Kongamano la Pili la Katiba: Jumamosi, 02 Aprili 2011

CCM wana beep, saa ya ukombozi ni sasa watanzania pandisheni maudhui ya maandamano hakuna sababu ya kupoteza muda any more kama mwenzetu aliyesema itangazwe wazi kwamba maandamano yoyote hata ya kushinikiza uongozi wa leo uachie ngazi ni halali kusiwe na sababu ya kumuomba kibali mtu yoyote yule
 
Wadau waukataa, umejaa kasoro, vitisho
Wataka urejeshwe serikalini ukasahihishwe
Kina Cheyo, Bagenda washushwa jukwaani

mjadala kuhusu mabadiliko ya Katiba, umeingia katika sura mpya, baada ya Muswada wa Marejeo ya Katiba ya Tanzania wa Mwaka 2011 kukataliwa na wadau, kwa madai kwamba umejaa upungufu mwingi na hivyo kutaka urejeshwe serikalini ukafanyiwe masahihisho kabla ya kupelekwa bungeni.
Miongoni mwa upungufu huo, ni pamoja na mapendekezo yanayompa Rais mamlaka ya kuunda tume maalum ya kuratibu mchakato wa Katiba na pia kutoa hadidu za rejea za kazi ya tume.

Upungufu mwingine, unahusu wananchi kuzuiwa na kuadhibiwa kwa kifungo au faini iwapo wataihoji tume, vyama vya siasa kuzuiwa kufanya kampeni ya kuhamasisha wananchi kushiriki katika kupiga kura ya maoni kuhusu Katiba mpya.
Kasoro nyingine ni Bunge kupewa mamlaka ya kutunga Katiba badala ya wananchi na kuzuia wananchi kugusa mambo kadhaa wakati wa kutoa maoni yao katika kujadili mabadiliko ya Katiba.
Cheyo, Bagenda washushwa jukwani
Wakati wadau wakiukataa muswada huo, Mwenyekitii wa Chama cha United Democratic (UDP), John Cheyo na Mwakilishi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Prince Bagenda, walipatwa na wakati mgumu katika kongamano hilo, baada ya wanakongamano kukatiza michango yao na kuwalazimisha kushuka jukwaani jana.
Msimamo wa wadau kukataa muswada huo, ulitolewa kwa nyakati tofauti wakati wakichangia hoja kuhusu mada kuu, ambayo ni "Maudhui ya msingi ya Katiba mpya", katika kongamano la pili la Katiba, lililoandaliwa na Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udasa), katika Ukumbi wa Nkrumah, chuoni hapo.

