Kohler utatufanya wana wa Arusha tuichukie CHADEMA

Unafikiri hili jamvi lilianzia kwa ajili ya kampeni za uchaguzi kama ulivyoingia wewe hapa?
Join Date : 18th October 2010
Posts : 1,413
Thanks172Thanked 412 Times in 224 Posts

Rep Power : 23
Na hii ndio maana huna mchango wowote hapa kwa hoja zako badala kuangalia nani kaingia lini na matusi. Kazi uliyoingilia imekwisha bora upunzike hadi Octoba ya 2015 uje tena kwa kazi ileile uliyoingilia hapo mwanzo.

Sawa sawa! Hakiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!................lol!
 
Nasikitika sana kuona jinsi wanadamu tunavyoshabikia njia za kibabe katika kudai tunachofikiri ni haki ilihali njia za kiungwana zipo!
CHADEMA acheni unafiki. Leo ndio mnajua kuna njia za amani? Eboo!! Aibu gani hii. Si nyie ndo mliotushawishi kuwa ni heri kufa tukipigania haki kuliko kufa kwa malaria au typhoid.?Sasa eti leo mnajifanya wapenda amani. Thubutuu! Na mkiendelea hivi chama hiki kitakufa Natural Dealth.
 
Mwanaharakati pole kwa memory hiyo but you must understand that "NOT EVERYTHING IT IS AS IT SEEMS TO BE". Kuna wakati inabidi ukubaliane na hali isiyokurithisha ili kuepuka athari za muda mrefu kwa jamii na kwa maendeleo. Mwenyewe sikupenda hali hii itokee lakini pia sikuwahi kufikiri watawala watakubali kuwa walikosea, siyo ccm hii wala serikali hii. For the sake of Arusha today and future kulikua na ulazima wa muafaka. Kilichotokea ni step katika mabadiliko yajayo. MABADILIKO NA MAISHA YETU HAYAISHII KWENYE UMEYA WE MUST GO ON, MUAFAKA HUU NI MSINGI WA MABADILIKO YAJAYO. CDM WAWATUMIKIE WANANCHI WA ARUSHA WALIOWACHAGUA MIAKA MITANO ISIISHIE KWENYE KUGOMBEA UMEA.
THAT'S POLITICS.
Very well said!!!!!!!!!! thanx.
 
Sitaisahau Jan, 5 nilipokoswa koswa na Risasi za moto, Mabomu ya machozi na Virungu vya FFU nilipokuwa kwenye Maandamano ya kupinga Uchaguzi batili wa Meya wa Arusha. Sitaisahau pia ile siku niliyoacha shughuli zangu zote na kwenda kwenye mazishi ya tulioamini ni mashujaa waliokufa wakitetea haki ya wananchi wa Arusha. Tuliimba nyimbo nyingi za kishujaa bila kujali manyunyu ya mvua yaliyokuwa yakitudondokea na kufuatia na jua kali likituchoma. Tulikusanyika kuanzia saa mbili asubui lkn viongozi
Jina la Mwanaharakati halikufai.Mwanaharakati wa nini?wa Upotoshaji?unaweza thibitisha unachokizungumza?Duu!
 
[h=2][/h]
quote_icon.png
By Horseshoe Arch
Nasikitika sana kuona jinsi wanadamu tunavyoshabikia njia za kibabe katika kudai tunachofikiri ni haki ilihali njia za kiungwana zipo!

CHADEMA acheni unafiki. Leo ndio mnajua kuna njia za amani? Eboo!! Aibu gani hii. Si nyie ndo mliotushawishi kuwa ni heri kufa tukipigania haki kuliko kufa kwa malaria au typhoid.?Sasa eti leo mnajifanya wapenda amani. Thubutuu! Na mkiendelea hivi chama hiki kitakufa Natural Dealth.
Vua Gamba nachukia watu mnaofikiri kwa kutumia masikio....nachukia...huhitaji PHD kutafakari!
 
Jina la Mwanaharakati halikufai.Mwanaharakati wa nini?wa Upotoshaji?unaweza thibitisha unachokizungumza?Duu!

Mheshimiwa si unakumbuka siku ile ya tarehe 5 Jan roho za watu watatu zilipoaga dunia kwa ajili ya kilewana Arusha na watanzania wengi walichokiamini kuwa haki haikutendeka kwenye uchaguzi wa umeya wa Arusha na uchaguzi ulikuwa null and void? hata viongozi wa kidini nao walisistiza msimamo wa chama wakisema hawamtambui meya wa Arusha kumbe kulikuwa kunawezekana kuzungumza na kupewa mnachokitaka iweje mlitumia ngazi ya kuvuruga amani na kusababisha umwagaji damu ilhali hilo lilikuwa linaweza kuepukika?
 
