Kiwanda cha Cement Wazo Hill hakichafui mazingira?

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,148
7,724
Swali hili nawauliza wataalamu wa mazingira NEMC. Je, kiwanda Cha Cement cha Wazo Hill hakina athari kwa afya za wakazi wa maeneo ya Tegeta, Ununio, Boko, Madale, Bunju na Basihaya?

Uchunguzi wangu usio rasmi umebaini nyumba nyingi za maeneo hayo zimeganda vumbi juu ya mabati. Je, Vumbi hili linalo toka juu ya kiwanda Cha wazo halina madhara kwa wakazi wa Madale, Tegeta, Ununio, Basihaya na Boko?

Naomba kujibiwa kitaapamu kutoka NEMC.

Naendelea kufanya utafiti.

kwa sasa nimepiga kambi maeneo ya basihaya.
 
Watu ndio walifata kiwanda sasa unataka kiwanda kisimame au watu wahame?
Nakubaliana na wewe kuwa watu wa maeneo hayo ndio wamekifuata kiwanda, lakina swali langu lilikuwa je kuna athari kwa afya za wakazi wa maeneo hayo?
 
Wakazi wengi wa Dar es salaam wanakula sanaaa na kuvuta sana sumu kutokea kwenye viwanda vilivyojirani na makazi yao. Lakini kwa sababu viongozi wetu hawawajali sana wananchi wanawaacha wateketee tuu mdogo mdogo.

Inasikitisha sanaaa, nenda vingunguti angalia mabati yalivyoliwa na kutu ndani ya muda mfupi tuu nyumba haina hata miaka 8 lakini bati lina kutu limeisha.
 
Sasa ni wakati wa kuhamisha kiwanda cha Wazo Cement kwasababu tayari kimekua karibu na makazi, pia eneo limekua dogo kutokana na msongamano wa watu na magari.

Wakati kinajengwa pale miaka ile palikua porini na mji ulikua bado hauja tanuka.

I'm sure viongozi wanaona ila wamekaza tu fuvu kwasababu ya maslahi yao binafsi
 
Sasa ni wakati wa kuhamisha kiwanda cha Wazo Cement kwasababu tayari kimekua karibu na makazi, pia eneo limekua dogo kutokana na msongamano wa watu na magari...
Kiwanda kipo pale hata kabla ya Uhuru wananchi ndio walioenda kuvamia ardhi ya wazo cement na hati za maeneo yote yanayo zunguka kwahiyo wananchi ndio wanaopaswa kuhama
 
Kiwanda kipo pale hata kabla ya Uhuru wananchi ndio walioenda kuvamia ardhi ya wazo cement na hati za maeneo yote yanayo zunguka kwahiyo wananchi ndio wanaopaswa kuhama
Nisawa mkuu, lakini kumbuka kabla ya uhuru Dar ilikua haijafika hata mwenge zaidi ya kambi ya jeshi tu.

Lakini sasa tunapaswa tukubali kwamba tayari mji umetanuka na kiwanda cha Cement Wazo kimezungukwa na makazi ya watu kila upande.

Hili ni jambo la kutumia busara tu kwamba ni wakati sasa kiwanda kinatakiwa kiupishe mji kwa afya na manufaa ya uma
 
Kwa msingi huo unaweza kusema kuwa;
Tegeta, Madale, Ununio, Basihaya, Boko na Bunju sio sehemu salama za kuishi, baada ya miaka 10 hadi 20 tutakuwa na ongezeko la wagonjwa wa TB na saratani.
 
Back
Top Bottom