapingamizi hayana Mashiko, Wakaja na Kesi ya DPP VS SHARIF Authentication ya Mahakama Inapaswa Kufanywa na Ushahidi Wa Shahidi.

Wakaomba Mahakama itofautishe Kesi ya DPP VS SHARIF ATHUMAN kwamba kesi ile Kielelezo Kilikuwa Gari na Kwenye Kesi hii Kielelezo ni Nyaraka, Wakarejea Kesi ya CHARLES GAZILABO dhidi Ya Jamhuri Kwamba Kesi hiyo iliweka Mambo Matatu ya Relevance, Competence na Shahidi Husika

Wakasema Kwamba Kwa namna ambavyo Shahidi alikuwa anatoa Ushahidi Wake ni Competent. Wakasema Kwenye Kesi Ya CHARLES GAZILABO Kwamba Mtu anaye weza Kuelezea Kielelezo NA kukitambua, Kitu ambacho Shahidi alifanya.

Shahidi alieleza Kwamba alifika kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam, Hiyo inathibitisha kwamba Shahidi anaweza Kufanya Utambuzi na wakaomba Mahakama Itupilie mbali, Upande wa Utetezi Walipata tena nafasi ya Kujibu na Kuona Bado Mapingamizi yao yanayo Sababu

Jaji: Na wakaendelea Kusema Kwamba Suala Zima la Chain of Custody, Mahakama Imeshatolea Maamuzi Kwamba Chain of Custody Inaweza Kujadiliwa Mwishoni, Wakasema Shahidi alijitahidi Kueleza Kwamba aliweka Entry na hilo pekee ndiyo lina fanya Shahidi aonekane anaweza Kukitambua.

Jaji: Kwenye kesi Ya SHARIF ni kwamba wanaona Kanuni inaweza Kutumika Kwenye kesi yoyote, Na Kwamba Shahidi ameeleza Entry na a siyo Kielelezo Chenyewe na Kwamba Suala la Authentication halijaweza Kukidhiwa, Na swala Zima la Kuamua Chain of Custody Wali endelea Kusema Swala La Kupinga Kielelezo ni Jukumu lao Kupinga Wakati Wa Uchukuliwaji, Upande wa Mashtaka wamekosa Hoja za Msingi kuhusiana na Mapingamizi yao.

Na Kwamba Hakuna Features Mahususi Kuhusiana na Kielelezo hicho ili Kutofautisha Detention Register na Detention Register zingine zinazotumika katika Vituo Vingine.. Na suala la Chain Of Custody haijaelezwa Vizuri ni wapi Walipo toa Kielelezo hicho, Kwamba kwa Kumbukumbu zilizopo bado Kielelezo Kipo Chini ya Mahakama. Huo ndiyo ulikuwa Mwisho wa Muhtasari. Sasa twende kwenye maamuzi.

Jaji: Identification of EXHIBIT, Establishing Chain Of Custody, Identification of Objects. Haya siyo Maneno yangu ni Maneno ya Maamuzi ambayo nimeyanukuu hapo juu. Lengo la Chain Of Custody wanapaswa Kueleza Kielelezo Wamekitoa wapi.

Na Kuhusiana na Competence ya Shahidi imeelezwa Kwenye kesi ya CHARLES GAZILABO, KHAMIS ADAM Kwamba Mtu ambaye amekifanyia kazi Kielelezo siyo tu anaweza Kukitolea Ushahidi Bali anaweza za Pia Kukitolea Maelezo

Jaji anasoma maamuzi ya kesi hiyo aliyonukuu

MAAMUZI
JAJI: Tunakubaliana kwa pamoja Kwamba Pingamizi linapinga ipokelewaji wa Vielelezo na Siyo Jambo geni Mahakamani, Na Maamuzi Yamefanywa na Mahakama zetu katika Upokeaji wa Vielelezo Mahakamani. Maamuzi yameonyesha Taratibu, Kanuni na Muongozo.

Kufuatia Maamuzi ya SHARIF MOHAMMED na wenzake Mahakama ya Rufani Ilitoa Maamuzi Kwamba tunao Ushahidi Wa Namna Nne Uhalisi, Testimonial, Documentary Evidence, Na Kwamba Mahakama inaweza Kupokea Ushahidi Mahakamani Wakati wowote.

Mahakama Ijiridhe Kama Ushahidi ni Relevance, Material na Competence, Na Katika Maamuzi yake wamejadili kwa kina kuhusu Ushahidi Halisi. Nimesema Mpaka Mwisho Sijaona Kwamba Vigezo ambavyo vinatumika Katika Real Evidence haitakiwi Kutumika katika Kupokea Documentary Evidence.

- Jaji amemaliza kusoma Maamuzi ya Shauri hilo kama Rejea yake,

Jaji: Kimsingi hayo ndiyo maamuzi ya mahakama ya Rufaa.. Kwa sababu hiyo sasa ilikupima Competence ya Shahidi, Na Kwa Kesi hii Shahidi ameeleza Vizuri kuhusu Kielelezo hicho ambacho alikotumia Kuweka ENTRY ili Kumtoa.

Shahidi Kwenda Kumchukua Mtuhumiwa Maelezo yake. Kwa Maana hiyo anayo Competence. Kuhusiana na Relevance ni Ukweli kwamba Kipo Relevance sababu inadaiwa ndiyo walitumia Kielelezo hicho Kumtoa Mtuhumiwa

Kuhusiana na Materiality ni kweli kabisa kwamba kitasaidia Mahakama Kufanya Maamuzi, ikiwemo Katika Pingamizi Kwamba Mshitakiwa hakuwa hi Kuwepo Katika Kituo hicho cha Polisi. Mahakama hii inaona kwamba ni sahihi kabisa kuendelea kutumika.

Jaji: Imebakia suaala la Chain Of Custody, Ni kweli Shahidi namba Moja ameeleza Kwamba anaweza Kutambua Kielelezo hicho Kwa Majina yake na Sahihi Yake na Majina ya Mtuhumiwa, Ukweli ni kwamba ameweza Kukitambua, Ingawa Mr. MTOBESYA amepinga Kwamba Features zilizoelezwa ni za Entry na siyo Register Yenyewe.. Lakini Mahakama yenyewe inaweza Kutambua kuwa Kielelezo hicho huwezi Kutenganisha Entry na Register. Na Kuhusiana na Chain Of Custody Shahidi hajeleza Chain of Custody Kwamba ni Kwa namna gani Kielelezo hicho Kimemfikia.

Jaji: Ni kweli Kwamba hajaeleza ametoa wapi, Ni kweli Kwamba Kielelezo Kipo Kwenye Kumbukumbu ya Shauri Lingine, Ili Mahakama ione kama kilifuata Utaratibu kilipaswa kionekane kwamba ni kweli Kilifuata Utaratibu wa kiutawala kutoka Mahakamani.

Na Kwa namna hiyo Kielelezo kinajifuta Chenyewe kwa sababu Shahidi hakuonyesha namna gani kilimfikia, Assumption ni kwamba Kielelezo Kipo Kwenye Chumba cha Mtunza Kielelezo Cha a Mahakama, Hakuna Ushahidi Kwamba Shahidi alikipataje kuja Mahakamani.

Jaji: Kwa sababu hiyo mahakama inakikataaaaa kielelezo hiki natoa amri.

- Mawakili wa pande zote wanasimama na kuinama kuonyesha kukubaliana na uamuzi wa Jaji.

