Kuishi na Mashabiki wa Simba inaitaji moyo sana

babu onyango

JF-Expert Member
Jan 12, 2023
329
814
Wakuu kwema.. Hivi hawa watu nyie mnawezaje kuishi nao? Mbona ni watu wenye uelewa mdogo sana na huu mchezo wa soka?
Kuna jamaa zangu ni mashabiki wa Simba hapo juzi kabla ya mchezo wa Simba na Prisons walikuwa wakisema Simba ni timu tishio Africa, Aly Ahly, Mamelodi, Tp Mazembe wote kwa sasa wanaiogopa Simba, timu yeyote itayokuja mbele yao itapigwa goli kuanzia 6 na kuendelea..

Sasa mara baada ya mechi kuisha na Simba kupigwa goli 2-1 Maneno yao yamegeuka, utawasikia ooh Simba ni hovyo sana, pale hakuna timu, Uongozi haufai, tumesajili magarasa. Wengine wakaenda mbali zaidi na kusema timu nzima imejaza wazee, mara yule benchikha hamna kocha pale anabebwa na uwezo wa Chama tu....

Hivi nyie huko mtaani kwenu mnawezaje kuishi na viumbe vigeugeu wa namna hii??
 
Yanga yenyewe mbovu sana ukilinganisha na timu zote zilizotinga robo final..ndio timu iliyoingia robo kwa kufungwa sana,pia ndio timu iliyoingia robo kwa point za chini
 
Back
Top Bottom