Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Status
Not open for further replies.
Ikiwa ndo kweli mhe. anampango huo ni vema na haki yake kufanya hivyo. Nikimlinganisha zitto na baadhi wanasiasa tulionao na wengine wenye nyadhifa kubwa kuliko yeye (wengine wameshatajwa hapa), naona huyu ana afadhali na hivyo sipati shaka yoyote kwamba madaraka yatamlemea.
 
Zitto alichemka sana katika suala la Dowans.ni mapema sana kumkabidhi mikoba ya kukiongoza chama hasa tukizingatia umri na kuyumba yumba katika masula muhimu ya kitaifa.

Bwana Zitto pia alikuwa kioja katika suala la EAC alitofautiana na asilimia kubwa ya watanzania waliokataa kuharakishwa uundwaji wa shirikisho la Afrika mashariki.Kumpatia majukumu makubwa ni sawa na kumwangamiza kisiasa.Bwana mdogo bado anatakiwa kujifunza ili aweze kuja kuwa kiongozi bora.

Bwana Zitto alishatutangazia kwamba hatatetea kiti cha ubunge lakini baadae akabadili mawazo.Kwa maoni yangu nadhani huko ni kukosa msimamo na inaonyesha dogo ni mwanasiasa asiyekuwa na msimamo hii dosari kubwa sana kwa mtu tuanyetaka aje akiongoze chama.

Kwa maoni yangu nadhani Zitto anatakiwa abakie na nafasi yake ya ubunge tu,hafai kabisa kuongoza chama makini.
 
Zitto amekuwa shupavu sana katika mambo mengi kitaifa na katika siasa za Tanzania. Ameweza kuamsha hisia na hamasa mbali mbali kwa Watanzania na pia kuweza kushiriki vyema sana pamoja na washirika wenzake kuiinua CHADEMA na kuifikisha ilipo. Nampa pongezi sana kwa hili.

Kwa kiasi kikubwa sana, sina wasiwasi na uwezo wa Kabwe kukiendesha chama hata kufikia katika nafasi ya juu zaidi, kwanza ni msomi, mwenye kupenda kujifunza (hasa kwa kujisomea, kushirikia katika tafiti n.k), ameonyesha kuwa na uchungu na nchi, ana msimamo usio yumba na anajiamini vya kutosha.

Nafasi ya mwenyekiti ni nafasi nzito na ambayo wakati mwingine inabidi kutumia rungu la mwenyekiti. Hapa ndipo panapoleta shaka kidogo. Kwa maoni yangu namuona Zitto katika nafasi ya utendaji kwa sasa (Katibu Mkuu) kuliko kuwa mwenyekiti. Pamoja na kuwa mwenyekiti anapaswa kuwa na maamuzi na msimamo, lakini pia anatakiwa kuwa msikivu na mwenye kupokea pia mawazo ya upande wa pili kabla ya kuhitimisha, kidogo ule msimamo wake kwa Dowans, unanifanya nione kuwa anahitaji muda kidogo kuweza kukomaa kidogo ndipo awezekabidhiwa kiti cha M/Kiti. Sina maana kuwa yeye ni dhaifu kuliko watakaogombea/au wananaomaliza muda wao, ila wajipime ndani ya chama na kijiridhisha kuwa nani anafaa, hasa tukizingatia changamoto zilizopo.
 
Basi wasifanya uchaguzi kama ndo hivi, Zitto atatumiwa na MAFISADI hajakomaa kumbuka sakata la DOWANS
kukomaa kukojeeee?? kijana ana uwezo mkubwa tuu na ndani ya CHADEMA demokrasiaa ina nafasi zaidi kulikoo hisiaa na mitazamoo dume. Good move zitto.
 
naunga mkono kukomaa ndo nini Histori imetuonyewa wale waliokoma ndio mzizi wa ufisadi so hakuna maana sana
Twendwe kazi ZItto.
Lakini kwa mtazamo wangu mchango wake akiwa bungeni ni mkubwa kwa kitaifa kwa ujumla
Akiwa kwenye kiti wa chama mchango wake uta kuwa mkubwa kwa chama hakuna shaka katika hilo lakini namashaka kwa Taifa kama utakumkubwa tena.
 
