Kuhusu Tabia ya wanasiasa, Mh. Wenje you are very right

Baada ya utetezi huo, Watoto wako wansoma shule gani?

ijabahatika kuwa naye bado!

Unajua kwenye historia ya Lugha zamani nchi nyingi za ulaya kama Uingereza & Co. walikua wanatumia kilatini, na sababu hasa za wazungu wakiwemo waingereza kuacha kutumia kilatini ni kwamba kilatini ni lugha nyingine kabisa na haina uhusiano wowote na kiingereza kwa hiyo ilibaki kuwa lugha ya watu wachache tu "elite" na watu wa kawaida ambao walikuwa ndio wengi waliachwa nyuma (kama ilivyo Afrika leo), wakafanya mapinduzi yaliyoanzishwa na Martin Luther aliyetafsiri Biblia kwenda kijerumani na baada ya hapo mapinduzi yakaja na waingereza nao wakatafsiri kwa lugha yao "King James Bible", wakatoa kilatini na ndio maana unaona sehemu kubwa ya kiingereza na lugha nyingi za ulaya zina maneno ya kilatini, sasa wazungu wanalijua hilo na ndio maana wanakampeni sana kwa propaganda nyingi kwamba nchi za kiafrika zitumie lugha zao kwa maana wanajua zitabaki kueleweka na elite wachache ambao watawatumia kwa manufaa yao na waliobaki wengi kubaki kuburuzwa tu na elite wachache!

Duniani hamna jipya mambo yanakwenda yanajirudia hata hizo nchi zoote za kiafrika (Mungu atuepushe Tz) zinazotumia kiingereza/kifaransa/kireno ipo siku wakija kujitambua watafanya mapinduzi na kurudi kule kule wanakokupinga sasa hivi na nakuhakikishia haitakuwa kazi rahisi lakini ni lazima itafanyika!

Napingana na wewe kwa asilimia 100! kwa maana hata ufanye nini huwezi kuifanya Tanzania ikawa "an english speaking country" na ukisema Serikali ifanye hivyo kwamba lugha ya kufundishia iwe kiingereza tangu mwanzo bado hutaondoa matabaka na ndio utayazidisha na naandika hivi kwa sababu ndio nimekamilisha utafiti wangu wa matumizi ya lugha na nimetembelea nchi karibu zote za kiafrika zinazotumia huo mfumo unaoupendekeza na matokeo yake sio mazuri!
Hivi unajua kwamba nchi kama Uganda ni asilimia 8% tu ya wananchi wake wanaweza kutumia kiingereza, Kenya ni hapo hapo pamoja na kuwa na mfumo huo unaoupendekeza wewe?
Na kati ya hao asilimia 8% karibu wote ni watoto wa "elite" ambao wazazi wao wanatumia kiingereza nyumbani tangu watoto kwa hiyo kupendekeza huo mfumo sio suluhisho bali kusogeza tatizo mbele kwani ndio kutaleta matabaka amayo hayajawahi kutokea Tanzania, NAANDIKA HIVI KWA HISIA KUBWA SANA KWA MAANA NI KITU AMBACHO NIMEKIFANYIA UTAFITI KUANZIA NIGERIA MPAKA LESOTHO! Kwa hiyo nasema chonde chonde serikali wasiende huko na kama ndio sera ya CHADEMA basi nimeshapoteza matumaini nao!

Nina wasiwasi kama unayoyasema umeyafanyia utafiti kweli. Kenya asilimia 80% ya watu wa umri kati ya miaka 50 kurudi mpaka miaka 20 wanazungumza kiingereza na ndio maana wakenya when it comes kwenye ajira za makampuni ya kigeni they are more prefered kwa kuwa kiingereza kinapanda kuliko sisi watanzania. Na sijui hilo la kusema Tanzania is not an English speaking language umelipata wapi? Kila nchi ina lugha zake za ndani lakini inakuwa na lugha angalau moja ya kimataifa. Tunaposema DRC ni french speaking country haina maana hawana lugha zao nyingine. Tanzania ni English speaking Country.

Nakubaliana na Wenje wengi wa viongozi ni wanafiki tu katika hili.

Tiba
 
Watoto wa waziri wa elimu Kawambwa wanasoma mombasa, international school,wa Rage wanasoma usa na australia!WENJE U RE RIGHT 100% tuamue moja

aisee kazi ipo!wenje upo sawa.ss km ndo hivi watoto wa maskin ndo basi tena
 
Tukubali tukatae tanzania kwa sasa kuna matabaka ya elimu,hata vitabu vya kiada vinatofautiana mkoa kwa mkoa!KIKWETE UMESHA AHIDI MARA NGAPI KUANZISHA SCHOOL FEES REGULATORY AGENCY?acha usanii tekeleza hilo
 
napingana na wewe kwa asilimia 100! Kwa maana hata ufanye nini huwezi kuifanya tanzania ikawa "an english speaking country" na ukisema serikali ifanye hivyo kwamba lugha ya kufundishia iwe kiingereza tangu mwanzo bado hutaondoa matabaka na ndio utayazidisha na naandika hivi kwa sababu ndio nimekamilisha utafiti wangu wa matumizi ya lugha na nimetembelea nchi karibu zote za kiafrika zinazotumia huo mfumo unaoupendekeza na matokeo yake sio mazuri!
Hivi unajua kwamba nchi kama uganda ni asilimia 8% tu ya wananchi wake wanaweza kutumia kiingereza, kenya ni hapo hapo pamoja na kuwa na mfumo huo unaoupendekeza wewe?
Na kati ya hao asilimia 8% karibu wote ni watoto wa "elite" ambao wazazi wao wanatumia kiingereza nyumbani tangu watoto kwa hiyo kupendekeza huo mfumo sio suluhisho bali kusogeza tatizo mbele kwani ndio kutaleta matabaka amayo hayajawahi kutokea tanzania, naandika hivi kwa hisia kubwa sana kwa maana ni kitu ambacho nimekifanyia utafiti kuanzia nigeria mpaka lesotho! kwa hiyo nasema chonde chonde serikali wasiende huko na kama ndio sera ya chadema basi nimeshapoteza matumaini nao!

muongo mkubwa wewe, mwanafunzi wa sekondari wa kenya ana uwezo mkubwa wa kujieleza kwa kiingereza kuliko wa kibongo.
 
Hivi unachangia unaloelewa au ulilosikia? Wenje kasema sera ya elimu inaelekeza lugha ya kufundishia elimu ya msingi ni kiswahili, mbona elimu ya msingi kwenye english medium school inatolewa kwa lugha tofauti na maelekezo ya sera? Au kwakuwa watoto wetu (vionggozi) wanasoma huko? Basi kama ni hivyo, tuwafanye na watoto mamantilie vijijini nao wajifunze kwa kiingereza kwamaana timewanyanyapa kwa kuwa na double standard
 
Wenje nae kumbe jembe?
Ktk mchango wa Mh. Wenje kwa hotuba ya bajeti ya wizara ya Elimu, amewaeleza wabunge na mawaziri wote waache UNAFIKI wa kuweka sera ya elimu inayotaja wazi kwamba lugha ya kufundishia kwa shule za msingi ni Kiswahili, huku wao wabunge na mawaziri wakiwapeleka watoto wao shule zinazotumia Kiingereza.

Binafsi naomba niseme kwamba ni aibu mawaziri, wabunge, wakurugenzi, Rais, makatibu wakuu n.k hawaamini kwamba Kiswahili ni lugha inayowafaa watoto wao. Pamoja na imani hiyo wengi wanakuwa wanafiki kwa kusema lugha hii itumike ktk shule zetu zote. Tena wengine wanakwenda mbali na kutaka itumike hadi vyuo vikuu.

Nahisi wanasiasa wanataka kiingereza kibaki kuwa ni privilege yao na familia.

Tuache unafiki kama alivyosema Mh. Wenje, Tuseme ukweli kwamba wote tunahitaji kiingereza kuliko Kiswahili. Shule zetu zirudishe Kiingereza ili hata mtoto wa maskini aweze kutumia Kiingereza.
 
muongo mkubwa wewe, mwanafunzi wa sekondari wa kenya ana uwezo mkubwa wa kujieleza kwa kiingereza kuliko wa kibongo.
Mbona unanihukumu bila kunielewa? wapi nimesema au nimelinganisha uwezo wa kuongea kiingereza kati ya mwanafunzi wa Kenya na wa Tanzania?
Nimesema kwamba watu wenye uwezo wa kuandika, kuzungumza au kukitumia kiingereza nchini kenya wako chini ya asilimia kumi na sio Kenya tu Uganda ni asilimia 8, na ndio maana wanasiasa wa Kenya au Uganda au sehemu nyingine yoyote Afrika kwenye kampeni zao hawakampeni kiingereza kwa nini? mbona bungeni wanaongea kiingereza?

