Tatizo la kujawa na mate mdomoni usiku ninapokuwa usingizini

zayat

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
337
42
Mimi tatizo langu najaa mate mdomoni nikiwa usingizini.Nikishtuka nameza lakini huwa yanatoka mpaka mto wangu unaroa na mto una nuka sana.
PLEASE HELP KUNA DAWA?
 
Sababu yawezekana una ugonjwa unaitwa duodenal ulcer, kwani na zenyewe husababisha mate kujaa ukiwa usingizini
But waweza kwenda kwa Doc atakupa jibu zuri zaidi.
 
Habari yenu wanajamvi? Naomba niweke wazi tatizo linalonisumbua kwa muda sasa... Nina shida ya kujawa na mate mdomoni usiku, mate hayo huwa yanatema harufu ile mbaya endapo yatapata upenyo kutoka. Hii imekuwa kero kubwa kwangu.

Nimejaribu kuzingatia kupiga mswaki kila niamkapo na kabla ya kulala lakini tatizo bado lipo.


Naombeni ushauri madaktari wa vinywa na ninyi wenye uzoefu ambao mliwahi kukumbwa na tatizo kama langu.
 
Tatizo halijaanza muda mrefu? Inawezekana una maradhi ya koo kama chronic tonsilitis? Nakushauri ukamuone ent haraka. Huenda ukahitaji matibabu. Pole sana
 
Asante !!! Tatizo limeanza muda kidogo miezi kama 6 hivi... Nashukuru kwa msaada wa mawazo nitakimbia kwa tabibu haraka maana hii sio kawaida kwa kweli.
 
Pia inaweza kuwa ni dalili ya kupungukiwa chumvi mwilini. Jaribu kutafuna punje 1 au 2 za chumvi ya mawe ya baharini kila unapoenda kulala kwa muda wa wiki 2.
 
Na kama unapenda vitu vya sukari punguza nayo pia inachangia.
Ila kwenda hospital nako pia inahusu
 
Asanteni kwa ushauri wanajamvi.. nayafanyia kazi yote mliyoshauri. Inaudhi na kukera sana kwakweli...
 
Usiogope sana, kila unapoenda kulala hakikisha unapiga mswaki na usile kitu chochote baada ya hapo, jaribu leo then utaona matokeo, na hiyo ndo iwe tabia yako, then uje unipe majibu, trust me

Asante kwa ushauri nimeanza upya zoezi hili naamini nitarudi na majibu mazuri kwako.
 
Back
Top Bottom