Kubana matumizi Serikalini vs shilingi kutoimarika

Sasa ni rasmi 1 USD = 2200 TSH. tunakoelekea siko. Wachumi wetu BoT & Planning Commission tusaidieni kwa hili asee
 
Nashangaa pamoja na viongozi hawasafiri ila bado dollar iko juuu au importation zimeongezeka
sarafu ina imarika kwa kuongeza balance of payment lazima u export zaidi kuliko ku import then sarafu inapata nguvu zingine porojo za kisiasa
 
tukiweza kubana maeneo yafuatayo lazima shilingi inyanyuke zaidi;
1. Kukomesha Ununuzi wa Mashangingi (tunaagiza kwa USD)
2. Kusitisha matumizi ya USD nchini Kulipa Ada, Kulipia Vibali vya Immigration, Bandarini & Tozo kadhaa kwa USD badala yake tutumie Tsh.
3. Kuzalisha zaidi bidhaa badala ya kuwa mawakala wa bidhaa za nje tu.
4. Kubana matumizi zaidi (Mbio za mwenge, Sikukuu za kitaifa zipunguzwe zaidi)
5. Balozi zetu zitumike kama sehemu ya kuvutia wawekezaji (Wapelekwe mabalozi wenye weledi, elimu & uzoefu wa Biashara/uchumi & diplomasia kidogo sana na sio makada wa chama walioshindwa chaguzi wenye upeo hafifu kuhusu ECONOMIC DIPLOMACY.).
6. Kupunguza japo kwa 20% ya mishahara/pensheni zaviongozi wa ngazi za juu serikalini (wakiwemo wastaafu).
7. Kulazimisha taasisi zote zinazofanya kazi nchini ( za umma & binafsi) kutumia malighafi & bidhaa zinazopatikana hapa nchini badala ya kuagiza toka nje kwa mfano Samani/fenicha, Simu za mezani za TTCL, shirika la ndege la taifa, Air Tanzania.
8. Kupunguza idadi ya mikoa, wilaya, halmashauri.
 
Wachumi nielimisheni kwa hili bado sijaelewa. Pia kuongeza tozo kwenye mihamala ya pesa simuni. Si ndo kuta-discourage wajasiriamali wadogo kufanya biashara maana wengi hutumia mitandao hiyo kutumiana pesa kwenye malipo/manunuzi?
 
Katika hii dunia hakuna vibaka lakini waoga kama Wahindi. Wahindi wanachoamini kwa sasa kwamba kuna dalili za mambo ya Uganda na Iddi Amini kutokezea hapa Tanzania. Mpaka sasa hakuna kiongozi wa Jumuia yoyote ya Kihindi aliyewapa wafuasi wake guarantee ya mali zao. Wametorosha hela zao na wamesimama kuweka benki hizo wanazobabaishia.

Hayo ya import & export ni theory za darasani tu kwa Tanzania mpaka sasa. Hatuna export level itakayoleta impact kwenye uchumi wetu mpaka sasa hivi, japokuwa opportunities za ku export tunazo nyingi tu.

Ushauri wangu ni kuwa viongozi wa juu wa Serikali wafanye mazungumzo na investors wa kweli na genuine business owners wawape guarantee ya investments na savings zao, kwa kipindi hichi kigumu, atleast, while the top man is clearing the bad apples!
 
ndugu ikipendaroho. Asante kwa maoni yako je hatupaswi kuendelea kubana matumiz zaidi ili tupunguze matumiz makubwa ya forex? tunaweza kupunguza kwenye mishahara ya viongozi na mashangingi yapigwe mnada tubaki na landcruiser mkonge (zilizopo) tusinunue mapya kwa sasa.
 
Uongozi hauna hata mwaka mnatoa lawama tufanye kazi kwa bidii tuache kulalamika
 
Chapa kazi mh magufuli ,sh. Itapanda tu ,wanaotaka ipande kwa muujiza wakaitafute huko inakopatikana hapakazitu

Uchumi ni 'kanuni' haibadiliki ,usitarajie Uchumi kupanda tu kwa maneno matupu kama haya yako hapa ..
 
Uongozi hauna hata mwaka mnatoa lawama tufanye kazi kwa bidii tuache kulalamika
Wewe unayeona miezi 8 ni michache, soma historia ya maendeleo ya Dubai. Mabadiliko yalikuwa ndani ya miaka 15 tu. Na ili kuyapata mabadiliko ndani ya miaka 15, kila mwaka kulikuwa na mambo kadhaa makubwa ya kiuchumi yaliyofanyika na yaliyoonekana wazi. Naomba mwisho wa mwaka wa utawala huu unioridheshee mambo makubwa angalao matano ya kiuchumi yatakayokuwa yamefanyika yanayoonekana kwetu sote.
 
The problem mnsuzungumzia uchumi tokea juu. Huku dodoma nimekutana na watu wanalalamika meli haziji chukua ufuta bei imeporomoka toka 3000 hadi 1000?????zao la ufuta limekuwa engine ya uchumi kanda ya kati kwa kipindi sasa.

Tuzungumzie uchumi tokea chini.....na kuumanisha na yanayoendelea....

Tunapoona mizigo ya azam inapungua barabarani ni nini tafsiri yake? Tuendelee kushangilia???

Tunavyozungumzia exportation. Kwa sasa.kwetu it means ufuta...na pengine matunda na unga.these are what makes our shilling stronger

...
Tusizungumzie viwanda ambavyo bado kujengwa....people also

need to eat now..
 
Uchumi ni 'kanuni' haibadiliki ,usitarajie Uchumi kupanda tu kwa maneno matupu kama haya yako hapa ..
Nimefurahia kanuni yako ya kujibu thread ya February mwezi June, by the way pole kwa kutumbuliwa.
 
Utawavutia vp wawekezaji kutoka nje wakati hata wajumbe wenyewe unawakaribisha kama wanafunzi mstarini, wawekezaji wengi kwa sasa wanafunga ofisi zao, na wanahamia nchi zingine wanazoona zinasera nzuri za uwekezaji.JK alizunguuka dunia nzima kuitanga tz ingawa analaumiwa kua safari zake nyingi ni za anasa. Bado tunahitaji Msaada kutoka ng'ambo, tz ilikua haijulkani baadhi ya nchi nyingi huko, hadi uwaambie nimetokea kwenye nchi yenye mlima Kilimanjaro. leo wakisema HATUTAKI BIDHAA ZENU,NA BIDHAA ZETU HATUWAPI. Baada ya mwezi tu tutaanza kuilamu serkali,na kama mnakumbuka wakate EAC inaanziasha wenzetu walitupa ofa kwa bidhaa zetu, tukiweza kupeleka kwa wanatupunguzia kodi kuliko wao kuleta kwetu. Hakika kwa jinsi wanavyobana hali utakua ngumu sana kwa mwananchi wa kawaida, lakini labda wana malengo mazuri, maana unaweza kubana kwa wananchi huduma za kijamii zikawa nzuri, unaweza kubana kwa wanaoishi mijini ukaachia wa vijijini (million 50,50) ili wasio na kazi mijini waludi vijijin wakalime.PIA KWA UBANAJI HUU INGUKUA KWA NCHI ZA KIJAMAA NI SAWA LAKINI KWA NCHI ZA KIBEPARI TUJIANDAE KWA MAUMIVU TU.
Hapo kwenye "sera nzuri za uwekezaji" ndipo tunapopigiwa kila siku na kubaki tunalalama na kushikana mashati wenyewe.
Dangote anataka apewe gas kwa bei ya kisimani, hizi ndizo sera nzuri kwa wawekezaji.
 
Hapo kwenye "sera nzuri za uwekezaji" ndipo tunapopigiwa kila siku na kubaki tunalalama na kushikana mashati wenyewe.
Dangote anataka apewe gas kwa bei ya kisimani, hizi ndiyo sera nzuri kwa wawekezaji.
Sio lazima kuhangaika na wawekezaji kama kina dango, mtu anataka apewe hadi sehemu ya bahari,yaani ajenge bandari yake kwenye nchi ya watu,mtu wa aina hiyo ni hatari sana kwa usalama wa nchi.ninachotamani mimi kuona,angewapa fulsa zaidi wawekezaji wa ndani,asiwabane saana kwenye kodi na kuwatishia kuishi kama masheta maana hawa ndio wanaotoa ajira nyiki,hawa wawekezaji wa nje wanatakiwa kuwanao makini sana,
Nakumbuka kipindi kile kiwanda cha bia kilipobinafsishwa wale makabulu walituingiza mkenge,walisema ngani yetu haina ubora,natokeo yake wana toa ngano A.kusini,sisi mashamba yetu yanakufa,lakini bado hawajifunzi wanataka kumuacha dangote alete mkaa kutoka kulekule,ujinga kabisa.
 
Kwa maono yangu. Japho sio mchumi.serikali kama inabana matumizi, hizo pesa zinazopatikana kwa kubana hayo matumizi . Waongezewe mishahara watumishi wa umma.kutasaidia uongeza mzunguko wa pesa.nina imani kutasaidia kuimarisha shilingi.
 
Ndinani uko sahihi. Serikali yetu iko makini hata kwa mfano kitendo cha kukatalia kiwanda cha Dangote kutaka kuagiza makaa ya mawe toka South Africa wakati makaa ya mawe yapo hapa petu ya kutosha ni moja ya njia ya kupunguza matumizi ya fedha zetu za kigeni pasipo msingi. Viva Magufuli na watendaji wako.
 
Back
Top Bottom