Montserrat
JF-Expert Member
- Sep 9, 2011
- 10,273
- 13,847
Imeshuka kutoka pale udsm ilipokuwa inatoa graduate mwenye phd anayeuzika mpaka kutoa graduate wa phd asiyeuzika na ambaye hawezi kuongea hata sentensi tatu za kiingerezai) Ni ni vigezo vya elimu kushuka au kupanda? Kumekuwa na kilio kwa muda sasa kuwa elimu yetu imeshuka sana; nimkewa najiuliza na nakuulizani nanyi pia, imeshuka kutoka wapi?
Naona kile kilio cha wananchi wa Serengeti kama kilivyonukuliwa katika makala ya Maggid kimeanza kutupa mwanga.Kwamba wazazi wamekataa watoto wao waende shule wakati hata kusoma na kuandika hawajui. Kumbe kigezo kimoja hapa cha chini kabisa ni kujua kusoma na kuandika . Je, katika hili tulikuwaje huku nyuma na sasa tupo wapi. Nafikiri kuna waja wenzetu kina Maggid katika makala zao zijazo kuainisha vizuri zaidi katika haya majambo.
ii) Je, Wizara ya Elimu imechukua hatua gani baadhi ya kupewa ushahidi na wazazi kuwa watoto wao waliibiwa mitihani? Hivi kweli ni sawa wizara ikae kimya tu katika jambo zito la namna hii?
iii) Kuna hoja kubwa zaidi. Kwamba watoto wa viongozi wetu hawasomi katika shule za serikali. Japokuwa Maggid hakutoa takwimu katika kushibisha hoja yake, napenda niamini hivyo. Na tunaweza kujumuisha na kusema kuwa wakubwa hawatumii huduma za jamii za serikali wanayoiongoza.Je, hili nalo ni sawa? Ni haki kweli viongozi wetu kukataa kutumia mahospitali na shule zetu halafu wakati huohuo tuwatarajie kuboresha hizi huduma? Inakuja kweli hii?
Wakati umefika tuanze kuhoji uhalali wa viongozi wetu kutokutumia huduma za jamii za serikali na wakati huohuo wakidai kuwa huduma hizo sasa zimeboreka na zimepata mafanikio makubwa.
Kama alivyosema Maggid, akili mkichwa!