Kubenea acharuka, apinga bajeti ya jiji la Dar kupelekwa bungeni

1. Jiji la Dar lina wilaya tatu na zingine mbili ziko mbioni kuanzishwa.
2. Kila wilaya hizo ina halimashauri yake ya manispa yenye madiwani na mameya wao. Kila manispaa nchini huandaa bajeti na kupitiwa mabaraza yao ya madiwani, na baada ya hapo huwasilishwa kwa waziri wa TAMISENI. Ofisi ya mayor ya jiji la Dar ni ceremonial hivyo haina mamlaka ya kuzibadili hizo bajeti. Anaweza tu akatoa ushauri kabla ya uandaaji wake. Madiwani wa halmashauri husika walishazipitia sasa Kubenea analalamika nini?
Ukiona hivyo, Bajeti hizi hazikuandaliwa na UKAWA kama mtu mmoja alivyojaribu kutuaminisha hivi karibuni. Alitamba sana Ukawa wameandaa bajeti ki historia, leo wanaikana wenyewe
 
Huyu mleta anachonikera ni ushabiki wake anapoleta habari za Kubene...,, eti mbunge wa taifa my foot

Kama wewe ni mwanaume jitazame upya aisee
 
idawa

Swali hilo na mie linaniumiza sana. Hivi ni dhambi gani kwa mtanzania mwenzako aliyepewa ruhusa ya kikatiba na watanzania wenzake kusimamia mali na maendeleo ya mahali flani, wewe uliyeshinda karibia asilimia 60 nchi nzima na halmashauri kibao uwe na wivu juu yake?

Najaribu kwa nguvu zote kumwamini Mh. Rais kama mtu anayependa HAKI na MTANZANIA zaidi kuliko UCcm wake lakini nashindwa!
....

...tuna safari ndefu sana ila
 
Huyu mleta anachonikera ni ushabiki wake anapoleta habari za Kubene...,, eti mbunge wa taifa my foot

Kama wewe ni mwanaume jitazame upya aisee
kumchukia Erythrocyte hakutakusaidia chochote mjomba , unachotakiwa kuangalia ni hoja iilyoletwa mezani .
 
Hivi CCM kwa nini wasiwape UKAWA uhuru wa kuendesha halmashauri ili tujue uwezo wao.

Kwa nini wanawazonga zonga kila wanapotaka kuonyesha weledi.

CCM waelewe hawawakwamishi UKAWA ila wanatukwamisha wananchi tunaotaabika kila siku.
Huku Kinondoni mayor amegeuka kuwa mtendaji (mkurugenzi) wa manispaa.
 
Waliapa kuwakwamisha UKAWA wasifanye kazi, hii ndio CCM

Watakalo litakuwa na huo nakwambia ni mwanzo tu.Wataipeleka kwa nguvu na mkiisusia wataijadili upande mmoja na kuifanyia marekebisho makubwa na kuutaka uongozi kuifuata.Mkurugenzi ni wao na ndie mtekelazaji kwa maagizo ya chama chao.Spika mnaetaka kumwendea ni wa kwao na sio ukawa mtapita wapi?Hizo sheria watekelezaji ni wao na wamejipanga kuwakwamisha na huko huko kuna makubwa wanataka yasahaulike kwa wananchi kwa kuwaacha wakihangaika na kituko cha bajeti ya halimashauri/jiji kukimbizwa bungeni hata kabla ya kufanyiwa marekebisho na wahusika.Kwani mmeshasahau mbinu za serikali wakitaka kufukia yao?Hii inaitwa kucheza na akili za watu kuwasahaulisha makubwa na kumenyana na vi issue visivyo maana.
 
hapo sheria zote zitakanyagwa ili kulinda maslahi ya ccm na wasomi wetu watapongeza. hii nchi imejaa wachumia tumbo na wasubiria vyeo kama udc,na urc....
 
Kula sumu mkuu

Hata mimi siwezi Kimsikiliza huyu jamaa hakawii kujasema alidanganywa, hata atokwe na mapovu vipi siwezi muamini labda kama hoja ni nzuri awe anaangalia mtu mwenye credibility ndo aiwasilishe lasivo apo amna kitu
 
nasema sija wahi kuona chama chenye fikira za kijinga kama ccm baada ya kufikiri kutuletea maendeleo wao nanafikir wataendelea vip kukaa madarakani na kufelisha mipango ya wapinzani ili mipango yao ikwame huu ni ujinga uliyo wa fanya ccm wikatae katiba ya warioba
 
Mbunge huyo makini ambaye Wengi wanapenda kumwita mbunge wa Taifa kutokana na uzalendo wake wa kulinda maslahi ya nchi , amesema ni lazima kwanza bajeti ijadiliwe na madiwani wa jiji kabla ya kupelekwa bungeni .

Haiwezekani bajeti iliyoandaliwa na watendaji wa jiji ipelekwe moja kwa moja Tamisemi badala ya kupitia kwanza kwenye baraza la madiwani ili ijadiliwe na mapungufu yarekebishwe .

Mh huyo kwa msisitizo amepanga kupeleka barua kwa spika kumjulisha juu ya jambo hilo .

My Take - ninaona harufu ya UKAWA kuhujumiwa kwa udi na uvumba katika mikakati yao ya kuboresha jiji .

Hoja ya kubenea ina mantiki, lakini msije mkamhadaa na swala la "ubunge wa kitaifa". Yeye ni mbunge wa Ubungo tu.
Kama hajui madhara ya kujipachika hicho cheo cha kitaifa amuulize mtangulizi wake J.Mnyika.
 
Hivi CCM kwa nini wasiwape UKAWA uhuru wa kuendesha halmashauri ili tujue uwezo wao.

Kwa nini wanawazonga zonga kila wanapotaka kuonyesha weledi.

CCM waelewe hawawakwamishi UKAWA ila wanatukwamisha wananchi tunaotaabika kila siku.
Kwann UKAWA hawakuwapa wanachama haki ya kuchagua mgmbea uraisi
Dunia duara Mkuu
 
Watakalo litakuwa na huo nakwambia ni mwanzo tu.Wataipeleka kwa nguvu na mkiisusia wataijadili upande mmoja na kuifanyia marekebisho makubwa na kuutaka uongozi kuifuata.Mkurugenzi ni wao na ndie mtekelazaji kwa maagizo ya chama chao.Spika mnaetaka kumwendea ni wa kwao na sio ukawa mtapita wapi?Hizo sheria watekelezaji ni wao na wamejipanga kuwakwamisha na huko huko kuna makubwa wanataka yasahaulike kwa wananchi kwa kuwaacha wakihangaika na kituko cha bajeti ya halimashauri/jiji kukimbizwa bungeni hata kabla ya kufanyiwa marekebisho na wahusika.Kwani mmeshasahau mbinu za serikali wakitaka kufukia yao?Hii inaitwa kucheza na akili za watu kuwasahaulisha makubwa na kumenyana na vi issue visivyo maana.
patachimbika .
 
Back
Top Bottom