Kuelekea laini za simu zisizosajiliwa kuzimwa; Ushauri wa namna bora ya kufanya ili kutovunja sheria za nchi

By Happiness Tesha, Mwananchi htesha@mwananchi.co.tz
Kigoma. Serikali ya Tanzania imesema itatumia hekima kuwasaidia wananchi walioshindwa kusajili laini za simu kwa sababu ya kukosa kitambulisho cha Taifa na namba licha ya kuanza mchakato wa kupata kitambulisho hicho.

Imesema wananchi hao taarifa zao zipo katika Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), huenda wamekosa kitambulisho au namba kwa sababu zilizo nje ya uwezo wao.

Hayo yameelezwa leo Jumapili Januari 19, 2020 na naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye katika mkutano wa ndani wa CCM mkoani Kigoma.

"Serikali itaona jinsi ya kutumia hekima kwa wananchi ambao taarifa zao zipo katika ofisi za Nida kuona namna ya kufanya lakini kwa wengine ambao hawajajaza fomu laini zao zitazimwa,” amesema Nditiye.

Amesema ambao laini zao zitazimwa ni wale waliosajili laini chache na kuacha nyingine licha ya kuwa na kitambulisho hicho.

Amebainisha kuwa usajili wa laini za simu ni endelevu licha ya baadhi ya wananchi kupuuza.


Kesho Jumatatu Januari 20, 2020 laini zote za simu ambazo hazijasajiliwa kwa alama za vidole zitazimwa. Ili uweze kusajili laini ni lazima uwe na kitambulisho cha Taifa au namba ya kitambulisho hicho.
 
Tutatafuta namana ya kuwaibia nyie wakoromije hata kama mkisajili line kwa kutumia vikojoleo
Kuna mbinu wamebuni wanaongea na mawakala wanaosajili line unaweza ukaweka ya kwanza alama za kidole kwenye mashine ya fomoco ikaenda msg kwenue line ya wakala pembeni

Ukaambiwa turudie tena ndio anakusajili sasa ukiondoka tu anabaki na line aliyoisajili kwa alama za vidole vyako hapo sasa anawauzia wazee wa tuma hela kwenye number hii

Bado kunachangamoto kubwa kwenye hilo

sent from toyota Allex
 
Utawala huu wa Magufuli ni rahisi sana kutabiri kitu na kikatokea.
Nilitabiri Babu Seya atatoka ile December 9 2017 ikawa, nilitabiri 2019/2020 watumishi wa umma hawataongezewa hata senti ikawa. Leo narudia tena kutabiri utabiri huu mgumu kuwa line za simu zisizosajiliwa kwa namba ya NIDA kesho tarehe 20 kuelekea tar 21 hazitafungwa.
Kama unabisha tuwekeane dau
Kwa hii kauli ya waziri nimeuamini utabiri wako
 
Kusajili line ni jambo jema lkn tatizo ni timing - wananchi wengi ambao ni wakulima kipindi hiki wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa fedha

Mwananchi kwa mfano wa Mugunzu au Nyamutukuza Kakonko kutoka kwao kufika Makao Makuu ya Halmashauri ni takribani kilomita 90 - 100. Sasa mwananchi huyu ambaye anategemea mazao ya kilimo ambayo hayajaiva kumpa kazi ya kufuatilia line ni kumtesa sana.

Ushauri:-
Serikali iendelee kuona umuhimu wa kuongeza muda wa usajili ili wananchi wasajiliwe. Lkn pia utaratibu uwekwe ili kazi hii ifanywe kwenye kata.
 
Kwanza maisha ni magumu, halafu wewe unaongeza ugumu kwa kufunga laini za simu.

Wapiga kura wako, wengi wapo vijijini na hawajawahi kupata namba za NIDA. Octoba wanaenda kukuchinjia baharini (au una plan B ya kushinda?)

Unaenda kuvunja mahusiano ya watu, kuzuia miamala yote ya fedha na kujenga chuki kati yako na wananchi.

Ulitakiwa kuwawajibisha viongozi wa NIDA wala si wananchi. Nyota yako inazidi kufifia. Kwanini kila unachogusa kinafeli?

Je, mbona mnakomalia namba, tutaishia kupata namba tu bila vitambulisho?

Tarehe 20 ni usiku huu, lets wait and see if mzee wa font fed atafanya yake.
Kadri siku zinavyokwenda ndivyo ccm inavyojichimbia shimo la kujiangamiza. Baada ya kuziba mianya ya vyama vya upinzani kujitokeza kwa wananchi kupitia mikutano ya hadhara na upinzani kutumia njia mbadala ya mitandao ya kijamii na sms kujiimarisha ccm imekuja na mbinu ya kuzima laini za simu kwa kisingizio cha kitambulisho cha taifa. Kama kungekuwa na nia nzuri serikali ya ccm ingewekeza nguvu nyingi katika suala zima la vitambulisho, maana haiwezekani miaka zaidi ya 50 wananchi hawajulikani uraia wao kama samaki. Kitendo cha kuwazimia watu laini za mawasiliano kwa kosa ambalo sio lao nikujenga chuki kati ya wananchi na serikali yao.
 
Muda mwingine Wabongo hatupo makini kabisa tunawalaumu NIDA bure, hili zoezi toka limetangazwa watu walikuwa hawana muda nalo kabisa ukifika ofisi za NIDA unakuta watumishi wa NIDA wanapiga tu stori hakuna kazi ila deadline inapokaribia kila mtu yupo bize kuhangaikia na NIDA na malalamiko juu.

Mchakato wa kupata kitambulisho cha taifa umeanza zaidi ya miaka minne nyuma, Mlikuwa wapi siku zote.

Kabisa me nakumbuka nilipata kitambulisho changu mwaka juzi 2018 mwezi wa 6 safi kabisa sema tuna shida ya kupuuzia mambo tena nilikipata ndani ya wiki mbili


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kwa hii kauli nimeuamini utabiri wako
Hapa nasubiri wakati wa tamko tu
 
NIDA kumekuwa na folen ya kufa mtu sio kwa kuwa watu wanataka vitambulisho vya Taifa bali kwa kuwa wanapigania namba zao za simu zisizimwe

Yaan watu hawana mpango na vitambulisho sema tu inabidi wawe nacho kukamilisha usajili

I.e line ya simu ni muhimu kuliko kitambulisho
ikitangazwa kuwa usajili wa line sio muhimu kitambulisho cha NIDA basi folen inaisha fasta
Wa Tanzania n waoga kwelikweli
 
Binafsi nilijiandikisha tena mara mbili lakini nimefuatilia namba zangu NIDA kama naomba mkopo benki. Hakuna nilichoambulia. Uzembe wa NIDA usumbufu nabebeshwa mimi.

Matokeo yake naambiwa nijiandikishe upya, yaani nianze taratibu za kwenda kwa Mtendaji, Uhamiaji halafu NIDA.

Acha wafungie nimejiandaa kisaikolojia!

Sent using Jamii Forums mobile app
Wa Tanzania n waoga sana, eti hapa wanaogopa tuline, mnapimwa yoga kampen zinakaribia
 
Back
Top Bottom