Kuanzisha kampuni

Mrekebishaji

Senior Member
Mar 19, 2009
168
63
Hbr wana JF.
Naomba msaada wa namna ya kuanzisha kampuni ambayo itamilikiwa na watu wawili(in principle), baba na mke. Au ya kumilikiwa na mtu mmoja. Pengine kwa kuraisisha swali ni, je unatakiwa ufanyeje ili uwe na kampuni yako kama vile ilivyo kwa IPP ni ya mengi.


Natanguliza shukrani
 
Hongera sana kwa swali lako zuri. kwanza kabisa uwe unajua unataka kufanya nini. Pili fanya makadirio (rough) ya mapato na matumizi ukiwa nyumbani hii, ni pia na uchunguzi wa soko. ukiridhika; 1. Tafuta sehemu ya kufanyia biashara yako. ingia mkataba wa upangaji kama ni lazima kwa kutumia jina la KAMPUNI yako. Kama kiwanja ni chako basi toa photocopy ya umiliki wa kiwanja chako.
2. Nenda TRA ya karibu kabisa na eneo lako. Hapo omba TIN kama huna kwa jina la kampuni yako. Ila Kama unayo TIN waandikie barua ya kuomba wakufanyie makadirio ya kodi ya mwaka ukiwaeleza matarajio yako ya mapato kwa mwaka. 3. Kwa kuwa Utahitaji kampuni basi rudi brela kasajili jina la kampuni yako upate certificate of Incorporation na nambari ya kampuni yako. 4. Nenda kwa wanasheria au kwa wajuzi ili upate kujitengenezea Memorundum and articles Association ya kampuni yako iliyosajiliwa. 4. jiulize je biashara yangu inahitaji approval toka wizara yoyote? Mf. biashara ya utalii. basi nenda ktk wizara husika huko utapewa maelezo (au nenda kwenye ofisi ya biashara ktk wizara ya Biashara huko utapewa fomu maalum bure itakayokuonyesha kama biashara yako inahitaji wizara au ofisi ya manispaa. Taadhali; ofisi za manispaa huzitoa huduma hizi kwa hongo kubwa sana lakini kwa sheria fomu hizi ni bure). 5. Kama ni kampuni chini ya manispaa utalipia malipo dirishani mostly less than 4,000/=. Hapa utapewa leseni ya biashara siku hiyo hiyo baada ya kukamilisha kuijaza fomu uliyolipia chini ya tsh. 4,000/=.
Shughuli zote ni bure. Kama ni wizarani; utatakiwa kupeleka Business Plan. pamoja na masharti mengine ikiwamo ada maalum. Ngoma iko kwenye Business Plan (ukiniona nitakusaidia). Wizara ikiridhishwa na business plan ya na masharti mengine basi unapewa Leseni ya biashara hiyo. 6. Unapeleka leseni hiyo wizara ya biashara huko utapewa leseni kama ile ya manispaa bure kabisa.
Mengine utayajua ukiwa ktk mzunguko. hasa ya aina ya wamiliki wa biashara kama ni saba , watano au wawili. Hiyo utamwambia mwenye ku-draft Memorundum.
 
Bw. Maji ya shingo majibu yako tayari nimeisha yajibu yote. Tumia njia uliyoitumia kuyapata.
 
Danniair Uko busy tumia wataalamu ufanikishe mambo yako kwa urahisi na ufanisi tuwasiliane nikusaidie kufikia lengo lako la kuwa na kampuni nipigie simu 0755394701
 
Back
Top Bottom