Napingana na wewe kwa asilimia 100! kwa maana hata ufanye nini huwezi kuifanya Tanzania ikawa "an english speaking country" na ukisema Serikali ifanye hivyo kwamba lugha ya kufundishia iwe kiingereza tangu mwanzo bado hutaondoa matabaka na ndio utayazidisha na naandika hivi kwa sababu ndio nimekamilisha utafiti wangu wa matumizi ya lugha na nimetembelea nchi karibu zote za kiafrika zinazotumia huo mfumo unaoupendekeza na matokeo yake sio mazuri!
Hivi unajua kwamba nchi kama Uganda ni asilimia 8% tu ya wananchi wake wanaweza kutumia kiingereza, Kenya ni hapo hapo pamoja na kuwa na mfumo huo unaoupendekeza wewe?
Na kati ya hao asilimia 8% karibu wote ni watoto wa "elite" ambao wazazi wao wanatumia kiingereza nyumbani tangu watoto kwa hiyo kupendekeza huo mfumo sio suluhisho bali kusogeza tatizo mbele kwani ndio kutaleta matabaka amayo hayajawahi kutokea Tanzania, NAANDIKA HIVI KWA HISIA KUBWA SANA KWA MAANA NI KITU AMBACHO NIMEKIFANYIA UTAFITI KUANZIA NIGERIA MPAKA LESOTHO! Kwa hiyo nasema chonde chonde serikali wasiende huko na kama ndio sera ya CHADEMA basi nimeshapoteza matumaini nao!

Mkuu acha kudanganya uma na hilo neno utafiti? Kwa taarifa yako utafiti wenye kuleta majibu ya kweli ni kwenye sayansi na sayansi ya jamii. Hizi tafiti zenu za masomo ya MBA, MPA, MA (Political Science, etc), LLM na PhDs zake ni uzushi tu! Tafiti za kutoa majibu ya uhakika ni tafiti za Magonjwa, mambo ya ki engineer na tafiti ambazo moja kwa moja unaingia maabara, haziko biased hata kidogo. Acha kabisa kuja na tafiti zako za kizushi! Tumefanya tafiti nyingi sana za namna ya kwako na zinaishia kwa makaratasi tu! Kwanza data zako zinaonekana ni za uongo sana na unaonekana uko biased hata kabla hujaanza hiyo tafiti yako. Nipe link kwenye hiyo paper yako na tuone ume publish wapi na pia tukukosoe, usije na neno tafiti ukazani ndo umemaliiiiiza! Kwa taarifa yako kwa ulimwengu huu, hata enzi za Yesu na Mtume S.A W (P B U H) matabaka yalikuwepo tu! Hata tukifundisha kwa Kiswahili matabaka hayataisha!
 
Mbona sikuelewi unatoa tu kashfa, sasa unachopinga ni nini? manake nimeandika vingi, sema haswa unachopinga ili nikujibu!
 
...Kwa hiyo nasema chonde chonde serikali wasiende huko na kama ndio sera ya CHADEMA basi nimeshapoteza matumaini nao!

Yaan kwa hili tu ndiyo upoteze matumain na chadema? Mim kama intelectual naamini sana ktk utafiti-maana ndiyo pekee ya kupata ukweli, lakin wakati mwingine utafiti unakuwa "very convenient" kulingana na matakwa ya mtafiti au mfadhili wa utafiti.

Mfano: kuna mtu anafanya utafiti ili atimize vigezo vya kumaliza masomo (thesis/dessertation)-wanafunzi wengi kote duniani wamekuwa wakishawishika kuongeza "sukari" ili matokeo ya utafiti yawe "matamu". Pia kuna wafadhili wa utafiti-nao wanakuwa na indirect influence ktk matokeo ya utafiti. Ni vizuri wakati mwingine kuelezea kwa undani kuhusiana na utafiti wako-mfano kwanini ulifanya utafiti, nani wafadhili, n.k.

Mwisho, hata nchi zile ambazo hapo awali zilitilia mkazo sana lugha yao (e.g. China, South Korea), leo zimekigeukia kiingereza. Ktk nchi hizi, kingereza kinaabudiwa na kuhusudiwa. Kuna mashindano makali ya kiingereza CCTV internation-wao wanasema kujua kuingereza ndiyo kupata ticket ya kwenda ulimwenguni kutafuta maisha (our resources).

Miaka takribani 2, kuna Mkorea kusini alipata average score ya 8.0 ktk IELTS (highest score being 9.0). Hii ilikuwa ni breaking news ktk national tv maana hapakuwahi kutokea mkorea akafanya vizuri kiasi hicho ktk mitihani ya kingereza inayosimamiwa na british council. Kwa kifup, graduate wa korea kusin hawez kupata kaz kirahis kama hajui kiingereza. Sasa korea kusini ni nchi iliyoendelea, sembuse tz? Tunashangaa viongozi wetu wanapenda safari za kuhudhuria mikutano nje ya nchi lakini wakifika huko wanakuwa bubu?
 
ni vizuri umetolea mifano ya hizo nchi zote, lakini hujasema kama wameamua kubadilisha mfumo wa kufundishia tangu awali mpaka elimu ya juu kwa kiingereza, na kama hawajafanya hivyo ni kwa nini?
 
Kinacho semwa hapa ni kuondoa UNAFIKI kama ni lugha itumike moja kote private school na gvt school si nyinyi wenu wansoma english medium sisi tunasoma kilugha maana katika ushinda wa ajiri tutapimwa sawa kwanini tutofautiane kwenye elimu?
 
Wachangiaji mnaompinga Wenje mnasahau kuwa huo mfumo anaodai mheshimiwa sio mpya bali ndio mfumo uliokuwa ukitumika hapo zamani na hakuna lililoharibika.
Kiswahili kuwa somo na kiingereza kuwa lugha ya kufundishia haimaanishi kuwa kiswahili kitaacha kuwa lugha ya taifa na watanzania watashindwa kuongea kiswahili.
Mfano mzuri ni hawa watoto wetu wanaosoma english medium academies....je kwani hawaongei kiswahili kizuri tu wawapo majumbani? tuache kuja na tafiti za ajabu ajabu, na kusema kiswahili ni lugha rahisi waulize watanzania vijijini hasa usukumani kinavyowatoa jasho!
Kama kiingereza ndio tumekichagua kuwa official language lazima tuwe serious ili tunapokuwa tumehitimu elimu za juu tuwe na uwezo mkubwa wa kutransfer knowledge officially and unofficially....yaani kwa kiingereza na kiswahili as interview requires fluency in both langauages!
 
Napingana na wewe kwa asilimia 100! kwa maana hata ufanye nini huwezi kuifanya Tanzania ikawa "an english speaking country" na ukisema Serikali ifanye hivyo kwamba lugha ya kufundishia iwe kiingereza tangu mwanzo bado hutaondoa matabaka na ndio utayazidisha na naandika hivi kwa sababu ndio nimekamilisha utafiti wangu wa matumizi ya lugha na nimetembelea nchi karibu zote za kiafrika zinazotumia huo mfumo unaoupendekeza na matokeo yake sio mazuri!
Hivi unajua kwamba nchi kama Uganda ni asilimia 8% tu ya wananchi wake wanaweza kutumia kiingereza, Kenya ni hapo hapo pamoja na kuwa na mfumo huo unaoupendekeza wewe?
Na kati ya hao asilimia 8% karibu wote ni watoto wa "elite" ambao wazazi wao wanatumia kiingereza nyumbani tangu watoto kwa hiyo kupendekeza huo mfumo sio suluhisho bali kusogeza tatizo mbele kwani ndio kutaleta matabaka amayo hayajawahi kutokea Tanzania, NAANDIKA HIVI KWA HISIA KUBWA SANA KWA MAANA NI KITU AMBACHO NIMEKIFANYIA UTAFITI KUANZIA NIGERIA MPAKA LESOTHO! Kwa hiyo nasema chonde chonde serikali wasiende huko na kama ndio sera ya CHADEMA basi nimeshapoteza matumaini nao!

wewe ni mpumbavu mkubwa, huo upuuzi wako peleka kwa hao hao wapuuzi, nyie ndio mnatuziba macho tusione? ili muendelee kuongoza wenyewe, gamba mkubwa wewe, toka hapa!
 
Swali zuri, Kiswahili kimeweza kukubalika sio kwa sababu za kisiasa bali za kihistoria, kiswahili kimekuwa kikitumika Tanzania au sehemu ambayo leo tunaiita Tz kwa miaka mingi sana zaidi ya 1000, na kuna sababu nyingi za kusambaa kwake nyingine zikiwa nzuri nyingine zikiwa mbaya na sababu kubwa ni biashara kati ya pwani na tz interior lakini sababu kubwa kabisa ni kwamba kiswahili ni KIBANTU kwa hiyo ni rahisi sana kwa mzaramu au msukuma au mngoni kukitumia, na ndio sababu wamasai (SIO WABANTU)wengi kiswahili kinawapa shida!

