Kuhusu Wamasai

Kwani wanaovaa hivyo wamelazimishwa?.


Hawajalazimishwa bali wanadanganywa na kutumiwa, utasikia jamani wamasai wanapendeza yaani wanadumisha mila lkn wewe unayesema hivyo ukiambiwa uvae kama Mmasai hautaki na siku ukimuona mtoto wako kavaa hivyo huwezi hata kukubali atoke nyuimbani!
 
Unamaanisha nini mtoa mada kwamba Lowasa na familia yake hawavai mavazi ya kimaasai

images
 
Unamaanisha nini mtoa mada kwamba Lowasa na familia yake hawavai mavazi ya kimaasai

images


Na hicho ndicho ninachomaanisha kwamba wanavaa lkn kwa ajili ya show tu na siyo maisha yao ya kila siku na familia zao lkn wanawaambia Wamasai wengine masikini wavae kila siku kila mahali ili wadumishe utamaduni mbona wao hawavai hayo mashuka kila siku kama hiyo mila ni nzuri hivyo???!
 
Huu ni uchokozi na dharau kwa ndugu zetu wa kimasai .... Endelea tu maaana utapata unachokitafuta.
 
Mtoa mada inaonekana hujatembea kwenye vijiji vya nchi yako sio wamasai tuu wanaovyaa kimila bado kuna makabila mengi yanayofuata tamaduni zao.
 
utalii utafariki, acha wavae, wasiende SHULE wawe wanatembeza mikanda, viatu, urembo kitaa.
 
utalii utafariki, acha wavae, wasiende SHULE wawe wanatembeza mikanda, viatu, urembo kitaa.


Hilo sawa lkn swali ni kwamba ni kwa nini Wamasai masikini tu ndiyo wadumishe Mila na Tamaduni?? Kwa nini wale Matajiri na wanasiasa wao pmj na watoto wao hawadumishi hizo Mila kama ni muhimu hivyo??
 
Hivi unawazaga nini ?? Sio wewe juzi hapa unasema sijui Obama nini hana maadili kisa sio mzungu au mwafirka sijui point 5 ,

Mimi masai aisee na sio Magufuli wala yeyote yule atakaye badilisha utamaduni wangu ,shuka navaa ,sime pembeni ,naenda olpul ,naua simba nipewe mke ,nafuga rasta ,napaka lokariya ,nafuga ,mtoto hatairiwi hospital naoa mke zaidi ya moja nk ....
Na lugha nadumisha ,
Utake usitake masai ndio moja ya watu wenye utamaduni wenye nguvu iliyobaki Africa ikiwa ni pamoja na Wazulu na Xhosa

Tabaraki taa ena tasat
 
Wamasai, watu wanaovutia na wanaofuga wanyama, wanaishi katika pori la Bonde Kuu la Ufa nchini Kenya na Tanzania huku Afrika Mashariki. Wao bado huishi kama vile mababu wao wa kale walivyoishi zamani. Watu hao hawajali saa, bali hufanya kazi zao kuanzia mapambazuko hadi machweo, na kwa kufuatana na majira.

Wamasai wana ustadi unaohitajika kuishi katika pori la Bonde la Ufa. Wao hutembea mbali sana kutafuta malisho na maji kwa ajili ya mifugo yao, nao huchunga mifugo miongoni mwa makundi ya kongoni, punda-milia, twiga, na wanyama wengine wanaoishi katika pori hilo.


Wamasai wanaamini kwamba ng’ombe wote duniani ni mali yao. Imani hiyo inatokana na hekaya inayosema kwamba hapo mwanzoni Mungu alikuwa na wana watatu, naye alimpa kila mmoja zawadi. Yule wa kwanza alipokea mshale wa kuwindia, yule wa pili alipokea jembe la kulimia, na yule wa tatu alipokea fimbo ya kuchunga ng’ombe. Inasemekana kwamba yule mwana wa mwisho alikuwa babu wa kale wa Wamasai. Ijapokuwa watu wa makabila mengine wanafuga ng’ombe, Wamasai wanaamini kwamba ng’ombe hao ni mali yao.

View attachment 327444


Nyumba za Wamasai hujengwa na wanawake, nazo hujengwa kwa matawi na nyasi na kisha hukandikwa kwa samadi ya ng’ombe. Nyumba za Wamasai ni zenye umbo la mstatili nazo huzunguka boma ambamo ng’ombe hulala usiku. Nje ya nyumba hizo kuna ua wa matawi yenye miiba unaowalinda Wamasai na ng’ombe zao dhidi ya fisi, chui, na simba wanaowinda usiku.Wamasai ni watu warefu, wembamba, na wenye sura nzuri. Wao hufunga mashuka yenye rangi nyangavu nyekundu na samawati. Wanawake hujirembesha kwa kuvalia mkufu mpana wenye shanga, na mapambo ya vichwani yenye rangi nyingi. Nyakati nyingine mikono na miguu hukazwa kikiki kwa nyaya nyingi nene za shaba. Wanawake na wanaume hurefusha masikio yao kwa kuvaa mapambo na vipuli vizito vyenye shanga. Madini mekundu yaliyosagwa huchanganywa na mafuta ya ng’ombe nayo hutumiwa kupamba mwili.

Vijana wanapokuwa wakubwa, wao hujifunza mila na sherehe wanazohitaji kupitia ili wawe watu wazima. Miongoni mwa mila ambazo wao hujifunza ni zile zinazohusu magonjwa, bahati mbaya, ndoa, na kifo. Wamasai huamini kwamba wasipofuata mila hizo watapatwa na balaa.

Wazazi wa msichana Mmasai wanaweza kupanga ndoa yake akiwa kitoto. Msichana huyo huposwa na mwanamume aliye na mifugo ya kutosha kulipa mahari ambayo babake atatoza. Mara nyingi wasichana huolewa na wanaume walio na umri mkubwa kuliko wao, ambao tayari wana wake wengine.

Mila za pekee na utamaduni wa Wamasai unatoweka kwa haraka siku hizi. Katika maeneo mengine, Wamasai hawawezi tena kuhamahama na mifugo yao ili kutafuta malisho bora. Sehemu nyingi za nchi yao ya zamani zinafanywa kuwa mbuga za wanyama, au kutumiwa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba, na ukulima. Wamasai wengi hulazimika kuuza ng’ombe zao wapendwa kwa sababu ya ukame na hali mbaya ya kiuchumi. Wamasai wanapohamia miji mikubwa, wanakumbwa na matatizo yaleyale yanayowapata watu wengine siku hiziView attachment 327444
Kwenye picha sio wamasai hao....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom