Siku nilipoamua kufunga biashara

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,495
5,532
Ilikuwa April 2017,

Niliamka Asubuhi nikiwa na mawazo mengi sana,Haikuwa mara ya kwanza mm kuamka asubuhi ila siku hii ilikuwa tofauti.Wawili kati ya watu niliokuwa nafanya nao kazi ambao walikuwa na uzoefu waliamua kuacha kazi na kwenda katika kampuni nyingine na nilibaki na timu ndogo ya watu wa chache sana ambao sijui kama na wao walikuwa na mpango wa kuondoka au la.

Hatukuwa na Pesa benki hata ya kuweza kulipia Bills za kawaida na tayari tulikuwa na madeni kadhaa ambayo yalikuwa yanaumiza vichwa vyetu.Vile vile tayari nilishaanza kuchoka hasa baada ya kuona kwamuda kwamba Biashara niliyokuwa nafanya bado ilikuwa haijawez kutengeneza mapato ya uhakika ya kuweza kugharamikia shughuli za kuendesha ofisi.Kwa ufupi hakukuwa na Mauzo kabisa.

Wenzangu ambao nilikuwa nafanya nao kazi hasa ambao niliwaajiri walikuwa wanajua tuna shida ila hawakujua ukubwa wa shida zetu na kwa kweli wazo al kuwaambia kwamba sasa tumeamua kufunga kampuni na kila mmoja aangalie ustaarabu mwingine ni wazo ambalo liliumiza sana moyo wangu.

Nilshajaribu kufikiri zaidi kuhusu namna bora ya kuweza kuhakikisha biashara inaendelea kuwepo ila jitihada nyingi zilikuwa hazina matokeo.Ulikuwa ni wakati wa maamuzi magumu.

Nilijianda kwa unyonge na kuelekea Ofisini ambapo nilikuta wafanyakazi wote wameshawasili.NIliitisha kikao cha wafanyakazi wote nikawaweleza hali halisi ya kampuni na kuwaambi sina namna zaidi ya kuachana na biashara niliyokuwa naifanya.Kwa kweli walipata mshtuko hasa ukizingatia kwamba wengi walikuwa ndio ajira yao ya kwanza na pia walishazoe mazingira ya kazi na tulishakuwa kama ndugu pale ofisini.Hivyo baada ya kuwaambia kwamba tunafunga kampuni moja kwa moja walijaribu kutoa maoni mbalimbali lakini mm nilishafanya maamuzi na ulikuwa ni wakati wa kwenda kufanya jambo jingine.

Baada ya kuwaeleza niliwaomba wote waandika barua ya kuomba kuacha kazi na kisha nitawaapa nyaraka zote za muhimu ikiwa cheti cha huduma bora,barua nzuri ya recommendation na msaada wowote ule ambao watahitaji katika kutafuta ajira mpya.

Baada ya kuwaeleza yote na kunielewa niliwapa nafsi ya kuuliza maswali.Mmoja wao aliniuliza swali ambalo lillinishangaza sana.Aliniuliza WHAT ABOUT YOU.Sasa itakuaje kuhusu WEWE?Kwanza sikutarajia swali kama hilo hivyo nilianza kwa kujaribu kudownplay kisha nikawaambia kwa kiingereza.

"I will have to hold the fort,I am a startup creature and I will move to the next Idea and hopeful the money will come" Kabla ya kuanzisha biashara hii nilishaanza biashara nyingine kadhaa na hata baada ya biasharahi nitaanzisha biashara nyingine.Katika ulimwengu wa biashara na hasa biashara zinazoanza kuna changamoto nyingi hata hivyo changamoto kubwa kuliko zote ni kupata wateja hasa wateja wanaoweza kulipa vizuri.

Ndio maana mara nyingi unapoanzisha biashara unashauriwa sana kuzingatio masoko/wateja kawani unapokuwa na uhakika wa soko basi kutengeneza bidhaa au huduma ni jambo rahisi sana.

Je, umewahi kulazimikakufunga biashara yako iwe ndogo au kubwa? Je, ulijisikiaje? Je kufunga biashara kulikufanya uvunjike moyo wa kuanzisha biashar nyingine? Je, uliendelea kuanzisha biashara mpya?Je umeshakutana na biashara ambayo imekutoa kifedha na kimaisha?Karibu tujadili zaidia.

