Kuelekea Uchaguzi Mkuu: Chama cha ACT-Wazalendo chapokea 21 waliokuwa Wabunge wa CUF

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
610
1,540
Salaam Wakuu,

Leo Muda si Mrefu, Viongozi Wakuu wa Chama cha ACT Wazalendo kitaongea na Wananchi na Dunia kwa Ujumla. Ni tukio kubwa haijawahi kutokea.
======

UPDATES:

1048HRS: Kwa sasa ni Burudani inaendelea

1100HRS: Viongozi Wakuu wa ACT Wazalendo wanaingia Ukumbini wakiongonzwa na

Zitto zuberi Kabwe- KIONGOZI WA CHAMA

Maalim Ssif Sharif Hamad- MWENYEKITI WA CHAMA.

ADO SHAIBU- KATIBU MKUU

JUMA DUNI HAJI-MAKAMU MWENYEKITI ZANZIBAR

DOROTHY SEMU- MAKAMU MWENYEKITI BARA

NASSOR AHMED MAZRUI-NAIBU KATIBU MKUU ZANZIBAR

JORAN LWEHABURA BASHANGE - NAIBU KATIBU MKUU BARA
1200hrs: Wabunge Waliohama CUF Wakabidhiwa kadi za ACT Wazalendo.

1215hrs: Webiro Wasira aka Wakazi, aka Beberu anapewa nafasi ya kusalimia. Anasema amekuwa aki0enda Sera, Misimamo ya Viongozi wa ACT Wazalendo. Uongozi bora ni Maarifa. Nashukuru ACT kwa kunialika kwenye Chama. Jimbo la Ukonga tulikabidhiwa kadi 126. Natangaza kutia nia Jimbo la Ukonga.

IMG_20200620_113336_064.jpg


1120hrs: Katibu Mkuu Ado Shaibu, anasimama kuelezea sababu ya WanaACT Kukutana hapa.

Ado: Hiki kinachotokea leo hakijawahi kutokea. Hii ya leo ni Kubwa kuliko. Leo tunapokea Ugeni mkubwa sana. Bunge limeshafika kamati. Leo chama chetu kitawapokea rasimi Waliokuwa Wabunge wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania 21. Ilishawahi kutokea hiyo?

Mbali na Wabunge, tutapokea Madiwani kutoka Dar. Tumeshapokea Madiwani Tanga. Walipokelewa na Maalim Seif. Leo tutawapa heshima Madiwani 9 kutoka chama cha wananchi CUF watakao jiunga nasisi.
Orodha ya Majina ya Wabunge na Madiwani waliojiunga ACT Wazalendo ni;

ORODHA YA WABUNGE, MADIWANI NA BAADHI YA WANACHAMA WASHUHURI WA CUF WANAOKABIDHIWA KADI ZA UANACHAMA WA ACT WAZALENDO LEO TAREHE 20, JUNI, 2020

1. Ndugu Suleiman S Bungara – Kilwa Kusini
2. Ndugu Juma Kombo Hamad – Jimbo la Wingwi
3. Ndugu Masoud Abdallah Salim – Jimbo la Mtambile
4. Ndugu Ally Saleh Ally Albator – Jimbo la Malindi
5. Ndugu Ali Salim Khamis - Jimbo la Mwanakwerekwe
6. Ndugu Hamad Salim Maalim – Jimbo la Kojani
7. Ndugu Khalifa Mohamed Issa – Jimbo la Mtambwe
8. Ndugu Mohamed Juma Khatib – Jimbo la Chonga
9. Ndugu Twahir Awesu Mohamed – Jimbo la Mkoani
10. Ndugu Khatib Said Haji – Jimbo la Konde
11. Ndugu Haji Khatib Kai – Jimbo la Micheweni
12. Ndugu Othman Omar Haji – Jimbo la Gando
13. Ndugu Dr. Suleiman Ali Yussuf - Jimbo la Mgogoni
14. Ndugu Mbarouk Salim Ali – Jimbo la Wete
15. Ndugu Nassor Suleiman Omar – Jimbo la Ziwani
16. Ndugu Yussuf Salim Hussein – Jimbo la Chambani
17. Abdallah Haji Ali – Jimbo la Kiwani
18. Ndugu Yussuf Haji Khamis – Jimbo la Nungwi
19. Ndugu Mohamed Amour Mohamed Jimbo la Bumbwini
20. Ndugu Mgeni Jadi Kadika – Mbunge Viti Maalum

MADIWANI WA DAR ES SALAAM
1. Ndugu Ramadhan Kwangaya – Manzese
2. Ndugu Jumanne Amir Mbunju – Tandale
3. Ndugu Ali Haroub Mohamed – Makumbusho
4. Ndugu Omar Thabiti (Kijiko) – Makurumla
5. Ndugu Jumanne Kassim Kambangwa – Mbagala
6. Ndugu Abdul Ali Matogoro – Azimio
7. Ndugu Abdalah Omar Kipende – Mianzini
8. Ndugu Haijat Safina Mgumba – Viti Maalum, Ilala
9. Ndugu Leila Hussein Madibi – Viti Maalum, Ubungo

1223hrs: Maalim Seif anaongea.

Karibuni sana. Chama hiki hakina Waasisi, Wote ninyi ni Waasisi. Wabunge hawa na Madiwani Walikuwa CIF lakini moyo wao upo ACT Wazalendo. CUF wanawaita eti ni Wasaliti. Hawa sio Wasaliti. Na leo Bwana yule sijui kama atalala. Tumewaachia chama chao. Miezi 18 sasa kila bwana yule akisimama ni Maalim Seif Maalim Seif.. Nashangaa sana.. Maalim Seif yupo ACT Wazalendo ametulia kwa raha Mstarehe.

Bwana yule muulizeni, kakaa siku ngapi Pemba na nani Wamempata? Hawa wana haki kugombea popote. Kamati kuu kesho itakutana. Taratibu zote kuanzia uchukuaji fomu hadi kura za maoni, utaratibu utatolewa baada ya kikao cha kamati kuu. Jumatatu utaratibu utaratibu.

Kila mtia nia aache lugha ya kuwakashifu wenzake. Alete ajenda yake.

Pili hatitaki mtumie majina yetu. Kiongozi hana Mgombea. Viongozi wa ACT hawana Mgpmbea. Sisi ACT Wazalendo Wananchi wetu wana haki sawa. Na ukisema Kiongozi fulani wa chama ndo kanituma nigombee utakua umepoteza sifa. Mimi ndowenyekiti nasema.

La tatu hatutaki mitindo ya Rushwa kwemye chama chetu. Naamini Vijana wa Amani wataniletea taarifa. Wakisema fulani ametoa rushwa, tayari unakuwa umepoteza mya. Wagombea mnatakiwa mubehave.

Mimo kazi yangu ilikuwa kukaribisha wageni. Tumekusudia kuongia kwemye uchaguzi, hatuendi kushiriki, tunakwenda kushinda. Kila mmoja wetu hilo aweke mbele. Sisi sio chama sindikiza bali chama cha Ushindi sababu tuna viongozi wazuri.

Waongoza Dola wameshindwa kuongoza Nchi.

Wanasema fly overs, ndege, sijui nini.. yote sawa. Lakini wameenda kuwaona wananchi wanaishi vipi?

Namsikia Magufuli eti Uchaguzi utakuwa huru na haki? Haya ni maneno tu. Utakuwaje hiri na haki kwa Tume hii aliyoichagua yeye? Vyombo vya Ulinzi vina damu ya CCM, Wakurugenzi wote wanatishwa. Sawa sawa?

Zanzibar wamezoea kutuibia.. Hiyo sasa ni Historia. Mara hii Chini ya kiongozi Zitto Kabwe, hamtunyang'any ng'o. CCM wamepoteza Mvuto. Sasa hivi wananchi wanakunywa chai maji matupu. Sasa imetosha. Kama ni noma na iwe noma. Bara mtusaidie Zanzibar mara hii. Wao wanasema Maalim ana huruma sijui nini. Huruma nmeitia mfukoni sawa sawa?

Msubiri tarehe 28 Msikie maumuzi yangu ni yapi. Kila mtu Insha'Allah atayapenda. Sawa sawa?

1250 Zitto Kabwe anaongea kwa kusema.

Viongozi wenu tunatambua kwamba Watanzania wanataka Mabadiliko. Na sisi tumejiandaa kwa njia zote kuhakikisha kwamba Wananchi wanapata mabadiliko.

Nchi yetu inahitaji Sera itainua uchumi

Nchi yetu inahitaji Katiba Mpya

Nchi yetu inataka usawa kuhusu Muungano. Sisi tutafanya hilo.

Mwenyekiti wetu kashasema tarehe 28 atatuambia kitu.

Mimi nmechaguliwa na Wanakigoma Mjino, lazima niende kushairiana nao. Ukitaka kuruka unaagana na nyongo. Nyonga yangu ipo Kigoma. Naamini watatupa ishauri mzuri wa kuibadilisha nchi yetu.

Kutokana na kukubalika kwa ACT Wazalendo, Magwiji hawa wabunge 21 wameamua kujiunga nasi chama kinachokua kwa kasi zaidi kuliko chama chochote pamoja na kwamba kulikuwepo na maswala ya kuunga juhidi.

HOTUBA YA ZITTO KABWE...

HOTUBA YA NDG. ZITTO KABWE, KIONGOZI WA CHAMA CHA ACT-WAZALENDO KATIKA HAFLA YA KUPOKEA WANACHAMA WAPYA WALIOKUWA WABUNGE WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, DAR ES SALAAM, TAREHE 20 JUNI, 2020.

Ndugu Viongozi waandamizi wa ACT Wazalendo;
Ndugu Wanachama wenzangu wa ACT Wazalendo;
Ndugu Wanahabari;
Mabibi na Mabwana;
Assalaam Alleykum!

UTANGULIZI
Ndugu zangu;
Leo ni siku ya furaha sana kwetu sisi wana ACT- Wazalendo, ni siku ambayo jitihada zetu za kujenga Chama imara, mbadala na kimbilio la wapenda demokrasia zimeanza kuzaa matunda!.

Zikiwa ni siku chache baada ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuvunjwa na siku chache baada ya kuwa tumempokea Mwamba wa Kusini Mheshimiwa Suleiman Bungara, almaarufu Bwege, na pia kumpokea msanii maarufu wa kizazi kipya, Ndugu yetu Wakazi, leo tunakutana kuwapokea waliokuwa Waheshimiwa Wabunge 20 katika Bunge lililovunjwa hivi karibuni.

Hii ni heshma kubwa kwa Chama chetu na uthibitisho kwamba Chama chetu kinazidi kuimarika, kuaminika na kushamiri miongoni mwa wapenda maendeleo wa nchi hii. Kutokana na kukubalika kwa ACT Wazalendo, magwiji wengine 20 tena waliokuwa Wabunge katika kipindi ambacho tulishuhudia baadhi ya Wabunge wakiuza utu wao na imani waliyopewa na wananchi, kwa kile kilichoitwa kuunga mkono juhudi wameamua kujiunga nasi katika Chama kinachokua kwa kasi kuliko vyama vingine vyote hapa nchini, Chama cha ACT Wazalendo.

Kwa niaba ya Wanachama wenzangu, ninawashukuru sana kwa imani kubwa mliyoionesha kwa Chama chetu na kuwakaribisha sana kwenye Mabadiliko ya kweli!.Karibuni sana, na Kazi Iendelee!

KWA NINI TUMEWAPOKEA?
Ndugu zangu;

Pengine mnajiuliza kwa nini imekuwa rahisi kuwapokea wanachama hawa wapya. Jibu ni rahisi sana, kwanza, Chama chetu kiko wazi kwa kila Mtanzania mwenye nia njema na nchi yetu kujiunga nasi; pili, wanachama hawa wapya kama walivyo Watanzania wengine wengiwamekuwa nasi bega kwa bega wakati wote bila hata kuwa Wanachama rasmi; tatu hawa ni miongoni mwa Wabunge makini walioendelea kusimama imara kusemea kero za wananchi na hivyo kuongeza sauti ya ACT Wazalendo Bungeni katika kupambania haki za kiraia na haki za kiuchumi kwa wananchi wote.

Baada ya kujiridhisha na mwenendo wa Chama chetu, umadhubuti wa Sera zetu katika kuleta mabadiliko ya kweli na ukuaji wa kasi wa chama chetu, ndugu zetu hawa, wameona huu ni wakati muafaka wa kujiunga Rasmi na Chama kinachokua kwa kasi kubwa nchini na kilichojipatia ukubalifu mkubwa miongoni mwa makundi mbalimbali ya kijamii.

Ninapenda kutumia fursa hii kuwakaribisha watu wote wenye mapenzi mema na nchi hii kujiunga na ACT Wazalendo na kuiunga mkono katika harakati zake za kuirudisha nchi kwenye misingi iliyoasisiwa na waasisi wa Taifa hili.

JUKUMU KUU MBELE YETU
Ndugu wanachama wetu wapya,

Baada ya kujiunga rasmi na ACT Wazalendo, mko huru na mnazo haki zote kama mwana ACT Wazalendo mwingine yoyote. Kwetu hakuna mwenye Chama! Hiki ni chama cha wanachama wote na ni chama cha umma wote wa Watanzania.

Hivyo, kuanzia leo, mnalo jukumu moja kubwa, nalo ni kuhakikisha tunashinda uchaguzi wa Rais wa Zanzibar na tunaulinda na kuhami ushindi wetu. Vilevile, tunalo jukumu la kuhakikisha tunang’oa mizizi ya chama katili na dhalimu nchini mwetu kwa kushinda uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na viti vingi vya Ubunge, na hivyo kuunda Serikali ya Jamhuri ya Muungano ili kuleta furaha kwa Watanzania.

MATUMAINI MAKUBWA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU
Ndugu wananchi;

Tunazo sababu nyIngi za kujivunia waliokuwa wabunge kujiunga na ACT Wazalendo na bado milango ipo wazi kwa wanaotaka kujiunga kwenye jukwaa la uhakika wa mabadiliko. Tunajivunia Wabunge ambao walitumia muda wao kufanya kazi ya kuisimamia Serikali na kutaka mabadiliko ya muundo wa Muungano ili Tanzania iwe na Muungano ulio sawa, wa haki na kuheshimiana.

Licha ya kwamba walikuwa wanaisimamia Serikali tukutu, isiyosikia na isiyojali, lakini wanao uzoefu mkubwa wa kukabiliana na mikingamo, dhoruba na mapito mazito. Ni watu wasioyumba na ambao walidharau ukandarasi wa kununua utu wa watu kwa kinachoitwa kuunga mkono juhudi!.Tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu wa kihistoria, tukiwa na watu wa aina hii, tunaingia kwenye uchaguzi tukiwa na matumaini makubwa sana, na tunakuombeni Watanzania mtuunge mkono!.

Wabunge hawa wastaafu wanahitajika zaidi katika miaka mitano ijayo ambapo mambo ya msingi ya Muungano ambayo hayaleti usawa, haki na kuheshimiana vinatakiwa kuzikwa kwenye kaburi la sahau. Ni miaka mitano ya kuunda Serikali Mpya ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Zanzibar zitakazosimamia uundwaji wa Tume ya Pamoja ya Fedha za Muungano, kuondoa unyonyaji, ukandamizwaji na kudogoshwa kwa sehemu moja ya Muungano.Ni miaka ya kuirudisha nchi kwenye misingi!.

Sina mashaka, wanachama wetu hawa wapya na wengine watakaojiunga hivi karibuni wataendeleza ukali wa hoja hizi wakiwa ACT Wazalendo na kwa uwezo wake Mola mwaka huu tutakapounda Serikali zote mbili tutaanza hatua muhimu ya kurekebisha muundo wa Muungano na kufanya maboresho makubwa ya kiuchumi.

KAZI NA BATA DHIDI YA KAZI TU!