Kongamano hilo lililoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Udasa, ambaye pia ni mratibu wa kongamano hilo, Dk. Kitila Mkumbo, lilirushwa moja kwa moja na Kituo cha Televisheni cha ITV na Radio One.
Watoa mada walikuwa ni Jaji Mkuu Mstaafu, Barnabas Samatta na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Francis Kiwanga.
Kongamano hilo linafuatia lile la Januari 15, mwaka huu, lililojadili kwa kina haja ya kuwa na mchakato wa Katiba mpya, ambapo wasemaji wakuu walikuwa ni Mwenyekiti wa Kigoda cha Taaluma cha Mwalimu Julius Nyerere cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Issa Shivji, mwanahabari aliyebobea katika fani hiyo, Jenerali Ulimwengu na Mhadhiri wa Mwandamizi wa UDSM, Dk. Xavery Rweitama.
Profesa Shivji: Muswada umejaa upungufu
Akichangia hoja katika kongamano la jana, Profesa Shivji alisema muswada huo una upungufu mwingi wa kiufundi, kimantiki, kilugha na kisiasa na kwa hiyo unaleta hofu kubwa kwa wananchi.
Kabla ya Profesa Shivji kutoa maoni hayo, Kiwanga, alisema muswada huo umetungwa kwa kiwango cha chini, hivyo haustahili kupelekwa bungeni kama inavyotarajiwa kufanywa na serikali. Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, muswada huo, unaweza kuwasilishwa katika Mkutano wa Bunge unaotarajiwa keshokutwa.
Kiwanga alisema wameupitia muswada huo na kujiridhisha kwamba kuna mambo ambayo hayakupaswa kabisa kuwamo kwenye muswada.
Alisema mojawapo ya mambo hayo, ni pamoja na Kifungu kinachopendekeza Rais kuwa na mamlaka ya kuunda tume maalum ya kuratibu mchakato wa Katiba na kutoa hadidu za rejea kwa kushirikiana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).
"Kama tutaridhia pendekezo hili, tutakuwa tumeporwa haki yetu ya kutengeneza Katiba," alisema Kiwanga na kupendekeza Rais asihusike na uundaji wa tume hiyo kwa sababu naye kama ilivyo mihimili ya dola ni zao la Katiba.
Alipendekeza tume kutoundwa na mtu mmoja kwa vile anaweza kuteua watu wa itikadi yake, pia tume iwe na sura ya kitaifa kwa kuwa na uwakilishi wa makundi yenye maslahi katika jamii; kama vile wanawake, watoto, walemavu, wafanyakazi, wakulima na wafungwa.
Alisema jambo lingine, ambalo halikupaswa kuwamo kwenye muswada huo, ni zuio la wananchi kuihoji tume kwenye mahakama, ambapo alisema kwa mujibu wa muswada huo, atakayefanya hivyo atakuwa ametenda kosa la jinai na adhabu yake itakuwa kifungo cha jela au faini isiyozidi Sh. milioni 5.
Jambo lingine, alisema pia licha ya muswada huo kutoa uhuru kutoa mawazo yao kuhusu mabadiliko ya Katiba, katika kutoa mawazo, unawazuia wananchi kugusa mambo kadhaa; ikiwamo Muungano, mihimili mitatu ya dola, urais, umoja wa kitaifa, uchaguzi, ulinzi na utetezi wa haki za binadamu na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).
"Huu si muda wa kuweka vikwazo katika kujadili Katiba," alisema Kiwanga, ambaye alionyesha masikitiko yake kwa muswada huo kutotaja ripoti ya Jaji Robert Kisanga, Azimio la Arusha na kusisitiza ulazima wa kuwapo na utaratibu wa kuwashirikisha wananchi, kuacha kuogopa na mchakato wa mabadiliko ya Katiba usiwe wa kutafutana mchawi.
Mwakilishi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mabere Marando, alisema kitendo cha kuletwa muswada huo, kinaashiria kwamba, serikali imeshafanya maamuzi kwamba, Katiba ya sasa ipitiwe upya na si kuandikwa Katiba mpya kama wanavyotaka wananchi.
Marando ambaye ni wakili maarufu nchini, alisema upungufu mwingine uliomo kwenye muswada huo, ni kifungu kinachoielekeza tume hiyo kupeleka taarifa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa SMZ, ambao alisema wote ni wanachama wa CCM.
Alisema upungufu mwingine umo kwenye sehemu ya tano ya muswada huo, ambayo inapendekeza tume iliyoundwa na Rais, ambaye ni mwanaCCM kuandaa muswada, na Rais huyo kuutia saini na kuwa sheria kabla haujafika kwa wananchi na kuwataka wanakongamano kuukataa muswada huo.
Marando alisema pia muswada huo umevinyima vyama vya siasa, ambavyo vinaungwa mkono na wananchi wengi, kujihusisha na kampeni za kuhamasisha upigaji wa kura ya maoni, ambao umependekeza kuwa kufanya hivyo ni kosa la jinai na kwamba, atakayepatikana na hatia, adhabu yake ni kifungo cha miaka miwili bila kulipa faini.
Alisema upungufu mwingine wa muswada huo, ni kule kuiruhusu tume kufanya kazi na wenyeviti wa serikali za vijiji, mitaa na shehia, ambao alisema kwa uhalisia ni vyama ambavyo siyo CCM kwa sababu ina wakuu wa wilaya na makatibu tawala, ambao watakuwa wakikifanyia kampeni chama hicho.
Dk.Mvungi: Ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa
Mwaklilishi wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Dk. Sengondo Mvungi, alisema walisikitishwa sana baada ya kuupitia muswada huo kwa vile umeonyesha kuwa makelele yao ya tangu miaka ya 1990 ya kutaka kuandikwa Katiba mpya, yameambulia patupu. "Imekuwa sawa na kumpigia mbuzi gitaa."
Alisema tangu miaka hiyo wamekuwa wakidai kuandikwa Katiba mpya na kwamba hawajawahi kutamka wanataka marejeo ya Katiba, kama muswada huo wa serikali unavyoeleza.
Dk. Mvungi ambaye pia ni Mhadhiri Mwandamizi wa Sheria wa UDSM, alisema muswada huo haukupaswa kupewa anuani hiyo, bali ulipaswa kuitwa: "Muswada wa Sheria ya Baraza la Kutunga Katiba Mpya."
"Nchi hii ni yetu sote. Lakini waliotunga muswada huu utadhani si Watanzania kwa sababu wangekuwa Watanzania wangekuwa wanatusikiliza tunasema nini. Sasa tukae mkao wa kiharakati, kwani tukienda mahakamani watakamatwa hapo na watamwambia Jaji asiamue," alisema Dk. Mvungi.
Mwakilishi wa Chama cha Wananchi (CUF), Julius Mtatiro, alisema wakati Rais Jakaya Kikwete anatangaza nia ya serikali ya kuruhusu mabadiliko ya Katiba, alionyesha tabasamu iliyoashiria nia njema ya serikali kuhusu suala hilo, lakini wanashangaa kuona muswada huo ukiwa hauna hata chembe ya tabasamu lile waliloliona kwa Rais Kikwete.
Kutokana na hali hiyo, alionya kuwa iwapo Watanzania hawatapata Katiba mpya wanayoitaka katika kuelekea mwaka 2015, linaweza kuzuka balaa kubwa nchini.
"Kama una nia njema ya kutengeneza Katiba ya kudumu, kuna haja gain ya kutoa vitisho? Sasa tunasema kampeni ya kura ya maoni, tukae kimkakati, kama panataka kuchimbika, pachimbike. Vyama vya siasa tujihusishe kwa nguvu. Kama ni kutupeleka magerezani watupeleke sote," alisema Mtatiro na kupendekeza kabla ya kuhitimishwa mchakato wa kupata Katiba mpya, uanzwe mchakato wa kupata tume huru ya uchaguzi.
Cheyo, ambaye ni Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP), alianza kwa kuwataka wanakongamano kujadili suala la Katiba kwa amani na kushauri kupelekwa muswada huo ukajadiliwe bungeni, hakuweza kuendelea na hoja zake baada ya wanakongamano kumkatiza kwa kelele za makofi na miguno iliyomfanya alazimike kuteremeka jukwaani, huku utetezi wa Dk. Mkumbo kwake ukipuuzwa.
Hali hiyo ilimkuta pia Mwakilishi wa CCM, Bagenda, baada ya wanakongamano kuchukizwa na kauli yake ya kukipamba chama hicho.
Hata hivyo, hoja ya Cheyo ya kupelekwa muswada huo bungeni, iliungwa mkono na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa, Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe na Jaji Kiongozi Mstaafu, Amiri Manento.
Jaji Mstaafu Thomas Mihayo, alisema mtu yeyote mwenye akili timamu, anaweza kushangazwa na mapendekezo ya muswada huo kuwa kosa la jinai kuihoji tume hiyo.
Prof. Maina: Muswada umeandikwa Kiingereza
Profesa wa katika Shule ya Sheria ya UDSM, Chris Maina, alisema miongoni mwa upungufu mkubwa wa muswada huo, ni pamoja na kuandikwa kwa lugha ya Kiingereza, kitendo ambacho kinabagua robo tatu ya Watanzania kutoufahamu kutokana na kutojua lugha hiyo.
Mbunge wa Muhambwe (NCCR-Mageuzi), Felix Mkosamali, alisema muswada huo hakubaliki kwa vile umeandaliwa kana kwamba suala la Katiba ni jambo la dharura wakati si kweli.
TAWLA: Tume haijazingatia uwiano wa jinsia
Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA), Maria Kashonda, alisema hakubaliani na muundo wa tume uliopendekezwa na muswada huo itakayoundwa na watu 30; 15 wakiwa kutoka Tanzania Bara na 15 kutoka Zanzibar.
Kashonda alisema haiwezekani Tanzania Bara yenye watu zaidi ya milioni 40, itoe idadi sawa ya wajumbe wa tume hiyo na Zanzibar yenye watu milioni moja.
Pia alisema hakubaliani na muswada huo, ambao umependekeza wajumbe wa tume 28 kuwa wanaume, huku wanawake wakiwa wawili tu, kitu ambacho alisema hakijazingatia uwiano wa kijinsia.
Prof. Shivji: Katiba siyo mali ya mtu
Profesa Shivji, alitaja baadhi ya vifungu vya muswada huo, kimoja kikiitambua serikali ya Tanganyika na Zanzibar, badala ya Jamhuri ya Muungano, mgongano wa baadhi ya vifungu na kusema: "Kwa jinsi ulivyoandikwa hata mwanafunzi
Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, alisema Katiba siyo mali ya mtu, hivyo watakuwa tayari kuheshimu amani iwapo itakwenda sambamba na haki ya Watanzania wote na kumtaka Rais Kikwete kutoipoteza fursa hiyo ya mabadiliko ya Katiba.
"Tutakwenda bungeni, lakini kama Bunge litaleta ushabiki wake wa kisiasa tutarudi kwa wananchi," alisema Mbowe.
Jaji Manento, alisema muswada huo unaonyesha mawazo ya serikali na kuwataka wabunge waliohudhuria kongamano hilo kulifikisha suala hilo bungeni.
Jaji Samatta: Mwandishi wa muswada amechanganya mambo
Jaji Samatta alisema mwandishi wa muswada huo amechanganya mambo yaliyomo kwenye Katiba ya sasa na inayotarajiwa na kupendekeza kwamba, kabla Katiba mpya kuandikwa, wakuu wa vyama vyote vya siasa wakutane na kukubaliana itikadi moja itakayoingizwa kwenye Katiba na chama kitakachounda serikali kiongoze kwa kufuata itikadi hiyo.
Awali, Jaji Samata, ambaye alikosoa mambo mengi yaliyomo kwenye Katiba ya sasa, ikiwamo Rais kuruhusiwa kuwa dikteta, alipendekeza katika mabadiliko ya sasa ya Katiba, kiwemo kifungu kitakachotambua rasmi kuwapo Mungu na kushauri mahabusu na wafungwa kuulizwa katiba wanayoitaka wakati wa kukusanya maoni.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
 
Kitila you are doing a greate job Mungu akulinde na kukuinua. Lakini angalia isiwe kwenye mambo ya politics tu iwe pia kwenye innovations and on how to integrate our universities with civil servants, politicians na commoners. Universities are supposed to bring about development na development ni continuum/cut across concept so yenyewe inatakiwa ku influence almost everything kwenye jamii ili kuleta welfare. It used to be so zamani hapo Nkurumah thanks you are now trying to revive that spirit.
 
UDASA TUNAHITAJI KONGAMANO NCHI NZIMA NA VYOMBO VYOTE VYA HABRI TUNAHITAJI KUVIONA MSTARI WA MBELE ZAIDI KATIKA HILI

UDASA tafuteni fedha zaidi toka kokote kule; tunahitaji kongamano nchi nzima na kuwashirikisha wadau wote muhimu, wanafunzi, wahadhiri wa vyuo mbali mbali, UDASA nyinginezo katika vyuo vikuu vingine na vyama vya siasa nchini.

Agenda kuu ni kwamba wananchi tunahitaji mchakato wa katiba nchini ambapo serikali ni facilitators tu lakini hatua zote za upangaji, uteuzi, maamuzi, utekelezaji na uwajibikaji wooote ubakie mikononi mwa wadau wa katiba ambapo serikli ni mmojawapo tu.

Haki ya umma kusimamia mchakato mzima wa katiba kamwe haitokaa ipotee; bora wakataa mabadiliko wenyewe ndio wakapotee!!!
 
quote_icon.png
Originally Posted by MwanaCBE

Kuna mchungaji leo katika kongamano la katiba pale udsm kasema ''Mungu hapendi maandamano''.

Katika kitabu cha Yoshua 6:2-5 Mungu anamuagiza Yoshua kuongoza maandamano ya siku 7 ili wauangushe ukuta wa Yeriko na kuuangusha utawala wake.

Mchungaji huyu je aliwahi soma hiki kifungu na vingine vingi katika biblia vinavyoelekeza watu kuandamana??

Nimeipenda sana hii; huyo mchungaji wa maslahi si tofauti na wengine kibao tulionao huku mitaani ambao kazi yao ni kusoma Biblia kwa kuruka mistari na vifungu visivyompendeza.

- Ni kama Brother Jero kwenye kitabu chake Prof Wole Soinka w Nigeria.

 
MASIKITIKO KWA WANAHABARI

TBC1

Yaani ni maskitiko yangu kuwa hii TBC ina waandishi na watangazaji mfu, na Mungu anawaona watakuja KUFA :rip:HIVI HIVI bila ya kuguswa na mtu (Sala Za Watanzania zitafanya WAFE WAZIKWE KAMA MBWA)
Hawezekani kuwa TBC walikuwa hawajui kama kuna mdahalo UDSM kushidwa kutuma report wake hata watuwekee kwenye taarifa yao ya saa2 hakuna. TBC go to Hell

Limepoteza credibility yake kama shirika la Taifa,majadiliano kuhusu katiba hawakuona umuhimu huo..,kumbe mara mia alivyokuwepo Tido alikuwa na kauthubutu..
 
Japo siungani nawe kwa kutumia tafsiri ya kuuzunguka ukuta wa Jericho(hayo tunaweza kuyaongea baadae),lakini naungana nawe kumpinga huyu mch. Temba. Kwa kuwa nmfahamu japo kwa sehemu kdogo, ninamuelewa kama mtu mmoja ambitious sana ambaye yupo tayari kutmia mbinu yeyote mbele yake kutimiza malengo yake. Kwa matamshi yake mara nyingi na kwa vitendo vyake, amejaribu sana ku-seek attention na kupanda ranks kwa nguvu katika namna ambazo mtumishi mnyenyekevu wa Mungu asingezitumia. Kuna mengi lakini kupata walau a glimpse of who this guy really is:
Msome bwana Temba hapa kuhusu DECI

Katika hali inayoonyesha kwamba suala hilo limeingia kwenye siasa, Mchunguji Alphonce Temba, alisema kwamba kwa kiongozi yeyote ambaye ataunga mkono kampuni hiyo, uwezekano wa kushinda ubunge ni mkubwa na yule atakayebainika kuipinga, hataweza kuchaguliwa tena.
Mchungaji Temba alisema DECI ni taasisi ambayo imeanzishwa kwa nguvu za Mungu, hivyo mtu yeyote atakayejaribu kuihujumu ataumia mwenyewe kwani mwasisi wake alionyeshwa maono ya Mungu.
Msome bwana Temba hapa kuhusu urais wa Kikwete
Mchungaji wa Kanisa la Penuel Healing Ministry, Alphonce Temba alisema: "Mwaka 2005, nilikuwa wa kwanza kueleza kuwa Kikwete nji chaguo la Mungu…bado anakubalika na Mwenyezi Mungu atamwezesha kushinda tena kwa kishindo mwaka huu."
Nimekuonesha tu namna alivyo,sijasema mengine..:tape:

quote_icon.png
Originally Posted by MwanaCBE

Kuna mchungaji leo katika kongamano la katiba pale udsm kasema ''Mungu hapendi maandamano''.

