Krismas mbaya kwa Kikwete

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
302
VIONGOZI mbalimbali wa dini wamemuonya Rais Jakaya Kikwete kwamba matatizo mengi ya kiutawala anayoyapata yanatokana na usaliti wa wasaidizi wake wa karibu huku wakisisitiza serikali itende haki ili kuepusha vurugu.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Mennonite, Stephen Mang’ana amesema baadhi wa viongozi wa CCM na serikali wanamsaliti Rais Kikwete kwa kumpa taarifa za uongo na uchochezi ili wapate nafasi ya kuendelea kuwepo madarakani. (Dk Edward Hosea)?

“Baadhi ya viongozi hawana utashi wa kuongoza, wapo kwa ajili ya kumsaliti Rais Kikwete na kusababisha kuwepo kwa migogoro kila sehemu, kuchochea vurugu na maandamano hasa katika baadhi ya maeneo,” (Makamba)?

Paroko wa kanisa Katoliki parokia ya Mtakatifu Fransisko wa Asizi Mugumu Serengeti, Padri Alois Magabe alisema vitendo vya uchakachuaji vinazaa dhuluma, uonevu,manyanyaso na mateso kwa watu wengi na ni matunda ya nguvu ya shetani aliyeteka nyoyo za watendaji.

Alisema uchakachuaji wa mambo yanayogusa jamii una madhara makubwa kwa jamii husika na wanaofanya hayo hawana roho ya Mungu ndani yao, kwa kuwa ni mateka wa ibilisi na kuzaliwa kwa Kristo kunatakiwa kuwabadilisha.

“Hata zamani uchakachuaji ulikuwepo, Eva alimchakachua Adamu kwa kutumiwa na shetani na matokeo yake dhambi iliingia duniani na mateso yakaanza na wanaofanya kwa sasa vitendo hivyo vinavyoleta mateso kwa jamii wanahitaji kuzaliwa upya na Kristo,”

“Vitendo vya uchakachuaji si vizuri kwa kuwa vinabadili haki na kuleta dhuluma ,uonevu,ukatili,na maisha magumu kwa watu. Si vya kunyamazia lazima tuwatake wahusika wazaliwe upya na Kristo mwenye uweza wa ajabu,” alisema bila kufafanua uchakachuaji upi.

Mkururugenzi wa Shirika la Familia la Farijika nchini Tanzania na Kenya, Padri Baptiste Mapunda alisema viongozi wa siasa ndio wanaochochea udini. Padri Mapunda alisema viongozi wa siasia wamekuwa wakiibua hoja kwamba nchi ina udini ili waendelee kutawala.

“Nchi haina udini kama wanavyodai wanasiasa, wanatapatapa tu, walitakiwa watuulize sisi viongozi wa dini kama kweli nchi hii ina udini.

Alikwenda mbali na kusema viongozi wa siasa wanataka kuleta vita ya udini iliyokemewa vikali na serikali ya awamu ya kwanza ya hayati Mwalimu Julius Nyerere na akawataka Watanzania kuikataa dhambi hiyo.

Kuhusu katiba, alisema umefikia wakati kwa Watanzania wote kushirikishwa katika uundwaji wa katiba mpya na si kuziba kubadilisha vipengele.

Alisema hivi sasa nchi inaelekea kubaya hadi kufikia hatua Jeshi la Polisi kuwapiga wabunge na wanafunzi wanaozungumza mambo kwa maslahi ya taifa na afafanisha matendo hayo na utumwa.

Mwadhama Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Eusebio Nzigilwa alisema hatua ya mtandao wa Wekileaks kuingia nchini na kutoa siri za serikali na viongozi wake ni fundisho kwa viongozi wabadhirifu.

Kuhusu Katiba, alisema: “Katiba sio Biblia, ni maandishi yaliyoandikwa na wanadamu na kila mwanadamu anaweza kukifanyia mabadiliko kitu alichokiandaa.”

Alisema katiba ya nchi inaweza kubadilishwa muda wowote kulingana na mahitaji ya wananchi ambapo madai ya katiba mpya yameanza kupata baraka ya viongozi wa juu serikalini baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kukusudia kumshauri Rais kuhusu suala hilo.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF) Zakaria Kakobe alisema tathmini zilizofanywa baada ya uchaguzi mkuu hazikuwa za haki.
Kakobe alisema tathmini hizo zililenga kumjenga mgombea wa chama tawala ambaye anadai hakustahili kupewa haki hiyo.

Akaongeza:“Chanzo cha machafuko ni inapofikia mtu amepewa haki isiyokuwa yake na yule anayestahili haki hiyo akanyimwa,”.

"Jamii inatakiwa kuondokana na fikra potofu za chama kimoja kushika hatama ya uongozi, huo ni ukale, na hiki ni kizazi kingine,” alisema Kakobe.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Katoliki, Mwashamu Kadinali Pengo,
Alisema yeyote anayehubiri amani, lazima kwanza awe na amani moyoni mwake na suala la kuleta ama kulinda amani ni jukumu la kila mtu na haiwezi kuletwa na viongozi au mataifa makubwa kama ambavyo baadhi ya watu wanafikiria.

“Amani haiji kwa mabavu bali kwa paji la Mwenyenzi Mungu, amani haitegemei wenye mamlaka bali ni kila mmoja wetu bila kujali mali zetu, ilimradi tumtumikie bwana na kutenda mema.

Askofu wa Mkuu wa Kanisa la Anglikana, Dk Valentino Mokiwa aliunga mkono hatua zinazochukuliwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kwa kuwataka wananchi waliochukua viwanja vya wazi kuvirudisha.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi.
 
Askofu Mkuu wa Kanisa la Mennonite, Stephen Mang'ana amesema baadhi wa viongozi wa CCM na serikali wanamsaliti Rais Kikwete kwa kumpa taarifa za uongo na uchochezi ili wapate nafasi ya kuendelea kuwepo madarakani. (Dk Edward Hosea)?

"Baadhi ya viongozi hawana utashi wa kuongoza, wapo kwa ajili ya kumsaliti Rais Kikwete na kusababisha kuwepo kwa migogoro kila sehemu, kuchochea vurugu na maandamano hasa katika baadhi ya maeneo," (Makamba)?

Paroko wa kanisa Katoliki parokia ya Mtakatifu Fransisko wa Asizi Mugumu Serengeti, Padri Alois Magabe alisema vitendo vya uchakachuaji vinazaa dhuluma, uonevu,manyanyaso na mateso kwa watu wengi na ni matunda ya nguvu ya shetani aliyeteka nyoyo za watendaji.

Alisema uchakachuaji wa mambo yanayogusa jamii una madhara makubwa kwa jamii husika na wanaofanya hayo hawana roho ya Mungu ndani yao, kwa kuwa ni mateka wa ibilisi na kuzaliwa kwa Kristo kunatakiwa kuwabadilisha.

"Hata zamani uchakachuaji ulikuwepo, Eva alimchakachua Adamu kwa kutumiwa na shetani na matokeo yake dhambi iliingia duniani na mateso yakaanza na wanaofanya kwa sasa vitendo hivyo vinavyoleta mateso kwa jamii wanahitaji kuzaliwa upya na Kristo,"

"Vitendo vya uchakachuaji si vizuri kwa kuwa vinabadili haki na kuleta dhuluma ,uonevu,ukatili,na maisha magumu kwa watu. Si vya kunyamazia lazima tuwatake wahusika wazaliwe upya na Kristo mwenye uweza wa ajabu," alisema bila kufafanua uchakachuaji upi.

Mkururugenzi wa Shirika la Familia la Farijika nchini Tanzania na Kenya, Padri Baptiste Mapunda alisema viongozi wa siasa ndio wanaochochea udini. Padri Mapunda alisema viongozi wa siasia wamekuwa wakiibua hoja kwamba nchi ina udini ili waendelee kutawala.

"Nchi haina udini kama wanavyodai wanasiasa, wanatapatapa tu, walitakiwa watuulize sisi viongozi wa dini kama kweli nchi hii ina udini.

Alikwenda mbali na kusema viongozi wa siasa wanataka kuleta vita ya udini iliyokemewa vikali na serikali ya awamu ya kwanza ya hayati Mwalimu Julius Nyerere na akawataka Watanzania kuikataa dhambi hiyo.

Kuhusu katiba, alisema umefikia wakati kwa Watanzania wote kushirikishwa katika uundwaji wa katiba mpya na si kuziba kubadilisha vipengele.

Alisema hivi sasa nchi inaelekea kubaya hadi kufikia hatua Jeshi la Polisi kuwapiga wabunge na wanafunzi wanaozungumza mambo kwa maslahi ya taifa na afafanisha matendo hayo na utumwa.

Mwadhama Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Eusebio Nzigilwa alisema hatua ya mtandao wa Wekileaks kuingia nchini na kutoa siri za serikali na viongozi wake ni fundisho kwa viongozi wabadhirifu.

Kuhusu Katiba, alisema: "Katiba sio Biblia, ni maandishi yaliyoandikwa na wanadamu na kila mwanadamu anaweza kukifanyia mabadiliko kitu alichokiandaa."

Alisema katiba ya nchi inaweza kubadilishwa muda wowote kulingana na mahitaji ya wananchi ambapo madai ya katiba mpya yameanza kupata baraka ya viongozi wa juu serikalini baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kukusudia kumshauri Rais kuhusu suala hilo.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF) Zakaria Kakobe alisema tathmini zilizofanywa baada ya uchaguzi mkuu hazikuwa za haki.
Kakobe alisema tathmini hizo zililenga kumjenga mgombea wa chama tawala ambaye anadai hakustahili kupewa haki hiyo.

Akaongeza:"Chanzo cha machafuko ni inapofikia mtu amepewa haki isiyokuwa yake na yule anayestahili haki hiyo akanyimwa,".

"Jamii inatakiwa kuondokana na fikra potofu za chama kimoja kushika hatama ya uongozi, huo ni ukale, na hiki ni kizazi kingine," alisema Kakobe.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Katoliki, Mwashamu Kadinali Pengo,
Alisema yeyote anayehubiri amani, lazima kwanza awe na amani moyoni mwake na suala la kuleta ama kulinda amani ni jukumu la kila mtu na haiwezi kuletwa na viongozi au mataifa makubwa kama ambavyo baadhi ya watu wanafikiria.

"Amani haiji kwa mabavu bali kwa paji la Mwenyenzi Mungu, amani haitegemei wenye mamlaka bali ni kila mmoja wetu bila kujali mali zetu, ilimradi tumtumikie bwana na kutenda mema.

Askofu wa Mkuu wa Kanisa la Anglikana, Dk Valentino Mokiwa aliunga mkono hatua zinazochukuliwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kwa kuwataka wananchi waliochukua viwanja vya wazi kuvirudisha.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi.

dini na siasa vinaingiliana? au maaskofu wanaposema tusichanganye dini na siasa huwa na maana gani?
 
Penye dhuluma hakuna haki na pasipo haki hakuna amani na utulivu......................................

Wanaoasa amani wangeelekeza nguvu zao zote kujenga misingi ya haki na kuheshimiana tu..baragumu la amani na utulivu bila ya kukemea maovu ni sawasawa na kuendesha mtumbwi baharini bila ya makasia.................
 
Penye dhuluma hakuna haki na pasipo haki hakuna amani na utulivu......................................

Wanaasa amani wangeelekeza nguvu zao kujenga misingi ya haki ya kuheshimiana tu..baraguju la amani na utulivu bila ya kukemea maovu ni sawasawa na kuendesha mtumbwi bila ya makasia.................

why in this time, not for Mkapa?
 
dini na siasa vinaingiliana? au maaskofu wanaposema tusichanganye dini na siasa huwa na maana gani?
Jaribu kutofautisha DINI na UDINI ni vitu viwili tofauti, dini ni mafundisho ya imani ila udini ni uchonganishi baina ya dini na dini (tofauti) unaendana na kudharau mafundisho ya dini nyingine.
 
Baadhi ya viongozi wa dini, pia ni wanafiki kwa kuwatupia wasaidizi wake, badala ya kusema ukweli kuwa tatizo ni kikwete mwenyewe, Kwa nini wanaogopa kusema ukweli? Tabia/miendendo ya mtawala inaimpact hata kwa wale waliochini yake. Mfano kama mtawala ni mwizi basi hata wale waliochini yake watakuwa na tabia ya udokozi na nk. Wasaidizi wa kikwete wanaiga kutoka kwa bosi. SIONI SABABU YA KUWALAUMU WASAIDIZI WAKE, WAMLAUMU KIKWETE MWENYEWE. Unafiki mbaya.
 
A,/2'_*Angekua na uwezo wa kuichakachua christmas basi angefanya hivyo, maskini wee mambo haya yana mpata pabaya kweli..why today? huyu ndie atakae tupeleka kubaya, ameshaanza ku-side na upande flani ivi
 
Kweli bw. Masauni> ukiona mtu anawateua mwenyewe, jua mwenyewe karidhika, hawezi kuwa na mtu asiyemjua! Viongozi wa dini hawako sincere hapa, wanazunguka pembeni, they don't hit the point directly. Waoga, wanafiki
 
A,/2'_*Angekua na uwezo wa kuichakachua christmas basi angefanya hivyo, maskini wee mambo haya yana mpata pabaya kweli..why today? huyu ndie atakae tupeleka kubaya, ameshaanza ku-side na upande flani ivi
Sio atakae tupeleka, mbona ameshatupeleka kubaya siku nyingi. Niliwahi kusema katika moja ya post zangu kwamba kumrudisha kikwete madarakani ni grave mistake ambayo watanzania tutaifanya, and we did mistake already. Na bomu litakalolipuka siku za usoni litakuwa na madhara makubwa mno.
 