Jaji: Shahidi wenu yupo wapi tuendelee

Jaji: Shahidi nakukumbusha Upo chini ya Kiapo ambacho Ulikiapa wakati Unatoa Ushahidi Wako

Wakili wa Serikali Robert Kidando ameanza kuuliza maswali
Wakili wa Serikali: Shahidi Ulisema Kwamba Siku ya Tarehe 07 August 2020 ulimchukua Mohammed Ling'wenya Kwenda Kumchukua Maelezo, Eleza Siku hiyo alikuwa na hali gani

Shahidi: Wakati na chukua Mohammed Abdilah Ling'wenya alikuwa Mwenye Afya Njema na Hakuwa na Tatizo lolote

Wakili wa Serikali: Baada ya Kumchukua Ulimpeleka wapi

Shahidi: Nilimpeleka Pembeni Kidogo Kwenye Chumba Kwa ajili ya Mahijiano na Mtuhumiwa huyo

Wakili wa Serikali: Elezea Baada ya Kukaa Pamoja nini Kiliendelea

Shahidi: Nikijambulisha Kwa Majina Kwamba Mimi ni ASP JUMANNE MALANGAHE, Na Mtuhumiwa akajitambulisha kwa Majina yake Kwamba anaitwa Mohammed Abdilah Ling'wenya alimaarufu kama DOYI

Wakili wa Serikali: Elezea Ni kitu gani sasa Ulifanya Baada ya Kujitambulisha

Shahidi: Nilimuonya Kwamba anatuhumiwa kwa Makosa ya Kula Njama za Kutenda Matendo Ya Ugaidi, Nilimueleza kwamba Katika tuhuma hizo alazimiki kueleza Chochote isipokuwa kwa hiari yake Mwenyewe chochote atakachokieleza kinaweza Kutumika kama Ushahidi Mahakamani, Vilevile anayo Haki ya Kuwepo Mwanasheria Wake, Ndugu yake, Jamaa yake, Rafiki ili ashuhudie Wakati Maelezo hayo yakiandikwa, Baada ya Hatua hiyo, Mimi Nilisaini na Mtuhumiwa alisaini ilikuonyesha nilimuonya.

Shahidi: Baada ya kumaliza Hatua hiyo Mtuhumiwa Mohammed Abdilah Ling'wenya alimaarufu DOYI alijibu Onyo hilo.. Kwamba yeye Mohamed Abdilah Ling'wenya Alimaarufu DOYI ameonywa na Mimi ASP JUMANNE MALANGAHE anatuhumiwa kwa Kosa la Kula Njama kutenda Vitendo Vya Ugaidi Chini ya Sheria namba 24 ya Sheria ya Kupambama na Ugaidi, Kwamba alazimishwi Kusema Lote isipokuwa kwa hiari Yake Mwenyewe. Chocolate atakachoandika Linaweza Kutumika aka Ushahidi Mahakamani.

Na pia anaweza Kuwepo Mwanasheria Wake, Ndugu yake, Jamaa yake, au Rafiki ili ashuhudie Wakati Maelezo yake yakiandikwa. Baada ya Mtuhumiwa kuulizwa Onyo hilo kama Yupo Tayari Kutoa Maelezo yake, Mtuhumiwa akajibu Ndiyo Nipo tayari, Nilimuuliza nani awepo Wakati anatoa Maelezo yake, Mtuhumiwa alijibu yeye Mwenyewe anatosha Wakati wa Kutoa Maelezo yake, alisaini na Mimi nikasaini, baada ya hapo akawa tayari Kutoa Maelezo Yake, Saa 2 na Dakika 20 nilianza kuandika Maelezo Ya Mtuhumiwa,

Wakili wa Serikali: Wewe Ulifanya nini baada ya yeye Kusema yupo tayari Kutoa Maelezo

Shahidi: Nilimuuliza Mtuhumiwa Ushiriki wake Kuhusu tuhuma nilizomueleza

Shahidi: Nilimueleza kila anapohusika na ambapo yeye alikiri

Wakili wa Serikali: Wewe baada Kueleza ulifanya nini

Shahidi: Nilikuwa na andika Kwenye Karatasi, Fomu kile alichokuwa ananieleza

Wakili wa Serikali: Kilikuchukua amuda gani?

Shahidi: Muda wa Masaa 2 na Dakika 42

Wakili wa Serikali: baada ya Kumalizia Kuandika Ulifanya nini?

Shahidi: Nilimpatia Maelezo ayasome, ilikuweza Kuongeza, Kupunguza au Kufanya Marekebisho kwa yake aliyiyasema

Wakili wa Serikali: Baada ya Mtuhumiwa Kusoma Maelezo hayo akasemaje

Shahidi: Ameridhika na hana cha Kupunguza wala Kuongeza

Wakili wa Serikali: Ulifanya nini baada ya kuandika

- Kibatala: OBJECTION anachofanya Wakili anajua Hakiruhusiwi

Wakili wa Serikali: Baada ya kumaliza Kuandika Ulifanya nini?

Shahidi: Alisaini na Mimi nikasaini, na baada ya hapo nikaandika Uthibitisho wangu mimi Mwenyewe.

Wakili wa Serikali: Baada ya akumaliza Kuandika Uthibitisho huo Ulifanya nini

Shahidi: Niliandika Muda wa Kuandika Maelezo

Wakili wa Serikali: baada ya Kumalizia Kuandika Maelezo Ulifanya nini na Mtuhumiwa

Shahidi: Nilimchukua na Kumrejeaha Chumba cha Mashtaka

Wakili wa Serikali: Maelezo ya Mshitakiwa Mohammed Abdilah Ling'wenya uliyapeleka wapi

Shahidi: Kwa Assistant Inspector Swila

Wakili wa Serikali: Ilikuwa ni Lini?

Shahidi: Ilikuwa ni Siku hiyo hiyo

Wakili wa Serikali: Elezea Baada ya Shughuli hiyo Ulikutana wapi tena na Mtuhumiwa

Shahidi: Niliondoka Kwenda Kufanya Majukumu Mengine kwa Kadri nilivyokuwa naelekezwa na ACP kingai, Siku ya tarehe 08 August 2020 Majira ya Saa 5 Asubuhi Tukiwepo na Inspector Mahita, Tulielekezwa na Afande Kingai Kumuhamisha Mtuhumiwa na Kumpeleka Kituo cha Polisi Mbweni.

Wakili wa Serikali: Wakati Mlielekea Mbweni Ni kitu gani Kiliendelea

Shahidi: Hakuna Kilichoendelea, Tulipofika Tukiwakabidhi watuhumiwa, Na Kwenda Kuonana na Kiongozi wetu ACP KINGAI kwa Upelelezi wa watuhumiwa Wengine

Wakili wa Serikali: Elezea Baada ya hapo Ulionana naye wapi?

Shahidi: Sikuwahi Kuonana tena na Mtuhumiwa huyo..

Wakili wa Serikali: Kwa Ufahamu Wako Vituo ambavyo Mohammed Abdilah Ling'wenya aliweza Kufikishwa ni Vingapi?

Wakili wa Serikali: Unasema Siku Mnampeleka Kituo Cha Polisi Mbweni hakuna Kilichofanyika zaidi ya kumkabidhi pale, Sababu hasa ni nini?

Shahidi: Sababu zilikuwa za Kiupelelezi, Sababu Kuna Mwingiliano Wa watuhumiwa wengi wanaingia na Kutoka ni wengi.. Tulihofia Taarifa zinaweza Kufika Kwa Watuhumiwa ambao bado tunawatafuta Kwa urahisi.

Wakili wa Serikali: Siku unaandika maelezo ya Mtuhumiwa pale, unasema ulimpa Inspector Swila, Je Inspector Swila alipeleka wapi? -

- Mtobesya: OBJECTION Mheshimiwa Jaji huyo siyo Swila na hawezi Kujibu kwa niaba ya Swila

Wakili wa Serikali: Ngoja Nirudie Swali

Wakili wa Serikali: Ulipompa Swila hizi Karatasi, alifanya nini na Hizo Karatasi

Shahidi: Ndiyo tulikuwa tunampa Nyaraka zetu, Kwa hiyo alizochukua akaenda Kuweka kwenye Jalada

- Mtobesya: OBJECTION Mheshimiwa Jaji hizo ni hearsay

Jaji: Jiande uje kumuuliza labda walikuwa naye.

Shahidi: Swila amuda Mwingi tulikuwa naye, alienda Kuweka kwenye Jalada la Upelelezi

- Kibatala: OBJECTION Mheshimiwa Jaji Wakili anahama Eneo, Je ulichokiandika Siyo HearSay

Wakili wa Serikali: Sisi Bado hatuoni tatizo, huyu Mohamed Abdilah Ling'wenya amepinga Maelezo ya Onyo kwamba hakuwahi Kufika Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam na ajawahi Kuandika Maelezo hayo..

Shahidi: Siyo Kweli, Mimi Mwenyewe ndiyo Niliyempeleka Pale, Nikaenda Kumchukua Mimi Mwenyewe Kutoka Kwenye Chumba Cha Mashtaka Nikiwa Pekee yangu bila Uwepo wa Askari Mwingine yoyote akiwa na hali Nzuri, na Mimi Niliondoka nikiwa nje ya Kituo na yale maelezo, Nikampigia Assistant Inspector Swila yale achukue yale maelezo ili aweke kwenye Jalada la Kesi.

Wakili wa Serikali: Wewe una utbitisho gani kwamba uliandika Hayo Maelezo siku ya tarehe 07 August 2020

Shahidi: Alikuwepo Askari aliyekuwepo pale Chumba cha Mashtaka. Na baada ya kumaliza Kuandika Maelezo Askari huyo huyo alimpokea na Kumrudisha Lockup.

Wakili wa Serikali: anachosema ni kwamba ulimtishia kwa Bastola ilikutoa Maelezo

Shahidi: Siyo Kweli, Sikuwahi Kumtishia Mtuhumiwa huyo Kwani alikuwa na Ushirikiano, Sikuwa na Sababu hiyo

- Kibatala: OBJECTION, huyu labda hajasikia Vizuri Mapingamizi, nayasoma tena kwa sauti ayasikie

Wakili wa Serikali: Sawa Ngoja Nirudie, Ulimtishia Kwamba Asipo Saini Ile Karatasi ya Maelezo basi yale Mateso Mliyompatia Moshi Mtayarudia

Shahidi: Si kweli Sikumtishia kwa sababu sikuwa na sababu hiyo.

Wakili wa Serikali: Maelezo ya Mohammed Abdilah Ling'wenya ukiyaona unaweza Kuyatambuaje

Shahidi: Naweza Kuyatambua Kwa Majina Yangu, Sahihi yangu, Uwepo wa Majina ya Mtuhumiwa na Sahihi zak na Yote aliyo I eleza Nikaandika kwenye Karatasi ya Maelezo.

Wakili wa Serikali: Samahani Mheshimiwa Jaji tunaomba tumpatie Nyaraka Kwa sababu ya Utambuzi

- Shahidi anamkabidhiwa Nyaraka

Wakili wa Serikali: Angalia Nyaraka hiyo Kama Umeitambua na Useme ni Kitu gani?

Shahidi: Ndiyo nimeitambua Nyaraka hii Kama Maelezo Niliyoaandika kutoka kwa Mohamed Abdilah Ling'wenya Maarufu Kama DOYI,

Wakili wa Serikali: Umeitambuaje?

Shahidi: Kwa Majina Yangu, Sahihi Yangu Pamoja na Saini zake pamoja na aliyoyaeleza

- Kibatala: OBJECTION kwa Stage ya Utambuzi anatakiwa asifike kwenye aliyoyaandika Sababu ni Content

Wakili wa Serikali: Sisi hatuoni tatizo

Kibatala: Kwa Stage ya Utambuzi, aliyoyaandika ni Content

Jaji: content yake hatuingii, anaishia Kusema ameyaona

Wakili wa Serikali: Ungependa Mahakama ifanye nini katika Hayo Maelezo uliyoandika kutoka Kwa Mohammed Abdilah Ling'wenya alimaarufu kama DOYI

Shahidi: Ningependa Mahakama Iyapokee kwa Utambuzi

Mtobesya: Hatupingi Upokelewaji wa Maelezo haya Kwa niaba ya Mshtakiwa wa Kwanza Sababu ni Zifuatazo Naomba Iwe on record Kwamba Mahakama inayajua hayo Maelezo lakini Mshtakiwa wa tatu Amekataa hayo Maelezo Kutokupinga huku Hakumaanishi Kwamba Mshtakiwa anakubaliana na Content.

Wakili wa Serikali S Pius Hilla: OBJECTION Mheshimiwa Jaji natafakari kwamba hupingi lakini kwa conditions kwamba lazima sababu zieleweke, Kama hupingi, Lakini unapoongezea Vitu Vingine inamaana hukubaliani, Tunatengeneza Record gani kwa Mahakama. Kama kuna Jambo it's better akapinga tu hadharani..

Wakili wa Serikali Robert Kidando: kwa Kuongezea tu, hili zoezi la Trial Within Trial na Hii Conditions alizo +toa hapa hairuhusiwi.

Mtobesya: Mheshimiwa Jaji Sijui Kwanini Wenzangu Wamesimama, Wenzangu Waniambie Kwamba Ni Sheria gani inakataza Ninaposema sipingi siruhusiwi Kuongeza Maneno.. Sijui Wenzangu Wanahofu gani labda.. Wakasome Kesi ya Martha Weja sisi Kama Utetezi tunaruhusiwa Kuhoji content.

Jaji: katika Kesi yoyote Mahakama haijui chochote, Bila nyinyi Kueleza Mahakama, Mahakama Imeelekezwa Kwamba Isiyapolee yanayo Vunja Sheria yoyote, Sioni Tatizo Kwa Mtobesya Kuzungumza alichozungumza na huwezi kujua atakitumia wapi.

Mtobesya: naomba nikumbushwe niliishia wapi

Jaji: uliishia Mheshimiwa Jaji

Mahakama: Kicheko

Jaji: Unakubaliana na Mahakama Kupokea Lakini Hukubaliani na Content..

Mtobesya: naomba niishie hapo

- Anasimama Wakili Paul Kaunda...

PAUL KAUNDA: kwa niaba ya Mshtakiwa wa Pili tunaomba kufunga Mkono kilichozungumzwa na Wakili wa Mshtakiwa Wa Kwanza Fredrick Kihwelo: Tunakubaliana na Uwepo wa Nyaraka hii lakini hatukubaliani na Kilichopo Ndani

Kibatala: Kwa niaba ya Mshtakiwa wa Nne na sisi Hatupingi, Tunategemea Kuitumia Nyaraka hii katika Kuhoji Dodoso katika kesi hii Ndogo


Jaji: Yaliyosemwa na Mtobesya Mnalolote la Kujibu (Mashtaka) WS Wanateta Kidogo napokea kama ID namba 1

- Wote wanakubali.

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Naomba Dakika Mbili Nishauriane na Wenzangu Kuhusu Hoja ya Mtobesya kama Kuna la Kumjibu..

Wakili wa Serikali: Off Record Kwanza, Kuna Jambo la Mtobesya Kwamba Kwenye kesi ya Martha Weja, Tukasema tunaomba tujiridhishe kwanza.

Mtobesya: Kwa haki tuwaache wajiridhishe tu, Ni Kesi ambayo Imeripotiwa Kwenye TANZANIA LAW REPORT ya Mwaka 1982 Ukurasa wa 35..

Kibatala: nawakumbusha kwamba wenzetu wazingatie na muda kwa sababu leo tumeamza Saa tano na shahidi ana siku mbili kizimbani.

Jaji: Siku 3 labda kwenye kesi Ndogo ndiyo Siku 2..

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa tupewe tu Muda wa Kutosha kwa sababu hatuna hapa na hatuwezi Kupata ipo Ofisini

Jaji: Mtobesya ametaja Mpaka Kurasa labda anayo hapo.

Mtobesya: Hapana sina hapa ni kesi ya siku nyingi lakini tunatumia sana, Naweza kuiomba na Mimi ofisini Wakascan wakanitumia

Jaji: Natoa Hairisho la Dakika 45, tutarudi Saa 8 Jaji anatoka.

Zinapigwa kelele za kooooooortiiiiiii

Jaji ameingia.. Kesi inatajwa... Quorum zipo vile vile.

Mtobesya: Shahidi Wakati Mnamkamata Ling'wenya ni taarifa zipi Mlikuwa nazo tayari?

Shahidi: Taarifa tulizokuwa nazo alikuwa ni Miongoni Mwa Kundi ambalo lina fanya Njama Kwa Kufanya Vitendo Vya Kigaidi ambavyo ni Kushiriki katika Kulipua Vituo Vya kuuzia Mafuta Kukata Miti na Kuweka Barabarani, Kulipua maeneo yenye Mkusanyiko wa watu na Kuhamasisha Maaandamano ya siyo na Kikomo.

Mtobesya: Ni hizo Taarifa tu au Mlikuwa na Zingine?

Shahidi: Kimyaaa

Mtobesya: Ni nani aliwasaidia Kuwapa Taarifa Mpaka Mkajua Eneo alilokuwa Ling'wenya?

Shahidi: Nilikuwa na Mkuu wangu Afande Kingai yeye Ndiye alikuwa anajua aliyekuwa nampa taarifa nilikuwa naenda Field Kuthibitisha tuhuma kama Mtuhumiwa huyo anahusika

Mtobesya: Mueleze Mheshimiwa Jaji ilichukua muda gani, tangu unatengeneza Dhana hiyo Mpaka Mnamkamata Ling'wenya

Kimyaaaaaaaaaa kinatawala kwa sekunde kadhaa

Mtobesya: Nitakuwa sahihi Kwamba Mpelelezi yoyote kabla hajafanya Upelelezi anakuwa na dhana Kichwani unapoenda Field Unaenda kuthibitisha Kama ni Chanya au Hasi ni sahihi?

Shahidi: Ni sahihi

Mtobesya: Mueleze Mheshimiwa Jaji Kwenye Shauri hili Dhana yako ilikuwa ni nini?

Jaji: anamuuliza Shahidi kama ameelewa Swali

- Shahidi anapata kigugumizi kidogo anashindwa kuongea hapa.. Lakini anafanikiwa kuendelea..

Shahidi: Ni palepale nilipopata Taarifa na Kuanza Kutafakari na haikuchukua Muda Mrefu

Mtobesya: Mueleze Jaji Taarifa hizo ulizipata lini

Shahidi: Siku ya Tarehe 04 August 2020

Mtobesya: na Ling'wenya Mlimkamata tarehe ngapi?

Shahidi: Naomba nirejee Nyuma ya Swali Lako ulilokuwa Umeniuliza

MTOBESYA: enheeeeeeee!

Shahidi: UMENIULIZA Iinachukua Muda gani Kuniwezesha Kwenda Field

Mtobesya: Sijakuuliza Swali hilo Shahidi: Dhana ni Kama Kitu ambacho huna a Uhakika nacho

Mtobesya: Hapa namaanisha HYPOTHESIS, Mpelelezi Yoyote lazima awe na Hypothesis

Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa

Mtobesya: Nakurudisha Kwenye Swali Sasa, Je Mlimkamata lini Ling'wenya

Shahidi: Tarehe 05 August 2020

Mtobesya: Maelezo Ya Ling'wenya uliyaandika lini

Shahidi: Tarehe 07 August 2020

Mtobesya: Kwa hiyo nitakuwa Sasa Kwamba Wakati Unamuhoji ulikuwa na Taarifa

Shahidi: Hapana Sikuwa na Taarifa

Mtobesya: Siwezi Kukunyonga kwa Majibu yako. Haya Umesema Ling'wenya alikiri Kujihusisha Kufanya Vitendo hivyo ni Vipi

Shahidi: Kwamba kweli alijihusisha na Vitendo Vya kupanga Njama

Mtobesya: Nitakuwa sahihi nikisema Mpelelezi asiandike Maelezo ya Mtuhumiwa, Kwa sababu Mpelelezi anataarifa Nyingi Wakati anampeleleza?

Shahidi: Hapana Siyo Sahihi

Mtobesya: Kwa hiyo pale ambapo Kuna Askari Mwingine na Mpelelezi Yupo Hairuhusiwi Askari Mwingine Kuchukua Maelezo

Shahidi: Hapana Inaruhusiwa

Mtobesya: Zoezi la Kuchukua Maelezo lilianzishwa na nani

Shahidi: Mimi Ndiyo Wajibu wangu

Mtobesya: Kwa hiyo iingie kwenye Record Kwamba ni wewe Ndiyo Uliomba Kuchukua Maelezo?

Shahidi: ni Wajibu wangu

Mtobesya: Nitakuwa Sahihi kuna aina 2 Uchukuaji wa Maelezo, pale ambapo Mshtakiwa anaomba au Askari anataka Kufanya hivyo

Shahidi: Hapana Mtuhumiwa hawezi Kuomba

Mtobesya: Kwa hiyo Hakuna Sehemu Mtuhumiwa anaweza Kuomba Kuandikwa Maelezo?

Shahidi: inategemea na Mazingira

Mtobesya: Kwa hiyo tunakubaliana kwamba mtuhumiwa mwenyewe anaweza kuomba kuandikwa Maelezo?

Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa

Jaji: Kama hujamuelewa uliza wakueleweshe...

Shahidi: Natafakari kidogo

Jaji: Ujibu kwa speed sasa

Mtobesya: Kwa hiyo Kuna namna Mbili au Moja

Shahidi: Hakuna Namna mbili

Mtobesya: Maelezo uliyachukua kwa namna ipi Shahidi Kwa namna Mbili Baada Ya Kumuuliza na Yeye Kuwa anajibu

Mtobesya: Kwa hiyo Maelezo Yake yanatokana na Majibu yako

Shahidi: Kulikuwa na Maswali na Sehemu zingine pana Maelezo

Mtobesya: Nilikusikia wakati hujaanza Kuchukua Maelezo Kwamba Ulimpatia Haki zake za Kuwa na Wakili na Ndugu halafu akasema ataandika Mwenyewe, Lakini Hukusema Kwamba Wakati Wote Mnamkamata Mpaka Mnamchukua Maelezo kwamba Hamkuwezesha Kukutana na Ndugu.

Shahidi: Sahihi Sikusema

Shahidi: Ni yale yanayo chukuliwa Kuhusu Mtuhumiwa anahusishwa na Kutenda aina fulani ya Kosa

Mtobesya: Ni hivyo tu?

Shahidi: INATOSHA

Mtobesya: Nitakuwa Sahihi nikisema Maelezo ya Onyo Yanatakiwa Kuonyesha Mtuhumiwa Kosa analo tuhumiwa nalo

Shahidi: Ni sahihi

Mtobesya: Nitakuwa Sahihi Kwamba Kosa Unalomuonya Nalo ni lazima liwe limetamwaka Kwenye Sheria

Shahidi: Ni sahihi

Mtobesya: Nitakuwa Sahihi Kwamba Maelezo ya Onyo Yanatakiwa kuwa Sheria na inatakiwa Kuonyesha Kifungu Unachomuonya nacho

Shahidi: Siyo Kweli, unaweza Kumwambia kwa Maneno tu

Mtobesya: Kwa hiyo siyo Muhimu Kumtajia Kifungu unacho Muonya nacho?

Shahidi: Ni Muhimu kwa Minajiri ya Kumuonya mshtakiwa Mwenyewe

Mtobesya: Kwa hiyo kwako wewe Siyo Muhimu?

Shahidi: Nilisahau lakini nilikuwa nishamwambia

Mtobesya: Nitakuwa sahihi Kwamba ni Matakwa ya Kisheria, Baada ya zoezi la Kuonya Kuisha Tarehe, Mwaka na Muda lazima viwe katika fomu unayotumia Kumuonya

Shahidi: Ni sahihi

Mtobesya: na wewe Uliweka hivyo

Shahidi: Ndiyo Niliweka

Mtobesya: Tutaona baadae kama Uliweka

Mtobesya: na nitakuwa Sahihi Muda wa Kuonya Siyo Muda wa Kuchukua Maelezo, Unamuonya kwanza kisha Unamchukua Maelezo

Shahidi: Ni sahihi

Mtobesya: Kwa hiyo ni sahihi Kwamba muda wa Kuonya ni Tofauti na muda wa Kuchukua Maelezo

Shahidi: Ni sahihi

Mtobesya: Twende kwenye Hitimisho la Kuandika Maelezo pale unapotakiwa Kuthibitisha, nitakuwa Sahihi nikisema Ufungaji wa Maelezo ya onyo una namna Mbili au Tatu kwanza wa Mtu anaye Jua Kusoma na Kuandika na ameridhia Kwa anaye andika, ambaye ajui Kusoma na Kuandika au amekataa na Mwisho Mtu ambaye amekataa

Shahidi: Siyo Sahihi

Mtobesya: Haya tueleze Wewe Wa kwanza anathibitisha vipi

Shahidi: Yeye Mwenyewe anaandika Kwamba nimeyasoma na Kuyaelewa

Mtobesya: na hiyo inaonekana katika Statement uliyoiandika

Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa

Mtobesya: na wewe Mwenyewe Unaandikaje Mwishoni?

Shahidi: Unathibitisha Kuandika Maelezo ya Mtuhumiwa huyo

Mtobesya: huyo ambaye amesoma na kuandika, anathibitisha Vipi? KWA signature na Dole Gumba Maana havitumiki kwa Pamoja.

