Kuelekea Mkutano Mkuu wa Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF), Waziri Bashe aelezea msimamo wa Serikali kuhusu GMO

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Mkutano huu unafanyika kwenye Ukumbi wa Ikulu ya Magogoni Dar es Salaam ukishirikisha Wadau mbalimbali wa Kilimo, leo Jumapili Septemba 3, 2023.
Snapinsta.app_374763554_18205151326258462_8218895830700188430_n_1080.jpg

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Zuhura Yunus akizungumza na Viongozi pamoja na Wahariri kutoka Vyombo mbalimbali vya Habari kuhusiana na Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF-Afrika Food Systems Summit 2023), Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 03 Septemba, 2023.

photo_2023-09-03_09-12-59.jpg

Zuhura Yunus (Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu)
Mkutano huo ni Jukwaa linalowakutanisha Wadau mbalimbali, unatarajiwa kuhudhuriwa na watu 3,000 kutoka katika mataifa zaidi ya 70 wakiwemo Wakuu wa Nchi, watunga sera na wawekezaji, ambapo utafanyika kwa siku tatu, Septemba 5 hadi 8, 2023.

Tanzania ni mwenyeji kuelekea Mkutano utakaofanyika kwenye Ukumbi wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Tanzania ilichaguliwa kuwa mwenyeji kutokana na mageuzi makubwa yaliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan tangu aingie madarakani, ambapo nguvu iliongezwa katika uwekezaji kwenye sekta ya Kilimo.
Snapinsta.app_375159643_18205151338258462_780947239121908779_n_1080.jpg

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Zuhura Yunus.

Viongozi mbalimbali wanaoshiriki katika Mkutano huu ni:
Waziri wa Kilimo, Hussein Mohammed Bashe
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Geofrey Mweli
Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Abdallah Hamis Ulega
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi. Prof. Riziki Silas Shemdoe
Wizara ya Kilimo Umwagiliaji Maliasili na Mifugo, Shamata Shaame khamis
Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar, Suleiman Makame

Baada ya utambulisho wa Zuhura, Wanahabari wameuliza maswali mbalimbali ambayo yanajibiwa na viongozi walioshiriki hapa kwa zamu.
Snapinsta.app_375064637_18205155721258462_6432194533939488779_n_1080.jpg

Waziri wa Kilimo, Hussein Mohammed Bashe.

Waziri wa Kilimo, Hussein Mohammed Bashe:
Taarifa kuwa zao la Vanilla kilo moja inauzwa Tsh. Milioni 1.5 hizo ni taarifa za uwongo, ni vizuri kuchukua taarifa ambazo ni sahihi.

Bidhaa gani tukiamua kutoiuza Nje Nchi kutatokea nini?
Siku tukisema tuzuie kutoa Mahindi nje ya Nchi au Mchele, Nchi nyingi ambazo zinanunua mazao hayo Ukanda huu wa Jumuia ya Afrika Mashariki zitapiga kelele, tukizuia maharage itakuwa hivyohivyo ukitoa Afrika Kusini.

Tunaondoa dhana kuwa kuna mazao ya chakula na ya biashara, kila zao liwe la biashara ndio maana kuna ukuaji mkubwa wa mazao yetu kwenda nje kuliko hata Pamba ambayo tumekuwa nayo muda mrefu.

Kuhusu Migogoro ya ardhi
Ipo ambayo inatuhusu Wakulima na Wafugaji lakini hiyo pia inahusisha Wizara nyingine.

Tumekubaliana tusijadili mgogoro bali kwanini watu wanaenda kwenye mgogoro, mara nyingi ni malisho na maji, ndio maana Serikali tunatengeneza Mabwawa yatakayowawezesha mifugo kupata maji.

Kuhusu mbegu za GMO (Genetically Modified Organism)
Serikali ya Tanzania hatutumii mbegu za GMO, lakini kama Nchi hatuzuii utafiti unaohusu GMO, kwa kuwa huwezi kuzuia kitu ambacho haukifaamu.

Rais ametupatia fedha kwa ajili ya kujenga Kituo cha utafiti wa GMO, kutakuwa na vituo viwili vikubwa vitakavyofanya utafiti.

Wenzetu majirani wamefanya, wanataka kujaribu kwenye pamba ya GMO, lakini ukilinganisha mbegu yao na ya kwetu, ya kwetu ina ubora zaidi.

Kwa nini tunaikataa? Mbali la suala la afya, kuna suala la kibiashara, nani anaimiliki na nani atafaidika siku ya mwisho?

Snapinsta.app_374585573_18205152967258462_3690104361266067423_n_1080.jpg

Viongozi mbalimbali waliohudhuria Kikao kuhusu Mkutano Mkuu wa Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF-Africa Food Systems Summit 2023) Ikulu Jijini Dar es Salaam, Septemba 03, 2023. Mkutano huo wa Chakula unatarajiwa kufanyika Jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 05 -8 Septemba 2023.

Wizara ya Kilimo Umwagiliaji Maliasili na Mifugo, Shamata Shaame Khamis:
Aslimia 20 ya Uchumi wa Zanzibar inachangiwa na Kilimo, pia 40% ya Wakazi wa Zanzibar wanajihusisha na sekta ya Kilimo, kwa ufupi wategemezi au wanufaika wa Sekta ya Kilimo ni 70%.

Upande wa Zanzibar kwa jinsi ilivyo, zao la Karafuu ndilo lenye wanufaika wengi wakubwa nje ya Zanzibar, wachambuzi wanaeleza kuwa Karafuu inau bora kuliko nyingi za sehemu tofauti na ni zao la kimkakati.

Zanzibar kuna mifuko zaidi ya 271,000, Serikali imeongeza mkakati wa kuongeza ng’ombe wa maziwa.

Vanilla inafanya vizuri lakini kuna changamoto ya soko kwa kuwa hakuna soka la uhakika, kumekuwa na taarifa tofauti kuhusu soko la Vanilla.

Zanzibar pia tuna Hifadhi za Misitu ambayo imekuwa ikivutia wageni wengi.

Mbegu ya GMO
Msimamo wa Serikali ni kama ulivyoelezwa na Waziri Bashe lakini nasi tumeanza utafiti nab ado ni mapema kuweza kuweka wazi hatua ilipofikia.
Snapinsta.app_374205910_18205157044258462_8450967675316873465_n_1080.jpg

Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Shamata Shaame Khamis akizungumza na Wahariri wa Vyombo Mbalimbali vya Habari kuhusu Mkutano Mkuu wa Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF-Afrika Food Systems Summit 2023) Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Snapinsta.app_375058456_18205157317258462_1200096285365816178_n_1080.jpg

Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi, Suleiman Masoud Makame kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, akizungumza na Wahariri wa Vyombo Mbalimbali vya Habari kuhusu Mkutano Mkuu wa Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF-Afrika Food Systems Summit 2023) Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar, Suleiman Makame:
Serikali imewawezesha vijana wasiopungua 2,000 kutoka upande wa Unguja na Pemba katika mazao ya ufugaji wa Tango Bahari badala ya kumuita jongoo.

Tango Bahari kilo moja inaweza kufika hadi Tsh. Laki Tano (500,000), kuna utafiti unaendelea kuhusu ufugaji wa Tango Bahari na kuna wawekezaji watatu wakubwa wanaelekea kuwekeza kwenye mazao hayo.

Kuhusu mazao ya Samaki tumewawezesha vijana na wanaendelea na ufugaji.

Kuhusu migogoro ya Wakulima wa Mwani na wawekezaji wa Kitalii, ni kweli migogoro imetokea lakini si mikubwa sana, kupitia mradi tuliouanza tumegawa boti kwa ajili ya kusaidia kupunguza migogoro, tunashirikiana na Wizara ya Utalii ili kuratibu na kutatua changamoto hizo.
Snapinsta.app_375181380_18205156630258462_4981840530245122213_n_1080.jpg

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na Wahariri wa Vyombo Mbalimbali vya Habari kuhusu Mkutano Mkuu wa Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF-Afrika Food Systems Summit 2023) Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo:
Uwepo wa Mkutano huu unafaidisha vipi wananchi? Tuantegemea mshiriki mmoja katika zile siku tatu au nne atakazokuwa ndani ya Tanzania anaweza kutumia Dola 500, kwa atakayetaka kuliona jiji anaweza kutumia hadi Dola 800 hadi 1,000, hivyo hiyo ni faida kwa wenye hoteli na wafanyabiashara wengine.

Waziri Bashe:
Kilimo sio siasa, ni maisha ya watu ni shughuli za kiuchumi za watu, takwimu za Mwaka 2012, Mkulima alilipa Pamba Tsh. 660 kwa kilo moja, ikapanda 700, 750, 800, 1000, 1200, 1100, 1850, 1200, Mwaka jana baada ya UVIKO ilipanda bei kuwa 2000, sasa hivi tunauza 1060.

Hii ni ile Pamba ambayo inatoka shambani.

Ukienda Zambia, Mkulima anauza kwa Sh 780 hadi 800 kwa kilo, Kenya Sh 900 hadi 1000, Burundi Sh 700.

Wanasiasa wasipotoshe watu kuhusu kilimo
Tumejenga tamaduni mbaya kwenye siasa yetu, mara nyingi Mwananchi anamuamini kiongozi wake, hivyo ukimpotosha inakuwa mbaya.

Nilimsikia kiongozi anasema bei ya Pamba imeshuka eti kwa sababu mwenyekiti wa Bodi ya Pamba ni mfanyabiashara wa Pamba, anasahau mwenyekiti wake alikuwa Mfanyabiashara na alikuwa Mbunge la Tanzania.

Kuhusu zao la Tumbaku, tumevunja rekodi ya uzalishaji wa Tumbaku, kutoka Tani 60,000 hado Tani 120,000 bei ya wastani imepanda kutoka Dola 1.6 hadi Dola 2.3.

Managing Director Africa's Food Systems Forum (AGRF), Amath Pathé Sene:
Huu ni moja ya mkutano mkubwa wa Kilimo Afrika, tuna[ozungumzia mfumo wa chakula tunahusisha aina zote za mifumo ile ya kibiashara pamoja na ile ambayo inatuletea chakula mezani.

Kuna fursa nyingi ambazo zinaweza kupatikana kupitia Mkutano huo, ndio maana mwaka huu tumewakaribisha Wadau mbalimbali kutoka mataifa tofauti kwa ajili ya kushirikiana kutafuta utatuzi na kuboresha.
 
Tungeendelea na aina ya kilimo chetu, GMO inakwenda kuleta matokeo chanya lakini kinachoacha madhara kila sehemu, kuanzia kwa watumiaji na ardhi
 
Back
Top Bottom