Hawawezi kumpa MUISLAM dont fool yourself.

Itawaudhi lakini ndio ukweli wenyewe huo, haya njooni na jazba zenu sasa
 
kugombea ama kutogombea ni uamuzi wa zitto mwenyewe..na wote tunafahamu umuhimu na nafasi ya zitto katika harakati za kuinua upinzani ulioonyesha kudorola..na katika masuala ya misimamo kila mtu anapaswa kuwa na misimamo yake na kuisimamia...so kama anania hiyo tumuombee mungu.
 
Hawawezi kumpa MUISLAM dont fool yourself.

Itawaudhi lakini ndio ukweli wenyewe huo, haya njooni na jazba zenu sasa

Ohh, this is too low my brother/sister. Mbona sote tu wamoja tu. Sote tu waTanzania kabla ya kuwa waislamu au wakristo. Ingekuwa bora kama waarabu na wazungu hawakutuletea dini zao, kwani hakukuwahi kuwa na ugomvi ndani ya wale wanaoamini dini zao za asili.
 
HawawezHawawezi kumpa MUISLAM dont fool yourself.

acha kuongea vitu vya kufikirika wewe...aliekwambia chama kile ni cha wakiristo ni nani....hizi dini wala zisitake kuwagawa watanzania zimeletwa ili ziwatawale..its enough so tuamke sote sisi ni wabongo na ni wamoja...kama zitto anauwezo basi mwacheni atambe tatizo nini wajameni?
 
Zitto alichemka sana katika suala la Dowans.ni mapema sana kumkabidhi mikoba ya kukiongoza chama hasa tukizingatia umri na kuyumba yumba katika masula muhimu ya kitaifa.

Bwana Zitto pia alikuwa kioja katika suala la EAC alitofautiana na asilimia kubwa ya watanzania waliokataa kuharakishwa uundwaji wa shirikisho la Afrika mashariki.Kumpatia majukumu makubwa ni sawa na kumwangamiza kisiasa.Bwana mdogo bado anatakiwa kujifunza ili aweze kuja kuwa kiongozi bora.

Bwana Zitto alishatutangazia kwamba hatatetea kiti cha ubunge lakini baadae akabadili mawazo.Kwa maoni yangu nadhani huko ni kukosa msimamo na inaonyesha dogo ni mwanasiasa asiyekuwa na msimamo hii dosari kubwa sana kwa mtu tuanyetaka aje akiongoze chama.

Kwa maoni yangu nadhani Zitto anatakiwa abakie na nafasi yake ya ubunge tu,hafai kabisa kuongoza chama makini.

hatuwezi kumpima kiongozi bora kwa masuala ya kimaamuzi na ya kimsimamo na hasa yanayohitaji utaalamu..kesi ya dowans ilikuwa ni kesi kati ya uchumi,sheria na siasa kwa mantiki hiyo kamwe pasingeweza kupatikana suluhu katika pande hizo...alichokifanya zitto ni kuonyesha msimamo wake katika nyanja ya kiuchumi wakati watu fulani wao walisimamia mahitaji yao ya kisiasa....so aina ya viongozi wakina zitto wanaoweza kusimamia misimamo ayo bila ya kutetereka dnio tunao wahitaji kwa ujenzi wa taifa imara...
 
Zitto alichemka sana katika suala la Dowans.ni mapema sana kumkabidhi mikoba ya kukiongoza chama hasa tukizingatia umri na kuyumba yumba katika masula muhimu ya kitaifa.

Bwana Zitto pia alikuwa kioja katika suala la EAC alitofautiana na asilimia kubwa ya watanzania waliokataa kuharakishwa uundwaji wa shirikisho la Afrika mashariki.Kumpatia majukumu makubwa ni sawa na kumwangamiza kisiasa.Bwana mdogo bado anatakiwa kujifunza ili aweze kuja kuwa kiongozi bora.

Bwana Zitto alishatutangazia kwamba hatatetea kiti cha ubunge lakini baadae akabadili mawazo.Kwa maoni yangu nadhani huko ni kukosa msimamo na inaonyesha dogo ni mwanasiasa asiyekuwa na msimamo hii dosari kubwa sana kwa mtu tuanyetaka aje akiongoze chama.

Kwa maoni yangu nadhani Zitto anatakiwa abakie na nafasi yake ya ubunge tu,hafai kabisa kuongoza chama makini.

Tufike mahala watu watendewe haki kama watu .Zitto alitoa maoni yake kama Zitto na si mwanakamati .Ana mambo yake yeye kama Zitto ana yaamini kama alivyo toa maoni Prof.Wangwe .Dowans na EAC maoni binafsi kama Zitto je nalo hili asiwe na hali nalo ?
 
Hawa ndiyo viongozi tunaowahitaji Tanzania sasa hivi kama tunataka maendeleo ya nchi yetu. Kukomaa kisiasa kunakozungumziwa kunajionyesha sana pale ambapo watu kama kina Kingunge na familia zao wanakuwa wamekamata vitu muhimu kama kituo cha mabasi wakijineemesha tu na kusiwe na mtu wa kuwauliza. Huo ni ukiritimba ambao unahitaji kushughulikiwa. Na kina Zitto ndiyo watakaotusaidia. Wapo washauri watakaokuwa tayari kusaidiana naye.
 
Hawawezi kumpa MUISLAM dont fool yourself.

Itawaudhi lakini ndio ukweli wenyewe huo, haya njooni na jazba zenu sasa
Tunashukuru kwa kutuonyesha sura yako, kama ulidhani kuwa utaweza kugeuza mjadala, jua kuwa watu wamekugundua na wala hakuna atakayekufuata huko unakotaka tuelekee
 
If you wanna go Zitto you have my blessings.Nitapenda kuona yafuatayo kama itawezekana .Chadema ni cahama makini na tumaini la Watazania
Mwenyekiti wa Chama agombee Ubunge , na kartibu mkuu agombee Ubunge , na mtu mwingine ambaye si Mwenyeliti wa Chama agombee Urais .Kuna shida kubwa ndani CCM sote tunaona kudhania kwamba ukiwa mwenyekiti basi lazima ugombee Urais nk .Na mambo ya lofi za Chama na serikali yanaleta shida .Nitafuahi kama hili litatokea ndani ya Chadema ndiyo uwe mwanzo wa kujionyesha kwamba Chadema ni makini .
 
bado hajakomaa kisiasa. anahitaji muda kidogo kujijenga kisiasa.

Zitto uwe na subra.

Hivi nini maana haswa ya mtu kukomaa kisiasa?? Kuweza kuwadanganya sana wananchi kwa muda mrefu au nini??
nadhani watanzania tunatakiwa tukomae kimawazo zaidi.
Kumbuka enzi za Kijana Jeryy Rawlings wa Ghana alipochukua madaraka.
Matokeo ya uongozi wake ndiyo ukomavu wa demokrasia kule Ghana leo hii! Anaheshimika kule Accra anatembea anavyotaka bila woga ndani ya nchi yake. Mkapa alikomaa sana tena alifundishwa na Mwalimu Nyerere, akawa mwandishi wa Raisi Nyerere, akawa Waziri wa Mambo ya nje, Umoja wa Mataifa, Halafu akakomaaaaa! Ndiyo hivyoooo alivyokomaa!! Anaendelea kuikomaza NEC na CC pamoja na Kingunge wake. Is this what we need in Tanzania???
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom