Kongamano la Pili la Katiba: Jumamosi, 02 Aprili 2011

Kiwanga: Kifungu cha 20 cha Muswada wa Katiba mpya si kizuri, kinatoa kitisho kwa atakayeenda kinyume na mawazo ya tume inayokusanya maoni! Very ridiculous indeed!!
 
Duh,nimestuka wakuu,..kumbe huu muswada hautakiwi kupingwa?
Sasa hii ni demokrasia au udikteta?
 
Mfano:
wakenya watu walikuwa wanaunga na kupinga katiba kwa uwazi kabisa na hakukuwa na vitisho kama hivi vya Tanzania
 
Kiwanga: muswada unasema kuwa atakayefanya kampeni wakati wa kukusanya maoni ni kosa la jinai, si vizuri!
 
Kiwanga anatoa mawazo mazuri lakini, wawakilishi wa CCM hawapo sasa sijui itakuwaje.
 
Muundo wa Muungano hautakiwi kuguswa kwenye katiba hii?
Uchaguzi huru?
Uraisi hautakiwi kuguswa pia?

This is crazy,..ni kelele hapa na amestop kwa mda kuongea
 
Hata walio andaa muswada hawajui muundo wa muungano wa Tanganyika na zanzibar...huu ni muda wa uhuru jamani duh
 
Anakosoa Muswada wa katiba unasema wananchi mnaweza kujadili jambo lolote kuhusu katiba mpya lakini msiguse yafuatayo kifungu cha 2

  1. msijadili muungano
  2. serikali ya Zanzibar
  3. mihimili 3 ya dola
  4. urais
  5. national unity
  6. uchaguzi na democrasia
  7. ulinzi na utetezi wa haki za binadamu
 
Kiwanga: katiba ya sasa haina kifungu cha kujiua, anapendekeza Bunge litunge Sheria. Muswada umependekeza mambo yafuatayo yasiguswe: 1. Muungano wa Tz vs Zenj, 2. Urais wa JMT, SMZ, Bunge, Mahakama, Haki za Binadamu, nk. Kiwanga anasema kwamba kusiwe na "Immutable Principles" katika kuandaa Katiba mpya!
 
Kwanini katilka mchakato wa katiba mpya tunawekewa vikwazo vya nini tuongee na nini tusiongee?
Hivi ina maana vile tusivyo ongea havituhusu watanzania au vinahusu raia wa nchi gani?
 
Anakosoa Muswada wa katiba unasema wananchi mnaweza kujadili jambo lolote kuhusu katiba mpya lakini msiguse yafuatayo kifungu cha 2

  1. msijadili muungano
  2. serikali ya Zanzibar
  3. mihimili 3 ya dola
  4. urais
  5. national unity
  6. uchaguzi na democrasia
  7. ulinzi na utetezi wa haki za binadamu
Kwa nini hivyo visijadiliwe wakati ndivyo vyenye kasoro?
 
Kiwanga: kuna wanaojiona kuwa ni watz kuliko wengine, tuondoe woga. Kila mwananchi awasiliane na MP wake ili ampe maoni yake. Anamalizia, tujenge mifumo imara na si watu imara!
 
Hitimisho la kiwanga:
Tujenge mfumor huru wa kujitawala na kujiongoza,ambao utalinda maslahi ya Taifa
 
Back
Top Bottom