Utafiti: Mtanzania Anatumia Miaka 18 Kukamilisha ujenzi wa Nyumba Yake huku Asilimia 70% ya Watanzania Wanaishi kwenye Nyumba za Kupanga

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,076
49,767
Naunga mkono findings za Huu utafiti.

-Mtanzania anatumia Miaka 18 kukamilisha ujenzi wa nyumba yake ya kuishi.
-Asilimia 70% ya Watanzania wote wanaishi kwenye nyumba za kupanga
-Vipato vya Watanzania wengi ni kuanzia 80,000-1,500,000 Kwa mwezi na huvipata Kwa kudunduliza.

Kiufupi Watanzania wengi ni Maskini Sana maana hii ripoti haijadanganya hata ripoti ya Benki ya Dunia ilisema karibu nusu ya Watanzania ni maskini.

My Take
Serikali tunaomba mfanyie kazi Ushauri huu wa Watafiti hasa hapa wanapopendekeza kuanzisha mikopo midogo midogo ya kuwezesha Wananchi kujenga Ili wawe wanarejesha mdogo mdogo.

=====

DAR ES SALAAM: Asilimia 70 ya watanzania wanaishi katika nyumba za kupanga huku wanaojenga wakichukua muda mrefu zaidi ya miaka 18.

Hayo yameelezwa katika ripoti ya utafiti wa ‘Housing Microfinance (HMF)’ uliofanywa na Shirika la Habitat for Humanity International (HFHI) na Tanzania Mortgage Refinance Company (TMRC) iliyozinduliwa leo Novemba 9, 2023 jijini Dar es Salaam.

Utafiti huo ulifanyika katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na Dodoma kwa wananchi wenye umri wa miaka 25 hadi 50 wakiangazia hali ya vipato vyao.

Mkurugenzi wa Nyumba na Fedha kutoka Habitat For Humanity Internation, Daniel Mhina akizungumza amesema watanzania wengi hawana kipato cha kumudu kujenga nyumba na wanaojenga huchukua muda mrefu.

“Unapojenga nyumba muda mrefu kwa miaka 18 gharama zinaongezeka, zinakuwa kubwa kuna kurekebisha mabati, kupaka rangi kwa mtanzania wa kawaida anatakiwa kupata mkopo kwenye huduma za kifedha, changamoto tuliyoiona, huduma za kifedha hazina mikopo inayoendana na matakwa ya watanzania,”amesema Mhina

Utafiti huo umeonyesha kuwa kaya nyingi za kitanzania zinaishi kwa kipato cha chini na cha kati zinazopata kati ya Sh 80,000 ($34) hadi Sh milioni 1.5 ($630) kwa mwezi.

Ripoti hiyo inasema wananchi waliohojiwa walidai kuwa wangependelea kukopa na kila mwezi kurejesha sh 5,000 na wengine walipendekeza rejesho kuwa na ukomo wa sh 80,000.

Hata hivyo ripoti hiyo imeonyesha kuwa changamoto kubwa iliyopo kwa wahitaji wa mikopo ni kutokuwa na uwezo wa kumudu vigezo vinavyohitajika katika taasisi nyingi za kifedha ikiwemo mabenki, unyanyapaa na kutoaminika kwa wajengaji.-

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa TMRC, Oscar Mgaya amesema waliona ipo haja ya kuanzisha mikopo midogo ya nyumba kwa watu wa kipato cha chini na cha kati ambao wana tabia ya kujenga nyumba zao hatua kwa hatua kwa kutegemea pesa kidogo wanayopata.

“Mikopo hii itawezesha kuchukua mikopo midogo midogo kwa ajili ya kujenga nyumba zao kwa awamu. Kwa mfano, mtu anaweza kuchukua mkopo kujenga msingi, kisha baada ya kurejesha anaweza kuchukua mkopo mwingine kwa ajili ya kuendeleza ujenzi huo,” amesema.

Chanzo: Habari leo
 
Kwani NY ni asilimia ngap n wamiliki wa nyumba?
Dar n mji wa kibiashara n rahs capitalist kuumilik kuliko watu wa kawaida
 
Nilipofika Dar-es-salaam kwa mara ya kwanza mwaka 2010 nilishangaa kuona wazee wa makamo (miaka 50's) bado wamepanga na wanalipa kodi.

Ukitaka kujua hii nchi watu ni maskini panda basi kwenda mikoani utaona namna watanzania wanavyoishi kwenye vibanda.
 
Nchi hii ilibidi rais awe anatumia bajaji halafu waziri atumie bodaboda. MaV8 ya nn na umaskini wote huu??
 
Masikini katika nchi ya Tanzania wapo kwenye mikoa yote sio mikoani pekee. Mpaka hivi tunazungumza Kuna watu wanalala kwenye maboksi Kariakoo nje ya maduka na wengine wanakesha na abiria stendi. Hawana hata vibanda vya nyasi.
 
Back
Top Bottom