Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,485
- 40,014
Neno la Hekima: Kama kweli Mbowe na Team Lowassa wanaamini kuwa matokeo ya Urais yamehujumiwa wanahitaji kwa haraka kufanya hivi: Kwa matokeo ya majimbo 113 ambayo yametangazwa hadi hivi sasa watoe nakala za mawakala wao kwenye majimbo hayo ili wananchi waweze kulinganisha kama yanaendana na yale ya Tume hasa kwa vile Jaji Lubuva Tumatatu alisema kuwa wao wanatangaza matokeo yale yale yaliyosainiwa majimboni.
Wakifanya hivi wataweza kuonesha kama Tume inaweza kuaminiwa kuendelea kutangaza matokeo au la. Ushauri huu pia unaweza kuwafaa CCM nao wafanye hivyo hivyo ili tuone hili. Lakini pia natoa ushauri kama huu kwa TUme ya Taifa ya Uchaguzi Kuagiza Wasimamizi wa Uchaguzi kwenye Majimbo yote ambayo tayari yametangazwa rasmi na yale yatakayotangazwa rasmi kuweka hadharani nakala zao za majimbo na hivyo tutaweza kulinganisha matokeo ya vyama, wasimamizi wa uchaguzi na tume ili tuepushe mambo ya kuitana Ikulu tena kwa mazungumzo zaidi.
Ili vyama visijisikie kuwa kwenye mtego, Tume iruhusu vyama hivyo kuweka hadharani nakala za matokeo yao kwa majimbo yale ambayo yameshatangazwa na mengine baada ya kutangazwa ili kukata mzizi wa fitina.
Hii ndio njia pekee ya kufanya watu waamini matokeo yanayoendelea au la. M. M. Mwanakijiji