Kufikia mwezi wa 12, nitafunga kibanda cha M-PESA

Usifunge njoo pm na no yako iliyo tellegram tu...nikufundishe bottom line ya kufanya uwakala kwa faida zaidi na kutumia makato makubwa kama fursa...
 
Yaani hasara nimemuajiri mtu ninamlipa bado wateja wachache sana tofauti na kabla, sasa nimeweka interval hadi December kama hawajafanyia kazi bye bye
Unaandika kama vile unataka watu wakuoneee huruma.

Dunia haijawahi kuwa na huruma na mtu.
 
Wimbi la wafanyabiashara wa tigopesa kufunga limekuwa kubwa Sana kwasababu kuna wenzio wameshafunga biashara zao Kwa kukosa wateja.

Kwa muda ambao umejiwekea Hadi December ni plan mzuri kibiashara
Wanaofunga biashara kwa kasi sio wenye MPESA tu hata wenye maduka ya Mangi na ma bucha
 
Wimbi la wafanyabiashara wa tigopesa kufunga limekuwa kubwa Sana kwasababu kuna wenzio wameshafunga biashara zao Kwa kukosa wateja.

Kwa muda ambao umejiwekea Hadi December ni plan mzuri kibiashara
Mbona muuaji Chemba anasema transaction hazijashuka Sana maana yake watu wanatuma na kupokea miamala kama zamani? au propaganda?
 
kuna jamaa yy sasavihi anasema kwake ni sherehe.nilienda kwake kutoa laki 8 nikashangaa inaenda yote bila kukatwa alafu akanipa laki 7 na 90 ,nikamuuliza mnangu mbona sielew

akajibu man hapa 10k ndo faida.nikasema sinasikia zile laini za makato zinafungiwa jamaa akanijibu "bwnamkubwa jifunze kula na wakubwa,ukiwa na wakubwa hakiharibik kitu"

niliondoka nacheka yaan asubuh asubuh ameshakula 10k ??,kumbe kuna watu wanafungua mpesa af humo humo wana mbinu za kibaharia .

laki moja anakata 4000 washamfanyia vikao wafanyabiashara wenzake ila waapi.

wakuu nilikuw nafafanua kdg so asije mtu pm kuuliza anafanyaje mi sina chochote nachokijua kuhusu biashara ya mpesa
 
Yaani hasara nimemuajiri mtu ninamlipa bado wateja wachache sana tofauti na kabla, sasa nimeweka interval hadi December kama hawajafanyia kazi bye bye
Kuna jirani yako mwenye aina iyo ya biashara atamshukuru Mungu kwa kusikia ombi lake.
 
kuna jamaa yy sasavihi anasema kwake ni sherehe.nilienda kwake kutoa laki 8 nikashangaa inaenda yote bila kukatwa alafu akanipa laki 7 na 90 ,nikamuuliza mnangu mbona sielew

akajibu man hapa 10k ndo faida.nikasema sinasikia zile laini za makato zinafungiwa jamaa akanijibu "bwnamkubwa jifunze kula na wakubwa,ukiwa na wakubwa hakiharibik kitu"

niliondoka nacheka yaan asubuh asubuh ameshakula 10k ??,kumbe kuna watu wanafungua mpesa af humo humo wana mbinu za kibaharia .

laki moja anakata 4000 washamfanyia vikao wafanyabiashara wenzake ila waapi.

wakuu nilikuw nafafanua kdg so asije mtu pm kuuliza anafanyaje mi sina chochote nachokijua kuhusu biashara ya mpesa
hahahaaa mkuu mbona unasanua siri ya kambi??mi hapa nakamua tuu.voda wanakata 130 mteja nampa 4400 nabakiwa na faida ya 470 (hapo ni kwa mteja aliyetoa buku 5, fikira wale wakutoa laki laki

Screenshot_20210823-164037.jpg
 
Wabongo bana yani vikodi vidogo tudogo mnazokatwa na kutozwa yani mnalalamika kama vibinti vya chekechea vikicheleweshewa uji wa asubuhi. Lipeni kodi bana kwa CCM iwaletee maendeleo siyo kila kukicha ni kulialia tu.
Mkuu, hivi mantiki ya malalamiko ya 'taifa' ni kwa sababu ulizozitaja wewe?

Kila raia anapenda maendeleo ya nchi yafanywayo na serikali.

Tatizo lililopo ni kwamba, elimu haijatolewa kwa umma kuwajulisha kwanini kodi zao za vichwa(Vat) hazitoshi na vyanzo vingine vilivyokuwa vinatumiwa kukusanya mapato na kufanyia miradi hiyo ya Tarula nk, imeenda wapi, kwanini kodi juu ya kodi?

Hawana imani na security ya tozo hizo kwa sababu kila uchao mitandaoni na kwenye vyombo vingine, tunasikia 'mafisi' yakila ovyo bila hata kufuta damudamu zinazosalia midomoni mwao na hakuna 'hatua za maana' zinazochukuliwa.

Ukiona hatua zinachukuliwa, elewa ni kwa ajili ya kutoa tambiko la kafara na kufunika kombe ili mwana haramu apite.

Umeyasahau ya Tageta escrow, mumiani wale waliogawana pesa kwenye viroba vya sandarusi wapo jela gani?

Usiwaze ki dhiki dhiki unapowaza suala la taifa ama la umma.

Wanao lalamika siyo wajinga kama unavyodhania wewe wala dhiki kiviiilee, wana akili sana na point wanazo.
 
Back
Top Bottom