Kuanzi 1 March tutaweza kuhama mtandao bila ya kubadili namba, Mobile number Portability (MNP)

Wanauhakika gani wa kugonganisha namba mpya toka mtandao mwingine na namba iliyokuwepo katika mtandao anaotaka kujiunga mteja?

Mfano namba yangu ni ya mtandao wa Tigo mfano 0713ABCDEFG halafu nataka kuhamia Airtel lakini kuho kuna mtu ana namba 0787 ABCDEFG, nini hatma ya yule mwenye namba ya Airtel ambayo inafanana na yangu.
Utakuwa umemhamisha kwa nguvu.
 
Yaani hapa inamaana wanatutoa kabisa kutoka mitandao ya voda, tigo, airtel na zantel si ndio mitandao kongwe kwenda halotel na ttcl ila code za mwanza zitakuwa za halotel au ttcl lakini zinazofuata ni zilezile namba za zamani

hapo kwenye nyekundu siyo kweli. Kinachobadilika ni mtandao, namba yote inabaki ileile.
 
afadhali nihame huu mtandao.ila nahofia watakuwa wanachelewa sana kujibu request zitakazokuwa zinapelekwa kwao na mitandao hamiwa maana kwao hata suala dogo tu unaambiwa subiri masaa 72.
 
Munaimanisha kuhama kwa namna ip?
Ina maana ya kubadili laini kua laini moja itakua na uwezo wa kuwa na namba zangu zote za mitandao nilizo nazo na kuwa kwenye laini moja au ndio kivipi? Wadau tupeni majibu!
 
kwa maelezo wa watoa huduma wa voda ili uweze kuhamishwa lazima uwe huna deni lolote, uwe huna pesa m-pawa, na M-pesa, vinginevyo utaendelea kuburutwa
 
Yaani mambo ya teknolojia unaapizia kabisa kuwa haitakaa itokee? Unadhani waliofikia huo muafaka hawakufikiri na kutafuta solutions?

Pia kwa kumsaidia ukiwa voda na namba yako ukihama nayo ukaenda mfano TIGO maana yake kwa voda inakuwa imekufa na TIGO wanakupa line yao mpya ila namba ndo inakuwa ile ile
 
Please be informed mobile number portability service will be available effective 01.03.2017, for more information call 100 or visit any vodashop.
 
Huduma ya Mobile Number Portability itaanza rasmi Tar 01 March 2017.Huduma hii itakuwezehsa kuhamia mtandao wowote ule bila kubadilisha namba yako:

NB:Huu ndo muda wa makampuni ya simu kuboresha huduma zao. Watu wengi walishindwa kuhama mtandao kwa kuhofia namba zao.
tcra-jpg.461648
Tuseme mimi namba yangu ni Voda ya 0767 000 000
Na nimeona Voda Miyeyusho nataka nihamie Tigo labda napewa 0713 000 000,
Swali ni, what if hii tigo niliyopewa ina mtu tayari kwa sasa??
Labda tigo zote za 0655, 0652, 3tc zishachukuliwa
 
Back
Top Bottom