Kongamano la Pili la Katiba: Jumamosi, 02 Aprili 2011

Dr.Slaa na Mbowe,ni kwa nini hawa tu?wote wakristo wote kanda ya kaskazini...wamemtumia Prof.Abdallah Safari ili kuuwa udini tu lakini ishu iko pale pale

Hivi Mbowe ana uwezo gani katika mabo ya Sheria?Ndiyo dr.Slaa,najua ni mtaalam wa Canon law lakini bado hakuna uwakilishi wa Chama uliokamilika,bado kuna mapungufu.Haki itawale jamani
CCM je, kuna uwakilishi wa chama uliokamilika?
 
Kiwanga:Katiba ni chombo cha wananchi na sio mkataba kati yatawala na watawaliwa
 
Pongezi sana UDSM kwa kuwepo kwenu na kuunga mkono mambo ya msingi
 
Raisi asihusike moja kwa moja katika mchakato wa kutengeneza katiba kwa sababu raisi ni zao la katiba
 
Watu wameguna kwa wajumbe wa tume kuteuliwa na raisi,kwamba hawataki
 
Rais asihusishwe katika uundwaji wa katiba, tume ichaguliwe kulingana na matakwa ya sheria!
 
kazi ya uteuzi wa tume ni kazi ya sheria,sheria ndo iseme watu wa tume wanatakiwa wawe vipi,inabidi tume iwe na sura ya kitiafa na sio kuteua watu kihun huni,au watu wenye itikadi moja au kujuana
 
Tuwe na makundi mbali mbali katika uandaaji wa katiba,watoto,walimu,wafanyakazi,wakulima wafungwa,nk
 
Kiwanga: Rais asihusishwe kutengeneza Katiba kwa sababu yeye ni zao la Katiba. Wajumbe wa kutengeneza Katiba kuteuliwa na Rais si sawa. Hadidu za rejea si sawa kuwekwa na Rais, sheria ndio iseme kuwa wajumbe ni akina nani. Makundi mbalimbali yahusishwe: dini, wafungwa, wafanyakazi, wakulima, watoto, nk.
 
Tume lazima ihusishe makundi yote yaliyopo katika jamii yetu, wafungwa, watoto, na wengine wengi..
 
Anasema tume isiteuliwe na Rais, kwa kuwa adidu za rejea wapewa na rais
Hivyo anapendekeza Tume ya katiba itajwe kwenye sheria, na iwakilishe makundi mbalimbali ya jamii kama wakulima, wafanyakazi, wanawake nk.
 
Kwanini muswada unataka yeyote atakae onekana anazuia kuunga katiba atishiwe kufungwa?
 
Ili mchakato uwe huru,una paswa kuwa wa wananchi na tuwe na vyombo huru,..e.g
Tume iliyo huru na yenye sura ya kitaifa
 
Back
Top Bottom