Jinsi ya kuhamia mtandao mwingine bila kubadili namba ya simu

Infopaedia

JF-Expert Member
Oct 28, 2011
1,231
1,487
Huduma ya Kuhamia Mtandao Mwingine wa Simu Bila Kubadili Namba ya Simu ya Kiganjani (MNP)

UTARATIBU WA KUHAMA

Huduma ya hii itakuwezesha kubadili mtoa huduma wako wa simu za kiganjani Tanzania na kubakia na namba yako ileile. Ni huduma ambayo inakuwezesha kubakia na mamba yako bila kujali unatumia mtandao gani hivyo kukuondolea adha ya kuwaataarifu watu wako wa karibu unapobadili mtoa huduma wa simu za kiganjani. Kwa kuwa namba yako ya simu itabaki ilele, basi itakuwa ni kitambulisho chako, yaani NAMBA YAKO, UTAMBULISHO WAKO.

Huduma ya kuhamia mtandao mwingine bila kubadili namba yako itakuwezesha:-
1. Kubaki na namba yako ya awali unapohama kutoka mtoa huduma mmoja kwenda mwingine.

2. Utaweza kuchagua mtoa huduma ambaye unaona anatoa huduma bora zaidi, huduma nzuri kwa wateja, anakidhi matarajio yako na ana ubunifu katika kutoa huduma zake.

3. Kupokea simu na ujumbe mfupi wa maneno bila kujali ni mtandao upi umehamia bila kuwa na haja ya kuwataarifu marafiki, familia na wafanyakazi wenzako au washirika katika shughuli zako kwamba umebadilisha mtoa huduma wako.

4. Kuokoa fedha kwa kuwa hutakuwa na haja ya kununua laini mpya kwa kila mtoa huduma au kuwa na simu ya kiganjani zaidi ya moja.

MASHARTI YA KUHAMA

Mfumo wa kuhamia mtandao mwingine bila kubadili namba ya simu ya kiganjani utatumiwa na wateja wote nchini wanaolipia huduma kwanza na wanaolipia huduma baada ya matumizi. Ili kuingia kwenye mfumo huu, simu ya mtumiaji lazima iwe inatumika, yaani haijafungiwa au kusimamishwa kwa muda.

Ili kutumia huduma hii, inabidi kuzingatia masharti yafuatayo:-

1. Iwapo ni mtumiaji anayelipia kabla ya huduma, yaani Pre-Paid :-

a) Hutaweza kuhama na namba ambayo imefungiwa au kusimamishiwahuduma;

b) Hutaweza kuhama na salio lililopo na utatakiwa kutumia salio hilo kabla yakuhama la sivyo salio lako litapotea; Huduma ya Kuhamia Mtandao Mwingine wa Simu Bila Kubadili Namba ya Simu ya Kiganjani (MNP)

c) Hutaweza kuhama iwapo una mkopo kutoka kwa mtoa huduma wako hapa nchini kama vile chini ya mfumo wa M-pawa na NipigeTafu au mikopo mingine kwa njia ya muda wa maongezi, pesa mtandao na kadhalika;

d) Hutaweza kuhama iwapo namba yako inahusishwa na uhalifu na imefungiwa.

2. Iwapo unatumia huduma kwa utaratibu wa malipo baada ya huduma, yaani Post-Paid ; zingatia masharti yaliyotajwa hapo juu ya wateja wa “pre-paid “ na masharti mengine yafuatayo :-

a) Itabidi ulipe madeni ya matumizi yako kabla ya kuhama;

b) Itabidi ukamilishe masharti ya msingi ya mkataba na mtoa huduma wako wa sasa na kutimiza masharti ya malipo kila mwezi kwa mujibu wa mkataba kabla ya kuhama;

c) Utaendelea kupokea ankara za matumizi hadi namba itakapohamishiwa kwa mtoa huduma mpya. Utapokea ankara ya mwisho hadi siku 60 baada ya kuhamisha namba yako; kisha utapewa mpaka siku 30 za kulipa ankara hizo, vinginevyo utakuwa katika hatari ya uhamaji wako utasitishwa au namba yako kufungiwa.

ZINGATIA YAFUATAYO:

1. Hakuna gharama za kuhama na namba yako isipokuwa. Hata hivyo, kabla ya kuhama itabidi ununue laini mpya ya simu ya kiganjani, yaani “SIM card” kutoka kwa mtoa huduma mpya.

2. Wateja wote wanaotaka kuhama na namba zao na ambao wana salio katika akaunti ya pesa mtandao ni lazima walitoe salio hilo kabla ya kuhama vinginevyo salio litabaki bila mwenyewe na itabidi wafuate mchakato mrefu ili kuweza kupata pesa zao ambazo wakati wote zitakuwa salama hadi watakapokamilisha mchakato huo.

UTARATIBU WA KUHAMA

1. Nenda vituo vya mauzo au kwa wakala anayetambuliwa wa mtoa huduma unakotaka kuhamia na umueleze mhudumu kwamba ungependa kuhama na namba yako.

2. Mhudumu atakutaka ujaze fomu maalum ya maombi (fomu moja). Huduma ya Kuhamia Mtandao Mwingine wa Simu Bila Kubadili Namba ya Simu ya Kiganjani (MNP)

3. Sehemu ya Fomu ya maombi ya kuhama ni tamko rasmi kwamba unakubali kuwa utawajibika kwa madeni yoyote ambayo yanatokana na huduma ulizokuwa unapata kutoka kwa mtoa huduma wako wa awali kama yapo.

4. Utatakiwa kutoa vitu vifuatavyo: -

a) Kitambulisho chenye picha yako – kinaweza kuwa Kitambulisho cha Taifa, Kadi ya Mpiga Kura, Leseni ya Udereva au pasipoti au kitambulisho chochote rasmi kinachotambulika.

b) Simu ya kiganjani inayofanya kazi yenye namba unayotaka kubaki nayo.

5. Iwapo una salio katika akaunti ya pesa mtandao utashauriwa kutoa pesa kabla ya kuhama ili kuepuka usumbufu kama ilivyoelezwa kwenye masharti ya kuhama.

6. Utatakiwa kutuma meseji yenye neno “HAMA” kwenda namba ‘15080’ ambayo ni namba maalum ya kuhama. Msaada utatolewa iwapo utahitajika ili kufanikisha hili.

7. Utapokea meseji kukujulisha kwamba maombi yako yamepokelewa.

8. Iwapo namba yako haikuzuiliwa au kusimamishwa kwa muda kutokana na kutokukamilisha malipo ya madeni ya mtoa huduma wako wa awali, maombi yako yatashughulikiwa na utajulishwa kwa meseji kuhusu maendeleo ya mchakato huu.

9. Mtoa huduma wako mpya wa huduma za simu za kiganjaji atakupatia laini mpya.

10.Ili kuzuia kupokea mihamala ya fedha mtandao wakati wa kuhama, huduma za kifedha zitasitishwa kwa muda mpaka namba ikapohamishwa kwa mtoa huduma mpya, ambapo utatumia huduma zake za fedha mtandao kama utajiunga na huduma zipo.

11.Katika kipindi cha kuhama huduma za kupiga na kupokea simu na ujumbe mfupi zitaendelea kama kawaida.

12.Katika hali ya kawaida uhamaji utakamilika haraka, mara nyingi siku hiyo hiyo au, iwapo utachelewa sana, ndani ya siku mbili za kazi baada ya kukamilisha utaratibu wa maombi. Wakati huo namba yako itakuwa imeshahamishwa kwa mtoa huduma wako mpya na laini yako ya awali haitatumika tena. Utatumiwa ujumbe mfupi kuwa uhamaji umekamika na ubadilishe laini. Huduma ya Kuhamia Mtandao Mwingine wa Simu Bila Kubadili Namba ya Simu ya Kiganjani (MNP)

13.Ikifikia hapo, weka laini mpya uliyopewa na mtoa huduma wako mpya kwenye simu yako. Iwapo huna uhakika wa nini cha kufanya, unaweza kwenda kwa mtoa huduma wako mpya au wakala wake au kuwapigia simu na wataweza kukusaidia.

14.Mchakato umekamilika.
 
Hii huduma itaanza lini hasa kupatikana hapa Tanzania?

Sijasoma yote maana post za hivi nimezisoma sana humu so nadhani yamejirudia yale yale tu.
 
Ina Mzunguko Duuh
Mi nadhani haina mzunguko. Ila ni maelezo mengi tu, yamekaa kiserekali serekali. Kwa kifupi, hakikisha haudaiwa na mtandao wako kama mpesa au mpower. Hakikisha mpesa yako haina hela, andaa kitambulisho chako na hela ya kununua line mpya. Nenda kwa wakala anayeuza na kusajili line za mtandao unaotaka kuhamia. Mueleze shida yako. Ila nina uhakika wengi hawajui, coz inaonekana hii system haiko supported na network providers wengi.
 
Mi nadhani haina mzunguko. Ila ni maelezo mengi tu, yamekaa kiserekali serekali. Kwa kifupi, hakikisha haudaiwa na mtandao wako kama mpesa au mpower. Hakikisha mpesa yako haina hela, andaa kitambulisho chako na hela ya kununua line mpya. Nenda kwa wakala anayeuza na kusajili line za mtandao unaotaka kuhamia. Mueleze shida yako. Ila nina uhakika wengi hawajui, coz inaonekana hii system haiko supported na network providers wengi.
Sawa aisee maana Namuona mzee namba zake zote Zinafanana Yani
 
Mkuu, huu uandishi wako unachosha sana. Sehemu ya kuanza paragraph mpya hufanyi hivyo na sehemu ya kutoanza paragraph mpya unaweka paragraph mpya.

Unaruhusiwa kuanza paragraph mpya kama una wazo jipya. Huwezi kuikata sentensi na kuianzishia paragraph nyingine.

Nimekuelewa kwa taabu sana
 
Mkuu, huu uandishi wako unachosha sana. Sehemu ya kuanza paragraph mpya hufanyi hivyo na sehemu ya kutoanza paragraph mpya unaweka paragraph mpya.

Unaruhusiwa kuanza paragraph mpya kama una wazo jipya. Huwezi kuikata sentensi na kuianzishia paragraph nyingine.

Nimekuelewa kwa taabu sana
Ni kweli mkuu, ila umejitahidi sana. Haya maelezo nime-copy toka TCRA, yamekaa kiserekali serekali. Hahahahaaaa!!!
 
Kama mtandao naotaka kuhamia hiyo namba tayari kuna mtu anaitumia nafanyaje,manake hakuna maelezo ya hilo
 
Kama mtandao naotaka kuhamia hiyo namba tayari kuna mtu anaitumia nafanyaje,manake hakuna maelezo ya hilo
Haiwezekani kukawa na mtu anatumia. Labda hujaelewa wanaposema unahama na number yako. Maana yake unahama mzima mzima na tarakimu zako kumi. Ndio maana wanakwambia haina haja kuwataarifu watu kwamba umehama mtandao au kuwapa number nyingine. Kama ulikuwa Voda, wanaendelea kukupigia kwa number yako ileile na wanakupata. Ila wewe ni tigo na unakwangua vocha za tigo maisha yanaendelea.
 
Haiwezekani kukawa na mtu anatumia. Labda hujaelewa wanaposema unahama na number yako. Maana yake unahama mzima mzima na tarakimu zako kumi. Ndio maana wanakwambia haina haja kuwataarifu watu kwamba umehama mtandao au kuwapa number nyingine. Kama ulikuwa Voda, wanaendelea kukupigia kwa number yako ileile na wanakupata. Ila wewe ni tigo na unakwangua vocha za tigo maisha yanaendelea.

Kwa hyo hapa hadi codes za mtandao husika unaohama nazo mazima let say 0788uvwxyz??
 
Back
Top Bottom