Kucheleshwa kwa pesa ya kujikimu kwa watumishi wapya wa Umma

Sosthenes Maendeleo

JF-Expert Member
Oct 24, 2012
2,649
1,497
Pamoja na serikali yetu kujitangaza kufanya vizuri hasa katika viwanda na kuleta uwajibikaji wa watumishi katika taasisi mbalimbali, ni serikali hiyo hiyo imeshindwa kuwajali watumishi wetu wazalendo. Waliajiliwa kwa kuambiwa kwamba pesa ya kujikimu na usafiri watapata halmashauri. Cha ajabu hadi leo hakuna dalili ya kupewa pesa hizo tangu mwezi wa nne mwaka huu.

Watumishi wanaishi maisha magumu kwani wanadaiwa madeni walikotoka. Wengine walikopa katika taasisi yao ya kazi ili kusonga mbele watarudisha mara tu pesa za kujikimu watakapo pewa. Baadhi ya taasisi zinawalazimisha walipe kutoka mshahara wao ingali hata mshahara hautoshelezi mahitaji yao. Hongera kwa mh. waziri mkuu kwa kutoa siku kumi mwishoni mwa mwezi wa sita pesa za kujikimu ziwe zimewafikia watumishi hawa wapya.

Swali ni je mh. Kassim Majaliwa Kassim hafaham suala hili na aliwadanganya watumishi wapya na watanzania kwa ujumla?
 
Back
Top Bottom