Kujenga nyumba - Gharama za engineer na mafundi wake

Aika Mndumii

Senior Member
Jan 19, 2013
164
46
Wakubwa zangu:

Kuna rafiki yangu anataka kujenga nyumba ya ghorofa moja. Ukubwa wa nyumba ni wastani wa mita za mraba 350 (chini chumba kimoja, jiko, sebule, store, public toilet, study room na dinnig. Juu (Vyumba vitatu) na kila chumba ni self contained.

Materials mwenye nyumba atanunua mwenyewe kulingana na alivyopewa na engineer wake. Gharama za material mpaka kupaua inakadiriwa kuwa 80m

Swali: Engineer na mafundi wake walipwe kiasi gani kwa kuanzia setting ya nyumba, kujenga mpaka kupaua (kuweka vigae) basi. Kiwanja kiko maeneo ya mbweni ni eneo tambarare sana. Kwa mwenye uzoefu naomba asaidie makadirio inaweza kuwa kiasi gani (kwa gharama za mafundi fundi peke yake).

Shukrani sana
 
Mkuu,
Kwa jinsi mafundi wetu walivyo hapo utajidanganya iwapo mtakubaliana bei ya kazi nzima. You need to phase your project.

Kubaliana naye msingi mpaka kunyanyua level 1. Halafu kumwaga slab na kunyanyua level 2. Halafu kuezeka.

Bei kamili inategemea na mahali kiwanja kilipo, jinsi level ilivyo, tabia ya udongo. Lakini kwa makadirio ya harakaharaka kujenga msingi mpaka level 1 including ngazi ni sh. mil 2.5.
Level two ni the same price.
Kuezeka, inategemea na manjonjo ya paa lako na aina ya materials utakayotumia lakini in general ni kama sh. 1.2 milion.
Kwahiyo ukiwa na mil 6.2 unaweza kuwa na uhakika kuwa hela ya ufundi tayari unayo.

Kama utataka engineer unaweza kuwa unamlipa per visit kama elfu 50 iwapo unampa usafiri to site. Engineer ukitaka kumlipa jumla atataka milioni na nusu hivi kwa kazi nzima, lakini atakuwa anaenda site once in a while sio kukaa pale full time.
 
Alilosema mchangiaji hapo juu ni sahihi kabisa....unatakiwa kugawa project yako kwa phase.ndo ivo nimefanya na nimeona inasaidia sana..hizo gharama zake sina uhakika nazo..maana mi fundi nimempa mil 1.5 for level 1 ambayo ni kuse nguzo na foundation in general excluding kumwaga jamvi..na ni eneo mbele ya lako.
 
jamani naweza jenga ghorofa 1 nyumba ya kuishi kwa kuingia dau na fundi bila engineer? au lazima engineer awepo mwanzo hadi mwisho wa kazi?
 
Engineer sio lazima. Ila hakikisha fundi ni mzoefu.

Hata hivyo sheria zinataka engineer. Akili kichwani...
 
Mkuu,
Kwa jinsi mafundi wetu walivyo hapo utajidanganya iwapo mtakubaliana bei ya kazi nzima. You need to phase your project.

Kubaliana naye msingi mpaka kunyanyua level 1. Halafu kumwaga slab na kunyanyua level 2. Halafu kuezeka.

Bei kamili inategemea na mahali kiwanja kilipo, jinsi level ilivyo, tabia ya udongo. Lakini kwa makadirio ya harakaharaka kujenga msingi mpaka level 1 including ngazi ni sh. mil 2.5.
Level two ni the same price.
Kuezeka, inategemea na manjonjo ya paa lako na aina ya materials utakayotumia lakini in general ni kama sh. 1.2 milion.
Kwahiyo ukiwa na mil 6.2 unaweza kuwa na uhakika kuwa hela ya ufundi tayari unayo.

Kama utataka engineer unaweza kuwa unamlipa per visit kama elfu 50 iwapo unampa usafiri to site. Engineer ukitaka kumlipa jumla atataka milioni na nusu hivi kwa kazi nzima, lakini atakuwa anaenda site once in a while sio kukaa pale full time.
ZeMarcopolo umenena sawa kabisa. Hapana shaka una uzoefu mzuri wa haya masuala.
Natumai muulizaji atafatilia hili kwa ukaribu
 
Last edited by a moderator:
wangwana naomba na mimi mnisaidie maake najikongoja nijenge ka ghorofa kwa wenye uzoefu hatua za kwanza za msingi wa level ya kwanza na level ya pili millioni 50 inaweza kutosha kwa kuanzia au hapo bado kabisa nahitaji cost za kuweka boma tu kwanza
 
Haya jaman asanten washauri mnaojenga dar especially kigambon,kongoe,mbagala,mikwambe etc karibu na ujenz wa magorofa ya nssf wakati wenu huu kuna magorofa kama 700 yanajengwa.kwa wazoefu wanaelewa kuna zaga kwa bei nafuu sana mi nimejenga nyumba yangu ya kawaida nzuri nkikuambia kiasi cha vifaa hutaamin na ndo mana nataka kuandaa ghorofa.ukiingia dukan utakimbia jaman rangi,marumaru,bati,milango,marine plywood,mbao,cement,nondo mm16,mm12 n.k kila kitu kwa bei chee unamaliza nyumba hadi unashangaa waliojenga jiran na eneo wanajua nn naongea.wapendwa tunaopenda kujenga ila mifuko imetoboka kazi kwenu.mbinde linaanza mwezi ujao.ni taarifa tu.
 
Majo, hii taarifa muhimu sana lakini umeitoa "kichoyo mno" ; imekuwa kama unawaringishia tu wadau- joke. Nyumbulisha taarifa ili wadau waweze kuitumia vizuri.

Toa namba za simu za mtu/watu wanaoweza kuwapa watumichongo ya kupata vifaa.

By, the way, hizi ghorofa za nani? NHC au NSSR maana pale kuna miradi miwili imepakana mmoja wa NSSR mwingine NHC.
 
Haya jaman asanten washauri mnaojenga dar especially kigambon,kongoe,mbagala,mikwambe etc karibu na ujenz wa magorofa ya nssf wakati wenu huu kuna magorofa kama 700 yanajengwa.kwa wazoefu wanaelewa kuna zaga kwa bei nafuu sana mi nimejenga nyumba yangu ya kawaida nzuri nkikuambia kiasi cha vifaa hutaamin na ndo mana nataka kuandaa ghorofa.ukiingia dukan utakimbia jaman rangi,marumaru,bati,milango,marine plywood,mbao,cement,nondo mm16,mm12 n.k kila kitu kwa bei chee unamaliza nyumba hadi unashangaa waliojenga jiran na eneo wanajua nn naongea.wapendwa tunaopenda kujenga ila mifuko imetoboka kazi kwenu.mbinde linaanza mwezi ujao.ni taarifa tu.

Mkuu tusaidie na sisi tunufaike basi, si unaona swali lako ulivyopata jibu straight toka kwa ZeMarcopolo, ndo faida ya JF
 
Last edited by a moderator:
pale kutakuwa na makampun 17 yatayofanya kazi ni mradi wa nssf phase 3,mkabala na nyumba za NHC.kuna ujenzi wa magorofa means ghorofa 2na kuendelea. mi npo kwenye moja ya kampun zitazojenga na kipindi kilichopita tulijenga kwa hiyo ni mzoefu wa zaga.mfano wa bei za vitu
cement mfuko 10,000 zaga zikiwa nyingi hadi 5000 kwa mfuko.
-nondo tunanunua
mm :12 sh.10,000 kwa
mm: 16 sh. 15,000-20,000
mm: 10 had 8 sh.8000
ndoo za rangi weather guard ya 150,000 dukani tunanunua 50,000 zikizidi hadi 30,000
ndoo za rangi nyeupe au za kawaida 15,000 hadi 20,000.
bati za kisasa maelewano hata 3000 kwa moja unachukua kutegemea mafundi wamefulia vp.
marine plywood hata mi nimeuza sana sh.15,000 moja
mbao 4by 2 sh.3000,
mbao 3 by 2 sh.2500
mbao 2by 2 sh.1500
milunda sh 500
malumalu,grill jamani.nani na nani wa kuwapata ntawajulisha naogopa kurusha no. za watu humu usije ukawa unaeuliza ni bosi wangu kibarua kitaota nyasi ila kwa atayetaka sisemi uongo cku mtu tembelea ufanye utafiti kuna muda zaga zinakosa watu mafundi wanatafuta pesa za misokoto tuu.kaka zangu dada zangu kwa mshahara wangu ningestaafu cna nyumba ila nimejenga watu wakiiona nyumba yangu hawanisomi.ila siri ni zaga na bonge la project linakuja kwa maskin ni furaha kwetu.ntajua watu gani wa zaga watakuwepo safari hii ntarusha no. zao shughuli itapoanza kwan tunasubir muda wowote kazi zianze.kwa wenye muda unaweza fanya upelelez mwenyewe utapata wauza saga wataokuletea hadi ulipo ila cjui wao huko mtaan wanafanya bei gani kama una muda unatafuta vijana wananunua na kukuletea kwa bei nlizoandika au chini ya hizo.nadhan nimeeleweka ndugu zangu.
 
Angalizo. Hakikisha unapata building permit maana siku hizi wanasumbua wakikuta huna kibali hasa kwa ujenzi wa viwanja vilivyopimwa na tena bweni na bunju b.
 
Kujenga kama unatumia fundi mchundo/engineer wa mtaani. Lazima ugawe kwa phase lakini kaka umegawa kwa bei rahisi sana. Msingi umegawanyika, kwanza kuna kuchimba msingi hapa sio chini ya 800,000 kisha baada ya hapo kuna kumwaga zege la blinding hapa napo weka kama 500,000 kisha kuna kusuka nondo za beam za chini na base vitako hapa weka kama 300,000. Kisha kuna kupandisha kuta za msingi weka kama 800,000. Kisha kuna kutoa udongo ulioza, kujaza mchanga na kupanga mawe weka 1,000,000. Baada ya hapo kuna kusuka nondo za beam kabla ya slab hapo weka 500,000. Kisha unamwaga jamvi weka 1,250,000.

Sijakuchanganulia slab ya juu ambayo imegawanyika sehemu kuu tatu. kwanza kuna foarmwork ambayo sio chini ya 1.25 million, kuna kusuka chuma ambapo ni kama 1.25 million, kuna fundi umeme weka 700,000 kumwaga slab weka 1.5 million.
 
wangwana naomba na mimi mnisaidie maake najikongoja nijenge ka ghorofa kwa wenye uzoefu hatua za kwanza za msingi wa level ya kwanza na level ya pili millioni 50 inaweza kutosha kwa kuanzia au hapo bado kabisa nahitaji cost za kuweka boma tu kwanza

Kaka nyumba inakubwa gani? Mimi nimejanga 12 kwa 12 msingi ulikula kama 21 million, kati hapo kama 9Million na zege la kati kama 30 million. Hapo gofu limesimama na hata juuu hujaanza 60 million kwao.

Lakini kama una 50 nakushuri uanze, inakufikisha kwenye slab.
 
pale kutakuwa na makampun 17 yatayofanya kazi ni mradi wa nssf phase 3,mkabala na nyumba za NHC.kuna ujenzi wa magorofa means ghorofa 2na kuendelea. mi npo kwenye moja ya kampun zitazojenga na kipindi kilichopita tulijenga kwa hiyo ni mzoefu wa zaga.mfano wa bei za vitu
cement mfuko 10,000 zaga zikiwa nyingi hadi 5000 kwa mfuko.
-nondo tunanunua
mm :12 sh.10,000 kwa
mm: 16 sh. 15,000-20,000
mm: 10 had 8 sh.8000
ndoo za rangi weather guard ya 150,000 dukani tunanunua 50,000 zikizidi hadi 30,000
ndoo za rangi nyeupe au za kawaida 15,000 hadi 20,000.
bati za kisasa maelewano hata 3000 kwa moja unachukua kutegemea mafundi wamefulia vp.
marine plywood hata mi nimeuza sana sh.15,000 moja
mbao 4by 2 sh.3000,
mbao 3 by 2 sh.2500
mbao 2by 2 sh.1500
milunda sh 500
malumalu,grill jamani.nani na nani wa kuwapata ntawajulisha naogopa kurusha no. za watu humu usije ukawa unaeuliza ni bosi wangu kibarua kitaota nyasi ila kwa atayetaka sisemi uongo cku mtu tembelea ufanye utafiti kuna muda zaga zinakosa watu mafundi wanatafuta pesa za misokoto tuu.kaka zangu dada zangu kwa mshahara wangu ningestaafu cna nyumba ila nimejenga watu wakiiona nyumba yangu hawanisomi.ila siri ni zaga na bonge la project linakuja kwa maskin ni furaha kwetu.ntajua watu gani wa zaga watakuwepo safari hii ntarusha no. zao shughuli itapoanza kwan tunasubir muda wowote kazi zianze.kwa wenye muda unaweza fanya upelelez mwenyewe utapata wauza saga wataokuletea hadi ulipo ila cjui wao huko mtaan wanafanya bei gani kama una muda unatafuta vijana wananunua na kukuletea kwa bei nlizoandika au chini ya hizo.nadhan nimeeleweka ndugu zangu.

Ushauri tuu kumbuka muoshwa huoshwa. Usijenge gorofa kama huna pesa ambayo ni determine utaacha gofu mjini hapo
 
mi npo moja ya makampuni yaliyopata kazi pale na kipind kilichopita tulijenga pia.hivyo ntakapojua nani na nani watakuwa wananunua au kuuza zaga ntawajulisha.wapendwa ni chance nzuri sana jamani tuliozoea tunawaza mafundi tutawalipa nn ila sio gharama za vifaa jaman mafund kuna muda wanatoa zaga ili mradi wapate pesa ya misokoto basi .muda ukifika ntatoa no. ya kuwasiliana nao.hayo cjui 30milion cjui ngapi ukidhamilia utasikilizia kwenye bomba niamini wapendwa naogopa kutoa no yangu isije ikawa bosi anapitia humu c mnajua tena?ila kwa kuwa napenda ndugu zangu mnufaike ntajitahid kuwapa no. kwa msaada zaidi.
 
Kuulizia profession kwenye social networks ni kuwanyima wenye fani zao riziki...what if na mimi kesho nakuja na post ya "Nimeua,gharama ya kesi bei gani?"...Tueshimu taaluma za watu...
 
Back
Top Bottom