Sikujua wapo Raia Mjini analipa kodi ya nyumba 2M kwa mwezi?

Pantomath

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
796
3,248
Hapa sizungumzii kodi ya fremu ya biashara, Sizungumziii Ma-Celebrities hao najua wanazidi hata hapo, sizungumziii Matajiri sijui wa kutoka wapi huko, nazungumzia Mtu mwenye Mishe zake za kutosha za kumuingizia kipato Mjini, haya ma Gap ni makubwa aisee, Nimeshangaa sana.

Najiuliza ni katika mazingira gani mtu huyu anatoa 2M kwenye nyumba ya kupanga?

Jee yupo mjini kwa muda?

Yupo vizuri sana kwamba hio hela ni nukta kwake, huku akiwa anajenga?

Kweli tukubali kutofautiana..., watu wana pesa zao.

Huwezi kusema huyu mtu hana malengo na Mipango, Maana mpk mtu ameweza hivyo tayari ni mpango huo..
Ila mtu huyu ni vigumu kumuelewa katika normal sense na hio ndio siri na utofauti kati ya wewe na yeye...
 
Najiuliza ni katika mazingira gani mtu huyu anatoa 2M kwenye nyumba ya kupanga?
Unashangaa nini babu kwa mtu kutoa 2M za madafu kwa malipo ya kodi ya nyumba kwa mwezi mmoja?

Kuna wengine wanatumia hiyo hela kulala kwa usiku mmoja tu hotelini na hulala hadi miezi 3.

Tafuta hela babu ule mema ya nchi, acha kushangaa shangaa hapa duniani tunapita tu 😂
 
SSa
sa kama mtu una daladala tano tu mjin, kila daladala kwa siku inaleta laki,jumla kwa siku laki 5, utashindwa kodi ya 2 m kwa mwezi? hayo ni mapato yake ya siku nne tu

Unashangaa nini babu kwa mtu kutoa 2M za madafu kwa malipo ya kodi mwezi mmoja?

Kuna wengine wanatumia hiyo hela kulala kwa usiku mmoja tu hotelini na hulala hadi miezi 3.

Tafuta hela babu ule mema ya nchi, acha kushangaa shangaa hapa duniani tunapita tu 😂
Tunatafuta ila hazkamatiki!Lete mbinu.
 
Hiyo hela ya kawaida sana.

Ukiweka kwenye dola ni usd 800 tu.

Masaki, mikocheni, upanga, hiyo ni kodi ya nyumba ya kawaida tu.

Pia kuna nafasi ukizipata kazini. Haupaswi kuishi sehemu ambayo sio salama.

Mfano upewe cheo cha CFO, CEO, MD, bank ama shirika kubwa.. lazima utazame utulivu na usalama wako kwanza.

Hivyo hata kama una nyumba yako kinyerezi, tegeta ama Bunju ni vizuri ukaihama na kwenda kuishi maeneo yenye utulivu na usalama mkubwa.
 
Back
Top Bottom