CUF inakufa kwa upuuzi huu huu wa mgawanyo wa madaraka na wezi wa mchana.Sasa CDM Arusha Mwigamba,Nassari,Lema Mnatueleza nini?Hatushabikii vurugu lakini maelfu ya watu wana uchungu na dhuluma na mauaji yaliyofanya na Polisi wa CCM hivyo maelezo ya kina na yenye mshiko tunayataka pale NMC haraka iwezekanavyo kabla hatujawaadabisha.

Mimi neseme bora ya CUF!!! wao walipigwa virungu, kuteswa na hata kuuliwa kwa miaka 15! ndipo wakahiari kufunga ndoa na CCM, lakini CDM wamenistua sana...yaani kutoka November 2010 mpaka June 2011 (hardly miezi 7 !!!), wako chali na wameridhia ndoa. Naamini watawapa wapinzani wao hoja kama kumbe nao ni opportnist tu! kama CCM Taifa ikiridhia serikali ya mseto..CDM hawana ubavu wa kukataa.

Kwa majumuisho haya, nao pia tuwaite ni CCM-D?
Kikwebo.
 
Nakubaliana nawe kabisa kuwa kuna tatizo la kutumia makalio katika kufikiri na ndio maana wenzenu mliwakimbizia huko kunakotumiwa makalio kwa vile fikira zenu na akili zenu ziko huko mnakokusema. Unakataa nini iwapo kama wenzenu walipoingia muafaka mlisema wameolewa sasa kitendo ndio kilie kile unafikiri kitabadili maana. CHADEMA Arusha wameolewa na Magamba kwa mujibu wa msamiati wenu kwa neno muafaka.
waliitukana sana cuf kuwa wameolewa na ccm,ila wao sasa wamebakwa tena mchana kweupee.
 
Jina la Mwanaharakati halikufai.Mwanaharakati wa nini?wa Upotoshaji?unaweza thibitisha unachokizungumza?Duu!
Duu! Kweli wabunge wa viti maalumu ni mzigo. Kama huwezi hata kukumbuka vifo vya watu wale 3 mliowaita mashujaa. me nahisi hata bungen huwa husimami kwa miguu yako bora H.mdee.
 
Jina la Mwanaharakati halikufai.Mwanaharakati wa nini?wa Upotoshaji?unaweza thibitisha unachokizungumza?Duu!

Muhishimiwa usitake watu waamini hizi picha ndio gharama ya unaibu meya............. mmepata nyie wamekosa wanafamilia jiweke kuwa ungekuwa mke au dada wa waliokufa ungelionaje hili jambo?
 
Attachments

  • mazishiyachadem5.JPG
    mazishiyachadem5.JPG
    31.4 KB · Views: 17
  • mazishiyachadem6.JPG
    mazishiyachadem6.JPG
    104.3 KB · Views: 22
  • mazishiyachadem7.JPG
    mazishiyachadem7.JPG
    37.4 KB · Views: 22
mheshimiwa, ustaarabu wa mtu au chama pia hupimwa katika uwezo wa kujadiliana, kusamehe na kusahau. Ingekuwa si hivyo South Africa leo ingekuwa bado haikaliki. lakni Mandela na wote waliosota Robin Island gerezan walikubali kujadiliana, kusamehe na kusahau yooooooote na matokeo yake ndiyo hiyo bondeni (RSA) ambayo leo inasitawi! Au mwenzetu wewe ni wa jino kwa joni???
Mulipo amua kuilamu CUF kumbe mlisahau kuwa Mja hajesha Kuumbwaaa
 
Bwana Shossi ni imani yangu kua tunamtumikia bwana mmoja...tunachotofautiana ni aina ya utumishi wetu; Hatutafikia mwisho kuita CUF ni chama cha kimwinyi na CHADEMA cha kisultani...na vibwagizo vya 'kiongozi mmoja wa dini kasema hivi ama vile..'
Huwezi kuifananisha Chadema na CUF hata kidogo,CUF ni NGO'S ya Bwana Shariff ambaye baada ya kupata alichopokonywa mdomoni CUF itabakia history labda apokwe mwingine tonge mdomoni aje na taasisi yake..
Sisemi Chadema ni chama cha mitume ama malaika,ni chama kinachoongozwa na watu wenye mazuri na mabaya kama ilivyo desturi ya wanadamu,ila tofauti ni kwamba Chadema pamoja na kua na maadui wengi ila ni chama pekee kilichodhubutu kuilazimisha serikali walau kufuata taratibu!..unaweza kunigrade vyovyote unavyotaka ila ukweli utabakia pale pale kwamba mnaoshabikia vurugu na uhasama uliotokea Arusha wakati ule ni miongoni mwa wale mnaowaombea mabaya wenye mtazamo chanya wa mambo ili waonekane hawafai na wana wishes zao.
 
