BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,007
Ukweli ni kwamba hatujui yatamsaidia vipi mwananchi, lakini yanaweza kabisa kuleta mabadiliko makubwa ya uongozi katika Tanzania. Chama kipya kinaweza kuingia madarakani na kikaja na sera tofauti ambazo zitapunguza au kuondoa kero na manun'guniko mbali mbali ya wananchi kama vile mikataba ambayo haina maslahi kwa Tanzania na Watanzania.
CCM (TANU) imekaa madarakani miaka 46 sasa lakini bado maendeleo yetu ni madogo mno. Tunaweza tukasema wakati wa mwalimu tulikuwa hatuna vianzo vingi vya mapato kama ilivyo sasa. Tunakusanya kodo ya bilioni 260 kwa mwezi, tuna mikataba ya madini ambayo haina maslahi yoyote kwa Tanzania, gesi kuna afadhali kidogo. Ufujaji wa mali ya umma umekithiri, kwa mfani ununuzi wa magari ya kifahari.
Sasa kama CCM itameguka lolote linaweza kutokea, ama kwa manufaa ya Tanzania na Watanzania ama kwa manufaa ya wajanja wachache. Kama nchi inaweza kuongeza ukusanyaji wa mapato hadi kufikia bilioni 260 kwa mwezi na bado wananchi wengi hawaoni mabadiliko yoyote basi kuna kasoro kubwa sana.
Baada ya miaka 46 ya uhuru kuna haja ya CCM kumeguka, hili linaweza kabisa kuwa mwanzo wa mapinduzi ya kweli ndani ya Tanzania, hakuna haja ya kusubiri miaka mingine 46.
Sioni kama kuna usanii wowote, usanii ni kuombea dua CCM iendelee kubaki madarakani na nguvu ilizonazo ili kufuja pesa za walala hoi na kudai eti kumeguka kwa CCM hakutakuwa na manufaa kwa mwananchi. Wote hatulijui hili kunaweza kukawa na manufaa au la.