Kuenguliwa kwa Mwakalebela kwasababisha vurugu Iringa

xfucyh.jpg


:becky::becky::becky: Imenikumbusha yule mkuu wa wilaya wa BK:becky::becky::becky: Check Lowasa alibana miguu MP anajuta ya nini alichakuguliwa kuongoza Serikali :becky::becky::becky:
 
Pesa za Tafuna Fedha Fasta(TFF) ndizo zilizomfikisha hapo,pole sana huku TFF Kayuni anabunya masele tuu!
 
Haya na tusubiri hiyo Oktoba 31 tuone matunda ya huo "Mji Mzima" kuandamana mahakamani,Mwaibula alijaribu lakini fitna za chama mwenyewe alichemka
 
Ile katuni imeniburudisha!!! Shurti viongozi waunge foleni wapate mboko. Haya ni matatizo ya cheap politics!!!
 
hapo ndipo panaponiacha hoi, lile jamaa halihojiwi, haliguswi wala halisogelewi na kina Kikwete, sijui anawafanyaga nini , kweli sielewi.

Kwa sababu lile lijamaa ni "King maker". Hawa vibaraka hawana jinsi isipokuwa kulipa fadhila tu. "Money talks".
 
xfucyh.jpg


:becky::becky::becky: Imenikumbusha yule mkuu wa wilaya wa BK:becky::becky::becky: Check Lowasa alibana miguu MP anajuta ya nini alichakuguliwa kuongoza Serikali :becky::becky::becky:

Siyo miguu tu amekinga sehemu nyeti kwa mikono utadhani kuna mpira wa adhabu unataka kupigwa.
 
Jamani lakini tuwe wakweli.

Huyu bwana kuna minong'ono imezagaa Iringa kwamba katika mchakato wa kura za maoni kamwaga rupia kiasi cha kutosha. Hoja kwamba wengine hawakukamatwa haina msingi mana huwezi tenda kosa kwa sababu tu wengine wanatenda na hawakamatwi.

Kama kweli ana nia ya kuleta mabadiliko basi ameshaharibu maana njia aliyotumia si sahihi. Kwani ameshatoa picha mbaya. Angeweza kuchukua mifano ya wana CCM wachache ambao licha ya chama kugubikwa na rushwa wao walisimama imara. Mfano mzuri ni Nape. Watu wote wa Ubungo wanakubali kuwa jamaa alikuwa si mtoaji.

Kwa hili kajitakia. Tumwombee Mungu yaishe vizuri ila yapaswa ajifunze.
 
Bora abaki kimyaa akianza kuongea atasukiwa zengwe pale TFF na kwanza alipeleka mipira ya misaada kwenye ligi ya Iringa
 
Acheni utani jamani. Na huyu naye ameshakuwa MPAMBANAJI wa rushwa? Du kazi ipo

tatizo wabongo tunasahau haraka sana, juzi hapa tulikuwa tunalalamikia TFF kwa kutosimamia vizuri michezo na pesa nyingi viongozi ndiyo walijineemesha (+mgao wa mapato ya uwanja mpya). Wachezaji wamekuwa wakilipwa kidogo sana au wanadhulumiwa kabisa. kambi za mazoezi zimekuwa zikidorora kisa hakuna pesa.
kabla ya kura za maoni kulikuwa na maelezo kuwa huyu bwana anamwaga misaada balaa kwa wanamicchezo wa pale Iringa
sasa tunatahamaki nini??????
na mbaya zaidi tunamwita mpambanaji jamani!!!!!!!!!!!!!
 
:becky::becky::becky:, nimecheka si kawaida - serikali yote imelala :becky::becky::becky:,

Hata wanao ku-'negotiate' mikataba huwa ndo zao. migodi ndo maana wanachukua dhahabu bure! Hiyo ndo Serikali itakayo ondoa umasikini Tz! :confused2:
 
Huu ndio mji mzima wa Iringa? Tupeni picha ya umati huo ama acheni propaganda zenu hapa.......

umeniwahi kaka yangu....
sijaona picha yamji mzima!!!anyway..tutajuaje kama hao wote wamekuja kwa ajili ya mwakalebela..tutajuaje kama dhamira zao ziko upande wa mwakalebela au wana sababu zingine??/ najua hapa nimetibua nyongo za watu ila tuache ekzajiresheni ...tupunguze ushabiki usio na tija
mix with yours
 
Mwakalebela ni "outsider". Ajaribu tena mwaka 2015. Mwenzake Rage kule Tabora kimeeleweka!

Chadema wangekuwa strategic haya ndio majimbo ya concentrate kwani probability ya kuyachukuwa ni kubwa!!
TAKE ADAVANTAGE OF THE DISGRUNTLED electorate.
 
ukisikia mtu unakuwa mateka, ndio huyu katibu mtendaji mstaafu wa TFF, hapa narudia tena anatakiwa kuwa mpole na kuwasaidia kwenye kampeni, ama sivyo watamaliza tukukukuru/ccm wana mikono mirefu saana , yaani hapa wakimwambia kata kulia yeye akate kona tu, kushota, simama nae asimame, maana kama mchangiaji moja alivyo sema wakimkosa hapo iringa watasema kule tff kumeonekana mapungufu haya na haya nk, na zaidi ya hapo mke wake yupo nae matataji, na sijui kwanini aliamua kuachia tff kwa sasa.
 
Back
Top Bottom