Kuchomwa moto ofisi ya kamanda wa polisi

Makene

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
1,475
282
Taarifa za kukamatwa raia kuhusiana na kuchomwa kwa ofisi ya kamanda wa polisi ni uonevu na matumizi mabaya ya nguvu za dola.
Haingii akilini kusikia eti ofisi ya kamanda imechomwa moto.
Mbona hatusikii ni hatua gani zimechukuliwa kwanza dhidi ya askari waliopaswa kuwa lindo. Hii ni aibu kwamba ofisi ya wanaodai kulinda raia haina ulinzi. Raia waliokamatwa wanafanyiwa uonevu kwa udhembe wa askari wetu wachovu wasio na kazi.
Hata baadhi ya raia wamehama makazi yao kuhofia masaibu yatakayowakuta.
Isitoshe maelezo ya raia yanaonyesha kuna askari waliofanya uporaji vibanda vya raia na bila shaka ndio waliochoma moto huo.
Je tulitegemee jeshi la polisi kwa ulinzi wa mali zetu sisi raia?
 
Ni kweli polisi inapaswa kuwa makini sana na mambo mengine inayofanya. Kitendo cha kituo cha polisi kuchomwa moto kuna uzembe wenyewe wa polisi.

Tukienda mbali zaidi hii inatoa picha ya watu kuchoka manyanyaso ya polisi wetu.

Kuna haja ya Jeshi la Polisi kujipanga kuon ni wapi limekosea na kurekebisha.
 
Kituo kikuu cha polisi mji wa Tandahimba

Ni jengo la Ofisi za OCD na ofisi za Upelelezi za Polisi mkuu...

Kituo cha polisi kipo salama,mahabusu salama,silaha zote salama.. Ila pana umbali wa takribani Km 1,kati ya majengo hayo mawili.

Na hapo kituoni kuna canteen yenye kuuza vinywaji baridi na vikali,na pana ukumbi mkubwa watu mbalimbali huwa wanarefresh..
Hapo napo vinywaji vinanyweka na chips,nyama choma zinalika..
 
Nyambulisha kwenye red!!!:A S-rap:
 
Taarifa za kukamatwa raia kuhusiana na kuchomwa kwa ofisi ya kamanda wa polisi ni uonevu na matumizi mabaya ya nguvu za dola.
Haingii akilini kusikia eti ofisi ya kamanda imechomwa moto.
Mbona hatusikii ni hatua gani zimechukuliwa kwanza dhidi ya askari waliopaswa kuwa lindo. Hii ni aibu kwamba ofisi ya wanaodai kulinda raia haina ulinzi. Raia waliokamatwa wanafanyiwa uonevu kwa udhembe wa askari wetu wachovu wasio na kazi.
Hata baadhi ya raia wamehama makazi yao kuhofia masaibu yatakayowakuta.
Isitoshe maelezo ya raia yanaonyesha kuna askari waliofanya uporaji vibanda vya raia na bila shaka ndio waliochoma moto huo.
Je tulitegemee jeshi la polisi kwa ulinzi wa mali zetu sisi raia?

Huo utakuwa ni udhembe uliodhidi kupita kiadhi!
 
Back
Top Bottom