Shahidi: Vyote Vinatumika

Mtobesya: na huo ndiyo Ushahidi wako

Shahidi: Ndiyo

Mtobesya: Unafahamu PGO ni Nini

Shahidi: Nafahamu Ndiyo

Mtobesya: Nitakuwa sahihi Kwamba Ndiyo Kitendea Kazi chenu cha Kila Siku

Shahidi: Ndiyo

Mtobesya: Haya Mwambie Mheshimiwa Jaji PGO inasemaje

Shahidi: Kwa yule ambaye anajua Kusoma na Kuandika ataweka Sahihi na Kuweka Dole Gumba na Yule ambaye hajui Kusoma na kuandika atashindwa Kuweka Dole Gumba,

Mtobesya: Huyo Ling'wenya alifanya nini kama ulivyo tueleza

Shahidi: Alisaini Pamoja na Dole Gumba

Mtobesya: Kule Chini Mnapoweka Ithibati Kuna Vifungu Mnaviandika

Shahidi: sahihi Mtobesya: Mueleze Jaji kwenye Maelezo yenu Mlitumia Vifungu gani

Shahidi: Ilikuwa Imeshaandikwa Kwenye Karatasi, niliona hakuna haja ya Kuweka hiko Kifungu

Mtobesya: Kitaje Kifungu

Shahidi: Kilikuwa Kifungu Cha 57(3)

Mtobesya: Umekitaja Maana Yake unakifahamu Mueleze Mheshimiwa Jaji kama hicho Kifungu aya zake

Shahidi: Sikumbuki Kama Zipo hizo aya

Mtobesya: Mheshimiwa Jaji naomba nipatiwe ID 1

- Mahakama inampatia Mtobesya ID1

Mtobesya: Na Kuonyesha Kielelezo Cha Mahakama Nikuulize Maswali Machache, Iambie Mahakama Kama Baada Onyo Uliweka Muda

- Shahidi anakuwa mbishiiiii hapa, Mbishi, lakini Mwishoni anasema HAKUNA MUDA..

Mtobesya: tuonyeshe uthibitisho amesoma na Kuyaelewa Sehemu gani

Shahidi: Mtuhumiwa amesaini na Kuweka Dole Gumba

Mtobesya: na Kifungu cha Sheria

Shahidi: Ndiyo nimesema Kwamba Karatasi ilikuwa Tight sikupata nafasi ya kuweka

Mtobesya: Mueleze Mheshimiwa Jaji Pale ambapo Maelezo ya Mtuhumiwa anathibitisha Kuna Kifungu cha Sheria au Hakipo

Shahidi: Hakipo Kifungu cha Sheria

Mtobesya: Mueleze Mheshimiwa Jaji Ulipoishia wewe Kuthibitisha, Kama Kipengele cha Mwisho Kifungu kimelezwa ni Kifungu 57(3) na aya zake au Hapana

Shahidi: Tunaona Kifungu Cha 57(3)

Mtobesya: Mheshimiwa Jaji naomba Kurudisha Kielelezo

Mtobesya: Ni kwanini Hamkuweza Kuchukua Maelezo ya Mtuhumiwa Mkiwa Moshi?

Shahidi: Tulikuwa tunawatafuta watuhumiwa wengine na Watuhumiwa walikuwa ni sehemu ya Kusaidia na Pia Shauri Lenyewe lilikuwa DSM na Pia Nature ya Tukio ilikuwa inaenda Kutokea Mikoa ya Dar es Salaam Arusha Kilimanjaro, MBEYA, Mwanza na Morogoro

Mtobesya: Mweleze Mheshimiwa Jaji Kama Unatambua Utaratibu wa Kuchukua Maelezo halafu baadae unaweza za Kuandika Maelezo ya Ziada (Additional Statement)

Shahidi: Sitambui

Mtobesya: Mtajie mheshimiwa Jaji Kama ni Kanuni au sheria gani inayo kulazimisha kwenda kuchukua maelezo sehemu uliyofungulia shauri

Shahidi: Siyo sheria wala Kanuni lakiniiiiiiiiiiii

Mtobesya: hakuna cha lakini hapa, Mheshimiwa Jaji naomba kuishia hapo...

MALLYA ANAANZA KUULIZA MASWALI
Mallya: Kabla hujahamia Arusha ulikuwa Ofisi ya Upelelezi Dar es Salaam

Shahidi: Sahihi

Mallya: Kwa Muda gani Shahidi: Kwa Miaka 7

Mallya: Ni sahihi Ulikuwa katika Ofisi ya DCI

Shahidi: Ni sahihi

Mallya: Nitakuwa Sahihi nikisema Uinajua Dar es Salaam

Shahidi: Siyo Sahihi

Mallya: Ramadhan Kingai kabla hajawa RCO alikuwa Msaidizi wa ZCO Dar es Salaam

Shahidi: Ni Sahihi

Mallya: Kwenye Timu yenu nikisema kwenye timu yenu angalau Kuna watu Wawili Wa naijua Vizuri Dar es Salaam nitakuwa Sahihi

Shahidi: Siwezi Kusemea Wote

Mallya: Ofisi ya DCI ipo Katikati ya Jiji la Dar es Salaam au Sema Ipo wapi

Shahidi: Mtaa wa OHIO

Mallya: Makao Makuu ya Polisi Mpaka Dar es Salaam ni Umbali gani Kwa Kukadiria

Shahidi: Siwezi Kukadiria

Mallya: lakini Unajua Kuwa Makao Makuu ya Polisi na Polisi Mjini Kati Dar es Salaam Vipo Wilaya Moja

Shahidi: Sahihi

Mallya: Kituo cha Polisi Mbweni Unakifahamu

Shahidi: Nakifahamu

Mallya: Kituo cha Polisi cha Mbweni ni Kituo cha Wilaya ya Kipolisi Kawe

Shahidi: Sina Uhakika

Mallya: Kwamba Wakati Unapeleka Watuhumiwa Mbweni ulikuwa ujui Kuna Kituo cha Polisi Cha Wapi

Shahidi: Nilikuwa najua ni Kituo cha Polisi tuh

Mallya: Je Kuna Kesi yoyote Umeshawahi Kusikia kwamba Kuna Mtu alienda Kutoa Taarifa Kwamba watuhumiwa wamekamatwa Ututajie

Shahidi: Ni Mambo ya siri

Mallya: nimesikia una Mwambia Mtobesya Wakati Mnawakamata Kipaumbele Kilikuwa Matukio yasitokee

Shahidi: Ni sahihi

Mallya: Ni sahihi Kwamba Wakati Wote Polisi mnapaswa Kutenda kazi Kwa Mujibu wa Sheria

Shahidi: kimyaaa

Mallya: Kwamba Wakati Unapeleka Watuhumiwa Mbweni ulikuwa ujui Kuna Kituo cha Polisi Cha Wapi

Shahidi: Nilikuwa najua ni Kituo cha Polisi tuh

Mallya: Je, Kuna Kesi yoyote Umeshawahi Kusikia kwamba Kuna Mtu alienda Kutoa Taarifa Kwamba watuhumiwa wamekamatwa Ututajie

Mallya: Wakati mnapokea Simu ya Boaz Kwamba Mrudi Dar es Salaam ilikuwa Mkoa gani

Shahidi: Kilimanjaro Moshi

Mallya: kilichoWafanya Msiwaandike maelezo Muda huo ni nini baada ya Kuambiwa zoezi la Kuacha Kumtafuta Lijenje

Shahidi: Tulikuwa tunawahi Kuja Kuendelea Kuwatafuta Watuhumiwa Wengine Dar es Salaam na Kuendelea na Upelelezi

Mallya: Je Mohammed Ling'wenya alitishiwa au alitoa kwa hiari

Shahidi: Alitoa kwa Hiari

Mallya: Ulipata Kufahamu Kuwa Mohammed Ling'wenya alishawahi Kuwa Moshi

Shahidi: Nakumbuka alikwenda Mara Mbili

Mallya: alikaa kwa muda gani

Shahidi: alilala Siku Moja

Mallya: Wapi

Shahidi: Hotel ya Aishi

Mallya: Mlangoni au Bar?