Masauni hope ulikua sahihi sana, huyu jamaa wala si watendaji wake ni yeye mwenyewe ndo hafai na hawezi, si anatuhumiwa kutaka kumpa uwaziri Salma na Unaibu balozi Ridhiwan? acha uchafu mwingine wa kusimama majukwaani na kusema kuna udini, sijui hua anauona ndotoni! mmh haya, nimefurahi sana alipoacha kuhutubia wala kupngea chochote kwa jamii since then...
 
Viongozi wa dini kazi yao ni kuhubiri amani na kukemea maovu, haijalishi maovu yamefanywa na nani, awe mwana siasa au la. Kazi yao ni kuwafanya viongozi wa kidunia waongoze watu wao kulingana na mapenzi ya Mungu.
 
Ninaomba rais Kikwete asichukulie ujumbe huu kama 'udini'. Naomba afungue mawazo yake na kuona kuwa hii ni changamoto ambayo serikali yake inapaswa kuifanyia kazi kwa ajili ya mustakabali mwema wa watanzania wote.
 
Nahisi JK anawakati mgumu sana, kwani ni ajabu kauli za 'JK ni chaguo la Mungu' zinapotea ghafla mno, na huu ni mwanzo tu. Dhuluma imezidi
 
dini na siasa vinaingiliana? au maaskofu wanaposema tusichanganye dini na siasa huwa na maana gani?

shirikisha brain wewe......
Sio kila lisemwalo na askofu dhidi ya ustaadh JK ni kuchanganya dini na siasa. Ingekua hivyo hao waislam wasingeandika rasimu ya katiba ambayo kwa vyovyote 80 yake lazima iwe siasa. Anza kujifunza kuchanganya dini na siasa maana yake nn kabla ya kujibu hoja zenye nature hii
 
dini na siasa vinaingiliana? au maaskofu wanaposema tusichanganye dini na siasa huwa na maana gani?

Laiti tungejua dini na siasa viko kwa sababu gani.Ki mantiki vyote vinafanana and have one purpose, human enslavement.Kwa mazingira feki tuliyojengewa, ni tofauti,lakini katika uhalisia wa mambo, ni kaka na dada.
 
Ana hali mbaya na ndo maana kashindwa kutoa hata salaam za x-mas.Acha wamseme

VIONGOZI mbalimbali wa dini wamemuonya Rais Jakaya Kikwete kwamba matatizo mengi ya kiutawala anayoyapata yanatokana na usaliti wa wasaidizi wake wa karibu huku wakisisitiza serikali itende haki ili kuepusha vurugu.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Mennonite, Stephen Mang’ana amesema baadhi wa viongozi wa CCM na serikali wanamsaliti Rais Kikwete kwa kumpa taarifa za uongo na uchochezi ili wapate nafasi ya kuendelea kuwepo madarakani. (Dk Edward Hosea)?

“Baadhi ya viongozi hawana utashi wa kuongoza, wapo kwa ajili ya kumsaliti Rais Kikwete na kusababisha kuwepo kwa migogoro kila sehemu, kuchochea vurugu na maandamano hasa katika baadhi ya maeneo,” (Makamba)?

Paroko wa kanisa Katoliki parokia ya Mtakatifu Fransisko wa Asizi Mugumu Serengeti, Padri Alois Magabe alisema vitendo vya uchakachuaji vinazaa dhuluma, uonevu,manyanyaso na mateso kwa watu wengi na ni matunda ya nguvu ya shetani aliyeteka nyoyo za watendaji.

Alisema uchakachuaji wa mambo yanayogusa jamii una madhara makubwa kwa jamii husika na wanaofanya hayo hawana roho ya Mungu ndani yao, kwa kuwa ni mateka wa ibilisi na kuzaliwa kwa Kristo kunatakiwa kuwabadilisha.

“Hata zamani uchakachuaji ulikuwepo, Eva alimchakachua Adamu kwa kutumiwa na shetani na matokeo yake dhambi iliingia duniani na mateso yakaanza na wanaofanya kwa sasa vitendo hivyo vinavyoleta mateso kwa jamii wanahitaji kuzaliwa upya na Kristo,”

“Vitendo vya uchakachuaji si vizuri kwa kuwa vinabadili haki na kuleta dhuluma ,uonevu,ukatili,na maisha magumu kwa watu. Si vya kunyamazia lazima tuwatake wahusika wazaliwe upya na Kristo mwenye uweza wa ajabu,” alisema bila kufafanua uchakachuaji upi.

Mkururugenzi wa Shirika la Familia la Farijika nchini Tanzania na Kenya, Padri Baptiste Mapunda alisema viongozi wa siasa ndio wanaochochea udini. Padri Mapunda alisema viongozi wa siasia wamekuwa wakiibua hoja kwamba nchi ina udini ili waendelee kutawala.

“Nchi haina udini kama wanavyodai wanasiasa, wanatapatapa tu, walitakiwa watuulize sisi viongozi wa dini kama kweli nchi hii ina udini.

Alikwenda mbali na kusema viongozi wa siasa wanataka kuleta vita ya udini iliyokemewa vikali na serikali ya awamu ya kwanza ya hayati Mwalimu Julius Nyerere na akawataka Watanzania kuikataa dhambi hiyo.

Kuhusu katiba, alisema umefikia wakati kwa Watanzania wote kushirikishwa katika uundwaji wa katiba mpya na si kuziba kubadilisha vipengele.

Alisema hivi sasa nchi inaelekea kubaya hadi kufikia hatua Jeshi la Polisi kuwapiga wabunge na wanafunzi wanaozungumza mambo kwa maslahi ya taifa na afafanisha matendo hayo na utumwa.

Mwadhama Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Eusebio Nzigilwa alisema hatua ya mtandao wa Wekileaks kuingia nchini na kutoa siri za serikali na viongozi wake ni fundisho kwa viongozi wabadhirifu.

Kuhusu Katiba, alisema: “Katiba sio Biblia, ni maandishi yaliyoandikwa na wanadamu na kila mwanadamu anaweza kukifanyia mabadiliko kitu alichokiandaa.”

Alisema katiba ya nchi inaweza kubadilishwa muda wowote kulingana na mahitaji ya wananchi ambapo madai ya katiba mpya yameanza kupata baraka ya viongozi wa juu serikalini baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kukusudia kumshauri Rais kuhusu suala hilo.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF) Zakaria Kakobe alisema tathmini zilizofanywa baada ya uchaguzi mkuu hazikuwa za haki.
Kakobe alisema tathmini hizo zililenga kumjenga mgombea wa chama tawala ambaye anadai hakustahili kupewa haki hiyo.

Akaongeza:“Chanzo cha machafuko ni inapofikia mtu amepewa haki isiyokuwa yake na yule anayestahili haki hiyo akanyimwa,”.

"Jamii inatakiwa kuondokana na fikra potofu za chama kimoja kushika hatama ya uongozi, huo ni ukale, na hiki ni kizazi kingine,” alisema Kakobe.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Katoliki, Mwashamu Kadinali Pengo,
Alisema yeyote anayehubiri amani, lazima kwanza awe na amani moyoni mwake na suala la kuleta ama kulinda amani ni jukumu la kila mtu na haiwezi kuletwa na viongozi au mataifa makubwa kama ambavyo baadhi ya watu wanafikiria.

“Amani haiji kwa mabavu bali kwa paji la Mwenyenzi Mungu, amani haitegemei wenye mamlaka bali ni kila mmoja wetu bila kujali mali zetu, ilimradi tumtumikie bwana na kutenda mema.

Askofu wa Mkuu wa Kanisa la Anglikana, Dk Valentino Mokiwa aliunga mkono hatua zinazochukuliwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kwa kuwataka wananchi waliochukua viwanja vya wazi kuvirudisha.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi.
 
Nawapongeza sana viongozi wa Madhehebu ya Dini kwa kuingilia kati kutimiza moja ya Jukumulao lakukemea maovu katika Jamii.Maana wasipoanza kuangalia ustawi wa amani wa nchi wanaweza kukosa pahala pa kuhubiria neno la Mungu.

Viongo wa Dini mmetaja wasaidizi wake, mimi na nafikiri sababu kubwa ni Rais, Ukiona mtoto anaiba na baba anakaa kimya Ujue nyumba aishimo baba kajengewa na MTOTO kwa pesa ya wizi.
 
Back
Top Bottom