Kuanzia Januari 2016 wasanii kulipwa na Redio na Televisheni zitakazotumia nyimbo zao

matumbo

JF-Expert Member
Jul 9, 2011
7,225
3,944
attachment.php

Kuanzia mwakani wasanii watalipwa na radio na TV kwa nyimbo zao au tamthiliya kuonyeshawa. Hii imefikiwa leo kwa ushirikiano wa Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na Wizara ya Habari na Sanaa.

Na bado mambo mazuri yanaandaliwa kwa wasanii ili wafaidike na kazi zao kwenye kila sehemu zitakapotumika.

Magufuli aliwaambia wasanii sitowatumia ila nitawasaidia. Anaanza kutimiza mambo yake.
 
Attachments

  • CWW3WN5WUAAHHpD.jpg
    CWW3WN5WUAAHHpD.jpg
    23.6 KB · Views: 5,111
vp hawa wasanii mbona hawalipi kodi ya mapato kama walipavyo waajiriwa na wafanya biashara?
 
ufafanuzi please, analipa yeye kama msanii au mtumiaji au mnunuzi ndiye anaye lipa? nafikiri muuliza swali alimaanisha PAYE. Inatakiwa wakifanya onyesho popote 13% yamapato yote inaenda TRA, sawa? hapo tutaenda sawa
hehehheeee nasubiri jibu
 
ufafanuzi please, analipa yeye kama msanii au mtumiaji au mnunuzi ndiye anaye lipa? nafikiri muuliza swali alimaanisha PAYE. Inatakiwa wakifanya onyesho popote 13% yamapato yote inaenda TRA, sawa? hapo tutaenda sawa

Kazi ya msanii inapobandikwa stika na TRA inamaana wameshamkata kodi yao iwe tape au cd. Kuhusu shows sio zote zialipiwa kodi maana zingine zinaandaliwa kienyeji ila show kubwa lazima ulipie kibali ndio mapato yenyewe kwa serikali.
 
Duu ngoja nichane sasa napanda juu namwaga vitunguu kila mmoja apate chake tusilete kujuana kwani...... aisee nilikuwa mkali ngoja niende studio
 
Nafikiri hatujaelewana sehemu moja hiyo stika ya tra pesa analipa nani, mfano CD nainunua kwa sh 5000 ambayo ina include 18% kodi. hapo ni mie nimeilipa hiyo kodi wala siyo msanii. Pia kama wamekubaliana kulipwa kwenye kila wimbo utakao chezwa kwenye tv au radio basi wakubali kuwa na EFD mashine. tiketi zao zote viwe na nembo ya tra.

Kazi ya msanii inapobandikwa stika na TRA inamaana wameshamkata kodi yao iwe tape au cd. Kuhusu shows sio zote zialipiwa kodi maana zingine zinaandaliwa kienyeji ila show kubwa lazima ulipie kibali ndio mapato yenyewe kwa serikali.
 
Na radio zinazoweza kulipa wasanii nichache sana, kitakachofuata hata wasanii waliokuwa wanasikikasikika kwenye viredio wanapata show wanaingiza hata miambilimbili watakosa kabisa. Maana kitakachobaki ni kupiga tu nyimbo za majuu na Congo teh teh teh!

Haya mambo yanahitaji maandalizi mazuri, serikali ije na mkakati wa kuzisaidia radio hata kwa ruzuku kabla ya kuanza kuzibana na masharti kama haya wakati uhalisia wanaufahamu.

Wacha tusubiri
 
...msitegemee kuendelea kusikiliza bongo flava zinatawala vituo vya radio na television tena,zitaanza kusikika moja moja!
 
Nafikiri hatujaelewana sehemu moja hiyo stika ya tra pesa analipa nani, mfano CD nainunua kwa sh 5000 ambayo ina include 18% kodi. hapo ni mie nimeilipa hiyo kodi wala siyo msanii. Pia kama wamekubaliana kulipwa kwenye kila wimbo utakao chezwa kwenye tv au radio basi wakubali kuwa na EFD mashine. tiketi zao zote viwe na nembo ya tra.

OK ni hivi.. Unapotaka kuingiza sokoni kazi yao siku hizi lazima uwe na stika maalum ya tra ambayo haitolewi bure unailipia kila kazi inabandikwa stika ambayo unailipia tra au unainunua na ndio kodi yenyewe. Kwenye tv au radio kuna mfumo umewekwa wa kuhesabu rotation ya kila kazi ya ndani na nje kuna kampuni ya pfunk ndio inadeal na hilo so kila hesabu itapigwa mpaka mgao wa tra ni kama matangazo yanavyohesabiwa rotation yake. Wasanii ata wanapouza miito ya simu kuna pesa inakatwa bila wao kuosubmit.
 
Mwanzo wa watangazaji wa Radio kupiga macharanga.
8
Hiyo income tu kuwalipa watangazaji ni shida,sembuse kulipa wasanii

Tutaweka sheria ,asilimia,80 ya nyimbo zinazopigwa ziwe za bongo.

Sasa hizo redio zitakazogoma kupiga nyimbo kwa malipo wanadhani zinarekodiwa bure?
 
Kuanzia mwakani wasanii watalipwa na radio na TV kwa kazi zao kuchezwa. Hii imefikiwa leo kwa ushirikiano wa wizara ya viwanda na biashara pamoja na wizara ya habari na sanaa.

Na bado mambo mazuri yanaandaliwa kwa wasanii ili wafaidike na kazi zao kwenye kila sehemu zitakapotumika.

Magufuli aliwaambia wasanii sitowatumia ila nitawasaidia. Anaanza kutimiza mambo yake.
Kulipwa watalipwa ila itategemea na mikataba watayoingia na hizo radio na TV.
 
Back
Top Bottom