Kudesa tatizo sugu vyuo vikuu vyote!!!

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,148
kwa wanaoangalia TBC
Kuna mwalimu mmoja dk,wa moja ya chuo amekiri wanafunzi wengi wamekuwa wakides a ili kufaulu mitihani yao..hali ya kudesa ipo kila chuo watakachofanya ni kupunguza rate..mwalimu huyo mwenye miwani na macho ya kupendeza amekiri kudesa ni tatizo sugu...unakuta mtu anaingia na calculator mwisho kajaza full nondo ama ile ile kaichora maandishi madogo..wengine wamekuwa wakiweka mpka kwenye mapaja yao na kufunika na nguo!!!!sasa hata ukiona kumfwata uwezi mlazimisha akuvulie na akiamua kuondoka na kutoa malalamiko kama ujakamata ile karatasi unaumia....

Mmmmmmh Mmambo ya kudesa!!!
 
sio kweli kugeneralize kuwa vyuo vikuu vyote kwanza kuna vyuo hata hilo neno hawana kabisa ni msamiati ambao wanausikia wanaporudi likizo,
 
Hivi hii kweli ni breaking news? Tuangalie na vitu vya kuwa kwenye breaking news bwana.
 
kwa wanaoangalia TBC
Kuna mwalimu mmoja dk,wa moja ya chuo amekiri wanafunzi wengi wamekuwa wakides a ili kufaulu mitihani yao..hali ya kudesa ipo kila chuo watakachofanya ni kupunguza rate..mwalimu huyo mwenye miwani na macho ya kupendeza amekiri kudesa ni tatizo sugu...unakuta mtu anaingia na calculator mwisho kajaza full nondo ama ile ile kaichora maandishi madogo..wengine wamekuwa wakiweka mpka kwenye mapaja yao na kufunika na nguo!!!!sasa hata ukiona kumfwata uwezi mlazimisha akuvulie na akiamua kuondoka na kutoa malalamiko kama ujakamata ile karatasi unaumia....

Mmmmmmh Mmambo ya kudesa!!!

Una maana gani ya kusema kila chuo? Mimi University niliyosomea iko nje ya Tz na tatizo hilo halipo.
 
sio kweli kugeneralize kuwa vyuo vikuu vyote kwanza kuna vyuo hata hilo neno hawana kabisa ni msamiati ambao wanausikia wanaporudi likizo,

mbogela kati ya hivi taja kipi awajui kudesa sema kutoka moyoni mwako bila ushabiki

chuo kikuu cha dar es salaam

chuo cha tumain dar/iringa

chuo cha mzumbe

chuo cha open university of tanzania

.....

Labda nianze hapo juu namba moja ;kama walimu wakiwa serious
wanafunzi wengi wanafukuzwa hapo juu hasa law na engineering...

Nimesoma pale 1999-2002
hizo course tulifanikiwa kufanya mitihani pamoja kwenye vile vyumba viwili...opposite na geti la coet...wakaona soln ya kuacha kudesa ni man to man..wakaona soln kutuchanganya na law..tulifanya nao kama kile chumba kingekuwa kinapiga kelele kikiona madesa wallahi ingekuwa aibu....soln aikuwa kutuhanganya watu wakaja na videsa vidogo vidogo...anyway nasema hivi kueleza hili ili ipatikane sababu za kwa nini wanadesa na soln ya kudesa nini??

Open unniversity
mkulu baada nimemaliza degree yangu ya bba 2008

nalo de same maana wana kitu kinaitwa assignment..wanaanzia kudesa hapo ukifika pale nkurumah ukiwachekea vile vibinti vinavyosimamia ukionyesha red/brown kwenye bench.....nakuhakikishia atoki hapo atakulinda mpaka unamaliza mtihani toa vikaratasi vyako fungua mapaja yako hana dili na weweukitoka anatoka na wewe ;;;mnamalizana imagine hiyo ni mmoja,..kudesa itaisha???

Hili jamaa lihaya nalipenda lina phd yake na linaeleza uwazi na kueleza itafutwe tatizo nini kwa nini wanadesa wengi???
Kwa nini wanafunzi mfano open wanafanya mitihani wanashindwa kurudishiwa mitihani yao ;wakati huo huo ukienda uanaonyeshwa matokeo ukifika kwenye saries sehemu ya matokeo unakuta inc ukiuliza sana mwalimu aanakwambia sijui ilipo ...aijapita mwezi amekuonyesha na umeona umefaulu...kudesa itaisha??
 
mbogela kati ya hivi taja kipi awajui kudesa sema kutoka moyoni mwako bila ushabiki

chuo kikuu cha dar es salaam

chuo cha tumain dar/iringa

chuo cha mzumbe

chuo cha open university of tanzania

...kudesa itaisha??

Ndio vyuo vyote kwa Tanzania?

Kuna vyuo Including chuo nilichosoma mimi kwa kweli tulikuwa tunaumiza mgongo vibaya sana, na tulipokuwa tunasikia chuo cha wenzetu chuo cha jirani wanafukuzwa au wamekamatwa na vikaratasi tulikuwa tunashangaa sana. Kwetu sisi tulichokuwa tunajitahidi sana ni kuhakikisha kuwa umefanya vizuri practical zakona course work, kwani tulikuwa tunafaulu Practical na Theory 50:50 na pass mark yetu ilikuwa 40%. (si unajua practical report inavyoandikwa, lite revie marks, data Marks, analysis Marks, conclusion and recommendation Marks, Ukichemsha literature na data umekwisha, lakini kwa vile tuna muda wa wiki kusubmitt watu tunalala Libarary)

Lakini la muhimu hapo ni mfumo wa Elimu, nilipoenda kwa wenzetu vijana wanakuwa involved sana kwenye kufikiria, muda wote wanapewa reference current na wanapewa home work za issue inayoisibu jamii muda huo. sasa sisi hapo bongo mitihani ni ile ile miaka nenda rudi, kitabu kile kile ndio maan watu hata wahanunui kitabu tena.

Kosa lingine lipo sekondary, wakati ule tulikuwa tunakula Nelkon, tunasoma Lambert kwa hiyo ilikuwa kila kitu unasoma kuelewa the theory behind, siku hizi watoto wanasoma Pumphlets kuanzia form one mpaka form 6 yeye anakariri maswali na majibu tu, na anapata Div I sasa akifika chuo anatakiwa kusoma vitabu hajawahi hata siku moja kusoma hivyo vitu kwanini asiingie na desa?

Mfumo wa ufundishaji wa secondary school ndio mwanzo wa madesa chuo kikuu.
 
Mama Miaa umerudi?

waache waibie lakini kwenye kutafuta kazi wataibia pia? Good organisations will only employ smart ppl...
 
Njia pekee ya Kukomesha KUDESA ni kufunga CCTV kwenye vyumba vya mitihani na kuwa na wasimamizi wengi on ground na wengine wanafocus kwa kutumia CCTV Camera, Ikithibitishwa kwenye Camera kwa kutumia ground support ya invigilators basi ni kupigwa "DISCO" na kuzuiwa kujiunga chuo chochote kwa miaka mitatu. Hili litafanya watu kuwa makini na kujiandaa na mitihani.

sio kweli kugeneralize kuwa vyuo vikuu vyote kwanza kuna vyuo hata hilo neno hawana kabisa ni msamiati ambao wanausikia wanaporudi likizo,

Kinachoongelewa hapa ni kutumia kibuti/ Kudesa/ Mtutu (Haya yote yanaingia katika suala moja "udanganyifu katika mitihani")) - Sasa ni chuo gani hawafanyi huo mchezo na si kudesa kama msamiati.

"Kudesa ni universal problem"
 
kwa wanaoangalia TBC
Kuna mwalimu mmoja dk,wa moja ya chuo amekiri wanafunzi wengi wamekuwa wakides a ili kufaulu mitihani yao..hali ya kudesa ipo kila chuo watakachofanya ni kupunguza rate..mwalimu huyo mwenye miwani na macho ya kupendeza amekiri kudesa ni tatizo sugu...unakuta mtu anaingia na calculator mwisho kajaza full nondo ama ile ile kaichora maandishi madogo..wengine wamekuwa wakiweka mpka kwenye mapaja yao na kufunika na nguo!!!!sasa hata ukiona kumfwata uwezi mlazimisha akuvulie na akiamua kuondoka na kutoa malalamiko kama ujakamata ile karatasi unaumia....

Mmmmmmh Mmambo ya kudesa!!!
hapo sasa
 
Mhhh haya Bwana!!!! Mpaka hapo sijaona mtu ana propose solution. Kwani huyo Dr. alisema nini kifanyike?? The problem is bigger than we think. Kuanzia sekondari hadi vyuo vikuu.
 
kibuti/ Kudesa/ Mtutu (Haya yote yanaingia katika suala moja "udanganyifu katika mitihani")) - Sasa ni chuo gani hawafanyi huo mchezo na si kudesa kama msamiati.

"Kudesa ni universal problem"
SIO kweli hakuna msamiati hata mmoja unaofanana na huo niliokutana nao chuoni kwangu. Nachojua kibuti ni msichana kukukataa, tuliutumia shule moja ya kanisa pale Morogoro kwa hiyo bwana udhaifu wa walio wengi haimaanishi wote wamepita njia hiyo, tatizo la mavyuo yenu sio la vyote. Mlisoma the so called big/famous universities basi ndio hayo mnayofanya, lecture watu mko 200 mitihani mnawekwa Nkrumah kwanini watu wasiingie na madesa, lakini kozi mitu zipo 15 wapi na wapi, utachomolea wapi hilo desa lako???
 
Well said "Good organisation will employ smart people" Not every employer will look into how many degrees unazo ili akupe kazi wengi wanaenda na work experience,skills, smartness,language(English) etc.
Sio vyuo vya bongo tu hata vya Europa watu wanadesa sijui kudesi ukiambiwa mtu ana masters unajiuliza mbona ni mjinga mjinga tu ameipataje hiyo masters kwani mtu mwenyewe si smart kwa lolote. Thinking capacity ndogo, low common sense,Lugha za wenyewe tatizo hahahhaha elimu ya siku hizi kazi kweli kweli.
 
Umesoma Europe lakini? Nchi ipi hiyo kaka /dada yangu?? Alafu mimi huwa nashangaa mtu mbaye hajui kiarabu kwa mfano anakuambia fulani ni mkali wa kiarabu au ni mbumbumbuu, umemuassess vipi??? wakati wewe mwenywe hakipandi?? ndio hivyo hata kiinglish watu wengi bongo hatupandishi sasa tutawezaje kusema hao wa masters lugha inawapiga chenga wakati sisi wenyewe tupo zero?? Hata suala la uwezo wa kupembua mambo inawezekana sisi ndio tunashindwa kuwaelewa kwasababu ya upeo wetu mdogo na akili yatu ya kudesa desa kutoka kwenye vyuo vyetu basi tunabaki ooh hawawezi na masters zao
 
Njia pekee ya Kukomesha KUDESA ni kufunga CCTV kwenye vyumba vya mitihani na kuwa na wasimamizi wengi on ground na wengine wanafocus kwa kutumia CCTV Camera, Ikithibitishwa kwenye Camera kwa kutumia ground support ya invigilators basi ni kupigwa "DISCO" na kuzuiwa kujiunga chuo chochote kwa miaka mitatu. Hili litafanya watu kuwa makini na kujiandaa na mitihani.

Kinachoongelewa hapa ni kutumia kibuti/ Kudesa/ Mtutu (Haya yote yanaingia katika suala moja "udanganyifu katika mitihani")) - Sasa ni chuo gani hawafanyi huo mchezo na si kudesa kama msamiati.

"Kudesa ni universal problem"

Well said "Good organisation will employ smart people" Not every employer will look into how many degrees unazo ili akupe kazi wengi wanaenda na work experience,skills, smartness,language(English) etc.
Sio vyuo vya bongo tu hata vya Europa watu wanadesa sijui kudesi ukiambiwa mtu ana masters unajiuliza mbona ni mjinga mjinga tu ameipataje hiyo masters kwani mtu mwenyewe si smart kwa lolote. Thinking capacity ndogo, low common sense,Lugha za wenyewe tatizo hahahhaha elimu ya siku hizi kazi kweli kweli.

Afadhali mmezungumzia kuwa kwa sasa ni tatizo la kidunia si nyumbani tu. Nimeona nje watu wanadesa na sijasimuliwa, weupe na rangi zao. Kudesa kunategemea kozi na instructor na mara nyingi KUDESA NI TATIZO LA MWALIMU SIO MWANAFUNZI!

How to make sure you student will not desa

1. Epuka repeatation ya maswali(past papers), na kama unaona hutaweza kutunga maswali mapya basi hakikisha kila mtihani unaoutoa mwanafunzi hatoki na mswali, hii inaepuka kurithishana maswali

2. Broad their mind, usina- narrow kwenye notes zako pekee au kufanya materia yako ndiyo final, this will make student not to guee where question are coming from, then hataweza kuingia na madesa.

This is my view how to remedy the problem:

3. Tunga mswali ya kufikiria zaidi na siyo direct question-direct answer!

4. Make student to like your subject, most of the time there is a poor relations btn instructor and student, threats, na hofu ya kufeli, teaching student to fail results into defence

5. Assignments are the major means ya kumfanya mwanafunzi aelewe kozi, make sure you put you are effort kwenye assignments na hii itakwepesha wanafunzi kuzima moto, make sure unawabana kwenye assignemt hata kurudia warudie, let them present by writing, oral, gropu work, projects of different title etc.

6. Kwepa concept ya 'impart' rather than encourage discussion, through discussion you may know their wekness, viewe and is another way of evaluating them whether they understand what you teach.

I believe most of the time ni matatizo ya walimu ,kuwa wanafunzi kudesa kozi zao.

The students have their part, lakini kwa level za chuo instructor ana uwezo wa kwadhibiti, wawe wamezoea hivyo au issue za employment na nature ya ajira zetu ina encourage watu wawe na vyeti vizuri!
 
Kudesa siyo tatizo la vyuo vya Tanzania tu; nadhani kuwa hiyo inatokea duniani kote na inategemea zaidi na njia inyotumiwa na mwaliku katika kufundisha na kutunga mitihani. Najua kuwa marekani vyuo vingi vina kitu kinaitwa honor code ambapo mwanafunzi anatakiwa kusaini mkataba kukubali kuwa hatadanganya kwenye assignments pamoja na mitihani yote atakayofanya. Akishikwa basi akubali matokeo yake.

Hata hivyo, pamoja na kusaini hizo contracts, bado kuna baadahi ya wanafunzi ambao huwa wanadanganya. Njia kubwa sana ambayo ninayoamini kufanya kazi sawasawa, na kutunga mitihani inayopima uwezo wa mwanafunzi ku-transform material aliyofundihswa darasani kuwa solutions za practical problems. Maswali ya namna hiyo huwa hayahitaji desa kwani yanahitaji mwanafunzi kufikiri zaidi ya kukumbuka material. Mitihani hiyo ni mizuri sana na huwa ni open book, kwa hiyo hata kama mwanafunzi atelata library nzima kwenye chumba cha mitihani, hiyo ni ruksa kabisa na bado anaweza kuodoka na kishoka.

Mitihani ambayo mwanafunzi anaweza kupasi kwa desa ni ile inayotaka mwanafunzi ku-reproduce materiala aliyofundishwa darasani.
 
:confused:!! Mbogela shukrani kwa swali lako. Sijasoma Europe lakini nimesoma shule moja kati ya best schools in Tz.Nimekutana na watu wamesoma Europe/UK anakuambia amefanya degree sijui ya nini na nini lakini subiri achangie mada ndipo utakapojua hapa hamna kitu halafu unaishia kujiuliza hii degree inakuwaje kuwaje. Kwa ufupi hili tatizo lipo karibu kila mahali lakini ni tabia ya mtu kama unataka kuwa na degree ili watu wajue tu una degree basi mbele ya safari itakuwa vigumu sana.
 
Mama Miaa umerudi?

waache waibie lakini kwenye kutafuta kazi wataibia pia? Good organisations will only employ smart ppl...

Am back dear hii ndio

JAMII FORUMS
where we dare to talk openly

ndugu hadi kwenye kazi hao wanachukuliwa wala sio tatizo ;mkifika wote nyu na mnapigwa training sawa na wanatoka ;sawa !!!na wengine wakijua njia walizotokea wakifika kwenye kazi wanapiga mzigo usiseme!!!
 
Back
Top Bottom