Hili ni suala nimekuwa najiuliza sana huko Tanzania. Tunaelewa kuwa Mwaka huu mwezi Oct kuna chaguzi za Serikali za mitaa yaani kuchagua wenyeviti wa Serikali za mitaa na wajumbe wao.
naona kuwa mpaka sasa hakuna msisimko wowote wa maandalizi kwa vyama vya siasa na hata Serikali kijumla kama maandalizi ya chini chini aliyoanza kwa uchaguzi mkuu mwakani october.
Ukisoma Katiba ya Tanzania , Ibara ya 146 (1) inazungumzia madhumuni ya kuepo ka serikali za Mitaa ni kupeleka madaraka kwa wananchi.
katiba inazungumzia vizuri sana umuhimu wa kuimarisha demokrasia hususan katika ngazi za mitaa na kuelekea kwenye serikali kuu.
nauliza kwanini chaguzi zake hazina mashamsham?
Nitapembua kutoka kwenye katiba ya tanzania umuhimu na uhalali wa Serikali za mitaa ukilinganisha na serikali kuu.
Nasriyah Saleh Al-Nahdi.
.Hakika ukiangalia katiba ya Tanzania Ibara ya 146 (2)(c) inasema malengo ya Serikali za mitaa ni kuimarisha demokrasia na kutumia demokrasia kuharakisha maendeleo ya wananchi.
Sasa utaona hapa ni sehemu muhimu sana kwa Serikali ikiwa pamoja na vyama vya siasa kuanza kujikita ili kujihakikishia ushindi katika uchaguzi mkuu.
Ingawa demokrasia yenyewe imepindishwa na Sheria namba 7 na namba 8 za mwaka 1982 zinazoipa Serikali kuu mamlaka ya kuunda au kuvunja serikali za mitaa bila kujadiliana na wananchi husika.
Mtu anaepewa mamlaka kisheria kuvunja Serikali za mitaa ni waziri wa TAMISEMI. hapo utaona Serikali kuu ndio yenye mamlaka ya kuunda serikali za mitaa na sio wananchi.
Sasa ni vizuri wabunge wetu huko Tanzania mkajikita katika kurekebisha katiba na kuupa uchaguzi huu wa serikali za mitaa chachu ja demokrasia na maendeleo ya nchi.
Nasriyah saleh Al-Nahdi
na sisi miafirika tumezidi ujinga ndio maana tunaongozwa na viongozi wapumbavuKuiondoa CCM madarakani tuna kazi kubwa Wananchi. Manake wanatumia kila mbinu (fedha, danganya toto, tume za uchaguzi nk) kubaki madarakani.