Katika kitabu cha Yoshua 6:2-5 Mungu anamuagiza Yoshua kuongoza maandamano ya siku 7 ili wauangushe ukuta wa Yeriko na kuuangusha utawala wake.

Mchungaji huyu je aliwahi soma hiki kifungu na vingine vingi katika biblia vinavyoelekeza watu kuandamana??

Nimeipenda sana hii; huyo mchungaji wa maslahi si tofauti na wengine kibao tulionao huku mitaani ambao kazi yao ni kusoma Biblia kwa kuruka mistari na vifungu visivyompendeza.

- Ni kama Brother Jero kwenye kitabu chake Prof Wole Soinka w Nigeria.

 
Ili kuwahimiza vyama vya siasa kushiriki,jaribu kuwaandikia barua kuwataka waandae hoja zao waje kuwasilisha siku hiyo ili kujenga mazingira shirikishi kwa political actors ,pia serikali kupitia kongamano hilo ipate salaam kuwa wananchi wangependa KATIBA MPYA ipatikane mapema ili wananchi wawe na muda mpana zaidi wa kujipanga katika kuitekeleza kabla ya uchaguzi mkuu 2015 maana itabadilisha maisha yetu kisiasa,kiuchumi,kijamii,n.k.

Vile vile NGOs zenye nguvu zipeni fursa maalum zitoe hoja zao ili finally kuwe na strong solidarity kwa wadau mbalimbali katika nchi yetu maana suala la katiba sio suala la vikundi vidogo vidogo, linahitaji nguvu ya pamoja kwa maslahi makubwa zaidi ya Watanzania na sio siasa na wanasiasa pekee.

Kazi njema Dr.kitila Mkumbo na timu yako yote katika hili,mwisho mjiepushe na ushabiki wa kisiasa usio wa lazima ili kulinda professionalism na heshima ya UDSM as a great university katika Dunia hii.

Mussa Mnyeti,
Mdau.

Mimi pia niungane na wenzangu kutoa pongezi za dhati kwa Udasa na hususani DR Kitila kwa kubuni makongamano elimishi kama haya. Yamesaidia sana katika kuelewa kinachoendelea katika mchakato wa katiba mpya. Hata hivyo, ningeomba uwepo utaratibu maalumu wa kuwadhibiti baadhi ya watu wanaoharibu utaratibu wa mijadala na makongamano kwa kuwataka wazungumzaji wazungumze yale wanayoyataka tu. Hilo linaleta picha mkanganyiko ukizingatia kwamba msingi mkubwa wa mabadiliko ni kukuza demokrasia na kuboresha maisha yetu. Demokrasia inasimama katika upana wa mawazo na kuwa tayari kupokea mawazo tofauti na ya kwako. Mganganyiko unakuwa mkubwa zaidi ikizingatiwa kwamba kongamano linafanyika katika kitovu cha elimu na mlima wa ufahamu Tanzania ikiwahusisha tunaoamini kuwa ni wasomi wa kutuongoza.

Kwa mtaji huo inakuwa vigumu hata kupata katiba nzuri. Katiba nzuri (kwa maoni yangu) inapatikana kwa kuchanganya na kuchambua mawazo mbalimbali ya wananchi na kisha kuyaowanisha ili kupata mawazo muafaka kwa ajili ya wote au kundi kubwa la watanzania.

Tukubaliane kwamba watanzania tunatofautiana kwa mambo mengi na pia tunakubaliana kwa mambo mengi. Tofauti ya elimu, mtizamo wa kisiasa, upeo wa kifikra na maono inaweza kupelekea tofauti katika kutoa na kuchangia maoni. Tofauti hizi ni mhimu kwani Tanzania sio ya wasomi peke yao kama ilivyokuwa sio ya waelewa na wenye upeo mkubwa wa maono peke yao. Sio ya wana CCM na Chadema peke yao. Sio ya wanasiasa peke yao, sio ya wakulima au wafanyakazi peke yao.
 
