Krismas mbaya kwa Kikwete

Sijawahi ona Mashehe wakikemea serikali ya Kikwete kazi yao ni kusifia tu au wao wanaona maisha ni mswano tu.
 
wakuu... mimi nadhani madai kama ya katiba ni haki kwa kila asasi kuwa na matakwa nayo kwani hutimiza yale malengo ya wananchi.... hivyo madhehebu kama ya dini yakidai katiba sio kuingiza dini katika siasa.... hata wanasiasa kupitia vyama vyao wanajukumu la kudai katiba... hivyo tuwe makini tunaposema au kuhoji matamko ya viongozi wa dini kudai katiba mpya.... hata wafungwa nao wanahaki ya kudai katiba hii
 
Hivi na padre Slaa naye kasemaje? watalia sana maana padre mwenzao kashindwa, na yeyote atakayeletwa na kanisa au msikiti atashindwa maana nchi hii haina dini.
 
Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF) Zakaria Kakobe alisema tathmini zilizofanywa baada ya uchaguzi mkuu hazikuwa za haki.
Kakobe alisema tathmini hizo zililenga kumjenga mgombea wa chama tawala ambaye anadai hakustahili kupewa haki hiyo.

Akaongeza:"Chanzo cha machafuko ni inapofikia mtu amepewa haki isiyokuwa yake na yule anayestahili haki hiyo akanyimwa,".

"Jamii inatakiwa kuondokana na fikra potofu za chama kimoja kushika hatama ya uongozi, huo ni ukale, na hiki ni kizazi kingine," alisema Kakobe.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Katoliki, Mwashamu Kadinali Pengo,
Alisema yeyote anayehubiri amani, lazima kwanza awe na amani moyoni mwake na suala la kuleta ama kulinda amani ni jukumu la kila mtu na haiwezi kuletwa na viongozi au mataifa makubwa kama ambavyo baadhi ya watu wanafikiria.

"Amani haiji kwa mabavu bali kwa paji la Mwenyenzi Mungu, amani haitegemei wenye mamlaka bali ni kila mmoja wetu bila kujali mali zetu, ilimradi tumtumikie bwana na kutenda mema.


Chanzo: Gazeti la Mwananchi.[/QUOTE]

Maaskofu inabidi waendelee kuisema vizuri uongozi wa nchi hii hasa kipindi hiki, kuna dalili mbaya sana ya UDINI katika nchi hii, hasa kuanzia kipindi cha awamu ya nne. Serikali ya awamu hii inajifanya ya kiitelijensia zaidi wakati hakuna lolote la maana zaidi ya UDINI tunaoushuhudia sasa...
Kikwete na serikali yako badilini mwelekeo tuijenge nchi..
merry x-mass:party:
 
ni kweli mkuu, lakini lazima ujue kuwa kumtukana mtu si lazima unchagulie tusi, maana yake ni kuwa wao wameshafikisha ujumbe, mtoto wa samaki ni samaki pia wala hawezi kuwa tumbiri
Baadhi ya viongozi wa dini, pia ni wanafiki kwa kuwatupia wasaidizi wake, badala ya kusema ukweli kuwa tatizo ni kikwete mwenyewe, Kwa nini wanaogopa kusema ukweli? Tabia/miendendo ya mtawala inaimpact hata kwa wale waliochini yake. Mfano kama mtawala ni mwizi basi hata wale waliochini yake watakuwa na tabia ya udokozi na nk. Wasaidizi wa kikwete wanaiga kutoka kwa bosi. SIONI SABABU YA KUWALAUMU WASAIDIZI WAKE, WAMLAUMU KIKWETE MWENYEWE. Unafiki mbaya.
 
VIONGOZI mbalimbali wa dini wamemuonya Rais Jakaya Kikwete kwamba matatizo mengi ya kiutawala anayoyapata yanatokana na usaliti wa wasaidizi wake wa karibu huku wakisisitiza serikali itende haki ili kuepusha vurugu.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Mennonite, Stephen Mang’ana amesema baadhi wa viongozi wa CCM na serikali wanamsaliti Rais Kikwete kwa kumpa taarifa za uongo na uchochezi ili wapate nafasi ya kuendelea kuwepo madarakani. (Dk Edward Hosea)?

“Baadhi ya viongozi hawana utashi wa kuongoza, wapo kwa ajili ya kumsaliti Rais Kikwete na kusababisha kuwepo kwa migogoro kila sehemu, kuchochea vurugu na maandamano hasa katika baadhi ya maeneo,” (Makamba)?

Paroko wa kanisa Katoliki parokia ya Mtakatifu Fransisko wa Asizi Mugumu Serengeti, Padri Alois Magabe alisema vitendo vya uchakachuaji vinazaa dhuluma, uonevu,manyanyaso na mateso kwa watu wengi na ni matunda ya nguvu ya shetani aliyeteka nyoyo za watendaji.

Alisema uchakachuaji wa mambo yanayogusa jamii una madhara makubwa kwa jamii husika na wanaofanya hayo hawana roho ya Mungu ndani yao, kwa kuwa ni mateka wa ibilisi na kuzaliwa kwa Kristo kunatakiwa kuwabadilisha.

“Hata zamani uchakachuaji ulikuwepo, Eva alimchakachua Adamu kwa kutumiwa na shetani na matokeo yake dhambi iliingia duniani na mateso yakaanza na wanaofanya kwa sasa vitendo hivyo vinavyoleta mateso kwa jamii wanahitaji kuzaliwa upya na Kristo,”

“Vitendo vya uchakachuaji si vizuri kwa kuwa vinabadili haki na kuleta dhuluma ,uonevu,ukatili,na maisha magumu kwa watu. Si vya kunyamazia lazima tuwatake wahusika wazaliwe upya na Kristo mwenye uweza wa ajabu,” alisema bila kufafanua uchakachuaji upi.

Mkururugenzi wa Shirika la Familia la Farijika nchini Tanzania na Kenya, Padri Baptiste Mapunda alisema viongozi wa siasa ndio wanaochochea udini. Padri Mapunda alisema viongozi wa siasia wamekuwa wakiibua hoja kwamba nchi ina udini ili waendelee kutawala.

“Nchi haina udini kama wanavyodai wanasiasa, wanatapatapa tu, walitakiwa watuulize sisi viongozi wa dini kama kweli nchi hii ina udini.

Alikwenda mbali na kusema viongozi wa siasa wanataka kuleta vita ya udini iliyokemewa vikali na serikali ya awamu ya kwanza ya hayati Mwalimu Julius Nyerere na akawataka Watanzania kuikataa dhambi hiyo.

Kuhusu katiba, alisema umefikia wakati kwa Watanzania wote kushirikishwa katika uundwaji wa katiba mpya na si kuziba kubadilisha vipengele.

Alisema hivi sasa nchi inaelekea kubaya hadi kufikia hatua Jeshi la Polisi kuwapiga wabunge na wanafunzi wanaozungumza mambo kwa maslahi ya taifa na afafanisha matendo hayo na utumwa.


Mwadhama Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Eusebio Nzigilwa alisema hatua ya mtandao wa Wekileaks kuingia nchini na kutoa siri za serikali na viongozi wake ni fundisho kwa viongozi wabadhirifu.

Kuhusu Katiba, alisema: “Katiba sio Biblia, ni maandishi yaliyoandikwa na wanadamu na kila mwanadamu anaweza kukifanyia mabadiliko kitu alichokiandaa.”

Alisema katiba ya nchi inaweza kubadilishwa muda wowote kulingana na mahitaji ya wananchi ambapo madai ya katiba mpya yameanza kupata baraka ya viongozi wa juu serikalini baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kukusudia kumshauri Rais kuhusu suala hilo.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF) Zakaria Kakobe alisema tathmini zilizofanywa baada ya uchaguzi mkuu hazikuwa za haki.
Kakobe alisema tathmini hizo zililenga kumjenga mgombea wa chama tawala ambaye anadai hakustahili kupewa haki hiyo.

Akaongeza:“Chanzo cha machafuko ni inapofikia mtu amepewa haki isiyokuwa yake na yule anayestahili haki hiyo akanyimwa,”.

"Jamii inatakiwa kuondokana na fikra potofu za chama kimoja kushika hatama ya uongozi, huo ni ukale, na hiki ni kizazi kingine,” alisema Kakobe.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Katoliki, Mwashamu Kadinali Pengo,
Alisema yeyote anayehubiri amani, lazima kwanza awe na amani moyoni mwake na suala la kuleta ama kulinda amani ni jukumu la kila mtu na haiwezi kuletwa na viongozi au mataifa makubwa kama ambavyo baadhi ya watu wanafikiria.

“Amani haiji kwa mabavu bali kwa paji la Mwenyenzi Mungu, amani haitegemei wenye mamlaka bali ni kila mmoja wetu bila kujali mali zetu, ilimradi tumtumikie bwana na kutenda mema.

Askofu wa Mkuu wa Kanisa la Anglikana, Dk Valentino Mokiwa aliunga mkono hatua zinazochukuliwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kwa kuwataka wananchi waliochukua viwanja vya wazi kuvirudisha.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi.

Kwa urais wa kuchakachua jk hatakuja apate amani kamwe. Atasemwa mpaka siku ya mwisho.
 
Wasaidizi kama hawafanyi kazi kama inavyotakiwa anaweza kabisa kuwafukuza. Tangu aingie madarakani 2005 ni wasaidizi wangapi ambao amewafukuza kufuatia malalamiko mbali mbali kutoka kwa Watanzania? Alishawahi kutamka kelele za mpangaji........
 
Wala simlaumu jk. Wengine mlimchagua, na alioochakachua matokeo mkamuunga mkono. Alipoambiwa aende kwenye mdahalo wa wagombea akakataa, nyie hamkushtuka kwamba Hana hata uwezo wa kujenga hoja na mtoto wa darasa la ratu. Hajui hata kuwasha komputa nyie mko bize mtandaoni mnamjadili. Kila siku hutoa mifano kwamba anatazama tv, kwa sababu inamruhusu akae kizembe na kuchekacheka.

Endelea jk, kula bata na kupiga misele. Wapambe wako wakipeleka nchi machafukoni haikuhusu. After all, wao ndio wamekuweka madarakani wakijua huna uwezo.
 
Back
Top Bottom