Kukosa umeme kutwa nzima kwa siku kunaathiri vipi shughuli zako za kujipatia kipato?

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,626
Wakuu,

Tunajua "Upungufu wa Umeme" bado upo, na ratiba inafuatwa vilivyo!

Wengi wetu shughuli za kutupa michuzi ziko mchana na kwa kiasi kikubwa zinategemea umeme. Hii inafanya kukosekana kwa umeme kwa siku nzima kutupa hasara kubwa na kwa namna fulani kuturudisha nyuma kwenye harakati zetu.

Kwako vipi, kukosekana kwa umeme kutwa nzima kunaathiri vipi harakati zako za kusaka michuzi?
 
Eneo nililopo umeme haupo siku ya pili, kwa biashara nnayo fanya nmekosa siyo chini ya 50k.
NB. Kwa wafanyabiashara tunaoathiriwa na ukatikaji wa umeme tujitahidi kuwa na biashara zingine ambazo hazitumii umeme kama back-up.
TANESCO WALAANIWE
 
Mkazi wa Kahama - Kagongwa
Mimi nina biashara ya Stationery na ili nifanye kazi zangu za hapa ofisin ni lazima pawepo na umeme. Kiukwel kukatika kwa umeme kunaniathiri pakubwa sana kiasi kwamba baadhi ya siku sipati hata ile mia kisa umeme. Sijajua ni kwa nini serikali imeshindwa kabisa kulitatua hii tatizo la mgao wa umeme
😬😬😬😬😬😓😓😓😓
 
Umeme usio wa uhakika ni kikwazo kikubwa katika kutekeleza shughuli za kiuchumi na za kijamii kwa taasisi na hata watu binafsi.

kwa mfaano. Mfanyabiashara mwenye salon hawezi kufanya kazi bila umeme, majumbani vyakula vinaharibika hovyo hovyo, mfugaji wa kuku kama hana mbadala vifaranga wanakufa kwa kukosa joto.

Kwa ujumla tunahitaji suluhisho la kudumu. Inashqngaza sana kwamba hapo nyuma tuliaminishwa umeme unakatwa kwa sababu ya kupungua kina cha maji kutokana na ukame. Wakati huu wa Mvua sijui Kuna maelezo yapi.
 
Wakuu,

Tunajua "Upungufu wa Umeme" bado upo, na ratiba inafuatwa vilivyo!

Wengi wetu shughuli za kutupa michuzi ziko mchana na kwa kiasi kikubwa zinategemea umeme. Hii inafanya kukosekana kwa umeme kwa siku nzima kutupa hasara kubwa na kwa namna fulani kuturudisha nyuma kwenye harakati zetu.

Kwako vipi, kukosekana kwa umeme kutwa nzima kunaathiri vipi harakati zako za kusaka michuzi?
Kiukweli kunatuadhiri kwakiasi kikubwa kwani kunafanya huingizi chochote katika maisha
 
Kwa siku tunatumia umeme UNIT 100-130
Kukosekana kwa umeme kwanza Tanesco wanakosa mapato
Pili vibarua wanakosa pesa

Tatu sisi twakosa pesa
 
Kam hujui mwingine akishindwa kufanya kazi sababu ya kukosa umeme na wew kazi zako zitakwama bhasi una matatizo ya akilii.. wewe mama ntilie huitaji umeme ila unategemea kinyozi afanye biashara aje kununua chakula kwako sasa hapo huoni ni tatizo biashara kutegemeana.
 
Umeme usio wa uhakika ni kikwazo kikubwa katika kutekeleza shughuli za kiuchumi na za kijamii kwa taasisi na hata watu binafsi.

kwa mfaano. Mfanyabiashara mwenye salon hawezi kufanya kazi bila umeme, majumbani vyakula vinaharibika hovyo hovyo, mfugaji wa kuku kama hana mbadala vifaranga wanakufa kwa kukosa joto.

Kwa ujumla tunahitaji suluhisho la kudumu. Inashqngaza sana kwamba hapo nyuma tuliaminishwa umeme unakatwa kwa sababu ya kupungua kina cha maji kutokana na ukame. Wakati huu wa Mvua sijui Kuna maelezo yapi.
Maelezoo yaliyopo mkuu n kwambaa ,kukatika Kwa umeme haikuwa sababu ya ukosefu wa mvua alisikikaa nazan kiongozi mmoja akituambia wa Tz kupitiaa vyombo vya habari.

Habar hyo ipo uku km sikosei.
 
Kila mtu na madhila yake, na hapo ni umeme tu, hujaongelea madhila kwenye sekta nyingine, Afya, maji, miundombinu, Kodi, halmashauri na majiji n.k.
Maisha ya Mtz ni madhila masaa 24. Na bado ccm iko madarakani. WaTz tuamke!

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Hao jamaa mwaka jana walinipa stress sana, ikabidi nitumie karibia m kufunga backup. Mwaka huu sina habari nao, wakate sawa wasikate sawa!
 
Mkazi wa Kahama - Kagongwa
Mimi nina biashara ya Stationery na ili nifanye kazi zangu za hapa ofisin ni lazima pawepo na umeme. Kiukwel kukatika kwa umeme kunaniathiri pakubwa sana kiasi kwamba baadhi ya siku sipati hata ile mia kisa umeme. Sijajua ni kwa nini serikali imeshindwa kabisa kulitatua hii tatizo la mgao wa umeme
😬😬😬😬😬😓😓😓😓
Sisi wenye gesti zetu tunakosa sana wateja lakini ndoa za watu hazipati kashikashi umeme ukikatika...

Nimeamini kwenye ubaya pia kuna wema...

Mungu ibariki TANESCO iendelee kutuangazia masha.

Mungu ibariki CCM iendelee kutupiga mbele kwa mbele..

Mungu mbariki mama, aendeee kuupiga Mwingi....

Mungu mbariki Bashite... aendelee kunawiri....
 
Maelezoo yaliyopo mkuu n kwambaa ,kukatika Kwa umeme haikuwa sababu ya ukosefu wa mvua alisikikaa nazan kiongozi mmoja akituambia wa Tz kupitiaa vyombo vya habari.

Habar hyo ipo uku km sikosei.
Ukweli Tatizo ilikuwa mvua. Sasa mvua imenyesha, ukweli ni kwamba mabwawa yamejaa matope...

Tunawaombeni watanzania muendeee kuwa na subira na msiache kutuamini...

Tanesco inawaangazia maisha

KIGUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

CCM HOYEEEEE
 
kidumu ya nyokoo ...
 
Hao jamaa mwaka jana walinipa stress sana, ikabidi nitumie karibia m kufunga backup. Mwaka huu sina habari nao, wakate sawa wasikate sawa!
Me mwenyewe January nataka nifunge back up maana hii kitu ni kero kubwa....
Shuka mchanganuo tafadhali na brand za vifaa ulivyonunua
 
Back
Top Bottom