SOLD: Kiwanja Kipo Kivule - Kitunda (Ilala - DSM) mita 30 x 22 kinauzwa

Nov 17, 2011
40
7
Kiwanja chenye urefu wa mita 30 na upana wa mita 22 kinauzwa.
Kipo Kivule jirani na Kanisa (RC) la Kigango,
Kipo Tambarare,
Majirani wanaendelea kujenga na wengine wameshahamia,
Kinatazama barabara kubwa ya mtaa,
Kina faa kwa makazi au biashara,
Umeme bado kufika ila upo katika mpango (Tanesco wana sambaza nguzo)
Hakina Hati ya Wizara ya Ardhi (Unsurveyed plot) ila eneo limepangika vizuri sana (Pongezi kwa viongozi wa Mtaa)
Hakina mgogoro wowote.

Bei 7.5m (Negotiable)

Karibuni
 
Mimi mnataka sana kiwanja na ningependa kuja kukiona kama itawezekana Jumapili hii Mungu akipenda
Ila bei ni ghali sana kaka
Bei za viwanja kama hivyo angalau 3.5 kaka
Unasenmaje?
Nijibu
 
Mvumilivu wangu,
Unakaribishwa kukiona wakati wowote.
Ila kuhusu bei (7.5m) itaendelea kuwa hiyo hiyo kukiwa na mabadiliko ni kidogo sana. Bei unayopendekeza ya 3.5m sikupingi maana vipo vya bei hiyo ila sifahamu vizuri vinapatikana maeneo gani kwa huku Kivule. Ukitafuta zaidi labda unaweza kufahamu vipo wapi kisha utafute ulinganifu na hiki ninachokiuza.

Vitu vinavyopelekea bei kuwa hivyo (siwezi kusema ni juu au chini maana hakuna bei maalum) ni pamoja na eneo kilipo, majirani wanaokizunguka, ufikikaji wa eneo husika, jinsi kilivyo (tambarare), ukubwa wake, matarajio ya siku chache zijazo eneo hilo, nk, nk, nk.

KAribu sana
 
Hoyce,
Haswaaaaaaaa
Nitakuwa ni jirani yako japo mie siishi hapo.
Kiwanja chenyewe kipo mbele ya uwanja wa mpira uliopo karibu na Chekechea. kuna mchikichi mkubwa eneo hilo.
Unaionaje mitaa ya huko kuhusu barabara?
 
Nipe basi simu no. yako kaka. Mimi umenijibu lakini hujanipatia no. yako ya simu au hata email au unitumie no. yako ya simu kwa private message
nadhani umeniewa kaka
 
Nimepunguza bei sasa nahitaji 6.5m tu
Karibuni


kiwanja chenye urefu wa mita 30 na upana wa mita 22 kinauzwa.
Kipo kivule jirani na kanisa (rc) la kigango,
kipo tambarare,
majirani wanaendelea kujenga na wengine wameshahamia,
kinatazama barabara kubwa ya mtaa,
kina faa kwa makazi au biashara,
umeme bado kufika ila upo katika mpango (tanesco wana sambaza nguzo)
hakina hati ya wizara ya ardhi (unsurveyed plot) ila eneo limepangika vizuri sana (pongezi kwa viongozi wa mtaa)
hakina mgogoro wowote.

Bei 7.5m (negotiable)

karibuni
 
Kiwanja chenye urefu wa mita 30 na upana wa mita 22 kinauzwa.
Kipo Kivule jirani na Kanisa (RC) la Kigango,
Kipo Tambarare,
Majirani wanaendelea kujenga na wengine wameshahamia,
Kinatazama barabara kubwa ya mtaa,
Kina faa kwa makazi au biashara,
Umeme bado kufika ila upo katika mpango (Tanesco wana sambaza nguzo)
Hakina Hati ya Wizara ya Ardhi (Unsurveyed plot) ila eneo limepangika vizuri sana (Pongezi kwa viongozi wa Mtaa)
Hakina mgogoro wowote.

Bei 7.5m (Negotiable)

Karibuni

Kaka embu tufanye wote hesabu ndogo tu,
Eneo la kiwanja = 22 x 30=
660 Sqm.

Bei ya kiwanja = 6,500,000/-

Tshs/1sqm = 6,500,000÷660
=Tshs 9,848

Status = Unsurveyed

Kaka huoni kama unaua sana namna hiyo??

Bei za kiwanja cha serikali kilichopimwa Kibada au Gezaulole iwe Sawa na kisichopimwa kweli jamani??
 
Hivyo viwanja vya huko Kivule umenuna sana ni 2.5M, Mi napafahamu vizuri sana huko acha kuibia watu hapa.
 
Hivyo viwanja vya huko kivule umenuna sana ni 2.5M Mi napafahamu vizuri sana huko acha kuibia watu hapa.
Asante kwa mtazamo wako. Ni kweli sio 2.5m tu; hata BURE unaweza kupata. Nafurahi kukutaarifu kuwa nimekiuza jana kwa TZS 6,200,000.00 na aliyekinunua ni mwenyeji wa Kivule huko huko. Endelea kutafuta utapata vya bei ndogo usikate tamaa.Karibu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom