Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 14,939
- 20,399
Nchi ya Korea kaskazini inafanya maandalizi kurusha kombora la majaribio ambalo limebeba kituo cha satelite kwa ajili ya kutoa taarifa za hali ya hewa.
Viongozi wa kijeshi ambao wamekuwa wakifanya matayarisho ya majaribio wamesisitiza kwamba majaribio ya urushaji wa kombora hilo ni katika kuhakikisha kwamba makombora hayo yana uwezo wa kufikia maeneo ambayo itakuwa ni rahisi kujibu mashambulizi ya nchi maadui.
Kombora hili litarushwa kutoka katika kituo cha Sohae kilichopo karibu na mpaka na nchi ya China ambako maandalizi ya kombora hilo lenye urefu wa mita 30 na liitwalo Unha-3 yalikuwa yakifanywa. Sehemu hiyo ni ileile ambayo majaribio ya awali yalifanywa. Urushaji wa kombora hilo unatarajiwa kufanywa kati ya April 12 na 16.
Siku ya Jumapili waandishi kadhaa wa kigeni walipewa nafasi ambayo ni nadra sana kutolewa, kutembelea kituo hicho na wakajionea wenyewe maandalizi ya urushaji huo wa kombola la Unha-3.
Urushaji wa kombora hilo kwa mujibu wa mkurugenzi wa kituo hicho ni katika sehemu ya sherehe ya kutimiza miaka 100 kwa kiongozi muasisi wa kwanza wa nchi hiyo Kim II Sung ambae pia mwanae Kim iL Jong alifariki mwezi December mwaka jana na mjukuu wake (Kim iL Sung) Kim Jong Un akatwaa madaraka.
Eneo la maandalizi likiwa limekamilika
Nchi za US, Korea ya Kusini na Japan zimelaani mipango hiyo na kusema kwamba Korea Kaskazini inaficha azma yake ya kutupa makombora ya nyuklia, lakini China imesema maneno machache mno kuzingatia kwamba ni wachina wenyewe ndio wanaowapa Korea kskazini technolojia ya kutengeneza makombora hayo.
Nchi za Japan na Korea Kusini zimetoa onyo kwamba endapo mabaki ya kombora hilo yataelekea kwenye anga zao watajibu kwa kupiga makombora yao ambayo yataharibu kabisa mabaki hayo kitendo ambacho hakijawastua kabisa Korea Kaskazini.
Hofu tayari imezuka katika eneo lote la kipande cha Korea au Korean Peninsula) ambao lipo katika eneo zima la Asia Mashariki. Eneo hili limeundwa na pande la ardhi lenye urefu wa kilomita karibu 1100 na linalala likielekea kwenye bahari ya Pasific.
Upande wa mashariki eneo hili limezungukwa na bahari ya Japan na magharibi limezungukwa na bahari ya njano katikati pakiwa na pande la ardhi la Korea ambalo linaunganisha bahari hizo mbili.
Kabla ya vita kati ya Korea Kaskazini na Korea Kusini kwisha mwaka 1953 nchi hizi mbili zilikuwa ni kaichi kamoja na ni mkataba wa Armistice ndio unaotoa fursa kwa kila nchi kuwa huru na mambo yake Korea Kaskazini wakishikilia ukomunisti ambao unafadhiliwa na China na Russia na Korea Kusini kufuata ubepari ambao leo hii umeifanya nchi hiyo kuwa na soko kubwa na bidhaa za kitechnolojia zikiwemo za Samsung na LG.
Pia nchi ya Korea Kusini imewekeza sana kwenye elimu na ni nchi ambayo wananchi wake wote wanapata matangazo ya televisheni kupitia kwenye magari yao ambayo inaitwa DMB au digital Multimedia Broadcasting, pia ndio nchi ambayo inatengeneza magari maarufu na yenye bei nafuu ya KIA na Hyundai.