Shahidi: alilala Ndani

Mallya: alikaa wapi

Shahidi: mara ya Pili alifika Aishi Hotel na Baadae katoka akawa anakaa Moshi Mpaka tunamkamata

Mallya: Usiku huo alikuwa ametokea Kulala wapi

Shahidi: Sikumbuki

Mallya: Kwa Kumbukumbu zako Mohammed Ling'wenya ni Mwenyeji wa wapi

Shahidi: Mtwara

Mallya: Wewe Umekaa Moshi kwa Muda gani

Shahidi: Nyakati mbalimbali na Mafunzo mbalimbali

Mallya: Ulielezea Mahakama Utafutaji wenu ulikuwa wa Namna gani

Shahidi: Tulikuwa tunafika Maeneo Mbalimbali

Mallya: Kwa Siku Ya Kwanza Pasua Mlienda Saa ngapi

Shahidi: Majira ya alasiri

Mallya: ambapo Exactly Mlipoanzia ni Wapi

Shahidi: Rau Madukani

Mallya: Kutoka Rau kwenda Moshi police Central ni Umbali wa Kilometers ngapi

Shahidi: Siwezi Kukadiria

Mallya: Mheshimiwa Jaji naomba Jibu lake Lirekodiwe

Mallya: Kutoka Rau Kwenda KCMC Mlitumia Muda gani

Shahidi: Dakika 15

Mallya: Baada ya KCMC Mlienda wapi..?

Shahidi: Tulirudi Mpaka Majengo

Mallya: Unaweza Kukadiria Kama Muda gani

Shahidi: Kwa sababu Hatukuwa na Mwendo Sana tuliitumia Walau Dakika 45

Mallya: Moja ya Tunachojivunia Wachaga Moshi haina Foleni, ila endelea tu kujibu , Baada ya Majengo Mlienda wapi

Shahidi: Tukaenda Pasua,

Mallya: Mie napajua Kote, Mlitumia Muda gani Kutoka Majengo kwenda Pasua

Shahidi: Sikumbuki Muda Exactly nilikuwa siangalii Muda

Mallya: Ulikuwa ni Muda gani

Shahidi: Ulikuwa Muda wa Jioni

Mallya: Baada ya Kutoka Pasua Mkaenda wapi

Shahidi: Machame, Aishi Hotel

Mallya: Aishi ni Kitu gani Kijiji, Kata au Wapi

Shahidi: ni Hotel

Mallya: Ulipofika Aishi Mkafika Maeneo gani

Shahidi: Kingai aliingia Ka anaingia Ndani,

Mallya: Kwa hiyo ni Ushahidi Wako Kingai aliingia Ndani

Shahidi: hakuingia Ndani alielekea Sehemu ya Majengo

Mallya: Unaweza Kutuchorea Picha ya eneo la Aishi Hotel

Shahidi: Siwezi kuchora sababu Sikushuka Kwenye gari

Mallya: Baada ya Aishi Hotel Mkaenda wapi

Shahidi: Maeneo ya Boma Ng'ombe

Mallya: Mlitumia Muda gani Kufika BomaNg'ombe

Shahidi: Siwezi Kujua Muda nilitumia, Kikubwa tulichokiwa tunakifanya ni Kufanikisha Kazi yetu

Shahidi: Palikuwa peshaanza Giza

Mallya: Kwa Makadirio yako a kutoka Boma Mpaka Moshi ni Kilometer ngapi hivi

Shahidi: Inaweza Ikawa Kilometer 50 au Zaidi

Mallya: Nilikusikia unasema mlifika Moshi Sa 5 za Usiku

Shahidi: Saa 4 kwenda Saa 5

Mallya: Ulipata Kueleza Kwamba Kilichokufanya Usiandike Maelezo Muda huo ni nini

Shahidi: Nilishaeleza Mallya: hivi Mbowe Ukifika Kumuhoji saa ngapi Za Usiku Vile..?

Jaji: Suala la Maelezo ya Mbowe havipo Katika Kesi Ndogo

Mallya: Baada Ya Boma Ng'ombe Mlienda wapi

Shahidi: Mbele ya Boma Ng'ombe Kama Unaenda Arusha, Tulifika Maeneo ambayo tulihisi kwamba tungeweza Kuwakuta

Mallya: Kwa hiyo Wewe Ulikuwa unajiongeza Kwenda Sehemu zingine ambazo watuhumiwa awajakutajia

Shahidi: Ni sahihi

Mallya: Kwa hiyo Siyo lazima uende na Watuhumiwa Kwa sababu Ulikuwa aukitajiwa Sehemu A Unaweza Kwemda sehemu B

Shahidi: Watuhumiwa walikuwa wanatusaidia na pia Tulikuwa hatumjui

Mallya: Baada ya Boma Mlienda wapi

Shahidi: Tulirudi Moshi

Mallya: Palikuwa na Mwanga au giza

Mallya: naomba Nimuachie Mwenzangu amallizie Kuuliza Machache

KAUNDA: ulisema Ulipomkamata Mshitakiwa Wa 3 Ulimpeleka Central Police

Shahidi: Nili fikisha Kituoni

KAUNDA: Wakati huo Mlishafungua Kesi ya Madawa ya Kulevya

Shahidi: Ndiyo Unga Unaozaniwa kuwa madawa ya kulevya

KAUNDA: Wakati huo uliwaacha kwenye gari Muda wao wote wakiwa na Pingu Mikononi

Shahidi: Ndiyo

KAUNDA: haukuiambia Mahakama Kwamba ulipowarudisha ukiwafungulia Pingu

Shahidi: Ndiyo Sikusema

PAUL KAUNDA: na Hukusema Mahakamani Kwamba Uliwakabidhi Askari gani wa Chumba Cha Mashitaka kwa Majina yao na Force Namba zao

Shahidi: Sikuongozwa Kusema hivyo

PAUL KAUNDA: na Wala hujui Kilichotokea Kuanzia Muda unawakabidhi Watuhumiwa Muda Ule Usiku Mpaka Asubuhi

Shahidi: Sahihi

FREDRICK KIHWELO: ni sahihi Sahihi kwamba wewe Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Arumeru

Shahidi: ni sahihi

FREDRICK KIHWELO: ni sahihi Kwamba wewe Kazi yako Kuwasimamia Kazi Askari wa Chini yako

Shahidi: sahihi

FREDRICK KIHWELO: ni sahihi Kwamba Jeshi la Polisi limewafukuza Askari Wanne na Wasaidizi wa Polisi wawili, Wamesimamishwa

Shahidi: sahihi

FREDRICK KIHWELO: ni sahihi Wewe ni Mmoja wa Polisi wasaidizi waliosimamishwa Kazi Arumeru

Shahidi: Ni Masuala ya kiutawala Siyo Kesi hii

KIHWELO: ni sahihi Mohammed Ling'wenya Mlimtafuta Kupitia Mitandao ya simu

Shahidi: Siyo Sahihi KIHWELO: akitokea Mtu akasema Boazi aliitoa Malekezo Ya Watuhumiwa Kuletwa Dar es Salaam Siku ileile, Je Kati yake na wewe Nani atakuwa Muongo

Shahidi: Siwezi Kumsemea Mtu Mwingine

FREDRICK KIHWELO: ni sahihi Kwamba Watuhumiwa hawaKupokelewa Kituoni Moshi

Shahidi: Hakuna Utaratibu wa Kupokelewa Bali Kuna Sehemu ya kuandika Kuwakabidhi Watuhumiwa

KIHWELO: ni sahihi hapa Mahakamani hapa Kuna Nyaraka ya Kukabidhi watuhumiwa

Shahidi: Siwezi kulisemea

FREDRICK KIHWELO: nitakuwa Sahihi Nikisema Watuhumiwa waliingizwa Kituo cha Polisi Moshi Kwa Dhumuni la Kuwatesa

Shahidi: Utakuwa Haupo Sahihi

FREDRICK KIHWELO: ni sahihi Hukusaini Detention Register Wakati Unawakabidhi Watuhumiwa Kituo cha Polisi Moshi

Shahidi: NI SAHIHI

FREDRICK KIHWELO: ni sahihi Kwamba Watuhumiwa mliowakamata hawakuwa Wenyeji wa Moshi

Shahidi: Hautokuwa Sahihi

FREDRICK KIHWELO: una nyaraka Yoyote inayoonyesha Kwamba Mlipata BREAK DOWN Njia Panda Himo

Shahidi: Sina Kwa sababu Magari ya Serikali yana Utaratibu wake

FREDRICK KIHWELO: Akitokea Mtu akasema kwamba Central Police Dar es Salaam Siyo sehemu ya Kuhifadhi Watuhumiwa WA Ugaidi atakuwa sahihi

Shahidi: Sijui hilo

KIHWELO: Akitokea Mtu akasema Walipotoka Moshi Walifikia Polisi Tazara ambapo watuhumiwa wa ugaidi uhifadhiwa

Shahidi: Mimi Ndiyo nilikuwa na Watuhumiwa, Sikwenda Huko

KIHWELO: ni hayo tu

JAJI: Ingekuwa inaruhusiwa Ningekupigia makofi ila Upo Mahakamani, Umetumia muda Vizuri Kibatala Muda Utakutosha

Kibatala: Nitajitahidi Kibatala: Shahidi Unafahamu Kwamba UGAIDI ni Kesi Kubwa Sana

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Je Ulichukua Maelezo Kwa kifungu cha 57(3)

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Je unafahamu Kwamba Kifungu Hicho Kinakuruhusu Kuchukua Record ya %Video au Sauti Wakati anakiri

Shahidi: Siyo lazima kutumia Hiyo

Kibatala: Sasa Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Palikuwa na fursa hiyo ya Kisheria lakini hukutumia kwa sababu fulani

Shahidi: Si kumwambia

Kibatala: Unafahamu Kwamba Mtu anapokiri Makosa yake Kuna hitaji la Kumpeleka Kwa Mlinzi wa Amani

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Unafahamu Kwa Mujibu wa Maelekezo ya Jaji Mkuu kwamba Mtu anapopelekwa kwa Mlinzi wa Amani kwanza anatakiwa Kumkagua Mtuhumiwa Kama ana majeraha

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Je Mohammed Ling'wenya alipelekwa Kwa Mlinzi wa Amani

Shahidi: Hapana

Kibatala: na Unafahamu Kwamba Kukiri Kwa Mohammed Ling'wenya Kulipaswa Kupelekwa Kwa Mlinzi Wa Amani

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Unafahamu na Hukumpeleka

Shahidi: Kimyaaaaa

Kibatala: Ulimpeleka Mohammed Ling'wenya Kwa Daktati Kuona Alikuwa na Majeraha

Shahidi: Hilo sina Jibu

Kibatala: Uliwaza Kumpeleka Mtuhumiwa Kwa Daktari Kuthibitisha Kwamba hana majeraha

Shahidi: Siyo Taratibu zangu za Kazi

Kibatala: Kuna sehemu kwenye CPA au PGO inakataza Wewe Kumpeleka Mtuhumiwa Kwa Daktari Kwa ajili ya kujiridhisha

Shahidi: Hapana

Kibatala: ili tuone kama Kweli Hamkuwa Mmetumia Muda huo Kuwatesa, je Dada wa Moses Lijenje Unamfahamu Jina lake

Shahidi: Simfahamu

Kibatala: Maelezo Yako ya Kuharibikiwa Gari Himo Kwenye Maelezo Yako Uliandika au Hukuandika

Shahidi: Sikuandika

Kibatala: Watuhumiwa Wanasema Mlipowatoa Moshi Mliwapeleka Tazara kisha Mbweni, Je Sababu za Kuwahamisha ni za Kiupelelezi au Kiusalama

Shahidi: Zote zote

Kibatala: Tuanze na suala la Upelelezi, Kama Mohammed Ling'wenya ameshakiri tayari uliogopa nini

Shahidi: Taarifa Kutoka Nje, Kuna wengine tulikuwa tunawatafuta

Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Walipokuwa Central walikuwa in ISOLATION na Watuhumiwa wengine?

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Ulimwambia Jaji Kwamba Ulipowapeleka Mbweni waliwekwa IN ISOLATION na Watuhumiwa Wengine

Shahidi: Hapana

Kibatala: Je Kupima Ukweli Wenu, Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Ulimwambia Mkuu wa Kituo au OCD kwamba Watuhumiwa Watengwe

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Nimesikia Umesema Kwamba Sababu ya Kuwahamisha Watuhumiwa Kutoka Central Dar es Salaam kwenda Mbweni ni kwamba Watuhumiwa Walipo Dar es Salaam wasijue Kinacho endelea, Je Mbweni ni Mkoa gani

Shahidi: Ni Dar es Salaam

Kibatala: Unamfahamu Afisa wa Jeshi anaitwa Chuma Chugulu

Shahidi: Simfahamu

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji kama Kule Arusha Kuna washitakiwa wa Ugaidi au hawapo

Shahidi: Wapo wapi K

Kibatala: Gereza la Kisongo, Masheikh,

Shahidi: Wapo

Kibatala: Maelezo yao yalichukuliwa Dar es Salaam

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Je Kuna Kifungu chochote Cha Sheria ya Mwenendo Wa Makosa ya Jinai na PGO inayolazimisha Mtuhumiwa achukuliwe Maelezo Sehemu tu ambapo faili lilifunguliwa

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Na ulijua Kwamba Shauri hili litafika Mahakamani

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: na wewe Kama Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Arumeru(OC-CID), Jukumu lako ni Kufunga Mianya yote ya kuharibu kesi

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji kama Kuna sehemu yoyote Ambayo Umeonyesha Kwamba kama angekuwa Tayari ningempa Simu yake au Simu yangu awasiliane na Ndugu, Jamaa na Marafiki zake...

Shahidi: Sikusema

Kibatala: Kule Moshi, Nakuuliza Kuhusu Ufahamu wa Kuingia Na Kutoka Polisi Central Police.

Shahidi: Nafahamu kwa sababu nilisaini

Kibatala: Wewe Ndiye Uliyemuingiza Mohammed Ling'wenya na Kumtoa Mahabusu Moshi

Shahidi: nilikuwa na Afande Mahita

Jaji: liweke Vizuri hilo swali

Kibatala: Unataarifa sahihi Kuhusu Detention Register, Je Ulisaini Out Saa Ngapi,

Shahidi: Tarehe 06 Aug 2010 Saa 11 alfajiri

Kibatala: Kati yako wewe na Mahita nani alikuwa Custodian Officer wa Mohammed Ling'wenya

Shahidi: Mimi Mwenyewe

Kibatala: Aliyekimkabidhi Mohammed Ling'wenya pale CRO central.?

Shahidi: Mimi

Kibatala: Kingai alikwepo wakati mnawakabidhi polisi Central Dar es Salaam?

Shahidi: Ndiyo alikuwepo.... Lakiniiiiiiiiiiii

Kibatala: Hakuna cha lakiniiiiiiiiiiii hapa...

Kibatala: Wakati Unahojiwa na Wenzangu Kwamba Ulisema DCI BOAZI aliwambia kwamba Watuhumiwa Tuwapeleke Moshi

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Una' personal Knowledge ya Malekezo Ya DCI au Kingai Ndiye anayejua

Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa

Kibatala: Naomba niishie hapo Mheshimiwa Jaji

Jaji: Serikali

Wakili wa Serikali: Shahidi Umeulizwa swali Kuhusiana na kutosema kwenye Ushahidi wako kama Hukusema kama ulimpa simu, kwa nini Hukusema

- Kibatala: OBJECTION kwanini.., Siyo swali nililouliza..

Jaji: Swali haliingi kwenye Record za Mahakama

Shahidi: Kama angeomba Mtu aje, Utaratibu Ungefanyika, Simu ingepatikana

Wakili wa Serikali: Uliulizwa kuhusu Watuhumiwa Kutenganishwa Central na Kule Mbweni, Ukasema Hukusema Kwenye Ushahidi Wako Shahidi Mahabusu Wanatenganishwa...

- MTOBESYA: OBJECTION Kwenye Ufafanuzi, It's not an Open Check

Wakili wa serikali: Elezea kwa nini Hukusema Kama Mliwatenga

Shahidi: Kwa sababu anaye weza Kujua Watuhumiwa wamekaa Je huko Lock up ni Mtu wa Chumba Cha Lock Up

Wakili wa Serikali: Ukaulizwa Swali Ulikiri kwamba Mtuhumiwa anayekiri anatakiwa Kupelekwa Kwa Mlinzi Wa Amani, Ukaulizwa Ulimpeleka kwa Mlinzi wa Amani Ukasema Hapana, Ni kwanini

Shahidi: Hatukumpeleka kwa Mlinzi wa Amani, kwa sababu Tulikuwa tunawahi Kuhakikisha Hivyo Vitendo Vya Kigaidi havifanyiki

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Swali na Mtobesya Kwamba Kama Ulikuwa na Taarifa za Awali Ukasema Hukuwa na Taarifa

Shahidi: Nilikuwa na Taarifa za Awali, Siyo Za kina wakati namkamata Mtuhumiwa,

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji tunaomba Tukomee hapa

Jaji: Shahidi tunakushukuru Kwa Ushahidi wako Kwenye Kesi Ndogo

Wakili wa Serikali: Robert Kidando Mheshimiwa Jaji tunaomba Hairisho Mpaka Kesho tarehe 12 Mwezi wa 11 2021, Ilituendelee na Shahidi Mwingine Na Ilituweze Kujiandaa Tunaomba Kesi ianze Saa 4 Asubuhi

Jaji: Utetezi

Kibatala: Mheshimiwa Jaji hatuna Pingamizi

Jaji: Shahidi tunakushukuru Kwa Ushahidi wako Kwenye Kesi Ndogo

- Mawakili wa pande zote mbili wanakubaliana na Jaji

Jaji: Maombi ya hairisho yamekubaliwa, nahairisha Mpaka Tarehe 12.11.2021. Washtakiwa wataendelea Kuwa Rumande chini ya Magereza Mpaka Kesho Asubuhi Saa 4 Asubuhi

- Jaji anatoka
 
Pingamizi halina mashiko, tupilia mbali huko. Mawakili wa Mbowe wanapoteza muda bure na usumbufu kibao usio wa maana.
Waache kesi ya msingi ingurumee, mbona wana sua sua sana! Kwani wanaogopa nini? Si walisema hakuna ushahidi? Mbona sasa wanapapatua sana?! Ina maana kuna ushahidi mzito.
 
Nimekuwa nafuatilia hii kesi ya Mbowe kwa ukaribu sana.

Na nimeshuhudia mapingamizi mengi yakikosa nguvu ya kisheria hivyo kutupiliwa mbali mahakama.

Hii ni ishara inayoonyesha timu ya Jamhuri inayongozwa na prominent lawyer Robert kidando ni moto wa kuotea mbali.

Ninachokiona ni kwamba haya mapingamizi mengi yanayokatwa na upande Kibatala ni kujaribu kutengezea picture ya kuwaminisha wananchi yakwamba uwanja wanaochezea haupo fair; jambo ambalo ni utoto kabisa.

Pia wameonyesha kupanic panic pasipo sababu mfano mzee wa “what is tourism ” anatumia maneno makali mahakamani. Acha panic kijana, jenga hoja za kisheria vizuri
Hoja ya kwamba jamhuri inabebwa, wapinzani wamefanya kichaka cha kujifichia
 
Nimekuwa nafuatilia hii kesi ya Mbowe kwa ukaribu sana.

Na nimeshuhudia mapingamizi mengi ya kikosa nguvu ya kisheria hivyo kutupiliwa mbali mahakama.

Hii ni ishara inayoonyesha timu ya Jamhuri inayongozwa na prominent lawyer Robert kidando ni moto wa kuotea mbali.

Ninachokiona ni kwamba haya mapingamizi mengi yanayokatwa na upande Kibatala ni kujaribu kutengezea picture ya kuwaminisha wananchi yakwamba uwanja wanaochezea haupo fair; jambo ambalo ni utoto kabisa.

Pia wameonyesha kupanic panic pasipo sababu mfano leo mzee wa “what is tourism ” anatumia maneno makali mahakamani. Acha panic kijana, jenga hoja za kisheria vizuri
Hoja ya kwamba jamhuri inabebwa, wapinzani wamefanya kichaka cha kujifichia
Mahakama ya Wananchi inasema MBOWE SIO GAIDI
 
pingamizi halina mashiko, tupilia mbali huko.
mawakili wa Mbowe wanapoteza muda bure na usumbufu kibao usio wa maana.
waache kesi ya msingi ingurumee, mbona wana sua sua sana! kwani wanaogopa nini? siwalisema hakuna ushahidi? mbona sasa wanapapatua sana?! inamaana kuna ushahidi mzito.
Ushahidi ni pamoja na vielelezo vya kufoji kama DR iliyotolewa mahakamani awali kurudi Polisi kinyemela? Kama hujui kitu kaa kimya na upopoma wenu wa kipolisi.
 
pingamizi halina mashiko, tupilia mbali huko.
mawakili wa Mbowe wanapoteza muda bure na usumbufu kibao usio wa maana.
waache kesi ya msingi ingurumee, mbona wana sua sua sana! kwani wanaogopa nini? siwalisema hakuna ushahidi? mbona sasa wanapapatua sana?! inamaana kuna ushahidi mzito.

Elewa tu kwamba hizi ni taratibu rasmi za kuhakikisha kila hatua inaenda kwa kufuata sheria na taratibu za kimahakama.

Kama isingekuwa ni haki yao na ni kinyume na taratibu, basi jaji angetupilia mbali tangu mwanzo. Tuheshimu taratibu za kimahakama katika kulinda haki ya kila mmoja wetu.
 
pingamizi halina mashiko, tupilia mbali huko.
mawakili wa Mbowe wanapoteza muda bure na usumbufu kibao usio wa maana.
waache kesi ya msingi ingurumee, mbona wana sua sua sana! kwani wanaogopa nini? siwalisema hakuna ushahidi? mbona sasa wanapapatua sana?! inamaana kuna ushahidi mzito.
Umeamka na bangi tena leo. Huelewi kwamba pingamizi zipo kisheria na kwenye kesi ya kipumbavu pumbavu kama hii lazima ziwe nyingi na ikizingatiwa kwamba that is a Kangaroo Court.
 
pingamizi halina mashiko, tupilia mbali huko.
mawakili wa Mbowe wanapoteza muda bure na usumbufu kibao usio wa maana.
waache kesi ya msingi ingurumee, mbona wana sua sua sana! kwani wanaogopa nini? siwalisema hakuna ushahidi? mbona sasa wanapapatua sana?! inamaana kuna ushahidi mzito.
Kuna muhuni mmoja aliiba document ya mahakama akaipenyeza akampa shahidi.. yaani mahakama kama mtihani wa la saba vile mwalimu mkuu anakula dili na msimamizi, denti anapewa desa.
 
Nimekuwa nafuatilia hii kesi ya Mbowe kwa ukaribu sana.

Na nimeshuhudia mapingamizi mengi ya kikosa nguvu ya kisheria hivyo kutupiliwa mbali mahakama.

Hii ni ishara inayoonyesha timu ya Jamhuri inayongozwa na prominent lawyer Robert kidando ni moto wa kuotea mbali.

Ninachokiona ni kwamba haya mapingamizi mengi yanayokatwa na upande Kibatala ni kujaribu kutengezea picture ya kuwaminisha wananchi yakwamba uwanja wanaochezea haupo fair; jambo ambalo ni utoto kabisa.

Pia wameonyesha kupanic panic pasipo sababu mfano mzee wa “what is tourism ” anatumia maneno makali mhahakamani. Acha panic kijana, jenga hoja za kisheria vizuri
Hoja ya kwamba jamhuri inabebwa, wapinzani wamefanya kichaka cha kujifichia
 
Nimekuwa nafuatilia hii kesi ya Mbowe kwa ukaribu sana.

Na nimeshuhudia mapingamizi mengi ya kikosa nguvu ya kisheria hivyo kutupiliwa mbali mahakama.

Hii ni ishara inayoonyesha timu ya Jamhuri inayongozwa na prominent lawyer Robert kidando ni moto wa kuotea mbali.

Ninachokiona ni kwamba haya mapingamizi mengi yanayokatwa na upande Kibatala ni kujaribu kutengezea picture ya kuwaminisha wananchi yakwamba uwanja wanaochezea haupo fair; jambo ambalo ni utoto kabisa.

Pia wameonyesha kupanic panic pasipo sababu mfano mzee wa “what is tourism ” anatumia maneno makali mahakamani. Acha panic kijana, jenga hoja za kisheria vizuri
Hoja ya kwamba jamhuri inabebwa, wapinzani wamefanya kichaka cha kujifichia
Umesema umekuwa unafatilia hii kesi kwa muda mrefu, embu tuambia ni viashiria gani mpaka sasa umeviona vinaashiria ugaidi wa mheshimiwa mbowe na wenzake?
 
Judge ame beti kwenye hii kesi, maamuzi yake hata kwenye rulling iliopita yana ukakasi sana. Kibatala & Co Ltd wanaivua nguo serikali na mahakama kwa pamoja.

Hata mwanafunzi wa 1st year anaesoma LLB, hawezi kutoa rulling isio na mashiko kisheria kama yeye mwenye experience ya zaidi ya miaka 15 katika tasnia ya sheria. Aibu hii.

Yeye mwenyewe Judge analijua hilo, na roho inamsuta anavojaribu kuliokoa jahazi la wakina Jamhuri.
 
Back
Top Bottom