Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,810
- 15,401
Kule kwetu kijijini enzi zetu tulikuwa tunajua sikukuu tatu tu kwa mwaka, kulikuwa na sikukuu ya idi, Krismas na kuzaliwa kwa chama cha TANU, kwa hiyo wazazi walikuwa hawaumizi kichwa sana kuhusu nguo za sikukuu, kwani ni sikukuu moja tu tulikuwa tunapata nguo mpya. Kwa wakiristo walikuwa wanapata nguo mpya wakati wa Krismas na waislamu walikuwa wanapata nguo mpya wakati wa Idi.
Hata hivyo nikisema nguo mpya sina maana ya baba kwenda dukani na kununua nguo mpya kwa ajili yako, hapana. Nguo mpya ilikuwa na maana baba kuchukua suruali yake ya zamani, kuikata kwa wembe vizuri bila hata kukupima. Halafu angeipinda chini kwa umahiri mkubwa. Shughuli ingekuja kwenye ukubwa wa kiuno. Kwa sababu hakuwa na ujuzi wa kupunguza kiuno, angetafuta mkwiji, yaani tambara kama mkanda. Angekuita na kuanza kukupa semina kwanza kabla hajakupa hiyo nguo mpya. Angekwambia, yeye kama baba wa familia anajitahidi sana kuona familia yake inafurahiya sikukuu. Angesema, kuwa amejitolea hata kutoa nguo yake ya pekee kwa ajili yako. Halafu angekupa hilo suruali ambalo alikuwa analivaa siku akienda kuwasalimia wakwe zake tu.
Angekwambia ujaribu sulupwete hilo na angekupa pamoja na ule mkwiji ili sulupwete hilo lisidondoke. Angekusaidia kufunga mkwiji na kukuambia, 'hebu tembea.' Halafu angesema, ‘umependeza kwelikweli.' Kwa sababu ya utoto na ushamba wa wakati ule usingejua kwamba, sulupwete hilo linakufanya ufanane kama kifurushi cha viazi vitamu. Lakini, kwa sababu kule kwetu wakati ule, kila mmoja alikuwa anakatiwa kipande cha suruali na baba yake na kuhesabiwa kuwa amepata nguo mpya, hakuna aliyejali. Nawasifu sana wale wazee wa enzi za utoto wetu. Ni kweli kabisa, nguo mpya maana yake ni nguo ambayo hujawahi kuivaa. Kama baba yako aliivaa na kukupatia wewe, kwako ni lazima iwe mpya.
Lakini huku mjini na kwa watoto wa sasa, mambo ni kinyume kabisa. Krismas hii wanangu hawa watatu wamenitoa jasho kwelikweli, hususan huyu binti yangu Ngina, Binti huyu ananipa ugonjwa wa moyo kila uchao. Wiki moja kabla ya ujio wa sikukuu hii ya Krismas wanangu walitaka kujua nitawanunulia nguo za aina gani. Niliwambia hali ya uchumi hairidhishi na nikaona ni wazo zuri kusingizia umeme. Niliwaambia, kiwanda cha kutengeneza fedha kimesimama kuzalisha kwa sababu ya umeme. Huyu mwanangu Ngina mwenye kiherehere kama bibi yake mzaa mama, alinikata kalma na kusema, ‘baba fedha zinatengenezwa Ulaya siyo hapa nchini. Tuna orodha ya nguo tunazotaka tunataka kwenda na fasheni safari hii, mie bila skin jinzi hapatatosha hapa.'
Nikajua walimu wa siku hizi ni wataalamu hasa, yaani mtoto wa darasa la nne ameshafundishwa kuwa fedha zinatengenezwa Ulaya! Ikabidi nijifanye sikusikia maelezo ya huyu binti yangu ambaye kwa kawaida ndiye anayeongoza migomo kwenye familia yangu. Nikawaambia kama wanataka, nitajitahidi kila mmoja apate gauni, shati na suruali ya mtumba. Kusikia hivyo, watoto wakasema, itakuwa ngumu wao kukubali kuvishwea mitumba. Ngina alikuja na wazo mbadala, alisema, kama sina hela ni afadhali tuuze TV yetu. Lakini wenzake walipinga lile wazo wakidai watakosa kuona Ze Comedy. Ngina hakukubali kushindwa akaja na wazo lingine akitaka niuze Music System yangu ili wapate nguo za sikukuu. Nilipinga wazo hilo na kumfokea kwa kuwa na mawazo mufilisi. Lakini wapi, Ngina hakubali kushindwa, alinijia juu akidai ni jukumu langu kuhakikisha wao wanapata nguo za sikukuu, kwa hiyo nipunguze jazba tuweze kujadili hadi kufikia muafaka. Nilimuonya achunge kauli zake za maudhi.
Hata hivyo alikuja na wazo lingine, alinitaka nikakope. Alinishauri nikakope kwa jirani yetu mmoja ambaye aliwahi kunituhumu kwamba ninamilki mtandao wa wezi wa magari baada ya kuniona nikija na magari tofauti hapo nyumbani karibu kila siku. Magari ambayo yalikuwa ni ya kazini kwangu. Huyu jirani alinichongea Polisi nikaja kusachiwa na kupelekwa kituoni kutoa maelezo. Nilikuja kugundua kwamba ni nuyu jirani yangu ndiye aliyenichongea, kwani baada ya kukamatwa na kupelekwa Polisi huku nyuma alitamba kwamba mwaka huo lazima nifungwe.
Ilibidi nigeukie Dini na kuwaambia kwamba, hata bwana wetu Yesu Kristo katika kueneza Injili wakati huo alikuwa na nguo moja tu na hakuwahi kwenda na fasheni. Wote walinijia juu wakidai nimemkashifu Bwana Yesu Kristo na watamwambia mchungaji. Nikaona ule mjadala utakuwa hauishi kama nisipokuwa makini. Niliwaomba waandike mahitaji yao, kisha nitaangalia uwezekano wa kuomba mkopo kibaruani kwangu. Nikawa nimeufunga ule mjadala.Ama kweli watoto wa kizazi hiki, hawana maadili kabisa.