Ernesto Cheka

The Moment Of Truth:The Complete Text.(What Every Tanzanian Should Read)

by Ernesto Sheka

Ndoto na chuki zaja hadharani sasa;

Baada ya miaka takribani 26,Julai 1992 mfumo wa vyama vingi ukaanza.The same year Mtei akaanzisha Chadema na mpaka ninapoandika hili,in practical terms yeye ni mwenyekiti wa Chadema,kwake yeye ile ni fimbo maalumu ya kumchapa Mwalimu Nyerere siku akifanikiwa japo kila mara anakosea mahesabu huku jamii ikizidi kuamka na kujua historia ya taifa na kuchambua mambo hatua kwa hatua.Uzee wake umekuwa wa mashaka na wasiwasi.Ni dhahiri kuwa masterplan ya kuanza kwa Chadema ilianza kuandikwa Nairobi na baadaye Washington huku ikiuwaza ubepari na Ikulu kabla hata ya usajili.Lilian Mbowe ni mtoto wa kike wa Edwin Mtei ambaye aliolewa na Mbowe.Ni daktari ambaye kama nilivyosema awali anajishughulisha na kuendesha club ya usiku katikati ya jiji la Dar es salaam mtaa wa Mkwepu.Nyumba zao hutumika kukusanya vijana na wengi wana upofu na historia ya Chadema,wanaogundua huondoka mara moja.(Mtafuteni David Kafulila atawahadithia sehemu hii).
Je,ilikuwaje Mbowe akashinda uenyekiti na si Zitto Kabwe?
Edwin Mtei namnukuu akisema,”we can’t give this position to a man from nowhere” akimaanisha Zitto Kabwe,Zitto alitaka kuondoka ila alibaki kwa sababu zake.Tafakari hiyo kauli ya Mtei.Who’s a man from nowhere and who’s a man from somewhere??Ni ipi hasa masterplan ya mzee huyu aliyechekeana kinafiki na Nyerere?To revenge and take back his dignity and self interests.Ni ndoto yake ya ujanani na anaomba Watz tumsaidie aitimize.
Imefanikiwa kiasi gani?
Hali ni ngumu,ukabila bado umekuwa tatizo.Kifo cha Wangwe,maneno kuhusu viti maalumu

Kwa maana hiyo kama ilivyo CUF ni NGO ya bwana Seif Shariff tuamini CDM nayo ni NGO ya Mtei? au CDM ni NGO ya wachagga eti kwa kuwa mbunge wa ilemela ni mchagga na wabunge wengi wa CDM wanatoka kabila fulani mie sitaki niamini hivyo nataka niamini kuwa hivi ni vyama vya siasa vyenye malengo ya kuukwaa ukubwa na kushika dola!
 
Muhishimiwa usitake watu waamini hizi picha ndio gharama ya unaibu meya............. mmepata nyie wamekosa wanafamilia jiweke kuwa ungekuwa mke au dada wa waliokufa ungelionaje hili jambo?
Mdau,Na ile CD ya Lema ya maandamano na mauaji ya Arusha aina tena maana yoyote imekuwa kama tusi kwa wana Arusha
 
Mdau,Na ile CD ya Lema ya maandamano na mauaji ya Arusha aina tena maana yoyote imekuwa kama tusi kwa wana Arusha

Achana na CD kwani kilichokuwa kinatakiwa si kimeshapatikana? walisema uchaguzi ulikuwa batili lakini wataalamu wa siasa waliosomea siasa pale magogoni walijua kuwa hakuna cha uchaguzi hawa jamaa wanataka madaraka na ndio msingi mkuu wa chama chochote cha siasa ni madaraka na wakaamua kuwapa walichokitaka leo wanakana maneno yao! Hawa hawa walisema kuwa hawawezi kushirikiana na mafisadi kumbe yalikuwa ni maneno ya "sizitaki mbichi hizi" sasa tunaona wanazila baada ya kuinamishiwa mkungu uliokuwa mbali na kimo chao.

Ushauri wangu kwa wanandugu.

Siasa ndivyo zilivyo gharama za kuukwaa ukubwa tumeziona sehemu nyingi duniani na waliogharimu maisha huwa hawafaidiki lolote unless nchi iongozwe na mtu moja au chama kimoja lakini kwa dizaini hii unakubali huku unakataa kule tutaendelea kupigika kwa maana hiyo tuangalie ustaarabu wa kujikwamua na umasikini na kamwe tusiwategemee kina fulani watatuondoa umasikinini kwa kushusha bei ya sementi na sukari ni waongo!

Wanajua shida zenu wanazitumia kama karata zao ikisha wanawabwaga! tufanyeni kazi kwa bidiii kwani huo ndio msingi wa maendeleo.

Mwenye akili timamu na afikirie...

Ikiwa roho/nafsi tatu zina dhamani ya umeya/unaibu meya je dhamani ya ubunge na urais ni roho/nafsi ngapi? tuwapige vita wanaoleta maneno ya uchochezi yenye sura za kuvunja amani kwa kutaka madaraka wakati wanaweza kuzungumza na kuelewana. Tuwashauri wawe wanafanya njia za kidiplomasia zaidi kuliko kichochezi.
 
Mwanaharakat

Hilo ni sawa, nina uhakika kwa umakini wa viongozi wa chadema hilo litafanyika soon.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom