Kuchelewa kwa Mishahara ya watumishi wa umma mwezi October 2012

namanyele

JF-Expert Member
Oct 19, 2012
1,852
608
Jamani mie nipo kijijini huku Sumbawanga, naulizia mishahara ya mwezi huu kama imetoka, hali ngumu sikukuu ya kesho kwa sisi waalimu.

Nawasilisha
 
Miye Bosi wangu ni dini nyingine hawezi kunipa mshahara wala posho ila ingekuwa ile sikukuu nyingine angenipa tena mapema tu, ujanja nilioufanya nimebakiza baadhi ya vihela vyangu ili nile ubwabwa mchafu 'Chakula cha Peponi'.
 
nami nimegundua hicho hapo kunakaubaguzi fulani hivi,mbona sikukuu za kikristo hasa chrismas mshahara mapema kila mwaka na kila sekta,mm ni mwislaamu linaniuma sana hili jambo na ndio maana siku hizi kuna utata kwenye dini
 
kila jambo mnaingiza udini, umemuuliza mkurugenzi wako wa halmashauri akupe sababu?
 
watakuambia payllor bado hazijafika,ina maana hapo mpaka j'3
 
hongereni sie tupo mikoa na wilaya zenye viongozi wengi wakristo hivyo hawana haraka ya kutoa mishahara hata kama ipo
 
sherehe ya dini ni ibada au unataka sadaka? halafu we mwalimu subiri tukate madeni yetu ya finca, pride, bayport na vicoba, then tutakuletea tu zero percent yako ufanyie sherehe.
 
sherehe ya dini ni ibada au unataka sadaka? halafu we mwalimu subiri tukate madeni yetu ya finca, pride, bayport na vicoba, then tutakuletea tu zero percent yako ufanyie sherehe.

Jamani hebu kuweni wastaarabu kidogo
 
sherehe ya dini ni ibada au unataka sadaka? halafu we mwalimu subiri tukate madeni yetu ya finca, pride, bayport na vicoba, then tutakuletea tu zero percent yako ufanyie sherehe.

We ndo kilaza kwelikweli,serikali yenyewe inakopa sembuse kilaza wewe
 
Msitoane roho jamani. Kwa wale wafanyakazi wa Serikali wasahau kwa muda kama tarehe za mshahara zimefika. Mishahara haipo tayari, kuna matatizo ya kiufundi yamejitokeza kwenye tarakilishi za Hazina hivyo vuteni subra. Wenye vibubu vunjeni tu hakuna ujanja.
 
jamani mie nipo kijijini huku sumbawanga naulizia mishahara ya mwezi huu kama umetoka,hali ngumu sikukuu ya kesho kwa sisi waalimu.nawasilisha

kwani we muislamu?..............nnachojua sumbawanga hakuna waislamu
 
Kwa hiyo shida yako ilikuwa ni kutaja ukristo???

shida yangu ilikuwa ni kufananisha akili yako na kilaza mwenzio mulugo na sio kutaja ukristo,mnafanana akili na mulugo sijui ni pacha wako
 
Nashkuru cha sikukuu nmekiona n hapa napasua anga.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
watakuambia payllor bado hazijafika,ina maana hapo mpaka j'3

tatizo letu wabongo tumefanya utegemezi wa hali ya juu. Kwa hali hii hatufiki popote. Nakushauri mwl uanzishe hata kabustani ka mboga za majani utaona uzuri wa kujitegemea.
 
Msitoane roho jamani. Kwa wale wafanyakazi wa Serikali wasahau kwa muda kama tarehe za mshahara zimefika. Mishahara haipo tayari, kuna matatizo ya kiufundi yamejitokeza kwenye tarakilishi za Hazina hivyo vuteni subra. Wenye vibubu vunjeni tu hakuna ujanja.

Mkuu upo serious? So tutarajie kwenye tarehe ngapi labda?
 
Back
Top Bottom