Ndugu zangu, Watanzania wenzangu;

Baada ya uchaguzi wa mwaka 2020 sisi ACT Wazalendo tumedhamiria kuijenga Tanzania inayopaa kiuchumi yenye maisha ya raha na furaha kwa watu wetu wote, tukibuni na kutekeleza sera zitakazohakikisha Uchumi Shirikishi unaozalisha AJIRA.

Chama chetu kitaongoza Serikali zitakazovutia uwekezaji kutoka nje (FDI) ili kuongeza mitaji nchini na kupanua shughuli za uzalishaji mali. Tumekusudia kuongoza Serikali zitakazotumia nafasi yetu ya Kijiografia ya kuzungukwa na nchi nyingi zisizo na bahari kufaidika kiuchumi na kuhudumia nchi nyengine kwa kuifanya Tanzania kuwa Kituo Kikuu cha Usafirishaji na Biashara katika eneo la Maziwa Makuu.

Tutawekeza zaidi kwenye shughuli za wananchi wengi, haususan Kilimo kwa kuongeza eneo linalotumika kwa kilimo cha umwagiliaji, uvuvi na ufugaji, lengo la yote haya likiwa ni kuongeza shughuli za kiuchumi kwa watu. Uchumi wa watu ndio unaojenga Taifa imara na sio Uchumi wa Serikali. ACT Wazalendo inataka kujenga Uchumi wa WANANCHI kupitia Vyama vya Ushirika, Jumuiya za Wafanyabishara na Vyama vya Wafanyakazi.

Tanzania itakayoongozwa na ACT Wazalendo baada ya Oktoba mwaka huu, itakuwa ni Tanzania yenye huduma bora za kijamii, tukitoa elimu bora na inayokwenda na wakati, inayozalisha wahitimu wenye weledi, ubunifu na uwezo katika nyakati hizi za Sayansi na Teknolojia, Tanzania yenye wakufunzi wa kutosha, madarasa na vitendea kazi, huku mkazo ukiwekwa zaidi kwenye elimu ya ufundi.

Lengo letu ni kuwa na huduma bora na nafuu za afya, inayojikita kwenye kuwakinga na kuwatibu wananchi, kwa kuwa na Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali za kutosha, zenye watendaji wenye sifa, vitendea kazi na vifaa tiba vya kutosha. Huduma ya uhakika ya maji safi na salama ikiwa ni kipaumbele chetu ili kupunguza maradhi yatokanayo na matumizi ya maji yasiyo salama (ambayo hugharimu nusu ya Bajeti ya Dawa nchini).

Tutajenga mifumo imara ya utoaji haki nchini (Justice System) kwa kujenga uwezo wa kupambana na rushwa kwa haki na si kwa kukomoa, kuhakikisha watu wote walioonewa katika kipindi cha miaka hii mitano kwa kubambikiwa kesi kwanza wanaachiwa huru, na wale waliohukumiwa adhabu mbalimbali wakifutiwa rekodi zao za adhabu na uhalifu wasioutenda. Kwa kiasi kikubwa Tanzania hiyo ya ndoto yetu ACT Wazalendo ndiyo mahitaji ya Wananchi wengi - Tanzania yenye MAISHA ya RAHA na FURAHA (Yaani #KaziNaBata).


SABABU ZA KUKING’OA CHAMA KATILI NA DHALIMU
Ndugu zangu;

Miaka mitano tunayoimaliza ni miaka mitano ya ukandamizaji, unyanyasaji, ukatili, chuki na umasikini mkubwa wa Wananchi. Ni miaka mitano ambayo Wananchi wamekuwa na maisha magumu kwa ujumla.

Wakulima wameshuhudia kipato chao kikianguka,; wavuvi wakiharibiwa nyenzo zao za kazi; Wafugaji wakiondolewa kwa nguvu maeneo ya malisho ya mifugo yao, Wafanyakazi wakinyimwa nyongeza halali na za kisheria za mishahara yao; Wafanyabiashara wakilazimika kufunga au kuhamisha biashara zao, Waandishi wa habari wakipotea, wakifungwa jela kwa kubambikiwa kesi na vyombo vyao vya habari kufungiwa na Wanasiasa wa vyama vya upinzani wakihamishia ofisi zao kwenye korido za mahakama, jela au hospitalini..

Ni miaka mitano ya mateso makubwa ambayo yamewajaza wananchi wengi hasira na tafrani muda mwingi. Ni wajibu wetu kurejesha nyuso za furaha kwa Wananchi hawa kwa kuunda Serikali itakayojenga Tanzania inayopaa na yenye Watu wenye Raha na Furaha. Tunazo sababu zaidi ya elfu moja za kuing’oa CCM, na kwa hakika CCM ni lazima ing’oke ili nchi irudi katika misingi.

Tulipokuwa tunakusanya maoni kwa ajili ya kuandika Ilani yetu ya Uchaguzi ya mwaka 2020 tulikutana na Wananchi katika shughuli zao za kila siku. Siku moja tulikwenda kukutana na wauza madafu mtaani. Walitueleza kuwa kabla ya Serikali ya Awamu ya Tano kuingia madarakani muuzaji mmoja alikuwa anaweza kutembea mji mzima kwa siku na kuuza madafu ya wastani wa shilingi 80,000 yaani madafu 80. Tangu mwaka 2017 siku akiuza madafu 20, yaani shilingi 20,000 ni siku ya bahati sana. Mnaweza kuona namna ambavyo Sera mbovu zinazominya uchumi wa watu wa kati zinavyoweza kuathiri mwananchi wa chini kabisa.

Ninafahamu kwamba, Serikali ya CCM imebobea kwa ulaghai na uongo, tunatambua takwimu zao za kubumba zilizotolewa juzi wakati wa kuahirisha Bunge, tunao uchambuzi makini na wakati wa kampeni za uchaguzi tutauanika hadharani, ili wananchi wajiridhishe zaidi kwamba CCM haistahili kuongezewa hata siku moja kuongoza Tanzania.

HITIMISHO
Nihitimishe kwa kuwashukuru tena Waheshimiwa Wabunge wastaafu, ambao tuna imani miezi michache ijayo watarudi Bungeni kwa kishindo chini ya Serikali ya Muungano na Serikali ya Zanzibar zitakazokuwa zinaongozwa na ACT Wazalendo.

Ninawakaribisha wanachama wetu wapya na ninawahakikishia ushirikiano mkubwa katika kuhakikisha kuwa tunaleta MABADILIKO YA UHAKIKA kwa Watanzania. Watanzania wanataka Mabadiliko, ni Wajibu wetu kuwapa mabadiliko.

Asanteni sana na Karibuni sana Uzalendoni!

1315hrs: Mwisho na Viongozi wanatoka nje ya Ukumbi. Asanteni

======


Hapa chini ni picha ya wabunge na Madiwani waliojiunga ACT Wazalendo
IMG-20200620-WA0006.jpg
IMG-20200620-WA0008.jpg

4D1C3155-5D34-4960-8B79-D005DFF48C6D.jpeg




Lakini pia wapo Wanasiasa Mashauri watapata kadi leo. Hilo ndio limetukutanisha hapa.

Baada ya hapo, Viongozi wetu watapata nafasi ya kuhutubia Taifa.

IMG_20200620_112902_852.jpg

IMG_20200620_105056_405.jpg
IMG_20200620_105216_043.jpg
IMG_20200620_105248_763.jpg
 
Salaam Wakuu,

Leo Muda si Mrefu, Viongozi Wakuu wa Chama cha ACT Wazalendo wataongea na Wananchi na Dunia kwa Ujumla. Ni tukio kubwa haijawahi kutokea.

Nipo hapa kuwaletea kila kitakachojiri.

Stay tuned..

======

UPDATES;

1048HRS: Kwa sasa ni Burudani inaendelea

1100HRS: Viongozi Wakuu wa ACT Wazalendo wanaingia Ukumbini.
View attachment 1484010View attachment 1484011View attachment 1484012View attachment 1484013
View attachment 1484006
Ukumbi unavutia! Wameupamba vizuri! Tunasubiri yajayo
 
Wabunge 21 wa Viti Maalum au Majimbo?!