Mimi pia niungane na wenzangu kutoa pongezi za dhati kwa Udasa na hususani DR Kitila kwa kubuni makongamano elimishi kama haya. Yamesaidia sana katika kuelewa kinachoendelea katika mchakato wa katiba mpya. Hata hivyo, ningeomba uwepo utaratibu maalumu wa kuwadhibiti baadhi ya watu wanaoharibu utaratibu wa mijadala na makongamano kwa kuwataka wazungumzaji wazungumze yale wanayoyataka tu. Hilo linaleta picha mkanganyiko ukizingatia kwamba msingi mkubwa wa mabadiliko ni kukuza demokrasia na kuboresha maisha yetu. Demokrasia inasimama katika upana wa mawazo na kuwa tayari kupokea mawazo tofauti na ya kwako. Mganganyiko unakuwa mkubwa zaidi ikizingatiwa kwamba kongamano linafanyika katika kitovu cha elimu na mlima wa ufahamu Tanzania ikiwahusisha tunaoamini kuwa ni wasomi wa kutuongoza.

Kwa mtaji huo inakuwa vigumu hata kupata katiba nzuri. Katiba nzuri (kwa maoni yangu) inapatikana kwa kuchanganya na kuchambua mawazo mbalimbali ya wananchi na kisha kuyaowanisha ili kupata mawazo muafaka kwa ajili ya wote au kundi kubwa la watanzania.

Tukubaliane kwamba watanzania tunatofautiana kwa mambo mengi na pia tunakubaliana kwa mambo mengi. Tofauti ya elimu, mtizamo wa kisiasa, upeo wa kifikra na maono inaweza kupelekea tofauti katika kutoa na kuchangia maoni. Tofauti hizi ni mhimu kwani Tanzania sio ya wasomi peke yao kama ilivyokuwa sio ya waelewa na wenye upeo mkubwa wa maono peke yao. Sio ya wana CCM na Chadema peke yao. Sio ya wanasiasa peke yao, sio ya wakulima au wafanyakazi peke yao.


Leo pamekuwa na Kongamano la tatu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam la KIGODA CHA MWALIMU. Mada kuu ilikuwa ni nafasi ya Azimio la Arusha katika mjadala unaoendelea wa katiba mpya. Mjadala ulikuwa mzuri sana kuliko mijadala iliyopita. Wazungumzaji walivumiliwa licha ya kutofautiana kwa hoja. Huo ni utaratibu mzuri unaotupa matumaini ya huko tunakokwenda.

Nilikirudi katika mada yenyewe, Professor Shivji amezungumza kwa kina sana nafasi ya Azimio la Arusha katika mjadala wa katiba mpya. Ameanza kwa kubainisha wazi kwamba mjadala sio kuliingiza Azimio la Arusha kama lilivyo katika Katiba mpya bali kuiingiza misingi ya miiko na maadili ya Azimio la Arusha katika katiba yetu mpya. Kwa maoni yangu, Azimio la Arusha lilikuwa na mambo mazuri zaidi kuliko mabaya machache lililokuwa nayo. Kuanguka kwa Azimio kulitokana na mambo mengi pamoja na kuanguka kwa mfumo wa ujumi na siasa wa kijamaa kimataifa. Lakini pia kulikuwa na mapungufu katika kusimamia misingi na kanunu za Azimio la Arusha.

Pamoja na kutoweka kwa Azimo la Arusha, viongozi wetu nafsi zao ziliwasuta kulimaliza moja kwa moja. Ndio maana hadi leo Azimio linatamkwa katika Katiba kama msingi wa itikadi wa nchi japo mfumo mzima wa kiuchumi na siasa unaotamkwa katika Katiba unakinzana na Azimio.
 
Back
Top Bottom