Kuhusu Mfumuko wa Bei, Viongozi wachunge kauli

Peter Stephano 809

Senior Member
Feb 29, 2020
120
162
"Hatuwezi kutatua matatizo kwa kuyafanya hayapo" hii ni nukuu màarufu na inayopendwa na wanaharakati wengi.

Katika nukuu hii inaonyesha kuwa ili utatue tatizo ni lazima ukubali kuwa lipo kisha utafute suluhisho lake.

Pia nukuu hii inaonyesha kuwa huwezi kutatua tatizo kwa kulificha lisionekane.

Ni wazi kuwa mfumuko wa bei umetamalaki dunia nzima kwa sababu mbalimbali zinazotajwa na wataalamu wa uchumi Kama vile athari za ugonjwa wa virusi vya Corona na mgogoro wa Urusi na Ukraine.

Mfumuko wa bei kwenye bidhaa hasa mafuta na gesi umekuwa mkubwa na kupelekea ugumu wa maisha kwenye jamii.

Kama ilivyo nchini Tanzania nako hali si shwari kutokana na changamoto hii ya kupanda kwa bei za bidhaa. Kwa mfano bei ya mche mmoja wa sabuni kutoka 2000 mpaka 4000 kwa wastani, bei ya mafuta ya petrol na diesel kufikia 2800 kwa lita na kuendelea.

Huku bei ya mafuta ya kupikia ikiibua hisia za tofauti kwa kupanda hadi 8000 kwa lita katika baadhi ya maeno nchini. Kadhalika bei ya vifaa vya ujenzi imezidi kuwa gumzo kwa kuendelea kupanda kila kukicha. Mfumuko huu unahusishwa na sababu mbili nilizozitaja hapo awali.

Katika mtazamo wa kawaida sababu hizi zinaweza kuwa kuu kidunia lakini zina Sababu "sindikizi" nyingi ndani yake ambazo zimepelekea makali makubwa ya mfumuko wa bei hapa nchini.

Sababu anuai ni kauli za Viongozi wa serikali juu ya mfumuko wa bei ambazo zinaleta jeuri kwa wafanyabiashara kupandisha bei wanavyotaka kwakua wanajua Viongozi wa serikali hawana cha kuwafanya.

Wiki chache zilizopita Rais Samia Suluhu alisema Watanzania wajiandae na kupanda kwa bei za bidhaa. Kauli hii ilikua ni tahadhari lakini haikuwa na afya kutamkwa na kiongozi mkuu wa nchi.

Siku chache baada ya kauli hii ilianza kushuhudiwa bei za bidhaa kupanda kwa kasi zaidi ya ilivyotegemewa. Huenda wafanyabiashara na wasambazaji wa bidhaa waliichukulia kauli hii Kama mwanya wa kupandisha bei za bidhaa wanavyotaka.

Sababu ya pili ni kutokuwepo na chombo madhubuti kinachoshughulika na upangaji, usimamizi wa bei za bidhaa nchini hivyo kupelekea wafanyabiashara kujipangia bei wenyewe kinyume na uhalisia. Sababu ya tatu ni uwepo wa viashiria vya wafanyabiashara kufanya hujuma kama kuficha bidhaa kwenye maghala ili ziadimike Sokoni kisha wapandishe bei kwa makusudi.

Haingii akilini ukimwambia mwanachi wa Makete kule njombe ndani ndani ukimwambia kuwa bei ya sabuni inayotengenezwa kwa mawese ya Kyela imepanda kwa sababu ya Vita ya Ukraine. Hata aliye mjini hawezi kukubali kuambiwa kuwa bei ya simenti ya mtwara imepanda kwa sababu ya Vita ya Ukraine.

Sababu hizi kuu mbili zina mashiko kwa ukubwa wake lakini hazina uhalisia katika jamii iliyokubwa kushinda sababu nilizozitoa hapo.
Hayati Magufuli alifanikiwa kupunguza athari za Ugonjwa wa virusi vya Corona kwa kuaminisha raia kuwa Ugonjwa haupo na hauna madhara makubwa.

Silaha hii inaweza kutumika kuzuia mfumuko wa bei kwa serikali kuweka usimamizi makini katika upangaji wa bei za bidhaa nchini.
Viongozi wetu kuendelea kutuambia kuwa mfumuko wa bei katika bidhaa zote ni kutokana na vita ya Ukraine ni kuendelea kutuangamiza na huu ugumu wa Maisha.

1649047431061.jpg
 
Habari wanajamvi kitambo kidogo sijaweka comment wa uzi ili tuko pamoja.

Naona sasa pamoja na yote yanayoendelea huko duniani bado maisha yetu yanaend kuwa magumu sana kutokana na hali ya bidhaa kupanda bei hasa mafuta ya Petrol na Disel najua kunajitihada Serikali yetu inafanya lakini bado maumivu makubwa.

Ila wazo langu kama magari yetu sasa yanaweza wekewa mfumo wa kutumia Gesi ambao una faida kwa kupunguza gharama za uendeshaji na utunzaji wa MAZINGIRA Serikali yetu inakwama wapi kuongea na wadau hata kila wilaya tukawa na station moja ya gesi mbona mawazo hayahaya hitaji Masters ya Degree.

Pesa imekuwa ngumu ndindi maisha yanapanda.
 
Serikali inafanya jitihada gani ndugu muandishi? Wakati ndiyo wanaongeza kaa la moto, unasikia bidha imekua scarcity worldwide na bei kuwa tofauti then mnaambiwa tozo zinarudi, je mnataka tudate raia tumeshajitoa sana kuinusuru nchi
 
HAbari wanajamvi kitambo kidogo sijawek comment wa uzi ili tuko Pamoja

Naona sasa pamoja na yote yanayoendelea huko duniani bado maisha yetu yanaend kuw magumu sana kutok nA hali ya bidhaa kupanda bei hasa mafuta ya petrol na diseal najua kunajitihad serikali yetu inafany lakn bado maumivu makubwa

Ila wazo langu kama magari yetu sasa yanawez wekew mfumo wa kutumia Gesi ambao unafaida kwakupunguz gharama za uendeshaji na utunzaji wa MAZINGIRA Crikali yetu inakwama wapi kuongea na wadau ata kila wilaya tukawa na station moja ya Gesi mbona mawazo haya haya hitaji mastersyaDegree

Pesa imekuw ngumu ndindi maisha yanapanda
Sasa unataka serikali ndio ikubadilishie mfumo wa gari yako ?

Mwenye gari ndio hubadilisha mfumo wa gari yake toka ktk mafuta kwenda ktk gesi

Nafikiri ivyo vituo vya kuweka gas vipo vichache pengine ni kutokana na sababu so far wanao tumia gas ktk magari yao wapo wachache mfano Dsm izo gas station zipo 2 tu pekee
 
Sasa unataka serikali ndio ikubadilishie mfumo wa gari yako ?

Mwenye gari ndio hubadilisha mfumo wa gari yake toka ktk mafuta kwenda ktk gesi

Nafikiri ivyo vituo vya kuweka gas vipo vichache pengine ni kutokana na sababu so far wanao tumia gas ktk magari yao wapo wachache mfano Dsm izo gas station zipo 2 tu pekee
Ninacho maanish wanayonafas kuongea na wadau na kuwap mazngr wezeshe wawez kusambaz vtuo hvyo kila wilay/Halmashaur ,

Wachache wanatumia wakijua kuw n cheaper kiuendeshaji watahamia tuu
 
Back
Top Bottom