Iwapo una kampuni ambayo ni Dormant au biashara ambayo unataka kuifunga na unahitaji kupata uzoefu wetu na ushauri tafadhali wasiliana nasi kwa email masokotz@yahoo.com
 
Hii ni promo? Kama, zile hadithi za EFM kila siku, saa, moja, usiku,? Kuna, mdada huwa, anasimulia, mi, huwa, naona ni upuuzi, ni, za, kutunga, hazina, uhalisia, ila, Zika a lot of emotions, na, kuna watu wanaziamini,
Mi nilifikiri unaleta hapa, kitu kilichokutokea, kumbe ni kiki tu, za, kutafuta soko! Bro email za, Yahoo, gmail, hazionyeshi kama, upo serious, daaaa bongo kila, kitu ni janja, janja tu.
 
Hii ni promo? Kama, zile hadithi za EFM kila siku, saa, moja, usiku,? Kuna, mdada huwa, anasimulia, mi, huwa, naona ni upuuzi, ni, za, kutunga, hazina, uhalisia, ila, Zika a lot of emotions, na, kuna watu wanaziamini,
Mi nilifikiri unaleta hapa, kitu kilichokutokea, kumbe ni kiki tu, za, kutafuta soko! Bro email za, Yahoo, gmail, hazionyeshi kama, upo serious, daaaa bongo kila, kitu ni janja, janja tu
Mkuu,naelewa concern yako mkuu,Unaweza kuitazama kama promo,unaweza kuutazama kama mjadala hasa kama umewahi kuanzisha biashara ikafeli na ukafikia hatua ya kuifunga.All in all mm mtandaoni huwa nakuja kutafuta soko/wateja/biashara/fursa na nakushauri hata wewe jiweke katika mtazamo wa namna hiyo kwamba upo mtandaoni kutafuta pesa/soko/fursa/wateja/deals maana kiuhalisia unapoingia mtandaoni unatumia gharama na muda so ni muhimu sana uhakikishe unatumia mtandao kujifunza na kujiongeza.All in all iwapo umekwazika kwa namna yoyote basi haikuwa ni yangu zaidi ya kuleta mjadala hapa jukwaani.Kila la heri na karibu sana.Kuhus Hilo la Email upo sahihi kwamba Hazionyeshi kuwa nipo serious ila kiuhalisia Nipo serious kabisa.
 
Imenitokea mara nyingi sana.

Sometimes unataka kufunga na unamadeni tra so inakuwa kikwazo.
 
Hongera kwa uzi mzuri,

Ningependa kufahamu changamoto za kukosa fedha ambazo zilikupelekea kufunga kampuni yako za kwanza, uliweza kuzitatua vipi pindi ulipokuja kufungua kampuni nyingine?.

Asante.
 
Hongera kwa uzi mzuri,

Ningependa kufahamu changamoto za kukosa fedha ambazo zilikupelekea kufunga kampuni yako za kwanza, uliweza kuzitatua vipi pindi ulipokuja kufungua kampuni nyingine?.

Asante.
Asante kwa swali zuri,kama umeona kitu kwenye uzi basi nimezungumzia swala zema sok au wateja. Kimsingi biashara yoyote ile inapaswa iweze kujiendesha na kutengeneza faida.Na ili ifanye hivyo lazima iwena soko/wateja/mauzo.Katika biashara ambazo nilifanya baada ya kufunga hii si kwamba hili tatizo lilitatulika bali nilibadilisha mkakati na kuwekeza na kuangalia zaidi katika kupunguza gharma za uendeshaji.

Hii imenisaidia kupunguza kiwango cha hasara na gharama za uendeshaji.Nimekuwa nikitumia zaidi teknolojia na kujifunza vitu vingi zaidi ili nihakikishe kwamba katika hatua za mwanzo za kutengeneza biashara nahakikisha hasara inakuwa ndogo ili mauzo kidogo niyapatayo yaweza kumudu gharama za uendeshaji.
 
Back
Top Bottom