Kukaa na line ya simu nje ya nchi kwa zaidi ya mwaka bila kufungiwa

Mkuu wapigie hiyo Kampuni. Waaambie nchi unayokwenda kama wanafanya roaming. Kama wanafanya roaming basi ni rahisi kwako. Line yako itakuwa hewani.

Ingawa ni gharama sana kufanya roaming. Yaani mtu akikupigia simu na wewe unakatwa pesa

Lkn huduma za Mobile money .. USSD(kuangalia salio etc) ni Bure

Miamala utakuwa unafanya kama kawaida
 
Vika kwa mtoa huduma husika, watakupa huduma ya roaming, ila ni ghali

Kiwango cha chini ni TZS100,ooo - TZS1,000,ooo

maisha bora kwa kila mtumiaji wa huduma ya simu
 
Ni kutumia Mpesa au kununulia umeme ukiwa huko unaongea na mtu Tz anaweka hela kidogo unafanya miamala sio mwaka mmoja hata zaidi ya mwaka wakiona Mpesa ipo vizuri hufungiwi hii ni kwa Voda naona Nchi nyingi Mpesa ipo ok sijajua Tigo na wengine.
 
Vika kwa mtoa huduma husika, watakupa huduma ya roaming, ila ni ghali

Kiwango cha chini ni TZS100,ooo - TZS1,000,ooo

maisha bora kwa kila mtumiaji wa huduma ya simu
Siku hizi kuna pre paid roaming. Sio kama zamani . Mimi mfano naweka buku kwenye line. Natuma sms..chache.. na bado huwa natumia mobile money. Napata msg za internet banking etc
 
Wadau ,

Kwa wenye ufahamu naomba kujua ikiwa nataka kusafiri na line ya simu (sim card) , nifanyeje ili niweze kukaa nayo nje ya nchi kwa muda mrefu bila kufungiwa.

Natanguliza shukrani
Unaenda kwenye ofisi ya mtando husika au piga customer care waambie unatoa taarifa basi wanaihold, na kama ukirudi pia unawapa taarifa
 
Kwani wanafunga usipo tumia kwa mwaka mmoja?

Mimi nilipaki laini zaidi ya mwaka ila ilikuja kupiga kazi kama kawaida.
 
Easy, mimi natumia Tigo, wao wanafunga line usipoitumia kwa 3months, kwa hiyo kila baada ya mwezi na nusu namuomba mtu Tz aniunge na kifurushi cha 500Tsh, muhimu ni usisahau ni kila baada ya 2.5months, usivuke 3months.
 
Wadau,

Kwa wenye ufahamu naomba kujua ikiwa nataka kusafiri na line ya simu (sim card), nifanyeje ili niweze kukaa nayo nje ya nchi kwa muda mrefu bila kufungiwa.

Natanguliza shukrani
Mimi ninavyoelewa baada ya usajili kwa alama za vidole na namba za Nida, line hazifungwi, isipokuwa usipotumia kwa muda mrefu wanazi 'cease' na ukiitaka muda wowote wanai 'update' na unaendelea nayo.
 
Easy, mimi natumia Tigo, wao wanafunga line usipoitumia kwa 3months, kwa hiyo kila baada ya mwezi na nusu namuomba mtu Tz aniunge na kifurushi cha 500Tsh, muhimu ni usisahau ni kila baada ya 2.5months, usivuke 3months.

Ukiwacha hela kwenye tigo pesa sio sana kuifunga mimi bro wangu aliondoka miaka 2 kurudi kaweka vocha imekubali.

Lunatic
 
Siku hizi kuna pre paid roaming. Sio kama zamani . Mimi mfano naweka buku kwenye line. Natuma sms..chache.. na bado huwa natumia mobile money. Napata msg za internet banking etc
Ivi ukifanya roaming mtu akikupigia si mpaka aanze na code number ya hiyo nchi?
 
Ivi ukifanya roaming mtu akikupigia si mpaka aanze na code number ya hiyo nchi?
Hapana, anakupigia kawaida tuu. sema lazima uwe na pesa kwenye salio. Sababu ukipokea unakatwa pesa pia, Tena wewe unaepokea unakatwa pesa nyingi (according to roaming agreements)
Ila yeye anaekupigia anakatwa tuu kawaida, kama anavyompigia mtu wa local hapa
 
Back
Top Bottom