Kuelekea laini za simu zisizosajiliwa kuzimwa; Ushauri wa namna bora ya kufanya ili kutovunja sheria za nchi

Utawala huu wa Magufuli ni rahisi sana kutabiri kitu na kikatokea.
Nilitabiri Babu Seya atatoka ile December 9 2017 ikawa, nilitabiri 2019/2020 watumishi wa umma hawataongezewa hata senti ikawa. Leo narudia tena kutabiri utabiri huu mgumu kuwa line za simu zisizosajiliwa kwa namba ya NIDA kesho tarehe 20 kuelekea tar 21 hazitafungwa.
Kama unabisha tuwekeane dau
Hata mimi naamnini hivyo. Sioni aerikali inawezaje kukubali hasara kubwa ya kodi namna hiyo kwa suala ambalo linaweza kusubiri na likakaa vizuri hatimaye.
 
Utawala huu wa Magufuli ni rahisi sana kutabiri kitu na kikatokea.
Nilitabiri Babu Seya atatoka ile December 9 2017 ikawa, nilitabiri 2019/2020 watumishi wa umma hawataongezewa hata senti ikawa. Leo narudia tena kutabiri utabiri huu mgumu kuwa line za simu zisizosajiliwa kwa namba ya NIDA kesho tarehe 20 kuelekea tar 21 hazitafungwa.
Kama unabisha tuwekeane dau
Kwa hili mkuu nakubishia





Hajaacha kuniwekea mafuta ya taa kwenye ubwabwa
 
Unafikiri NIDA wanatoa vitambulisho kama unagawa karanga?
Sawa Wakati wao NIDA Walipo tutangazia zoezi la kwenda kusajiliwa Vitambulisho kwenye Mkoa wetu, Wao hawakujua hivyo Vitambulisho havitolewi kama Karanga?!
 
Kwanza maisha ni magumu, halafu wewe unaongeza ugumu kwa kufunga laini za simu.

Wapiga kura wako, wengi wapo vijijini na hawajawahi kupata namba za NIDA. Octoba wanaenda kukuchinjia baharini (au una plan B ya kushinda?)

Unaenda kuvunja mahusiano ya watu, kuzuia miamala yote ya fedha na kujenga chuki kati yako na wananchi.

Ulitakiwa kuwawajibisha viongozi wa NIDA wala si wananchi. Nyota yako inazidi kufifia. Kwanini kila unachogusa kinafeli?

Je, mbona mnakomalia namba, tutaishia kupata namba tu bila vitambulisho?

Tarehe 20 ni usiku huu, lets wait and see if mzee wa font fed atafanya yake.

.....UPDATES....

Serikali ya Tanzania imesema itatumia hekima kuwasaidia wananchi walioshindwa kusajili laini za simu kwa sababu ya kukosa kitambulisho cha Taifa na namba licha ya kuanza mchakato wa kupata kitambulisho hicho.

Imesema wananchi hao taarifa zao zipo katika Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), huenda wamekosa kitambulisho au namba kwa sababu zilizo nje ya uwezo wao.

Hayo yameelezwa leo Jumapili Januari 19, 2020 na naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye katika mkutano wa ndani wa CCM mkoani Kigoma.

"Serikali itaona jinsi ya kutumia hekima kwa wananchi ambao taarifa zao zipo katika ofisi za Nida kuona namna ya kufanya lakini kwa wengine ambao hawajajaza fomu laini zao zitazimwa,” amesema Nditiye.

Amesema ambao laini zao zitazimwa ni wale waliosajili laini chache na kuacha nyingine licha ya kuwa na kitambulisho hicho.

Amebainisha kuwa usajili wa laini za simu ni endelevu licha ya baadhi ya wananchi kupuuza.


....
Binafsi sijamuelewa kuhusu aina ya laini zitakazofungiwa.
Yote hio ni homa ya uchaguzi kuhofia chadema,aliyodhikiri ife anaumia sana kuiona iko imara
 
Hili jambo lina ukakasi kila siku asilimia kubwa kubwa ya watu wanadaiwa na mitandao ya simu wamekopa ni hasara za kiasi gani makampuni hayo yatapata hasara kubwa sana
 
Wakati Naibu Waziri wa Mawasiliano akisema serikali itatumia busara kuhusu usajili wa laini za vidole, ni busara dhidi ya nani au nini?

Ina maaana hili suala ni la kisheria hadi watumie busara? Nani alitoa tamko la usajili wa laini kwa njia ya vidole ili hali akijua uwezo wa NIDA?

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kadri siku zinavyokwenda ndivyo ccm inavyojichimbia shimo la kujiangamiza. Baada ya kuziba mianya ya vyama vya upinzani kujitokeza kwa wananchi kupitia mikutano ya hadhara na upinzani kutumia njia mbadala ya mitandao ya kijamii na sms kujiimarisha ccm imekuja na mbinu ya kuzima laini za simu kwa kisingizio cha kitambulisho cha taifa. Kama kungekuwa na nia nzuri serikali ya ccm ingewekeza nguvu nyingi katika suala zima la vitambulisho, maana haiwezekani miaka zaidi ya 50 wananchi hawajulikani uraia wao kama samaki. Kitendo cha kuwazimia watu laini za mawasiliano kwa kosa ambalo sio lao nikujenga chuki kati ya wananchi na serikali yao.
Naomba kuulizia hao wanaotimiza Leo miaka 18 kisheria na kesho wanatakiwa wawe na simu wanafanyaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom