Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,997
- Thread starter
- #21
Mzee ES, karibu na pole ya kupotea na heshima na wewe...! sijasema CCM ni safi, nilisema kuwa kama wapinzani wataendelea kuwa jinsi walivyo, CCM bado ni chaguo la Watanzania wengi (sijabadili msimamo huo!) Pia nilisema kuwa ni kutokuwa mkweli mtu akisema CCM haijafanya jambo lolote zuri kwa wananchi (sijabadili msimamo huo pia) Nilichosema kwenye makala hii (ambayo hujaisoma) ni kuwa mazingira yakiwa sawa CCM itaondoka! Unabii ninauzungumzia siyo wa kwangu wala wa sheikh Yahya, bali ni yale mananeo ya Mwalimu "CCM siyo Mama yangu"! Sikusema pia kuwa CCM itaondoka kama ukungu la hasha, kuna mambo lazima yafanyike! Na msimamo huo bado sijaubadili pia.
Njia kubwa ya kumfundisha mtu siyo tu kumwacha aendelee kuboronga, ni kumweka pembeni na kumuonesha jinsi mambo yanavyopaswa kuwa. Kama matatizo yangekuwa mwalimu mzuri kuliko wote, CCM basi wangekuwa washafuzu! Nafikiri kwa wengine matatizo ni mwalimu mkali ambaye hana huruma! Kama mwanafunzi hafundishi darasani, wakati mwingine tunamhamisha shule au tunampeleka tuition! CCM kwa miaka arobaini imeelewa kidogo, lakini haijajifunza, hadi pale tutakapoipa darasa nje ya serikali ndio wanaweza kuelewa somo la utawala!