Mnondwe
JF-Expert Member
- Apr 10, 2015
- 4,013
- 3,672
Wakistaafu hawarudi vijijini.inabidi hizo nyumba za masaki wapangishe waweze kuishi mjini.
Ha ha ha
Wakistaafu hawarudi vijijini.inabidi hizo nyumba za masaki wapangishe waweze kuishi mjini.
Shirika la nyumba limeshindwa kuhudumia wananchi wenye kipato kidogo. Shirika hilo lilianzishwa kwa madhumuni ya kuhudumia wananchi hasa waishio mijini ambapo shirika hilo mwanzoni liliijenga nyumba nyingi ambazo zilikuwa rahisi kupangisha. Wapangaji walikuwa wakilipa kodi kwa mwezi.
Shirika la nyumba la taifa la sasa limejenga nyumba ambazo zinauzwa kwa bei kubwa mno kiasi ambacho wananchi wengi hawawezi kumudu kununua. Ushauri wangu ni kuwa shirika hilo lirudi kwenye misingi yake ya awali kwa kujenga nyumba nyingi na rahisi kwa ajili ya kupangisha na kodi iwe inalipwa kwa mwezi. Nyumba hizo zijengwe kwa aina tofauti ili kukidhi mahitaji tofauti ya wapangaji. Kwa mfano zijengwe nyumba ambazo mpangaji anaweza kupanga chumba kimoja tu, au mwingine anaweza kupanga nyumba ndogo yenye vyumba viwili, sebule choo na bafu n.k
Kwa kufanya hivyo serikali itakuwa imewapunguzia wananchi wengi adha ya kutafuta mahali pa kukaa hasa mijini. Ikumbukwe pia kuwa si kila mtu anaweza kurudi vijijini. Wengi wapo mijini kwa shughuli za kikazi na zinginezo nyingi.
Wakati tunamaliza chuo pale UDSM nilibishana sana na marafiki zangu, msimamo wangu sitaki kabisa kuishi Dar wao wanakomalia eti hapa hatoki mtu. Nimewaacha huko bana. Dar hapafai kuishi mtu wa hela za kuunga unga, housing mbaya, sanitation mbaya, mara kipindupindu, joto mbaya, usafiri shida, foleni shida, maji shida, hupai fresh air kwa maeneo mengi.
Kuna kipindi nilikuwa na safari ya kikazi hapo Dar, nilifikia kwa rafiki yangu anakaa Kibada kigamboni. Goog thing alikuwa na nyumba kubwa sana na eneo kubwa na iko mlimani kwa hiyo at least ilikuwa nzuri. Sasa kituko, tunapishana siku tatu hatujaonana, alfajiri saa 11 kashaondoka anawahi foleni ili asichelewe ofisini, usiku anarudi saa tano mimi nimeshauchapa usingizi. Haya ni mateso na tunawanyima watoto wetu haki zao za msingi za kukaa na wazazi.
Karibuni huku mikoani aisee, nikiamka najiandaa dakika 15, na kwenda ofisini natumika dakika kumi