Kuenguliwa kwa Mwakalebela kwasababisha vurugu Iringa

Ex Spy

JF-Expert Member
Jan 15, 2007
213
1,726
Monday, 16 August 2010
Mwananchi


BAADA ya halmashauri kuu ya CCM kumuengua Fredrick Mwakalebela kugombea ubunge wa Iringa Mjini, kundi la wanachama wa chama hicho tawala wameahidi kurudisha kadi kwenye ofisi za matawi yao kuanzia leo kuonyesha kutoridhishwa na mchakato huo.

Halmashauri kuu, ambayo ilimaliza kikao chake mjini Dodoma Jumamosi, ilimuengua katibu huyo mkuu wa zamani wa Shirikisho la Soka (TFF) kwa sababu zilizoelezwa kuwa za kimaadili licha ya Mwakalebela kushinda kwa kura 3, 897 dhidi ya 2,989 za mpinzani wake, Monica Mbega, ambaye ni mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro na ambaye anatetea kiti chake.

Mwakalebela ni kati ya wagombea watatu walioshinda kwenye kura za maoni na wakaenguliwa na Nec na pia ni kati ya wagombea watatu waliofikishwa mahakamani na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa madai ya kutoa rushwa licha ya wagombea wengi wa CCM kuhojiwa na wengine kukamatwa na taasisi hiyo kwa tuhuma za kujihusisha na rushwa.

Mwananchi ilitembelea baadhi ya matawi ya chama hicho mjini hapa na kushuhudia makundi ya wanachama wakijipanga na kuendelea kuwashawishi wenzao jinsi kuzirudisha kadi za CCM katika ofisi za matawi yao.

Wanachama hao, ambao walikuwa wakitafakari uamuzi huo wa halmashauri kuu, walikuwa wakishawishiana kuiunga mkono Chadema ambayo imemsimamisha Mchungaji Peter Msigwa kuwania jimbo hilo.

Wanachama hao ni wa matawi ya Mwangata, Ruaha, Kichangani, Mtwivila, Kihesa, Wilolesi, Soko Kuu la Mjini Iringa, Mshindo na Igumbilo ambako wanachama walionekana kuguswa na uamuzi wa kumuengua Mwakalebela.

Baadhi ya wanachama hao walisema uamuzi wa halmashauri kuu ni wa kumtoa kafara Mwakalebela ambaye Takukuru ilimuhoji kwa tuhuma za kutoa rushwa kwenye vijiji viwili.

“Tumemchoka Monica Mbega; tulichotaka ni kubadilisha uongozi... hizi taarifa za Takukuru zinadai kwamba kwa kupitia mke wake ambaye naye hakukamatwa akifanya hivyo," alisema mmoja wa wanachama hao aliyejitambulisha kwa jina la David Butinini wa tawi la Mtwivila "Mwakalebela alitoa ushwa ya Sh 100,000 kwa wanachama 22 wa kijiji cha Mgongo, habari hizo zinaaminikaje wakati bado kesi haijaisha? Waturudisheie.”

Naye July Sawani wa tawi la Kichangani, alisema wakati Mwakalebela akienguliwa kwa madai hayo ya rushwa, inashangaza kuona Nec hiyo hiyo imeyapitisha majina ya Basil Mramba na Andrew Chenge ambao wana tuhuma kubwa tena nzito kuliko ya Mwakalebela.

Alli Mduba wa tawi la Kihesa alisema uamuzi wa CCM wa kuwataka wanachama wote washiriki katika kura hizo umekiwezesha chama hicho kujua wagombea wanaokubalika katika mbio hizo za uongozi, hata hivyo akasema majibu ya uamuzi uliofanywa na halmashauri kuu dhidi ya Mwakalebela yatayapata Oktoba 31 ambayo ni siku ya uchaguzi mkuu.

Mohamed Kassim wa Wilolesi alisema leo wanachama watarudisha kadi zao za CCM kwenye ofisi ya tawi katika tukio ambalo pia watalitumia kumtangaza rasmi mgombea watakayemuunga mkono.

Naye Edgar Sanga wa Igumbilo alisema wanachama watamaliza jazba zao za mgombea wao kuenguliwa kwa kumpigia kampeni na kura mgombea wa Chadema.

“Mwakalebela ndiye aliyekuwa chaguo letu vijana na wananchi wote wa jimbo la Iringa Mjini bila kujali rangi, itikadi, dini na makabila yao , tumesikitishwa na uamuzi wa NEC,” alisema mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Anna Michael wa tawi la Miyomboni.

Wakati wanachama hao wa CCM wakijiandaa kurejesha kadi, Chadema wanasherehekea wakidai kwamba sasa ni rahisi kulichukua jimbo kwa madai kuwa mgombea aliyekuwa tishio ni Mwakalebela ambaye alikuwa na kundi kubwa la vijana.
 
hivi inakuwaje tuhuma za sh.100,000/- zinawauma ccm kuliko za mabilioni ya shilingi? ati matumizi mamabya ya ofisi ua uwaziri si ishu, bali chai walizokunywa wanachama wa ccm amabazo hata thamani yake hazitoshi ada ya mtoto wa chekechea??

hivi haya ndio ya musa ama firauni?? i am totally confused!!!
 
Wana ccm wafuasi wa Mwakalebela wapo hapa Ofisi Kuu za CCM mkoa wakijadiliana jinsi ya kuanza maandamano yao baada ya kukataliwa kibali na polisi. Watu kama wanasua ila wanataka ntawapa update of the proceeds.
 
Wana ccm wafuasi wa Mwakalebela wapo hapa Ofisi Kuu za CCM mkoa wakijadiliana jinsi ya kuanza maandamano yao baada ya kukataliwa kibali na polisi. Watu kama wanasua ila wanataka ntawapa update of the proceeds.

Mwaka huu kazi ipo!
 
kw nn wanasumbuka? na solution ipo, inachowapasa ni kwenda upinzani moja kwa moja ili CCm wajue watu wamechoka
 
Wanaandamana nini?, kama una access na Mwakalebela, mwambie awashawishi wafuasi wake wasiandamane bali wahamasishwe wajitokeze kwa wingi siku ya kupiga kura, wachague chaguo lao. Naye ajiunge na Chadema, akachukue fomu kuitetea Iringa mjini, tuongeze majimbo ya ya upinzani Bungeni.
 
Wanahojiwa na waandish wa habari. Wakubwa wako ofisi ya makao makuu wanajadiliana. Watu wa Mbega na Mwakalebela wameingia 5 mins ago. Mwakalebela sijamwona.
 
wana JF mliopo iringa waelekezeni hawa waandamaji ilipo ofisi ya chadema

Taratibu mkuu. sema wanachadema tufanye hiyo kazi. Ukisema wanaJF Umekosea kidogo mkuu.
Nimelazimika kukurekebisha kwasababu Kuna tuhuma zimeanza kutolewa na jamii fulani humu Ndani.
 
Wanaandamana nini?, kama una access na Mwakalebela, mwambie awashawishi wafuasi wake wasiandamane bali wahamasishwe wajitokeze kwa wingi siku ya kupiga kura, wachague chaguo lao. Naye ajiunge na Chadema, akachukue fomu kuitetea Iringa mjini, tuongeze majimbo ya ya upinzani Bungeni.
Mwakelebela anatakiwa awe mstahimilivu, ujue ana kesi ya rushwa na pona yake abaki ccm, ama sivyo watamaliza kabisa, yeye awe mpole na kuomba miujiza itoke.
 
Mwakelebela anatakiwa awe mstahimilivu, ujue ana kesi ya rushwa na pona yake abaki ccm, ama sivyo watamaliza kabisa, yeye awe mpole na kuomba miujiza itoke.

Hapo umenena mkuu..hawaelekezwi Chadema, yeye apigane kumaliza soo la PCCB
 
Mwaka huu CCM watakiona cha mtema kuni maana kila sehemu ni maandamano na kutishia kurudisha kadi, dalili hizi zinaonyesha kweli siasa ya kidemokrasia imeiva bongo, mi nawashauri hao wanachama warudishe kadi kwani hata Pius alisema hawajali kama baadhi ya wanaCCM wakihama chama kwani wao ni sawa na mto ruvu ukitoa ndoo 2 za maji hujapunguza kitu, daaaaaaaaaaaaah dharau kubwa sana yaani maana yake nyinyi wanaCCM ambao mnataka kuhama CCM hamna dhamana kwa chama.Sasa jama mnangoja nini na mnawabembeleza nini hao sisiem? Maandamano acheni nyie nendeni ofisi za CHADEMA mkapate kadi mpya.
 
hivi inakuwaje tuhuma za sh.100,000/- zinawauma ccm kuliko za mabilioni ya shilingi? ati matumizi mamabya ya ofisi ua uwaziri si ishu, bali chai walizokunywa wanachama wa ccm amabazo hata thamani yake hazitoshi ada ya mtoto wa chekechea??

hivi haya ndio ya musa ama firauni?? i am totally confused!!!

Kwasababu hayo mabilioni waliiba wao wakafanyia kampeni
 
Sourse: francisgodwin.blogspot.com

'LIVE' KESI YA MWAKALEBELA MAHAKAMA NDOGO WANANCHI MJI MZIMA WATINGA MAHAKAMANI NA BARUA ZA DHAMANA


IMG_8712.JPG


Frederick Mwakalebela akiwa amezungukwa na umati wa wananchi wa jimbo la Iringa walioacha shughuli zao na kufika kusikiliza kesi yake

IMG_8742.JPG



Mahakama ya mkoa wa Iringa hapa hapatoshi ndani hakuna nafasi wengi wasikiliza kesi kwa nje

IMG_8751.JPG



IMG_8747.JPG


IMG_8728.JPG



IMG_8720.JPG




Wananchi wa jimbo la Iringa mjini wakiwa na barua za dhamana kwa Mwakalebela

IMG_8715.JPG


Ndani ya mahakama

IMG_8713.JPG


Ni vijana na wazee wajitokeza kumdhamini mahakimu wasema haijapata kutokea toka kuanzishwa kwa mahakama hiyo umati mkubwa kama huo kuja mahakamani kusikiliza kesi

IMG_8711.JPG




IMG_8707.JPG


Kwa sasa Mwakalebela amedhaminiwa kwa dhamana ya iliyosainiwa ya shilingi milioni 5 wadhamini wawili mahakama imekubali dhamana yake ,sasa kesi inayoendelea ni ya mke wake habari zaidi ndani ya gazeti la Tanzania Daima kesho ama katika mtandao wa Shwari dot com
 
Mwakalebela ni "outsider". Ajaribu tena mwaka 2015. Mwenzake Rage kule Tabora kimeeleweka!
 
Back
Top Bottom