Kona ya Soka la Zenji.... Ni hapa

ZFA: Karume Boys itakuwa ya kudumu

Haji Mtumwa, Zanzibar

CHAMA cha Soka Zanzibar (ZFA) kimesema hakitoivunja tena timu ya taifa ya vijana ëU-17í Karume Boys kama ilivyokusudiwa na badala yake kuimarisha ili kuwa kikosi imara.

Akizungumza na wanahabari, rais wa chama hicho Ali Fereji Tamimu, wakati wautambulisho kocha mpya wa timu ya taifa Abdelfatah El Masqsood kutoka nchini Misri kuchukua nafasi ya kocha Badr El Din Haddad, aliyemaliza muda wake.

Rais Fereji alisema lengo la chama hicho ni kuitunza timu ya vijana kwa muda mrefu.

Hivi sasa hatuna nia tena ya kuivunja timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, na badala yake tutaiimarisha ili kuwa kikosi bora zaidi,î alisema.

Tamimu alifafanua kuwa hatua hiyo imekuja baada ya kuonyesha kiwango cha kuvutia zaidi kwenye michuano ya vijana ya Chalenji iliyomalizika hivi karibuni nchi Sudan.

Alisema timu hiyo imethibisha ubora kwa kufika hatua ya robo fainali, ishara moja wapo ya kuwa kikosi ni imara na kinahitaji kupewa misingi tu.

ìKufika hatua ya robo fainali ni jambo la kujivunia kwa vijana wetu na soka ya visiwani hapa kwa ujumla kikubwa kinachohitajika hivi sasa ni kuboreshwa zaidi,î alisema.

Timu hiyo hivi sasa ipo chini ya kocha wake Hamad Moroco ilirejea nchini hapa hivi karibu kutokea nchini Sudan katika mashindano ya Chalenj, lakini ilitolewa katika hatua ya robo fainali na timu ya Eritrea kwa kuchapwa mabao 2-0.
 
KOCHA Marcio Maximo anajua atakuwa kwenye wakati ngumu zaidi kuliko kipindi chochote alichokaa Tanzania endapo kikosi chake cha Kilimanjaro Stars kitapoteza mchezo wa leo dhidi ya ndugu zao wa Zanzibar Heroes katika mechi ya kufa au kupona ya michuano ya Chalenji.

Mbrazil alishudia Kilimanjaro Stars wakipokea kipigo cha mabao 2-0 kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya mabingwa watetezi, Uganda, The Cranes.

Katika mchezo huo, Zanzibar ikishinda itakuwa imejihakikishia nafasi ya kuvuka hatua ya makundi huku Kili Stars ikibakiza saa chache za kuendelea kuishi mjini hapa ikishindwa kuvuka hatua hiyo ya awali ya michuano ya mwaka huu.

Hii ni mara ya pili kwa timu hizo kukutana katika mchezo wa kuamua hatma yao, katika michuano hiyo iliyofanyika mwezi Januari mwaka huu nchini Uganda, Tanzania ilikwenda kwenye mchezo dhidi ya Zanzibar wakihitaji kushinda ili kufufua matumaini yao ya kusoga mbele kama ilivyo sasa.

Katika mchezo huo uliochezwa mjini Kampala kwenye Uwanja wa Nakivubo, Kilimanjaro Stars ili shinda kwa mabao 2-1 shukrani kwa Danny Mrwanda na Athumani Idd, huku lile la kufutia machozi la Zanzibar likifungwa na Nadir Haroub 'Canavaro'.

Hali hiyo imemfanya kocha Maximo kusema kuwa hakuna shaka kwamba itakuwa ni kazi ngumu kwao hasa ikizingatiwa ukweli kuwa wachezaji wa timu hizo mbili wanajuana udhaifu, ubora.

"Wao wana pointi mkononi na mabao mengi tofauti na sisi. Mchezo huu utakuwa mgumu kwa vile wachezaji wetu wanajuana, lakini naamini kwa morali ya wachezaji wangu niliyoiona katika kipindi cha pili cha mechi dhidi ya Uganda inatia matumaini.

"Tutatumia mfumo wa soka ya kushambulia na kukaba nafasi kwa vile uwezo huo tunao na tuna wachezaji ambao wanaweza kufanya hiyo kazi.

Kwenye mchezo na Uganda tuliathirika baada ya Juma Nyosso kuonyeshwa kadi nyekundu.

"Kwa hiyo kila mmoja ilibidi afanye kazi ya ziada ya kukaba, ndiyo maana ikabidi na mfumo ubadilike. Lakini, katika mchezo dhidi ya Zanzibar, kikosi chote kitakuwepo.

"Kufungwa kwenye mechi ya kwanza hakuwezi kutufanya tupoteze matumaini na muda, bado tuna mechi mbili , dhidi ya Burundi na Zanzibar leo, tushirikiane tufanye kazi hawa vijana wana uelekeo."

Zanzibar ambayo inalingia kumbukumbu yake ya ushindi wa kishindo wa mabao 3-0 dhidi ya Tanzania Bara katika fainali zilizochezwa nchini Kenya, Oktoba 10, 1967 wakati huo lijulikana kama Kombe Palmares Chalenji.

Katika michuano iliyofanyika mwaka 2004 nchini Ethiopia ilishudia timu hizo mbili zikiaga mashindano hatua ya awali kwa Zanzibar kupata pointi tatu pekee baada ya kuinyuka Tanzania Bara kwa mabao 4-2.

Mabao ya Zanzibar yaliyofungwa na Said Abdella dakika ya 6 kwa mkwaju wa penalti, Abdella Juma 29, 73, Twaha Mohamed 85; huku yale ya Kilimanjaro Stars yakifungwa na Mecky Mexime 23, Athumani Machupa 32.

Kocha wa Zanzibar, Hemed Morocco alisisitiza kuwa mchezo wa leo utakuwa mgumu, lakini hawaihofii Kili Stars hata kidogo ingawa wanajua ni timu ngumu.

"Hapa tumekuja na jeshi kamili, ndio maana unaona watu wanacheza soka ya ukweli na ushindi unapatikana na utakuwa mkubwa, sisi hatuna maneno mengi njooni muone soka yetu dhidi ya Kili Stars.

"Tunataka kuendeleza rekodi yetu ya ushindi na kwa vyovyoe vile hatutakubali kushindwa,"alisisitiza kocha huyo akiungwa mkono na kiungo Abdi Kassim anayeichezea Yanga ambaye pia ni nahodha.

Mchezo huo unatazamiwa kuwa na ushindani wa aina yake hasa kutokana Zanzibar Heroes kuwa nao Nadir Haroub 'Cannavaro' kwenye safu ya ulinzi pamoja na Abdi Kassim na Abdulrahim Amour kwenye kiungo, wote ambao wanaichezea Taifa Stars chini ya Maximo.

Kili Stars imenufaishwa na kuwapo kwa Henry Joseph kwenye kiungo kwani ameonyesha mabadiliko makubwa kiuchezaji pale kocha Maximo alipomwingiza katika kipindi cha pili kwenye mechi dhidi ya Uganda.

Tanzania Bara pamoja na kuwa miongoni mwa waanzilishi wa michuano hiyo mikongwe 1926 ilifanikiwa kutwaa taji hilo kwa mara kwanza mwaka 1974 na kusubili kwa miaka 20 kuchukua kwa mara pili mwaka1994, huku ndugu zake Zanzibar wakitwaa ubingwa mara moja mwaka 1995.

Source: Mwananchi
 
Nawachukia sana watu wanaomsifia '*****' Maximo kwamba eti katutoa mbali.hivi ni lini tulikuwa na kocha aliyepewa facilities zote na wachezaji kuwa na mahela timu ikashindwa kucheza.hakuna na bado mara moja moja tuliweza ku achieve makubwa ktk hali ngumu.eti anasema kwamba kabla ya yeye tanzania ilikuwa haijulikani ktk soka wakati kuna kipindi tulikuwa wa 65 kwa ubora na kushiriki fainali za mataifa ya afrika tukiwa na makocha wazalendo !!.ukiangali hata mechi ya juzi tatizo ni upangaji mbaya wa timu ndo umetufungisha.kocha mzuri lazima apeleleze timu pinzani na haje na mbinu sahihi za ushindi.WANATULETEA MAKOCHA WA KINDER GARTEN BRAZIL na mijitu inashabikia kisa mbrazil.mazingira haya haya yaliyopo tumpe timu hii phiri afundishe tuone kama waafrika hatuwezi
 
Nawachukia sana watu wanaomsifia '*****' Maximo kwamba eti katutoa mbali.hivi ni lini tulikuwa na kocha aliyepewa facilities zote na wachezaji kuwa na mahela timu ikashindwa kucheza.hakuna na bado mara moja moja tuliweza ku achieve makubwa ktk hali ngumu.eti anasema kwamba kabla ya yeye tanzania ilikuwa haijulikani ktk soka wakati kuna kipindi tulikuwa wa 65 kwa ubora na kushiriki fainali za mataifa ya afrika tukiwa na makocha wazalendo !!.ukiangali hata mechi ya juzi tatizo ni upangaji mbaya wa timu ndo umetufungisha.kocha mzuri lazima apeleleze timu pinzani na haje na mbinu sahihi za ushindi.WANATULETEA MAKOCHA WA KINDER GARTEN BRAZIL na mijitu inashabikia kisa mbrazil.mazingira haya haya yaliyopo tumpe timu hii phiri afundishe tuone kama waafrika hatuwezi
Kamanda naona umepotea njia, hapa ni soka la Zenj tu, hayo malalamiko yako ya muuza matikiti maji yapeleke kwenye thread husika...

Hapo kwenye damu ya mzee ulikuwa na maana gani vile?
 
mpira unaanza saa ngapi? mtupe matokea jamani tujue kama machogo wametufunga
 
The competition continues on Monday when Kenya take on Uganda before Zambia play Zanzibar in the last eight.
Tuesday's matches will see Tanzania facing Eritrea while Rwanda take on Zimbabwe
More at BBC Sport
 
Uganda and Zanzibar triumph

_46875524_keeper6.jpg
Zanzibar keeper Mohamed Khamis saved two penalties to beat Zambia


Zanzibar beat Zambia 4-3 on penalties as defending champions Uganda eliminated hosts Kenya 1-0 to make it to the last four of the Cecafa Senior Challenge Cup.

Uganda and Zanzibar will now meet on Thursday in the first semi-final of East and Central Africa's regional championship.

Zanzibar held guest side Zambia to a goalless draw in normal time and the game then went straight to spot kicks.

Substitute goalkeeper Mohamed Khamis proved to be the hero for the islanders who saved two Zambian penalties.

Zambia's coach Herve Renard, the only man handling a team going to next month's Africa Cup of Nations in Angola, was clearly disappointed.

"We have gained a lot from this tournament, some of these players will be going to the Nations Cup," he said after the game.

"But of some concern is that if you cannot score penalties in the Cecafa tournament, you can't expect to be any better in the Nations Cup."

Zanzibar's coach Hemed Abdelatif of Morocco was understandably elated.
"It's absolutely fantastic to go through," he said.

"I just admire the players for taking the pressure and doing their best, Zambia is the best team in the tournament and will proud to have played well against them.

"We shall play to our full potential and hope to succeed in the semis and in the final itself."

More at BBC Sport
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom