Population Crisis: Kim akilia machozi kuwaomba Wanawake wa Korea Kaskazini kuzaa watoto ili kuongeza idadi ya watu

MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
31,654
48,432
Huyu jamaa na makombora yake sikujua naye anaweza kufikwa na huzuni mpaka abubujikwe machozi, akina mama pia nao wajiunga kwenye kulia machozi maana mkuu analia, hii ilikua baada ya kusoma taarifa jinsi uzao unapungua, mama hawazai tena kisa changamoto nyingi.

==================

Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amerekodiwa akilia wakati akiwaomba wanawake wa Korea Kaskazini kuzaa watoto zaidi, Wakati wa Kongamano la Tano la kitaifa la Wanawake lililofanyika mjini Pyongyang,nchini humo.

Ikumbukwe kuwa Idadi ya watoto wanaozaliwa nchini Korea Kaskazini inapungua kwa hivyo Rais Kim amewataka wanawake kuzaa watoto zaidi katika nia ya 'kuimarisha mamlaka ya kitaifa'.

Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong UN false amewasihi wanawake katika nchi hiyo ya Asia Mashariki wazae watoto zaidi na kuwalea kama "wakomunisti," na kulia alipokuwa akitoa hotuba ya hisia mbele ya hadhira iliyojaa hisia.

Kim.jpg
 
Nchi ambazo viongozi wake hujikita kushindana ki ufalume na USA, watu wake huishi maisha ya dhiki sana! Moja wapo ni hao North Korea
 
Ndio ajue kuna mambo muhimu ya kushughulikia kuliko kuwekeza kwenye majeshi. Wenzao Japan baada ya kupigwa Hiroshima wakasema sasa ugomvi ugomvi sio kipaumbele chetu tena
 
Akihutubia kwenye kongamano la Wanawake Rais wa Korea ya Kaskazini Kim Jon UN ameonekana Akilia kama ishara ya kuwasihi wanawake kuzaa zaidi Watoto Ili kuongeza idadi ya watu na Nguvu kazi Kufuatia Wimbi kubwa la wazee linaloinyemelea Nchi hiyo huku idadi ya Vijana ikizidi kupungua.

Ikumbukwe kwamba Nchi nyingi zilizoendelea za Ulaya na Asia ikiwemo China na Japan zinakabiliwa na tatizo la Kasi ndogo ya uzazi ambayo imekuwa haiendani na Ongezeko la Wazee kwenye Nchi hizo.

Haieleweki ni kwa nini jamii ikielimila Huwa Inapunguza Kasi ya uzazi na wakati mwingine Baadhi ya Wanawake hawataki kuzaa au wanazaa mtoto mmja tuu.

View: https://www.instagram.com/reel/C0gkGrAMOmE/?igshid=NmJiYWZiY2E0Mg==

My Take
Niliwahi weka makala hapa kwamba Future ya Dunia inalitegemea Bara la Afrika Kwa Sasa Ili kupata Nguvu kazi.

Pia soma 👇
 
Back
Top Bottom