Alfu Lela Ulela
JF-Expert Member
- Oct 29, 2010
- 1,255
- 77
Brigedia Jenerali mstaafu, Suleman Mohamed Yahya Al Adawi wa Saud Arabia amejitokeza hadharani na kudai kuwa mmiliki wa kampuni ya DOWANS (T) LTD.
Al Adawi ambaye alifanya mkutano na waandishi wa habari jumapili ya tar.19/02/2011 ktk ukumbi wa Hotel ya Kilimanjaro Kempisk, pamoja na kuwa alitoa maelezo yaliyoacha maswali mengi kwa Watanzania lakini pia maelezo yake hayamuachi salama mwandishi mkongwe na ambaye tumekuwa tukimhesabu kama shujaa ktk jamvi hili MM.MWANAKIJIJI.
Katika taarifa kupitia vyombo mbalimbali vya habari kwa nyakati tofauti, (hususan gazeti makini la MwanaHALISI) imekuwa ikidaiwa AL ADAWI amewahi kukanusha kuimiliki kampuni ya Dowans (T) Ltd.
Taarifa za kukanusha umiliki wa kampuni hiyo inadaiwa zinatokana na mahojiano yaliyofanywa kati ya mwandishi huyo aishie Marekani na AL Adawi mwenyewe.
Lakini AL Adawi amekuja nchini na kudai kuimiliki kampuni hiyo, tofauti na alipohojiwa na Mwanakijiji ambapo alikana.
Hii ina maana kuwa maelezo ambayo AL Adawi aliyatoa kwa mwandishi huyo wa Marekani, ni tofauti na aliyoyatoa kwa waandishi wa Tanzania.
Je ukweli ni upi? Je, Mwanakijiji haoni kuwa maelezo ya AL Adawi yanamuweka hatarini kwa kuonekana alitunga story??
Najua Mwanakijiji atakuwa amesikia taarifa ya Al Adawi kukiri kuimiliki Dowans. Je,amechukua hatua gani kuudhibitishia umma wa watanzania na dunia kwa ujumla kuwa hakutunga story?
Na je, Mwanakijiji haoni kuwa taarifa ya AL Adawi inamuumbua, na asipochukua juhudi za haraka, imani aliyojijengea miongoni mwa Watanzania wengi itapotea? TAFAKARI!!