Sasa basi leo hii kutaka kupindua Kiswahili na kuleta kiingereza ni kujidanganya kwani kamwe hakitaweza kukubalika na kupenya jinsi kiswahili kilivyopenya na sababu ni kwamba kiingereza ni lugha nyingine kabisa, na ndio maana nikakupa mifano ya nchi za kiafrika ambazo zimefanya hayo (sio kwa idhini yao) mnayosema na matokeo yake sio mazuri, siandiki kutoka HEWANI, kinachotokea ni hivi kwa sababu kiingereza ni lugha nyingine tofauti inabaki kuwa ya elite tu na ndio maana ukienda Kenya watu wa kawaida wanaongea kitu wanachokiita "sheng" (mchanganyiko wakila kitu) Nigeria, ghana & co. wanatumia Pidgin English, umeshajiuliza kwa nini?

Sasa kama sisi tumefanikiwa ni kwa nini unataka turudi nyuma badala ya kwenda mbele? Tuna Lugha tayari ambayo ina nafasi yake Duniani, inafundishika, iko "standardised" na ndio maana unaweza kusema fulani anaongea kiswahili kibaya na hiyo sio kazi ndogo kufika hapo!

Mwisho umaskini wetu hausabishwi hata tone na Kiswahili bali mambo mengine kabisa!

Ndugu yangu forget about politics. Matumizi ya lugha kwenye kufundishia(sio mawasiliano ya kawaida) yana uhusiano mkubwa sana na maendeleo ya technologia. Huwezi kutumia lugha yako kufundishia kama wewe sio mzalishaji wa technologia!!! Na ili uweze kufikia kiwango cha kuzalisha technologia ni lazima kuazima lugha ya weneye hiyo technologia ili uweze kuchota hiyo technologia kutoka kwa waliyonayo. Na ndio linapokuja suala la kutumia lugha ya kigeni kwenye elimu.

Mfano taifa kama China walipeleka watu wao nchi kama Urusi, America na Ulaya kuiba technologia (sio kwa kichina bali kwa lugha native za nchi hizo, kiingereza kikiwa na sehemu kubwa zaidi) then walivyo pata ujuzi na kuanza kuzalisha technoligia yao ndo wakaanza kutumia zaidi lugha yao(infact hii inakuja automatic haiwi promoted politically). Leo china wanapeleka chombo chao anga za juu na ukiangalia ndani ya control room unaona kabisa karibu controllers na scienticts wote humo ndani ni wachina na wanatumia lugha yao humo ndani. Hawakufikia hayo kwa ku promote matumizi ya lugha yao (politically) bali kwa kupromote maendeleo ya technologia.

Tunaweza kuaandika makala ndefu sana kuhusisha maendeleo ya technologia na lugha hapa lakini kwa ufupi ni kuwa kama wewe huzalishi kabisa technology(Tanzania ni mojawapo tunaagiza mpaka kiberiti, sindano ya kushonea nguo) basi ku attempt kutumia lugha yako kwa ajili ya kutolea elimu ni catastrophic move!!!!!

All politicians know this na ndo maana hakuna hata mmoja anayekubali kusomesha mtoto wake kiswahili medium schools. Only the few honest kama Wenje (i believe anasomesha mtoto wake english medium kama yupo) wana amua kufunguka, tuwape support.!!!! We need english (or chinese or any other which will anable us to grab technology) to be used as a medium for education in our country before its too late.

NB. Watu wengi kama wewe naona wanachanganya kati ya International Schools(if the are really international) na English Medium Schools. Naamini kabisa Wenje anazungumzia english as a medium of education. I stand to be corrected.
 
Swali zuri, Kiswahili kimeweza kukubalika sio kwa sababu za kisiasa bali za kihistoria, kiswahili kimekuwa kikitumika Tanzania au sehemu ambayo leo tunaiita Tz kwa miaka mingi sana zaidi ya 1000, na kuna sababu nyingi za kusambaa kwake nyingine zikiwa nzuri nyingine zikiwa mbaya na sababu kubwa ni biashara kati ya pwani na tz interior lakini sababu kubwa kabisa ni kwamba kiswahili ni KIBANTU kwa hiyo ni rahisi sana kwa mzaramu au msukuma au mngoni kukitumia, na ndio sababu wamasai (SIO WABANTU)wengi kiswahili kinawapa shida!

Sasa basi leo hii kutaka kupindua Kiswahili na kuleta kiingereza ni kujidanganya kwani kamwe hakitaweza kukubalika na kupenya jinsi kiswahili kilivyopenya na sababu ni kwamba kiingereza ni lugha nyingine kabisa, na ndio maana nikakupa mifano ya nchi za kiafrika ambazo zimefanya hayo (sio kwa idhini yao) mnayosema na matokeo yake sio mazuri, siandiki kutoka HEWANI, kinachotokea ni hivi kwa sababu kiingereza ni lugha nyingine tofauti inabaki kuwa ya elite tu na ndio maana ukienda Kenya watu wa kawaida wanaongea kitu wanachokiita "sheng" (mchanganyiko wakila kitu) Nigeria, ghana & co. wanatumia Pidgin English, umeshajiuliza kwa nini?

Sasa kama sisi tumefanikiwa ni kwa nini unataka turudi nyuma badala ya kwenda mbele? Tuna Lugha tayari ambayo ina nafasi yake Duniani, inafundishika, iko "standardised" na ndio maana unaweza kusema fulani anaongea kiswahili kibaya na hiyo sio kazi ndogo kufika hapo!

Mwisho umaskini wetu hausabishwi hata tone na Kiswahili bali mambo mengine kabisa!

Acha Porojo.
Dunia nzima inaunganishwa kwa kiingereza sisi tunang'ang'ania kiswahili cha nini? Haujui kwamba hata vimafanikio vidogo walivyonavyo Jirani zetu ni kwa sababu ya Kiingereza pia. CCM na Kiswahili wote mwisho wao ni 2015.

Tunaposema tuachane na mambo ya zamani au mira na desturi zilizopitwa na wakati ni lazima tufanye hivyo kwa mapana yake, Kiwahili na CCM ni moja ya mambo hayo.
 
Ktk mchango wa Mh. Wenje kwa hotuba ya bajeti ya wizara ya Elimu, amewaeleza wabunge na mawaziri wote waache UNAFIKI wa kuweka sera ya elimu inayotaja wazi kwamba lugha ya kufundishia kwa shule za msingi ni Kiswahili, huku wao wabunge na mawaziri wakiwapeleka watoto wao shule zinazotumia Kiingereza.

Binafsi naomba niseme kwamba ni aibu mawaziri, wabunge, wakurugenzi, Rais, makatibu wakuu n.k hawaamini kwamba Kiswahili ni lugha inayowafaa watoto wao. Pamoja na imani hiyo wengi wanakuwa wanafiki kwa kusema lugha hii itumike ktk shule zetu zote. Tena wengine wanakwenda mbali na kutaka itumike hadi vyuo vikuu.

Nahisi wanasiasa wanataka kiingereza kibaki kuwa ni privilege yao na familia.

Tuache unafiki kama alivyosema Mh. Wenje, Tuseme ukweli kwamba wote tunahitaji kiingereza kuliko Kiswahili. Shule zetu zirudishe Kiingereza ili hata mtoto wa maskini aweze kutumia Kiingereza.

Hilo halipingiki hata kidogo.
Mimi mwenyewe wala mume wangu hakuna mwenye hivyo vyeo ulivyovitaja lakini tunapeleka watoto wetu shule zinazofundisha kiingereza. hapa namaanisha kuwa, watu wengi kwa sasa ambao tuna hata angalau uwezo wa kukopa, tunakopa ili tupeleke watoto wetu huko.
nadhani sasa wakati umefika tukubali yaishe, kiswahili ni lugha yetu, na tunaipenda sana, lakini ibaki katika matumizi ya mawasiliano ya kawaida, isiwe kwa matumizi ya shule. shuleni libaki tu somo la kiswahili lakini siyo kufundisha jogfaria.

Mama yangu huyu Mbunge hakumaanisha nyie wenye uwezo wa ukopa au middle class earners. Population aliyoongelea ni ya wale wenzangu na mie yani sie Masikini amba hata michango ya hizi shule za msingi kama maji na kadhalika ni m tihani kulipia.

Hongera zako wewe mwenye uwezo hata wa kukopa kuliko sie tusio hata na vigezo vya kukopa mama yangu.

After all ametolea mfano kwa Mawaziri na wabunge coz wao ndio wapitisha Bajeti mbovu kwa vigelegele. kungekua na sera nzuri ya Elimu hata hizo pesa unazokopa usingekopa ili mtoto wako aende akasome English medium mama. Angesoma shule zetu hizi hizi.
 
Back
Top Bottom