Mkodoleaji
JF-Expert Member
- Apr 27, 2008
- 458
- 138
Jamani naona mimi kuna somo moja ambalo bado napenda kujifunza kwenye hilo bunge la katiba nalo ni somo la utawala bora. Hivi hawa wajumbe walioenda kule wakachagua mawaziri (mwenyekiti-Sitta na makamu-Samia) hawajui masuala ya utawala bora? Hawakuangalia mgongano wa maslahi? Hapa kuna viongozi wa serikali ambayo inaonekana ina msimamo fulani halafu hao wanachagulia kuongoza bunge la katiba ambalo linategemea lisiegemee upande wowote je kweli hili linawezekana?
Kwangu mimi somo ninalojifunza hapa ni kwamba wengi wa wajumbe somo la utawala bora na mgongano wa maslahi bado halijawaingia na inaonekana hata wakiongea kwenye vyombo vya habari huwa wanaongea wasichokiamini.