Hawa jamaa kwa upande wa Visiwani wako vizuri, ila huku Bara wanatakiwa kufanya jambo na "wenzao"..

Hao jamaa walimtapeli Lipumba.
 
Wabunge 21 wa Viti Maalum au Majimbo?!

Hawa jamaa kwa upande wa Visiwani wako vizuri, ila huku Bara wanatakiwa kufanya jambo na "wenzao"..
Tatizo ni wale "wenzao" wanajiona wapo vizuri ilihali wapo na hali mbaya. Niliwahi shauri humu hawa waungane na wale wenzao kwa maana hawa wapo vizuri zenji wale wenzao wapo vizuri bara sasa muungano wao utakuwa na matokeo chanya kwenye siasa za upinzani Tanzania.
 
TAARIFA LULU: Aliyekuwa Mbunge wa Malindi Ally Saleh na wabunge wenzake jumla 21 akiwemo Selemani Bungara Said "Bwege" wametangaza kuhamia ACT wazalendo kutoka CUF.

Wanapokelewa muda huu na Kiongozi wa Chama Zitto Kabwe na M/kiti Seif Sharif Hamad Lamada Hotel, Dar.

ACTwazalendo
IMG_20200620_114852.jpg
IMG_20200620_114745.jpg
 
Tatizo ni wale "wenzao" wanajiona wapo vizuri ilihali wapo na hali mbaya. Niliwahi shauri humu hawa waungane na wale wenzao kwa maana hawa wapo vizuri zenji wale wenzao wapo vizuri bara sasa muungano wao utakuwa na matokeo chanya kwenye siasa za upinzani Tanzania.
Muda bado upo tutulie tuone.
 
Salaam Wakuu,

Leo Muda si Mrefu, Viongozi Wakuu wa Chama cha ACT Wazalendo kitaongea na Wananchi na Dunia kwa Ujumla. Ni tukio kubwa haijawahi kutokea.
======

UPDATES:

1048HRS: Kwa sasa ni Burudani inaendelea

1100HRS: Viongozi Wakuu wa ACT Wazalendo wanaingia Ukumbini wakiongonzwa na

Zitto zuberi Kabwe- KIONGOZI WA CHAMA

Maalim Ssif Sharif Hamad- MWENYEKITI WA CHAMA.

ADO SHAIBU- KATIBU MKUU

JUMA DUNI HAJI-MAKAMU MWENYEKITI ZANZIBAR

DOROTHY SEMU- MAKAMU MWENYEKITI BARA

NASSOR AHMED MAZRUI-NAIBU KATIBU MKUU ZANZIBAR

JORAN LWEHABURA BASHANGE - NAIBU KATIBU MKUU BARA

View attachment 1484037

1120hrs: Katibu Mkuu Ado Shaibu, anasimama kuelezea sababu ya WanaACT Kukutana hapa.

Ado: Hiki kinachotokea leo hakijawahi kutokea. Hii ya leo ni Kubwa kuliko. Leo tunapokea Ugeni mkubwa sana. Bunge limeshafika kamati. Leo chama chetu kitawapokea rasimi Waliokuwa Wabunge wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania 21. Ilishawahi kutokea hiyo?

Mbali na Wabunge, tutapokea Madiwani kutoka Dar. Tumeshapokea Madiwani Tanga. Walipokelewa na Maalim Seif. Leo tutawapa heshima Madiwani 9 kutoka chama cha wananchi CUF watakao jiunga nasisi.

View attachment 1484060



Lakini pia wapo Wanasiasa Mashauri watapata kadi leo. Hilo ndio limetukutanisha hapa.

Baada ya hapo, Viongozi wetu watapata nafasi ya kuhutubia Taifa.

View attachment 1484033
View attachment 1484010View attachment 1484012View attachment 1484013
Siasa za nchi hii zimekosa mwelekeo kabisa kupokea wanachama wapya linageuka kuwa tukio la kitaifa na la kutangazia dunia.

Dah hapa ndipo tulipofika
 
Back
Top Bottom